Bandiko lako linatia uchungu na linakatisha tamaa japo limebeba uhalisia kwa 90%.
Mbali na uwoga wa wabongo ambao ndio sababu kuu ya watawala wa ccm kuendelea kutuburuza wanavyotaka... lakin pia ccm hususani hii ccm ya samia wametumia divide and rule strategy hili kufanya serikali iendelee kuwa na nguvu zaidi kuliko wanainchi.
Tukiachana na makada wa ccm, wengi wa wanainchi wasiokuwa na vyama ambao wanamsapoti Samia na kumtaka aendelee ni watumishi wa serikali.
Watumishi wa serikali karibu wote wanamsapoti samia sababu kajua kuishi nao jinsi wanavyotaka wao, Samia amewapa uhuru watumishi wa serikali yake wa kufanya kazi wajiskiavyo bila kuwafuatilia wala kuwawajibisha pale wanapofanya uzembe na zaidi amewapa mpaka uhuru wa kufanya ubadhirifu wa pesa uma, na ndio maana kila mtumishi unayekutana naye anakwambia "mitano tena kwa samia".
Sasa hii pekee tu inafanya zoezi kuwa gumu maana wakati sisi tunapanga kumtoa Samia madarakani kuna watu miongoni mwetu ambao wananufaika na serikali yake mbovu wanataka aendelee kuwepo na hivyo ni lazima watamlinda hata kwa kushirikiana na mapolisi.
Tatizo la mtanzania akishakuwa na uhakika wa kula,kunya,kunywa bia na huku nje ya nyumba yake amepaki IST basi anaridhika, yaan hapo hata akiskia viongozi wa serikali wameiba mabilioni ya kodi zake yeye hashtuki wala haumii... anahisi kama vile hamuathiri chochote.
Siku watanzania tukiacha ubinafsi wa kujiangalia maisha binafsi, itakuwa ni hatua nzuri sana kuelekea kwenye ukombozi.
Sasa hivi kwa vile hatuna solidarity yoyote ile, acha tu serikali ya ccm iendelee kutudharau na kufanya vyovyote wanavyotaka huku watoto wao wakituonesha dole la kati.
Siku wabongo wakiona haya maisha yaliyojaa manyanyaso kutoka kwa watawala hayana maana na wakiwa tayari kufa, basi ukombozi utapatikana mapema mno.
Tanzania hii hakuna ambaye yuko na wanainchi vyombo vyetu vyote vya ulinzi vimeungana na ccm kutukandamiza na kutufanya tuishi maisha ya mateso.