Ukweli usiosemwa: Siri kuu ya mafanikio ni ushirikiano (Tumikisha watu wengi ufaidike au kusanyeni wengi mbebane)

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,620
34,053
Utatafuta kila namna ila huu utabaki kuwa uhalisia.

Wengi wanajua stori za mnara wa babeli. Ni mnara unaodhihirisha nguvu ya ushirikiano. Mungu aliona kutokana na ushirikiano uliokuwepo wale watu walikuwa wanaenda kufanikiwa akaamua kuwavuruga lugha.

Ushirikiano ndio mafanikio ndio maana ni Jambo gumu mno kufanyika.

Hakuna penye ushirikiano pakakoswa mafanikio hata siku moja.

Sasa hapa kuna namna mbili.

1. Either uuze kitu/vitu au huduma kwa watu wengi (yaani uwafanye watu wengi wakupe pesa zao)

2. Mkae pamoja kama kundi, then mpeane kampani.

Kila mbinu ya mafanikio iko hapo.
 
Mkuu mnara wa babeli na space station, rocket,space ship kipi hatari? Mbona mungu hajazihujumu hizi teknolojia kufika huko juu.
 
Ok sahihi kabisa mkuu. Bahati mbaya wabantu hili halituingii akilini. Ingependeza kungeandikwa vitabu vingi kuhus namna ya kushirikiana kwenye shughuli za uchumi na motivational spika badala ya kuhubiri vitu siyo practical wahubiri ushirikiano.
 
Mkuu mnara wa babeli na space station, rocket,space ship kipi hatari? Mbona mungu hajazihujumu hizi teknolojia kufika huko juu.
Mnara wa Babeli ni takataka tu, kifusi cha mchanga cha kipuuzi kilichojazwa na Primitive Society.

Na haijawai kuwa tishio kwa Mungu bali Mungu anafanya mambo yake kwa utaratibu na atakavyo na kufanya funzo kwa wajao.
 
Ok sahihi kabisa mkuu. Bahati mbaya wabantu hili halituingii akilini. Ingependeza kungeandikwa vitabu vingi kuhus namna ya kushirikiana kwenye shughuli za uchumi na motivational spika badala ya kuhubiri vitu siyo practical wahubiri ushirikiano.
Watu wengi inaonesha hamujui hata motivation speaking au motivation ni nini lilibuka wimbi la ushamba wa kudhihaki Motivation, kimsingi hicho ulichokiona cha maana kaindika mtoa mada ni motivation pia na hizo unazosema wanahubiri sio practical ukoenda Zisikiliza ni motivation zinazo make sense.

Bado tujajua ni motivation
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom