Ukweli usiosemwa: Siri kuu ya mafanikio ni ushirikiano (Tumikisha watu wengi ufaidike au kusanyeni wengi mbebane)

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,617
34,062
Utatafuta kila namna ila huu utabaki kuwa uhalisia.

Wengi wanajua stori za mnara wa babeli. Ni mnara unaodhihirisha nguvu ya ushirikiano. Mungu aliona kutokana na ushirikiano uliokuwepo wale watu walikuwa wanaenda kufanikiwa akaamua kuwavuruga lugha.

Ushirikiano ndio mafanikio ndio maana ni Jambo gumu mno kufanyika.

Hakuna penye ushirikiano pakakoswa mafanikio hata siku moja.

Sasa hapa kuna namna mbili.

1. Either uuze kitu/vitu au huduma kwa watu wengi (yaani uwafanye watu wengi wakupe pesa zao)

2. Mkae pamoja kama kundi, then mpeane kampani.

Kila mbinu ya mafanikio iko hapo.
 
Mkuu mnara wa babeli na space station, rocket,space ship kipi hatari? Mbona mungu hajazihujumu hizi teknolojia kufika huko juu.
 
Wale wababiloni walikuwa na lengo la kuboresha maisha yao ambayo Mungu hakuwaboreshea.
Sasa hapo kulikuwa na kosa gani?
Ubora wa maisha sometimes ni relative term tu.

Sidhani kama walikuwa na maisha magumu, sema tu binadamu amejaa curiosity.
 
Ok sahihi kabisa mkuu. Bahati mbaya wabantu hili halituingii akilini. Ingependeza kungeandikwa vitabu vingi kuhus namna ya kushirikiana kwenye shughuli za uchumi na motivational spika badala ya kuhubiri vitu siyo practical wahubiri ushirikiano.
 
Mkuu mnara wa babeli na space station, rocket,space ship kipi hatari? Mbona mungu hajazihujumu hizi teknolojia kufika huko juu.
Mnara wa Babeli ni takataka tu, kifusi cha mchanga cha kipuuzi kilichojazwa na Primitive Society.

Na haijawai kuwa tishio kwa Mungu bali Mungu anafanya mambo yake kwa utaratibu na atakavyo na kufanya funzo kwa wajao.
 
Ok sahihi kabisa mkuu. Bahati mbaya wabantu hili halituingii akilini. Ingependeza kungeandikwa vitabu vingi kuhus namna ya kushirikiana kwenye shughuli za uchumi na motivational spika badala ya kuhubiri vitu siyo practical wahubiri ushirikiano.
Watu wengi inaonesha hamujui hata motivation speaking au motivation ni nini lilibuka wimbi la ushamba wa kudhihaki Motivation, kimsingi hicho ulichokiona cha maana kaindika mtoa mada ni motivation pia na hizo unazosema wanahubiri sio practical ukoenda Zisikiliza ni motivation zinazo make sense.

Bado tujajua ni motivation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…