Mkuu unafahamu kutengeneza Baiskeli? Kama ujuavyo Sweden na nchi nyingine nyingi za Ulaya, baiskeli ni usafiri wa kawaida na watu wengi hutumia. Nakushauri uanzishe sehemu ya kutengeneza.
Anza za majirani wanaokuzunguka badae wakishakujua utaanza kupokea za watu wengi. Jambo la msingi punguza tu bei maana garage za kutengeneza bike kwa Sweden ni very expensive. Unaweza ambulia hata 1000 kr kwa siku. Hiyo ni sawa na 260K za Bongo!
Kuna jamaa M-Kongo anapiga hiyo kazi pamoja na kunyoa watu nyumbani kwake tu kwa bei nafuu. Huwezi amini ana make pesa kimasikhra na maisha yanamwendea vizuri. Muhimu usichague tu kazi.
Mie kutokujua kutengeneza baiskeli na kutokujua kunyoa imenikosesha pesa za bure kabisa. Hapa kilichobaki ni kutafuta tu kazi ya kufanya delivery..