Story of Change Ulaghai unaofanywa na baadhi ya vyuo nchini, chukua tahadhari na usitapeliwe

Viprealestate

Senior Member
Jan 21, 2014
125
250
Vaa viatu vya mzazi/mlezi aliyejibana ili kijana wake apate elimu zaidi huku akiamini kabisa kuwa elimu ni daraja kuelekea mafaniko. Au mfikirie kijana aliyeamua kwa dhati kusoma kwa bidii ili tu kutimiza ndoto yake kupitia elimu.

Bahati mbaya sana mwisho wa haya unakuja kuambiwa kuwa kile alichosoma mwanao ni feki tu na hakina msaada wowote kwake na hata kwa jamii. Bahati mbaya zaidi ni namna mfumo wetu wa ajira unatazama zaidi vyeti kuliko ujuzi.

UJANJA WA VYUO ULIPO

Uzoefu wangu wa kufanya kazi kwenye vyuo vya kati umenifanya nifahamu mambo mengi kiasi kuhusu ujanja unaotumiwa na hawa wamiliki wa hizo taasisi.

●Kusajiliwa Chuo.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kwenda kusoma kwenye vyuo visivyosajiliwa kabisa na mamlaka husika, na wanafunzi/wazazi hufanya hivyo wakiamini maneno ya matangazo kuwa chuo kinatambulika na serikali.

Wengine wanafikiri kule kupeleka tangazo redioni au kwenye Televisheni basi inatosha kujiridhisha hicho chuo ni sahihi. BIG NO, hizo zote ni mbinu za kuwavuta wanafunzi wakajiunge.

●Chuo kimesajiliwa lakini Kozi haijasajiliwa.
Bahati mbaya hapa ni ngumu kufahamu utofauti wa hivi vitu viwili kama hauko makini na sio mfuatiliaji kufahamu mfumo wa hivi vyuo ulivyo.

Mzazi/Mwanafunzi anaweza akafanya utafiti akagundua ni kweli chuo kimesajiliwa na mamlaka husika mfano NACTE. Kumbe hii peke yake haitoshi kabisa bali inabidi aende mbali zaidi kufahamu na Kozi husika kama imesajiliwa pia.

Msomaji wangu hapa usichanganye, kuna kusajiliwa kwa Chuo na kusajiliwa kwa hicho kinachoenda kusomewa. Hivi vitu viwili lazima viende sambamba kabisa kwa maslahi ya kesho yako.

Mwisho wa siku unakuta kijana kasoma Chuo fulani kwa ngazi ya Stashahada na dhamira yake kuendelea elimu ya juu lakini anakwama kwenye kupata AVN kwasababu kama hizo hapo juu.

Lakini yupo ambaye kasoma chuo hichohicho lakini Kozi nyingine yeye kapata AVN na yupo Chuo Kikuu. Ukiona hivyo fahamu yule aliyekosa kama ufaulu wake wa kidato cha hauna shida na GPA yake ya Stashahada ipo sawa basi tambua ametapeliwa.

SASA NINI CHA KUFANYA?

Mzazi/Mwanafunzi kabla hujaomba hivi vyuo vya kati jiridhishe kwa kufuatilia taarifa ya Chuo kwenye mtandao wa Nacte wa www.nacte.go.tz utaenda kuna sehemu kuna orodha ya vyuo au utasearch jina la hicho chuo na utasoma taarifa zake.

Pembeni ya jina la chuo husika utaona aina ya usajili wake( kuna ngazi za usajili) utaona pia Kozi zilizoruhisiwa kufundisha na kwa levo gani.

NB: Viko vyuo vimesajiliwa na vimeruhusiwa kufundisha masomo kwa ngazi ya Astashahada tu na siyo vinginevyo. Kuwa makini.Mwisho.
 
Upvote 39

maficpgt

Member
Jun 16, 2016
10
45

UJANJA WA VYUO ULIPO.

SASA NINI CHA KUFANYA.

Mzazi/Mwanafunzi kabla hujaomba hivi vyuo vya kati jiridhishe kwa kufuatilia taarifa ya Chuo kwenye mtandao wa Nacte wa www.nacte.go.tz utaenda kuna sehemu kuna orodha ya vyuo au utasearch jina la hicho chuo na utasoma taarifa zake.

Pembeni ya jina la chuo husika utaona aina ya usajili wake( kuna ngazi za usajili) utaona pia Kozi zilizoruhisiwa kufundisha na kwa levo gani.

NB: Viko vyuo vimesajiliwa na vimeruhusiwa kufundisha masomo kwa ngazi ya Astashahada tu na siyo vinginevyo. Kuwa makini.Seriously!!
 
Tingitane

Senior Member
Apr 18, 2012
103

Tunashukuru sana kwa taarifa hii muhimu, natamani kama ingeweza kufika wizara husika ikatungwa sheria kudhibiti hivi vyuo vinavyofanya huu uhuni kwa kweli, inauma sana unasoma chuo chenye usajili halafu unaambiwa elimu yako haitambuliki.
 
Umeongea sahii saana.
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,190
2,000
Nilidhani ungeviongelea hata vyuo ambavyo 'vimesajiliwa'. Mbona na huko kote wanatoa elimu ya janja janja tu na siyo maarifa kamili ya kumsaidia mtahiniwa?
 
malunde_mc

Member
Jul 19, 2021
9
45
Hilo tatizo niliwahi kukumbana nalo chuo kilifungwa na tukahamishiwa chuo kingine matokeo take tukasoma diplomamiaka 4
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom