Ombi langu kwa TRA (Mamlaka ya mapato Tanzania)

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Nianze kwa angalau kwa kupongeza juhudi zao wanazozifanya katika kukusanya kodi. Ni ukweli uliowazi kuwa wafanyabiashara wengi hawapendi kulipa kodi. Hii inachagizwa zaidi pale walipakodi wanapokuwa hawaoni faida anayoipata kwa kulipa kodi. Wanapolipa kodi wanategemea huduma kwao ziboreke, ikiwemo huduma za afya, maji, miundombinu ya barabara na kadhalika. Au wengine wanapenda kujinufaisha wao tu.

Nikija kwenye ombi langu, serikali kupitia kwa waziri wa fedha iliwataka wananchi na wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti kwa kila bidhaa wanayouza au kununua. Kutoa risiti kunaiwezesha serikali kukusanya kodi halali kwa bidhaa iliyouzwa/kununuliwa. Mnunuzi asipodai risiti au mfanyabiashara asipotoa risiti anaisababishia hasara serikali kwavile mfanyabiashara ataficha kile kiwango alichotakiwa kukiwasilisha TRA na kubaki nacho yeye na hivyo kujinufaisha yeye binafsi na kuwakosesha wengi huduma ambazo zingetolewa na serikali baada ya kukusanya kodi husika.

Katika pitapita zangu za kujilidhisha na jambo hili, nimegundua wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za EFD licha ya kuwa wanazo machine za EFD. Mnunuzi akiwasisitizia risiti basi wanakimbia kumwndikia risiti za kwenye vitabu na anaposisitiza risiti za EFD basi wanaanza kutoa visingizio kibao. Utasikia ooh hakuna umeme, au imeharibika au haifanyi kazi na TRA wamechukua muda kuirekebisha, mradi kumkatisha tamaa mteja kuendelea kudai risiti hiyo. Mteja anapokomaa na kuonesha kuidai basi watamwomba wampatie ila kwa kuandika kiasi pungufu ya kile alicholipia. Hii yote ni mbinu wanazotumia ili kukwepa kulipa kiasi stahiki kwa serikali. Kitendo hiki kwangu mimi hakina tofauti na kuhujumu uchumi.

Suluhisho, TRA kwa kushirikiana na polisi waunde kikosi kazi cha kuhakikisha wale wote wanaohusika na ukwepaji kodi kwa kutotoa risiti wanachukuliwa hatua stahiki. Katika hili napendekeza adhabu kali hata ikiwezekana kuwafungia biashara. Wengi watanishangaa kwanini tufunge biashara wakati angalau analipa kidogo. Jibu langu ni kuwa lazima serikali ioneshe kuwa ipo seriuos na mtu yeyote anayekwepa kulipa kodi stahiki. Tafuteni vijana wawekeni katika maeneo mbalimbali ili wawe wanavizia watu wanaonunua vitu kwenye maduka na kuwataka waoneshe risiti zao, na risiti zikaguliwe ili kuona kama bei za vitu walivyonunua vinaleta uhalisia. Kama hawana basi wawapeleke kwenye maduka walikonunua ili kuweza kuwakamata wafanyabiashara wasio waaminifu kwa hatua zingine za kukwepa kodi. Wategeesheeni pia vijana katika manunuzi ili kubaini watu wasiotaka kulipakodi. Tumieni mbinu mbalimbali ili kuhakikisha utamaduni wa kutoa risiti na kudai risiti unazoeleka. Nchi zingine risiti yako unapewa pamoja na bidhaa zako. Hawasubiri uwaulize au uwadai. Wanakupatia kama sehemu ya bidhaa zako. Lazima nasi tufike huko kama kweli tunataka kukusanya kodi kwa kiwango kikubwa na si kuwaachia wahuni wachache.

Napendekeza pia kuwe na adhabu kwa wanunuzi wasiopenda kudai risiti. Zoezi la kuelimisha watu ili kudai risiti limekuwa likotolewa,kuna uwezekano watu wengi hawaoni umuhimu wa wao kudai risiti licha ya kuelimishwa mara kwa mara. Pindi wakijua kuwa kuna adhabu itawapata pale watakapokutwa na bidhaa zisizokuwa risiti wakati zilitakiwa kuwa zimekatiwa risiti kwa malipo waliyofanya,nadhani sasa wengi wataamka na kudai risiti. Adhabu kali zaidi itolewe kwa mfanyabiashara asiyetoa risiti. Kama mtu hajachukua risiti yake, mfanyabiashara yeye aiotoe risiti azikusanye mahali, baada kufunga biashara zitachomwa moto baada yakazi ila incase akakamatwa mtu hana risiti basi adhabu yake ibaki kwake pale tu mfanyabiashara atakapoweza kuonesha risiti aliyoitoa ila mnunuzi hakuichukua.

Nayesema haya baada ya kuona bado mwamko wa watu kudai risiti ukiwa bado ni mdogo na hauonekani kukua. Lakini pia na wafanyabiashara wamekuwa na mbinu za kukatisha tamaa wale wanaodai risiti au kwa kuwadanganya wawape zile za kuandika kwa mkono au wawaandikie pungufu.

Muhimu, kuna haja ya kuangalia bidhaa za kumkamata nazo mtu. Sio mtu amenunua kipande cha sabuni ngengeni basi unamdai aoneshe risiti. Maduka yote yanayotakiwa kutumia EFD machine basi yatoe risiti za EFD na si vinginevyo.

TRA msisubiri rais awaambie kuunda task force ya kusambaa kila eneo kama usalama vile. Mkiamka usingizini mtasaidia kodi stahiki kufika inakotakiwa. Wananchi nasi tuanze kudai risiti. Wafanyabiashara tutoe risiti kama tunavyorudisha change bila kukumbushwa. Iwe sehenu ya huduma zetu.

TRA anaglieni uwezekano wa kutoa machine za EFD bure, kisha mfanyabiashara atakuwa analipia taratibu kila anapokuwa analipia kodi. Utaratibu wa sasa nao unawafanya wafanyabiashara wenye mtaji mdogo nao washindwekutumia machine hizi za EFD na hivyo kuwafanya wenye mtaji mdogo kuneemeka kwa kufanya punguzo kubwa maana hawalipi kodi huku wale wenye EFD wakijikuta wanapoteza wateja maana pengine wanaogopa kushuka zaidi ya wale wasiokuwa na EFD na hivyo kuweka ushindani usiokuwa sawa.

Sitegemei uzi huu kupendwa na wasiopenda kulipa kodi.
 
unayopendekeza mbona yako kwenye sheria ambayo haitekelezeki-
 
Back
Top Bottom