Viprealestate
Senior Member
- Jan 21, 2014
- 128
- 129
Shukrani sana, usisahau kuvote hapo juuAsante sana kwa hii elimu
Umakini unatakiwa sana kwetu wazazi/walezi na wanafunzi wenyewe.HII NI HATARI SANA WAZAZI WANASOMESHA KWA TABU
Vaa viatu vya mzazi/mlezi aliyejibana ili kijana wake apate elimu zaidi huku akiamini kabisa kuwa elimu ni daraja kuelekea mafaniko. Au mfikirie kijana aliyeamua kwa dhati kusoma kwa bidii ili tu kutimiza ndoto yake kupitia elimu.
Bahati mbaya sana mwisho wa haya unakuja kuambiwa kuwa kile alichosoma mwanao ni feki tu na hakina msaada wowote kwake na hata kwa jamii. Bahati mbaya zaidi ni namna mfumo wetu wa ajira unatazama zaidi vyeti kuliko ujuzi.
UJANJA WA VYUO ULIPO.
Uzoefu wangu wa kufanya kazi kwenye vyuo vya kati umenifanya nifahamu mambo mengi kiasi kuhusu ujanja unaotumiwa na hawa wamiliki wa hizo taasisi.
●Kusajiliwa Chuo.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kwenda kusoma kwenye vyuo visivyosajiliwa kabisa na mamlaka husika, na wanafunzi/wazazi hufanya hivyo wakiamini maneno ya matangazo kuwa chuo kinatambulika na serikali.
Wengine wanafikiri kule kupeleka tangazo redioni au kwenye Televisheni basi inatosha kujiridhisha hicho chuo ni sahihi. BIG NO, hizo zote ni mbinu za kuwavuta wanafunzi wakajiunge.
●Chuo kimesajiliwa lakini Kozi haijasajiliwa.
Bahati mbaya hapa ni ngumu kufahamu utofauti wa hivi vitu viwili kama hauko makini na sio mfuatiliaji kufahamu mfumo wa hivi vyuo ulivyo.
Mzazi/Mwanafunzi anaweza akafanya utafiti akagundua ni kweli chuo kimesajiliwa na mamlaka husika mfano NACTE. Kumbe hii peke yake haitoshi kabisa bali inabidi aende mbali zaidi kufahamu na Kozi husika kama imesajiliwa pia.
Msomaji wangu hapa usichanganye, kuna kusajiliwa kwa Chuo na kusajiliwa kwa hicho kinachoenda kusomewa. Hivi vitu viwili lazima viende sambamba kabisa kwa maslahi ya kesho yako.
Mwisho wa siku unakuta kijana kasoma Chuo fulani kwa ngazi ya Stashahada na dhamira yake kuendelea elimu ya juu lakini anakwama kwenye kupata AVN kwasababu kama hizo hapo juu.
Lakini yupo ambaye kasoma chuo hichohicho lakini Kozi nyingine yeye kapata AVN na yupo Chuo Kikuu. Ukiona hivyo fahamu yule aliyekosa kama ufaulu wake wa kidato cha hauna shida na GPA yake ya Stashahada ipo sawa basi tambua ametapeliwa.
SASA NINI CHA KUFANYA.
Mzazi/Mwanafunzi kabla hujaomba hivi vyuo vya kati jiridhishe kwa kufuatilia taarifa ya Chuo kwenye mtandao wa Nacte wa www.nacte.go.tz utaenda kuna sehemu kuna orodha ya vyuo au utasearch jina la hicho chuo na utasoma taarifa zake.
Pembeni ya jina la chuo husika utaona aina ya usajili wake( kuna ngazi za usajili) utaona pia Kozi zilizoruhisiwa kufundisha na kwa levo gani.
NB: Viko vyuo vimesajiliwa na vimeruhusiwa kufundisha masomo kwa ngazi ya Astashahada tu na siyo vinginevyo. Kuwa makini.
Seriously!!
Pesa inatafutwa kwa shida aisew sio wachukue kirahisiUmakini unatakiwa sana kwetu wazazi/walezi na wanafunzi wenyewe.
Tuko pamoja
UbarikiweKeep it up
Tunashukuru sana kwa taarifa hii muhimu, natamani kama ingeweza kufika wizara husika ikatungwa sheria kudhibiti hivi vyuo vinavyofanya huu uhuni kwa kweli, inauma sana unasoma chuo chenye usajili halafu unaambiwa elimu yako haitambuliki.Vaa viatu vya mzazi/mlezi aliyejibana ili kijana wake apate elimu zaidi huku akiamini kabisa kuwa elimu ni daraja kuelekea mafaniko. Au mfikirie kijana aliyeamua kwa dhati kusoma kwa bidii ili tu kutimiza ndoto yake kupitia elimu.
Bahati mbaya sana mwisho wa haya unakuja kuambiwa kuwa kile alichosoma mwanao ni feki tu na hakina msaada wowote kwake na hata kwa jamii. Bahati mbaya zaidi ni namna mfumo wetu wa ajira unatazama zaidi vyeti kuliko ujuzi.
UJANJA WA VYUO ULIPO
Uzoefu wangu wa kufanya kazi kwenye vyuo vya kati umenifanya nifahamu mambo mengi kiasi kuhusu ujanja unaotumiwa na hawa wamiliki wa hizo taasisi.
●Kusajiliwa Chuo.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kwenda kusoma kwenye vyuo visivyosajiliwa kabisa na mamlaka husika, na wanafunzi/wazazi hufanya hivyo wakiamini maneno ya matangazo kuwa chuo kinatambulika na serikali.
Wengine wanafikiri kule kupeleka tangazo redioni au kwenye Televisheni basi inatosha kujiridhisha hicho chuo ni sahihi. BIG NO, hizo zote ni mbinu za kuwavuta wanafunzi wakajiunge.
●Chuo kimesajiliwa lakini Kozi haijasajiliwa.
Bahati mbaya hapa ni ngumu kufahamu utofauti wa hivi vitu viwili kama hauko makini na sio mfuatiliaji kufahamu mfumo wa hivi vyuo ulivyo.
Mzazi/Mwanafunzi anaweza akafanya utafiti akagundua ni kweli chuo kimesajiliwa na mamlaka husika mfano NACTE. Kumbe hii peke yake haitoshi kabisa bali inabidi aende mbali zaidi kufahamu na Kozi husika kama imesajiliwa pia.
Msomaji wangu hapa usichanganye, kuna kusajiliwa kwa Chuo na kusajiliwa kwa hicho kinachoenda kusomewa. Hivi vitu viwili lazima viende sambamba kabisa kwa maslahi ya kesho yako.
Mwisho wa siku unakuta kijana kasoma Chuo fulani kwa ngazi ya Stashahada na dhamira yake kuendelea elimu ya juu lakini anakwama kwenye kupata AVN kwasababu kama hizo hapo juu.
Lakini yupo ambaye kasoma chuo hichohicho lakini Kozi nyingine yeye kapata AVN na yupo Chuo Kikuu. Ukiona hivyo fahamu yule aliyekosa kama ufaulu wake wa kidato cha hauna shida na GPA yake ya Stashahada ipo sawa basi tambua ametapeliwa.
SASA NINI CHA KUFANYA?
Mzazi/Mwanafunzi kabla hujaomba hivi vyuo vya kati jiridhishe kwa kufuatilia taarifa ya Chuo kwenye mtandao wa Nacte wa www.nacte.go.tz utaenda kuna sehemu kuna orodha ya vyuo au utasearch jina la hicho chuo na utasoma taarifa zake.
Pembeni ya jina la chuo husika utaona aina ya usajili wake( kuna ngazi za usajili) utaona pia Kozi zilizoruhisiwa kufundisha na kwa levo gani.
NB: Viko vyuo vimesajiliwa na vimeruhusiwa kufundisha masomo kwa ngazi ya Astashahada tu na siyo vinginevyo. Kuwa makini.
Mwisho.
Hii tabia ipo hadi Vyuo vikuu kwa wanafunzi ambao wapo chini ya NACTE yaani Astashahada na Stashahada. We fuatilia hao wanafunzi wakitaka kuendelea na elimu ya juu wanavyopata changamoto kupata AVN.
Umeongea sahii saana.Tunashukuru sana kwa taarifa hii muhimu, natamani kama ingeweza kufika wizara husika ikatungwa sheria kudhibiti hivi vyuo vinavyofanya huu uhuni kwa kweli, inauma sana unasoma chuo chenye usajili halafu unaambiwa elimu yako haitambuliki.
Hiyo AVN ndo nini kwanza?Hii tabia ipo hadi Vyuo vikuu kwa wanafunzi ambao wapo chini ya NACTE yaani Astashahada na Stashahada. We fuatilia hao wanafunzi wakitaka kuendelea na elimu ya juu wanavyopata changamoto kupata AVN.
Ni AWARD VERIFICATION NUMBER Mkuu.Hiyo AVN ndo nini kwanza?
Kila kona majangaNilidhani ungeviongelea hata vyuo ambavyo 'vimesajiliwa'. Mbona na huko kote wanatoa elimu ya janja janja tu na siyo maarifa kamili ya kumsaidia mtahiniwa?