Ukweli Viongozi ni zao la wananchi maana wanatoka kwenye jamii , tatizo linaanzia kwenye jamii, mpe KIJANA wetu million 10 uone vipaumbele vyake!!

Ukweli Viongozi ni zao la wananchi maana wanatoka kwenye jamii , tatizo linaanzia kwenye jamii, mpe KIJANA wetu million 10 uone vipaumbele vyake!!

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
3,772
Reaction score
4,913
Huo ndo ukweli mchungu ,
Viongozi ndo picha ya halisi ya JAMII husika
Akili kubwa haiwezi kukubali kuongozwa na akili NDOGO

Vipaumbele vya viongozi ni vipaumbele vya jamii husika

Tunalaumu viongozi wanunua magari ya mabilioni kwenda kuzindua miradi ya mamilion au kutembelea wananchi wasio na uhakika wa Milo mitatu.
Kisha wanakopa hela za kujengea majengo

Wape vijana million 10 wa kitanzania uone asilimia kubwa watavyozitumia Kwa vipaumbele vyao.
Nakuhakishia asilimia kubwa watanunulia magari ya kwenda kula bata au club na kuchukulia wadada
Au kwenda nalo kwenye kazi ambayo haizidi km 5

Viongozi imara wanatoka kwenye jamii iliyoandaliwa vizuri.

Vile vile viongozi Bora wanatoka kwenye jamii Bora.

Taifa imara na lenye nguvu linatoka kwenye jamii imara

Watanzania wengi sio wote Wana tabia zinazofanana na viongozi wao.

Utapingaje ufisadi wa viongozi huku ukimwibia boss wako au Rasilimali za serikali
Unapinga.

Unatakaje wataalamu na viongozi wazuri huku ukilipia fedha watoto wako waonyeshwe mitihani au Unataka kufaulu kwa possible za practical,
Ndo possible Hadi kwenye maghorofa na kwa wagonjwa.

Hili Taifa lazima lianze kujengwa kuanzia chini kabisa.
 
Ni safari ndefu lakini hakuna namna ,
Ubabaishaji unaanzia huku chini kabisa
 
Back
Top Bottom