Uchaguzi 2020 Ukweli wenye ukali: Dkt. Magufuli lazima abadilike, runinga ya Watanzania aitazame na kuizingatia

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Iwe ameshinda au ameshindwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. John P. Magufuli lazima abadilike. Lazima awe mpya. Hawezi tena na kamwe kubaki alivyo. Anapaswa kujirudi; kujitathmini; kujiangalia na kuwaangalia watanzania wake na kujiuliza bila kujiliza: nimekosea wapi na nijirekebisheje? Lazima abadilike. Lazima afanye mambo na aseme maneno kwa namna mpya.

Runinga ya Watanzania imewashwa wakati huu wa kampeni. Inaonesha mambo ya kuogofya: watu wameumizwa na kuguswa na maneno na matendo ya Dkt. Magufuli. Wamevunjiwa nyumba zao; wamedhulumiwa korosho zao; wamevurugiwa uchumi wao; wameporwa ardhi zao; wamevurugiwa mipango yao; wamesimamishiwa maendeleo yao; wameshindwa kutimiza mahitaji yao; wamedhalilishwa kwenye kazi zao; wamedhulumiwa mishahara na marupurupu yao na kadhalika.

Watanzania, kupitia runinga yao ya kwenye kampeni na kwa wingi wao, wameumia na hawatarajii wafanyiwe tena hivyo. Watanzania wanatarajia haki, wajibu na maendeleo kutamalaki kwenye awamu itakayoanza baada ya uchaguzi mkuu huu. Watanzania wanahitaji mabadiliko. Lazima, Dkt. Magufuli abadilike kuendana nao. Lazima utendaji uendane na kusababisha furaha badala ya hasira; utulivu badala ya maumivu; mendeleo badala ya upendeleo.

Watanzania wameshatuma ujumbe wao kwa Dkt. Magufuli. Umemfikia. Wanamsubiria Oktoba 28!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mbeya, Tanzania)
 
Ameshakosa kibali cha watz imebaki kazi ya tume kutulazimishia tusilolitala
Screenshot_20200820_103832_com.android.chrome.jpg
 
ni dhahiri jamaa lazima atabadilika whether ashinde au asishinde...ndani ya nafsi atakuwa anajiuliza iweje kaupiga pini upinzani kwa miaka mi5 plus kuwaletea watz "maendereo" lakini leo watz hao hao wanampinga kwa maelfu?!.

hata sasa kaweka figisu kwenye media mikutano/habari za TL zipotezewe lakini wapi watu bado wapo naye tu...haya ni maajabu lazima kibinadam atashangaa tu hakuna namna!.
 
Alikuwa akijiita Rais wa wanyonge kwa kuwaumiza wale waliokuwa matajiri, akidhani kwa kufanya hivyo ndio maskini wangetajirika, mpaka leo hajapandisha mishahara, hajawapandisha watu madaraja kazini, wastaafu hawapati pesa zao kwa wakati.

Matokeo yake maskini wameendelea kutopea kwenye lindi la umaskini na hata wale waliokuwa na uchumi wa kati nao wamegeuka maskini, hakika anatakiwa ajitathmini, kuongoza nchi inahitajika busara na hekima, sio ubabe usiokuwa na maana, kwa kifupi utawala wake umekuja kuwageuza raia wa nchi hii kuwa maskini zaidi.
 
Huyu hawezi kubadirika!! Ni mtu mwenye kiburi, roho mbaya, chuki na ukatili wa hali ya juu kuzidi kawaida.

Na ikitokea akawa tena raisi ndo tutashuhudia vifo vya vigogo wa Ccm aliotofautiana nao na watu kupewa makesi makubwa kupindukia.

Dawa ya huyu mtu ni vyovyote vile asirudi ikulu mwaka huu!! Bora wazee wakubali tu Lissu achukue aweke mfumo imara na ku punguza madaraka ya Raisi ili tusije tena kupata raisi ambaye hatuwezi mfanya lolote hata akosee namna gani!!

Asipotoka sasaivi tujiandae kuwa na Iddi Amini hapa Tanzania 2020-2025
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom