GE2025 Ukweli usioufahamu kuhusu wanaosema wataandamana

GE2025 Ukweli usioufahamu kuhusu wanaosema wataandamana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wengi wenu mnajitahidi kuamini kuwa tarehe 29 watz wataandamana, ila kiuhalisia haiwezekani kwasababu zifuatazo.

1- Idadi ya wageni waliopo Tz ni kubwa mno, yaani wakongo, warundi, wamalawi, wahindi n.k. Hili kundi haliwezi kuandamana maana wapo nchini kwa hisani ya CCM. Kweli mhindi akaandamane akitaka haki?

2- Bado asilimia kubwa ya watz wapo vijijini hivyo hawajui yanayoendelea na asilimia chache iliopo mjini ndio wanajua.

3- Wengi bado wanaamini siasa sio vitu vyao, hata hafa JF tunaona mada zenye michango mingi huwa ni zipi.

4- Kuskiliziana, yaani kila mmoja anamsikilizia mwenzake aone kama ataandamana. Yaani nani alianzishe kutokana na woga.

5- Hofu ya kubambikwa kodi au makesi na kufilisiwa au hata kufukuzwa kazi.

6- Wengi wanaamini wakiandamana watauwawa au kuumizwa hivyo kuziathiri familia zao, umaskini utawafuata.

Kiuhalisia hakuna wakuandamana hiyo tarehe 29, kama tu mashabiki wa mpira walishindwa kuzomea wanasiasa siku ya matamasha ndio ije kuwa kutoka front.

Sina lengo lakuwakatisha tamaa, ila hata jana mahakamani wananchi walishindwa kuwa na umoja.
#TIMEWILLTELL

waambie watu wadownload TOR browser inakuruhusu kuaccess jamii forum bila shida wowote. hamna haja ya VPN, ni free kabisa, sitawafundisha kila kitu.
😀😀😀
 
Sio kuwa watu wote wanaweza kuandamana.

Wakitoka watu laki 2 tu, wakaandaman hata wiki tu, kwisha.

Serikali ya kijuha ambayo mpaka inamuogopa Sativa au Chaula mchoraji unadhani ina uwezo wa kushindana na watu elfu 50???
Sio watu laki mbili Mkuu watz tunajuana porojo mitandaoni nyingi vitendo tunatia uvivu inakera sana.
Mi nna uhakika watu wa kuandamana hata elfu Moja hawatafika hakika nakuambia hii nchi sijui ikoje aisee.
Au kweli ule Mwenge umewaroga watz
 
Huku Familia za wahamasishaji zikiwa US na Canada salama salimini. Siku ya maandamano wanajituliza kwenye masofa simu zikiwa na bundles huku pembeni popcorn kama za 230,000/= zikiwasindikiza kutazama nyumbu zinavyoshughulikiwa. Kimsingi wahamasishaji wamekosa kabisa uhalali wa kusema watu waandamane.
Tena Lema tarehe ya maandamano ikikaribia anaenda zake Canada
 
Kuna namna kadhaa uchaguzi utakuwa wa fujo
Fujo hazitakuwepo ila ninachojua INEC watapika takwimu kwa sababu wote wenye kujitambua hawatapoteza muda wao kushiriki hii najisi sasa ili kuficha aibu yao watasema waliopiga kura ni m39
 
Sio watu laki mbili Mkuu watz tunajuana porojo mitandaoni nyingi vitendo tunatia uvivu inakera sana.
Mi nna uhakika watu wa kuandamana hata elfu Moja hawatafika hakika nakuambia hii nchi sijui ikoje aisee.
Au kweli ule Mwenge umewaroga watz
Hata maandamnao yasipofanikiwa, hao wapuuzi muhimu wasilalale.

Na utayaona na magari meeengi yanapiga doria.

Mtu muovu hajawahi kuwa na amani.
 
Hapo kwenye "Watoto tu wabaki ndani", kwa hiyo maandamani ni amri sio uzalendo ?
Watu kama Lucas ni "watoto" tu, ni Bora wabaki nyumbani waangalie tv na katuni huku wakiimba mapambio.
 
Ww kama huyawez Baki nyumbani ukijichubua sio Kila mtu lazima ashiriki katika mageuzi,
 
Makanisa ya Ngwaji yalifungiwa, kiko wapi? Lisu yuko ndani kwa makosa ya kubumba, kila mtu yupo busy na mambo yake. Mdude yuko wapi? Ikifika siku wewe MTz ukawa tayari kutenda haki bila kuombwa na mtu basi jua mabadiliko yako mbioni.
Kuna Mods wakiona unapigapiga kelele hivi kukunyamazisha wanaziunganisha I'd zako zote pamoja
 
4- Kuskiliziana, yaani kila mmoja anamsikilizia mwenzake aone kama ataandamana. Yaani nani alianzishe kutokana na woga.
Kwenye yale maandamano yalioitishwa na Mbowe hata akina Erythrocyte walikacha, mbowe akaishia kuandamana na binti yake tu. Makamanda kwa kuchicken hawajambo. Wanataka sisi makapuku ndiyo tuingie kwa road wakati wao wanakula viyoyozi home na kutucheki tunavyopokea kichapo kwenye runinga tu. Nani wa hivyo?
 
Nina ID moja tu, hivo acha niendelee kuichangamsha JF yetu.
Unazo nyingi zitaunganishwa kisha wanakufungia usiweze hata ku-edit profile hata kuifuta akaunti yako usiweze
 
Kwa taarifa tu wamesoma akili za watz na kuwagundua walivyo hakuna wa kuandama ila note my maneno

Maandamano yatakuja kuanza kama utani utani pasipo mipango ghafla tu kwa kisa ambacho hakitategemewa na utatokea ukatili wa kutisha.
Mtu alikua anachezea virungu mbele ya camera; pale pale ndio ilibidi kinuke.

For sure; bongo kuandamana Bado sana Gen z wako bize kutafuta connection za kina gigy money
 
watanzania wamezizoea siasa kama mwanamke mwenye mume mwenye maumbile makubwa alivyomzoea mumewe!
Toka enzi za baba wa taifa, watanzania wamekuwa wakiuziwa mbuzi kwenye gunia na wanasiasa kiasi sasa wanaita siasa 'SI-HASA'!
WANAOHAMASISHA FUJO ZA KISIASA WANA KIBARUA BONGO!
... CHONDECHONDE, MSISEME WATU HATUJITAMBUI AU TUNAHITAJI ELIMU YA URAIA MAANA TUNAYO SANA NA IMEPITILIZA!
 
Back
Top Bottom