Ukwepaji Kodi umezidi. Serikali ibuni mfumo mzuri wa ulipaji Kodi

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Habari,

Wakuu wafanyabiashara wanakwepa sana kodi kwa kutotoa risiti na kutoa risiti pungufu ya mali iliyonunuliwa na wanunuzi hawadai risiti.

Ukidai risiti muuzaji anadiriki kusema eti risiti ni kwa wanunuzi wa jumla, rejareja hawatoi.Saa nyingine unaambiwa mashine imeharibika .

Kingine, ukidai risiti utaambiwa bei tofauti na ile ya kununua bila risiti lengo ni ku-discourage usidai risiti.

Bila kodi hatuwezi kuendelea kama nchi, TRA waje na mfumo wa kulipa kodi mapema kuliko kutegemea wanunuzi ambao hata hawajali, yaani matangazo ya ukiuza toa lisiti na ukinunua dai risiti hayajasaidia lolote.

Lakini pia vyombo vya law enforcement bado havitimizi wajibu wake ipasavyo,kama lisiti zingetolewa inavyostahiki TRA na Serikali wangekusanya pesa nyingi sana.
 
Pia nimemsikia mbunge fulani Jana akisema Serikali ipanue wigo kwa kutoza kodi kwenye matangazo madogo madogo nk yanayofanyika kwenye mitandao ya kijamii

Hii nchi ina mambo mengi ya kufanya bila kodi hatuwezi enda na kutegemea tuu mikopo na misaada hatufiki popote.

Tabia ya kubembeleza kulipa kodi haifai,ukikiuka upigwe faini angalau Ulipaji ndio unaweza wekewa mda
 
Niko kampuni moja ya....Kuna ishu wanazifanya kwaujumla wake mm cfurahishwi na wanafofanya kwa kutuelekeza cc maafisa wake jinsi ya kukwepa Kodi. Iko siku niatawazinguaa wacha nikuzannye data za kutosha nitawapelekeaa tra niwatinye jinsi mizigo inatoka pale kinyemela Hadi kwamlaji bila kutolewaa risiti halali.
 
Watanzania muda mwingine ni kama hatujui tunataka nini, tukipelekwa huku tunalalama, tukipelekwa kule tunazingua, naunga mkono hoja kwamba pamoja na Mh. Rais kusema TRA wasitumie mabavu lakini waje na staili ya kuwabana wafanyabiashara kwenye suala la kodi, wawe serious, uzembe umezidi kwenye risiti, hata petrol Station ni kama tunarudi tulikotoka.
 
Niko kampuni moja ya....Kuna ishu wanazifanya kwaujumla wake mm cfurahishwi na wanafofanya kwa kutuelekeza cc maafisa wake jinsi ya kukwepa Kodi. Iko siku niatawazinguaa wacha nikuzannye data za kutosha nitawapelekeaa tra niwatinye jinsi mizigo inatoka pale kinyemela Hadi kwamlaji bila kutolewaa risiti halali.
Siku zote mfanyabiashara anaangalia faida tu. Ni bora kuwa na wafanyabiashara wachache waaminifu wanaolipa kodi kuliko kuwa na wafanyabiashara wengi wasiolipa Jodi.
 
Siku zote mfanyabiashara anaangalia faida tu. Ni bora kuwa na wafanyabiashara wachache waaminifu wanaolipa kodi kuliko kuwa na wafanyabiashara wengi wasiolipa Jodi.
Kk ndug biashara haitaji kuwa mwaminifu swal la uhaminifu Ni swal la mtu binafsi. Kodi kukwepa hakujaanza Leo ishu ni je ss watz na wafanyakaz wa hao wafanyabiaehara na wawekezaji je tunawajibika kutoa taarifa na kukemea Jambo lile Wachina wanachezeaa uchumi wetu sanaa.
 
Tatizo bei za bidhaa madukani ni shaghala baghala kila sehemu na bei yake ni vizuri ikajulikana bei ya pepsi Tanzania nzima ni bei gani, mfano tu sasa tokea kiwandani itajulikana bei ni kiasi gani.
 
Niko kampuni moja ya. Kuna ishu wanazifanya kwaujumla wake mm cfurahishwi na wanafofanya kwa kutuelekeza cc maafisa wake jinsi ya kukwepa Kodi ....iko siku niatawazinguaa wacha nikuzannye data za kutosha nitawapelekeaa tra niwatinye jinsi mizigo inatoka pale kinyemela Hadi kwamlaji bila kutolewaa risiti halali
Njoo chemba tuongee
 
Wakuu Kodi miyeyusho, 🏃 unatoa Kodi , wateja wenyewe wa kulenga na manati alaf watu wanatembelea ma V8 na kupeana zawadi za mabenzi na majumba ya kifahari alaf tunasema et tunataka tuendelee....Bora mwendazake yeye aliamua kutembea na mkono wa chuma to the last .....!!!
 
Yaan Kodi zilizopo kwa wafanyabiashara Bora hata msiseme. Nyie mnaangalia tu vat. Mbona hamzungumziii kupunguziwa Kodi corporate tax ambayo inasimama kwenye asilimia 30 ya faida yako.

Pili Kuna msururu wa wakubwa kuingiza mizigo na kuuza kwa Bei rahisi hata ulisema ushindane nao na ulipe Kodi utafunga kesho tu.
Kuna watu kiatu China kinauzwa 20000 akija bongo anauza 25000 Sasa kauze weye na ulipe kodi
 
Wafanyabuashara wote wanatoa risiti na kufuata utaratibu wa kodi. Ila wachuuzi ndo wa kaidi wa kutoa risiti. Na bahati mbaya TZ ina wachuuzi wengi kuliko wafanyabiashara. Hivyo ni vyema kutofautisha haya makundi mawili.

Hata hivyo ni lazima kujua kwamba si kila mauzo yanayofanywa na kutolewa risiti yanaongeza kodi. Kuna wakati mwingine ukitoa risiti unapunguza kodi kwa serikali maana serikali inabidi ikurudishie wewe fedha.

Kimsingi TZ iliachana na mfumo wa sales tax (kodi ya mauzo). Kodi hii ndo ilikuwa inatozwa kwa kila mauzo yanayofanywa. Nchi hii iliacha mtindo wa kutumia hii kodi kwa sababu ya ugumu wa kuikusanya. Huwezi kuhakiki kila mauzo kila sehemu ili kupata kodi.

Sasa hivi tunatumia mfumo wa VAT au kodi ya ongezeko la thamani. Ingawa bado watu wengi wanadhani VAT ni kama sales Tax hivyo usipotoa risiti au kudai risiti umepoteza kodi. Yes inawezekana umepoteza au hujapoteza.

Mfuno wa VAT hutoza kodi ya VAT kwa kila bidhaa inayotakiwa kutozwa katika mnyororo mzima wa bidhaa.

Kwa mfano kama bidhaa inazalishwa nchini VAT inatozwa kiwandani pale. Distributor anaponunua bidhaa kiwandani analipia VAT. Distributor akimuuzia muuzaji wa jumla naye anatoza VAT, hivyo hivyo hadi mlaji wa mwisho. Inaitwa kodi ya ongezeko la thamani kwa sababu katika kila hatua kodi inayotozwa ni ya kile kithamani kidogo kilicho ongezeka.

Kwa mfamo mimi nimenunua bidhaa kwa shs 100 na nikalipa 18% ya VAT hivyo nitalipa Tzs 118. Kwenye bidhaa hii naenda kuuza TZS 110 yaani naongeza shs 10. Katika 110 naongeza VAT 18% ambayo ni TZS 19.8 hivyo nitamuuzia mteja wangu bidhaa kwa TZS 129.8. Kumbuka wakati nanunua bidhaa nilitozwa VAT ya TZS 18.. Mimi nimeuza nimemtoza mteja wangu VAT ya TZS 19.8 kiasi cha kodi kilichoongezeka ni TZS 1.8. Hii shs 1.8 ndo natakiwa kuipeleka TRA.

Mfumo wa VAT una hamasisha wafanyabiashara watoe risiti, na wafanyabiashara wanatoa risiti.

Tatizo ni nini?
Kama tulivyo ona kwa kadri unavyo shuka chini kaongezeko ka thamani kanashuka. Tatizo kubwa ni kwa katika level ya chini huku wachuuzi wengi hawako formal. Yaani matumizi yao mengi hayana risiti za VAT. Kwa mfano wanalipa frame hawapati risiti za EFD, wanalipa huduma na matumizi mengine ya ofisi bila kupokea risiti. Hivyo anashindwa kujua analipa VAT kiasi gani katika biashara yake (VAT output ) na ana ana kusanya kiasi gani (input).

Tatizo la pili ni uwepo wachuuzi waliosajiliwa kwenye VAT na wasio sajiliwa kwenye VAT. Unakuta wachuuzi wote wako sehemu moja na wanauza bidhaa zinazofanana ila mwingine kasajiliwa na mwingine hajasajiliwa. Aliyesajiliwa atalazimika kuongeza VAT kwenye bidhaa zake hivyo kuwa ghali kuliko yule aliye sajiliwa.

Tatu na mbaya zaidi TRA wanatumia data za kwenye EFD kukadiria mapato. Yaani siyo tu kuangalia kodi aliyokusanya bali wanaangalia volume nzima ya sales ka kukadiria kodi. Sasa volume ya sales inaweza kuwa kubwa lakini faida ni kidogo sana. Hivyo mchuuzi anaogopa kupitisha sales kubwa kwenye mashine.

Kimsingi TRA wanatakiwa watoe elimu na wabadilike. Siyo kwamba watu hawaoendi kulipa kodi ila wanaogopa kubambikwa kodi kubwa
 
Niko kampuni moja ya....Kuna ishu wanazifanya kwaujumla wake mm cfurahishwi na wanafofanya kwa kutuelekeza cc maafisa wake jinsi ya kukwepa Kodi. Iko siku niatawazinguaa wacha nikuzannye data za kutosha nitawapelekeaa tra niwatinye jinsi mizigo inatoka pale kinyemela Hadi kwamlaji bila kutolewaa risiti halali.
Tuwe wazalendo mkuu tukiona ukwepaji kodi tutoe taarifa maana mwisho wa siku tunawanufaisha wachache hao matajiri afu sisi tutaumia zaidi kwenye huduma
 
Muarobaini ni kuwalazimisha wafanyabiashara wote kuweka bei wazi kwa kuweka lebo kama ilivyo super market na kuondoa kabisa suàla la majadiliano kwenye bei. Kisha ikitokea mtu akakàmatwa bila risiti hiyo bidhaa inataifishwa
 
Back
Top Bottom