Ukwepaji Kodi umezidi. Serikali ibuni mfumo mzuri wa ulipaji Kodi

Usiu
Niko kampuni moja ya....Kuna ishu wanazifanya kwaujumla wake mm cfurahishwi na wanafofanya kwa kutuelekeza cc maafisa wake jinsi ya kukwepa Kodi. Iko siku niatawazinguaa wacha nikuzannye data za kutosha nitawapelekeaa tra niwatinye jinsi mizigo inatoka pale kinyemela Hadi kwamlaji bila kutolewaa risiti halali.
Usiunyee mkono unaokulisha, hzo kodi zenyewe zinazokusanywa zinapigwa balaa na hao viongozi wa serikali
 
Wafanyabiashara kwa sasa wanauza bidhaa zao bila kutoa risiti na ukidai unakwambia mashine imeharibika au nenda kwingine.

Kama ni mbali ukaamua kununua mashine inajazwa kiwango cha chini kwa kuepusha usumbufu mtu anaondoka
 
Pamoja na kwamba mada yako ina hoja ya msingi....ila kwa mm naona tungetumia nguvu nyingi kupambana na serikali....ili hicho kidogo kinachopatikana kupitia Kodi....kitumike kwa maendeleo ya kweli kwa manufaa ya wanainchi wote....pesa nyingi za walipa Kodi zinaishia mifukoni kwa watendaji wachache....mbaya zaidi hakuna hatua wanachukuliwa....cha kusikitisha zaidi....licha ya vipato vyao vikubwa hao wabunge na Mawaziri....nao hawalipi Kodi.
 
Umesema ukweli kabisa yaani wanoshadadia watu kuikwepa kodi hawajawahi kuuza hata promenade haujui gharama za frem hawajuj logistic charges running cost za biashara
 
Hapa mkuu mbona unatetea ukwepaji kodi? Ile mashine inachukua kodi ya serikali tuu ndio maana hawataki kutumia,mimi napendekeza kodi ya awali ndio zingine zifuatie au sheria iwe kali kwa wananchi kwamba ukikutwa bila risiti ule faini ya kutosha hapo mbona kodi tutalipa tuu?
Hiyo machine inachukua kodi ya serikali tu kweli
 
Hili suala ni Gumu sana.Hebu fikiria,mimi sijui kabisa bei ya soko ya bidhaa flani,naenda dukani nataka kununua(sema labda vitasa vya mlango) muuzaji ananiambia bei pamoja na VAT
Kitasa A. ni sh 25,000
Kitasa B. ni sh 40,000
Kitasa C ni sh 55,000
ila mimi nina sh.45,000 nimekipenda kitasa C.Muuzaji anakubali hiyo ofa yangu ya sh 45,000 kwa masharti kwamba sitapata risit ya sh 45,000 badala yake atanipa risiti ya kutembelea barabarani ya sh25,000.

Hapo mimi nimesave Tsh10,000(mafuta ya gari kunirudisha kwangu Ulongoni).

Kwa hiyo kwa Sh 25,000 VAT ni Sh 4,000 na kwa sh 55,000 VAT ni Sh8,400 .so kimsingi mmegawana,serikali imepata 4,000/= badala ya sh 8,400 na wewe umepata sh 10,000,na Muuzaji pia amepata kwa sababu atarecord mauzo pungufu,hivyo kulipa kodi kidogo.Kumbuka pia muuzaji anayo ile 8400- 4000.

Mwisho kabisa wanaoibia mapato serikali ni wanunuzi wenyewe zaidi kwa sababu,mfumo wa bei za bidhaa umewalazimsiha hivyo.Kwenye mafuta huu wizi haupo.

La pili ni udhaifu wa AUDIT ya TRA kwa sababu wanajua muuzaji aliingiza nchini stocks kiasi gani.ila kwa sababu ya uwezo mdogo wa maafisa wa TRA,mara nyingi wanakimbilia kuangalia vitabu vya mauzo tuu bila kuangalia stocks ziliingizwa ngapi au kuzalishwa na zimeuzwa ngapi.

Nini kifanyike?

Serikali itafute watalaamu wapya wa kutosha,kuhakikisha wale wafanyabiashara wakubwa wanafanyiwa stock audits rafiki lakini toshelevu(friendly but comprehensiveAudit).Mtu ameingiza stocks za milioni 500. Anaingiza tena stocks za milion500 ndani ya miezi miwili(Hizi kumbukumbu zote anazo comishina wa forodha).Mbona ni rahisi tuu kwenda dukani mwake kuona zimebak stocks kiasi gani,maana yake tofauti zitakuwa zimeuzwa.halafu inalinganishwa na mauzo halisi aliyo declare wakati wa kulipa kodi.

Kwa sababu bei ya soko ya bidha zote inajulikana.

La pili ni kuweka sticker ya TRA,kila stock inayouzwa iwe na sticker ya TRA,afisa wa kodi anayekagua resiti barabarani aweze kutambua bei halisi ya hiyo bidhaa na kulinganisha kodi iliyolipwa.

Sasa hiv TRA wameweza kutengeneza mfumo wa kuhakiki EFD receipts,nadhani waende mbele zaidi.

Kwa leo ni hayo
Biashara za namna hiyo hazipo nyingi hapo unadeal na distributors tu na sio supplier wadogo na pia utakuwa unapinguza wigo wa kodi
 
Tuwe wazalendo mkuu tukiona ukwepaji kodi tutoe taarifa maana mwisho wa siku tunawanufaisha wachache hao matajiri afu sisi tutaumia zaidi kwenye huduma
Yaani aisee,umenikumbusha kule Botswana.. Wale nafikiri majawapo ya vitu vingine vilivyowasaidia kupata angalau mafanikio waliyonayo, na kuweza kubana tabia za ufisadi, ni hulka waliyokuwa Watswana karibu wengi waliyojijengea,ya kuwa macho muda wote,kwa wananchi kuwa rahisi sana kutoa taarifa kwa authorities zao makini(i.e.kwa kuwa wananchi wanakuwa na imani kubwa kutoa taarifa kutokana na utendaji wa kazi usio shaka..) dhidi ya vitengo vinavyokubalika vya kifisadi... basically walijitahidi kila mtu kuwa ' watch man' wa mwenzake... hivyo kupunguza sana watu kuweza kufanya vitendo hivyo vya kwenda kinyume cha sheria kirahisi kwenye mambo mbalimbali....
 
Tuanze kufanyia kazi jambo hili,tungeweza kuwaripoti tungepunguza sana mambo fulani
 
Naenda nunua laptop ananiambia bila vat ni 800000 na vat ni 944000tshs, kisha naambiwa ni chaguo langu hapo, rais anatubembeleza tulipe kodi unafikiri nitachagua kipi?
Kuna shida kwenye chanzo cha uzalishaji wa bidhaa. Kama tangu kwenye chanzo VAT inalipwa, then muuzaji wa anayefuatia hadi wa mwisho asipotoza VAT hasara inakula kwake (labda kama hivyo aweke excessive price)
 
Pamoja na kwamba mada yako ina hoja ya msingi....ila kwa mm naona tungetumia nguvu nyingi kupambana na serikali....ili hicho kidogo kinachopatikana kupitia Kodi....kitumike kwa maendeleo ya kweli kwa manufaa ya wanainchi wote....pesa nyingi za walipa Kodi zinaishia mifukoni kwa watendaji wachache....mbaya zaidi hakuna hatua wanachukuliwa....cha kusikitisha zaidi....licha ya vipato vyao vikubwa hao wabunge na Mawaziri....nao hawalipi Kodi.
Vyote kwa pamoja vinatakiwa vifanyiwe kazi
 
Habari,

Wakuu wafanyabiashara wanakwepa sana kodi kwa kutotoa risiti na kutoa risiti pungufu ya mali iliyonunuliwa na wanunuzi hawadai risiti.

Ukidai risiti muuzaji anadiriki kusema eti risiti ni kwa wanunuzi wa jumla, rejareja hawatoi.Saa nyingine unaambiwa mashine imeharibika .

Kingine, ukidai risiti utaambiwa bei tofauti na ile ya kununua bila risiti lengo ni ku-discourage usidai risiti.

Bila kodi hatuwezi kuendelea kama nchi, TRA waje na mfumo wa kulipa kodi mapema kuliko kutegemea wanunuzi ambao hata hawajali, yaani matangazo ya ukiuza toa lisiti na ukinunua dai risiti hayajasaidia lolote.

Lakini pia vyombo vya law enforcement bado havitimizi wajibu wake ipasavyo,kama lisiti zingetolewa inavyostahiki TRA na Serikali wangekusanya pesa nyingi sana.
Nakuunga mkono... Yapasa wapate dawa ya ukwepaji wa kodi zilizopo kabla ya kubuni Kodi za kichwa (kama hizi za simcard na luku)
 
Back
Top Bottom