Uchaguzi 2020 Ukweli wenye ukali: Dkt. Magufuli lazima abadilike, runinga ya Watanzania aitazame na kuizingatia

Iwe ameshinda au ameshindwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. John P. Magufuli lazima abadilike. Lazima awe mpya. Hawezi tena na kamwe kubaki alivyo. Anapaswa kujirudi; kujitathmini; kujiangalia na kuwaangalia watanzania wake na kujiuliza bila kujiliza: nimekosea wapi na nijirekebisheje? Lazima abadilike. Lazima afanye mambo na aseme maneno kwa namna mpya.

Runinga ya Watanzania imewashwa wakati huu wa kampeni. Inaonesha mambo ya kuogofya: watu wameumizwa na kuguswa na maneno na matendo ya Dkt. Magufuli. Wamevunjiwa nyumba zao; wamedhulumiwa korosho zao; wamevurugiwa uchumi wao; wameporwa ardhi zao; wamevurugiwa mipango yao; wamesimamishiwa maendeleo yao; wameshindwa kutimiza mahitaji yao; wamedhalilishwa kwenye kazi zao; wamedhulumiwa mishahara na marupurupu yao na kadhalika.

Watanzania, kupitia runinga yao ya kwenye kampeni na kwa wingi wao, wameumia na hawatarajii wafanyiwe tena hivyo. Watanzania wanatarajia haki, wajibu na maendeleo kutamalaki kwenye awamu itakayoanza baada ya uchaguzi mkuu huu. Watanzania wanahitaji mabadiliko. Lazima, Dkt. Magufuli abadilike kuendana nao. Lazima utendaji uendane na kusababisha furaha badala ya hasira; utulivu badala ya maumivu; mendeleo badala ya upendeleo.

Watanzania wameshatuma ujumbe wao kwa Dkt. Magufuli. Umemfikia. Wanamsubiria Oktoba 28!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mbeya, Tanzania)
Mkuu tatizo lake kubwa ni kuwa, anaamini tu ktk kile ambacho anachokiona kupitia ktk lensi yake, yaani akili za kina Bashiru na Polepole.
tapatalk_1564750429057.jpg
 
Sio rahisi kubadilika. Hali inavo onekana tutarajie hali mbaya zaidi.
Wapinzani wataumizwa zaidi
Kwa visasi
Wafanya biashara watavutwa hela zaidi
Biashara zitadorora
Shughuli nyingi zitasimama kujaribu kuokoa miradi ya umeme na Sgr.
Trafic wata waana zaidi wenye magari.
Na tutatengwa zaidi na dunia
Uwezekano wa hili ni mkubwa sana.Cha msingi kila mtu atimize wajibu wa kupiga kura.Vote for change.
 
Kama Magufuli atang'ang'ania kuendelea kuwa Rais, miaka 5 inayofuata itakuwa ya majonzi na mateso makubwa kwa Watanzania:

1) Watu watalipishwa kodi hata wasizostahili. Uwe unatengeneza faida au hasara, lazima utalazimishwa kulipa kodi ili pesa ipatikane kwaajili ya miradi mikubwa iliyoanza ambayo haizalishi fedha. Kutokana na hilo, wengi wataendelea kufunga biashara zao na kufilisiwa kupitia TRA.

2) Wakati anaingia, bajeti yetu ilikuwa inachamgiwa na nchi wahisani. Kutokana na uongozi mbaya, wahisani wengi wamekata misaada. Safari hii, itakapodhihirika ameendelea kuchezea demokrasia, hata wale wachache waliokuwa wamebakia, nao watasimamisha. Kwa vile, naye hatapenda aabike ionekane miradi aliyoanza imeshindikana, pengo hilo litazibwa kwa kuwabambikia watu kodi zisizolipika, kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha matajiri ili waporwe fedha zao.

3) Harakati za wasiojulikana zitaongezeka maradufu. Kwa sababu kutakuwa na shida, manung'uniko yatakuwa mengi. Na yeye hatapenda yasikike. Hivyo kila mtu ambaye atasikika akinung'unika kwa uwazi au kwa kificho atakumbana na nguvu ya wasiojulikana. Kwa kuwa wanaolalamika hawataweza kupelekwa mahakamani, utaratibu wa kupotezwa utaimarika zaidi.

4) Uwekezaji utasinyaa sana. Kwa sababu ya mazingira ya hofu yanayojengwa na uonevu, watu wataogopa kuwekeza, hiyo ni kwa wawekezaji wa ndani na nje. Watanzania wenye mitaji mikubwa wataendelea kuwekeza nje ya Tanzania ili kujinusuru kufilisika. Jina la Tanzania litatajwa sana nje ya nchi kwa ubaya, na kusababishwa uwekezaji wa kutoka nje kukoma.

5) Kutokana na kusinyaa kwa uwekezaji, mzunguko wa fedha utakuwa mgumu sana, ukuaji wa ajira utazidi kuporomoka, vijana watazidi kupoteza matumaini kwa kukosa ajira

6) ili kupambana na wanaolalamika, sheria nyingi za kigandamizaji na kidikteta, zitatungwa ili kuzima sauti za wananchi.

7) Pamoja na kuwabambikia watu kodi zisizolipika, kuwatengenezea watu kesi za uhujumu uchumi, bado serikali haitakuwa na fedha za kukamilisha miradi iliyoanza. Hivyo serikali italazimika kuendelea kukopa mpaka kufikia uwigo wa mwisho wa kukopesheka. Hali hiyo, ikichangiwa na kupungua kwa mauzo ya nje, na kuendelea kuporomoka kwa ukuaji wa sekta ya utalii kutasababisha uhaba wa fedha ya kigeni na kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania. Serikali itadhibiti sana upatikanaji wa fedha za kigeni kwa watu binafsi.

8) Viongozi wa ngazi za juu kwenye serikali, NEC, vyombo vya ulinzi na usalama, msajili wa vyama, watawekewa vikwazo kimataifa. Hali hiyo itazidi kuharibu taswira ya nchi mbele ya mataifa na kuathiri sekta zote. Zimbabwe, kama nchi, haikuwekewa vikwazo. Vikwazo waliwekewa viongozi wa serikali, madhara yake kila mmoja anayajua.

Najua haiwezekani lakini Rais Magufuli kama anawahurumia Watanzania, alistahili kutogombea kipindi cha pili cha miaka 5. Amekwishajenga image mbaya kwa wengi. Hata akibadilika, haitakuwa rahisi kurudisha imani kwa wawekezaji wa ndani na nje. Ni rahisi kipngozi kuonesha ana mwelekeo tofauti na mtangulizi wake kuliko yule yule wa zamani kusema kuwa nimebadilika.

Wanasema ukitaka kupambana na nyoka, hasa nyoka jamii ya mamba, ukianzisha tu mapambano, ukamjeruhi, uhakikisha unamwua. Ikitokea amenusurika, kama ilikuwa ni eneo la shamba, hama kabisa, usionekane hapo shambani, maana mtaisha. Uchaguzi huu, mpaka hapa tulipo, umemjeruhi Rahisi mpendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah,wee jamaa umedadavua vizuri.Asubuhi ya leo nilikuwa nikijadiliana haya haya na mke wangu.Yaani kama una mpango wa kukopa kwa ajili ya biashara mwakani chukua tahadhari.Mauzo yataporomoka kuliko ilivyokuwa wakati corona imeshika kasi.Kila mtanzania apaswa kuchukua hatua kwa kutekeleza ile azima yetu:TUNA JAMBO LETU OCTOBA 28
 
Back
Top Bottom