Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,507
113,629
Wanabodi.

Naanza na kanuni ya haki duniani inayoitwa "the presumption of innocence until proven guilty" Yaani mtuhumiwa yoyote anahesabiwa kuwa hana hatia hadi atakapotiwa hatiani, na mahakama yenye mamlaka sahihi, hivyo Paul Christian Makonda anaendelea kuwa ni Paul Christian Makonda na Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka hapo itakapo thibitishwa vinginevyo, tena without any reasonable doubt kuwa Paul Christian Makonda ni mtu mwingine, na Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli na kupata sifuri, akaiba jina na vyeti vya Paul Christian na kuvitumia kujiendeleza as if yeye ni Paul Christian hivyo ni kweli huyu Paul Christian Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam ni kiongozi fake, anayetumia majina fake, vyeti fake na mtu halisi ni Daudi Albert Bashite aliyefeli darasa la Saba na kupata division 0 kidato cha nne!.

Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye hii fani hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, IJ, ila nimeamua kujikita katika kuandika habari za kimaendeleo tuu, "developmental news" ambazo ni habari zenye maslahi na impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ya udaku ambayo haina maslahi chanya kwa taifa, lakini kwa vile wabongo wengi wanapenda sana udaku hivyo hapa nitatoa maelekezo namna ya kupata uthibitisho wa uzushi na uongo huu unaoenezwa kumhusu Makonda kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite, na kuwa ameiba jina baada ya kufeli shule, na ame foji vyeti na kujiendeleza.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ukisemwa sana, bila kukanushwa mwishowe kugeuka kuwa ni ukweli.
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Sasa nimebadili msimamo baada ya kugundua kuwa, uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo tuu hata ukisemwa vipi au mara ngapi, hauwezi hata siku moja kugeuka ni ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli tuu hata usiposemwa. Ukituhumiwa kwa tuhuma zozote za uongo au kuzushiwa jambo baya lolote, as long as unajua ni uongo, huna haja ya kukanusha, wewe jinyamazie tuu kimya, ule msemo wa "tell the truth and the truth will set you free" ni msemo wa uongo, kanuni yangu ni "just keep silent about the truth, and the truth will remain the truth".

Mhe. Makonda, kwa vile ukweli ni wewe unayeujua na wengine wote ni waongo, licha ya kuujua ukweli huo bado umeamua kujimazia na kuuacha uongo utamalaki, endelea hivyo hivyo kunyamaza kimya wala usijitokeze tena kukanusha lolote, kwa sababu ni ukweli ndio utakaobaki hadi mwisho.

Hata Yesu alisingiziwa uongo, alipofikishwa kwa pilato alikaa kimya na akasulubiwa ila kwa kupigwa kwake sisi tuliponywa.
Nawe fanya vivo hivyo kaa kimya usijibu kitu, utateswa na kusulubiwa huku mtaani, lakini kwa kuteswa kwako, wote wenye majina ya bandia na vyeti vya kufoji wataponywa.

Sasa Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizi za Makonda kughushi vyeti na kutumia majina bandia, nimekuja kugundua kuwa kumbe tuhuma hizi na shutuma zote ni za uongo mtupu, ni za uzushi tuu kutaka kumfanyia fitna kwa kumpiga majungu, zinazazushwa na watu wenye wivu na kumuonea kijicho dhidi ya mafanikio yake kimaisha kutokana na kufanya kazi kwa kujituma kwa bidii, ukapata maendeleo ya haraka haraka hadi kufanya ziara ya ulaya na Amerika, huku kuna watu, ulaya wanaitamani na kuishia kuisikia tuu, wataacha kukuonea wivu?. Tule tujumba twa ghorofa tuliochipukia kama uyoga, kujenga Msikiti wa Bakwata kabla ya kupaka tuu angalau rangi ile shule yako ya Kolomije, vyote hivi vinasababisha wenye wivu kukuonea donge, roho zinawauma sana hivyo wanakuzushia. Umewamaliza kabisa jinsi alivyoshinda vita hii ya madawa ya kulevya kwa muda mfupi ajabu vita imekwisha madawa yamekwisha na wazungu wa unga na mateja wamekoma.

Wito wangu kwa Makonda mwenyewe ni kuendelea kunyamaza kimya na kutulia tulia hivyo hivyo kama ulivyo nyamaza, usijali chochote, usijibu chochote, hawakulishi, hawakuvishi, just ignore them, and keep calm, endelea kuchapa kazi kwa sababu hawa watu watakusema mchana na usiku watalala, kesho yake wateandelea kusema, watasema wee, watasema wee mwisho watachoka na wataalamu. Huu ni upepo tuu na utapita.

Kanuni ya tuhuma zozote kwa kawaida ni "he who alleges must prove" hivyo without any proof, allegations zinabaki ni allegetions tuu, na mtuhumiwa anahesabika innocent until proven guilt, hivyo waache waseme tuu na waendelee kujifurahisha kwa kujaza severs za JF, lakini mwisho watachoka na watalala.

Yote yanayosemwa kuhusu Makonda Kumbe hueanda yakawa ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Tuwapuuze mpaka tutakapo pata proof.

Na huu ni wito wangu kwa wazushi hawa, msiendelee kutujazia severs zetu. Kama tuhuma zenu zinaukweli wowote, kwanini mpaka leo mmeshindwa kuzithibitisha?!. We need solid proof na sio maneno maneno! .

Ningeamua kufanya investigative piece ya hii story lakini...
1. Hakuna hata mtu mmoja aliyekwenda kijiji cha Kolomije kuuliza majina ya wazazi wa Paul Cristian Makonda kama hayo yao na kuuliza jina la mtoto wao wa pekee kama kweli ni Paul Christian Makonda?. Pia watawauliza wazazi wake, Paul alizaliwa lini na wapi na alipewa majina gani, alikulia wapi, alibatizwa wapi, kwa majina gani, aliandikishwa darasa la kwanza lini, shule gani kwa majina gani, katika simulizi hiyo ya wazazi wake, kusipoibuka majina ya Daudi Albert Bashite, wanaweza kuwauliza wazazi wake kama wanajua lolote kuhusiana na majina ya Daudi Albert Bashite.

Baada ya kupata taarifa hizo, hizo zinakuwa ni primary sources, ukitoka hapo unazitafutia collaborative sources za majirani hapo kijijini ku verfy taarifa za wazazi wake.

2. Hatua ya pili ni kuripoti shule ya Msingi Kolomije si bado ipo, wameshindwa nini kwenda kuwauliza jina la huyo mwanafunzi Paul Chirtian Makonda waliotajiwa na wazazi wake kisha wamuulizie na Daudi Albert Bashite aliandikishwa lini alimaliza lini na kwa majina gani na kama alifaulu au alifeli.

3. Baada ya hapo ni kwenda Shule ya Sekondari ya Pamba na kuulizia mwafunzi aliyefeli shule ya msingi, amewezaje kuingia Sekondari ya serekali. Kisha waulizie kuhusu mwafunzi Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite walijiunga lini kwa majina yapi, wakamaliza lini na matokeo yao ni yapi.

4. Unakwenda chuo cha uvuvi Nyegezi unapata details na documentary evidence ya jina la Paul Christian Makonda alilojisajili na vyeti alivyo wasilisha wakati alijiunga na vyeti alivyo hitimu. Hapo Nyegezi ukikuta majina tofauti ya shule na vyeti, unafanya back to back ya shule ulizokuta na kuzipitia ku verfy Paul Christian Makonda alisoma hapo.
5. Unaripoti Mbegani unapata details za Paul Christian Makonda na documentary evidence ya majina aliyotumia kujiunga na vyeti aliyotumia na vyeti vya kuhitimu.

6. Unaripoti chuo cha Ushirika you do the same.
Mkumbuke hizo info zote ni public info ambazo ziko freely accessible. Kama Kuna any discrepancies zozote za majina kwenye hivyo vyeti kati ya Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite then una launch secondary investigation kwa kuandika barua kutumia kipengele cha sheria ya "the right to information act ku access protected info kutaka

7.Vizazi na vifo alipozaliwa aliandikishwaje? .

8. Idara ya Uhamiaji ina file la DN Number alipoomba passport aliwasilisha nyaraka gani za wazazi wake zikiwemo affidavits zao zina majina gani.

9. Unakwenda mamlaka yake ya ajira kuangalia aliwasilisha vyeti gani vyenye majina gani.

10. Unamkabili Paul Makonda mwenyewe na vielelezo vyote kuthibitisha yeye ni Daudi Albert Bashite bila kusema kuwa ni mwizi wa jina wala amefanya forgery or fraud. Unamtupia mezani kwake na kumpa kamba ama ajinyonge yeye mwenyewe ama ajinasue.

Hata Makonda akigoma kutoa ushirikiano, you have facts to go on with the story with or without Makonda's imput. Kazi ya mwandishi ni kuwalisha facts only hivyo unaibuka na big headline "Uthibitisho Paul Chritian Makonda ndiye Daudi Albert Bashite " huku umetutundikia hizo evidence.

Kinyume cha hapo sisi akina Tomaso wote ambao we belive in solid truth za allegetions without proof ni uzushi tuu, tunaendelea kuamini kuwa kumbe tuhuma zote hizi dhidi ya Makonda huenda ni za Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!.
Uthibitisho kuwa tuhuma hizi ni uzushi, ni huu ukweli bayana uliopo mbele yetu hadi sasa kuwa Mhe. Paul Christian Makondo ni mteule wa rais wa JMT aliyefanyiwa vetting na vyombo husika na kuthibitisha pasipo shaka wasifu wake hivyo akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa hapa tunavyozungunza, Paul Christian Makonda, ndiye Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, na huu ndio ukweli bayana na ukweli halisi uliopo, mkubali, mkatae, ukweli unabaki kuwa ukweli, mengine yote ni uzushi tuu!.

Jee wewe Mtanzania mwenzangu, kati ya wazushi hawa wanaomzushia Makonda kuwa ana jina la bandia na vyeti vya kughushi, na rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyemwamini Makonda hadi kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kuendelea kumwani mpaka hii leo, licha ya kuibuka kwa tuhuma hii, unamwamini nani kati ya wazushi na rais wako?.

Kwa maoni yangu Mkweli ni Rais wa JMT, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, kwa sababu tangu kuibuka kwa tuhuma hii, serikali kupitia vyombo vyake, ingeishafanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Anne Kilango alipodangwanywa tuu, alitumbuliwa pale pale!. Kitwaga alipopata kidogo tuu pale Bungeni, alitumbuliwa pale pale lakini kitendo cha Paul Makonda, hadi dakika hii, bado ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwangu ni uthibitisho tosha kuwa tuhuma hizi ni za uongo, ni za uzushi, ni za kutunga na za kubuni, haiwezekani kabisa mteule wa rais Paul Christian Makonda akaiba jina, akafoji cheti!. Huu ni uzushi wa kupuuzwa kabisa na ndio maana hata Makonda mwenyewe amezipuuza, na Rais hajachukua hatua yoyote, na wala hata chukua hatua yoyote kwa sababu soon wengi mnaojua Kuwait Paul Makonda ndiye yule ambages... "Huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu, ninaye pendezwa naye", hata akifanya nini, mtapiga tuu kelele za kujisumbua bure!, ndio maana mpaka sasa watu wametulia tuu na kuzipuuzia hizi kelele zote za kizushi huku wazushi wakiendelea kupiga kelele.

Wengi mliujua uwezo wa Makonda, alipoanza vita na wauza unga, sisi wengine, tuliujua uwezo wa Makonda toka akiwa DC na tulitoa ushauri ufuatao kwa Magufuli
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Tena tumependekeza
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana ...

Watanzania tupunguze kushadadia uzushi, tujiunge na rais wetu kumtia moyo Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda endelea kuchapa kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa wasiolitakia mema taifa letu.

Nawatakia Jumatano Njema ya Majivu, leo ni siku ya kufunga kwa sisi Wakristo Wakatoliki, tunaanza mfungo wa siku 40 za Kwaresma.
Kwaresma Njema
Paskali
Update.
17264702_718775568304844_5261692279740083297_n.jpg
17190714_1392690060794972_5029664959228244805_n.jpg

17203022_1392690067461638_1167658439358951614_n.jpg
huu pia ni uthibitisho wa jinsi watu walivyo waongo na wazushi kumhusu mtu huyu. Mkuu wetu wa Mkoa jina lake halisi na la ukweli ni Mhe. Paul Christian Makonda. Vyeti vyake viko kwenye mamlaka yake ya ajira ambayo sio hapa jf. Zile habari za Daudi Albert Bashite ni uongo wa mchana kweupe wala hakuna mtu kama huyo duniani, wala hakuna yoyote mwenye vyeti vya Bashite ulikuwa ni uongo tuu.

Mkuu wetu wa mkoa anaendelea kuchapa kazi za ujenzi wa taifa as if nothing has happened. Kelele za mlango hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

Paskali.
 
Wewe ni mwandishi wa habari sawa lakini wa level ya chini sana,kama Tanzania inategemea waandishi kama wewe basi tumekwisha
Habari unazohangaika nazo kila kukicha zinasaidia nini nchi yetu kama sio kukuonyesha udhaifu wako wa umbeya,achana na hizo habari hazitusaidii tena
 
Wanabodi.
Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye newsroom hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, ila kwa vile najitegemea nimeamua kujikita katika habari za kimaendeleo, developmental news zenye impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ambayo haina maslahi chanya kwa taifa.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ulisemwa sana, bila kukanushwa haweza kugeuka ni ukweli.

Kiukweli uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo hata ukisemwa vipi hauwezi kugeuka ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli hata ulisemwa.

Sasa Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizi za Makonda kughushi vyeti na kutumia majina bandia, nimekuja kugundua kuwa kumbe tuhuma hizi na shutuma zote ni uongo mtupu, ni za uzushi tuu kutaka kumfanyia fitna kwa kumpiga majungu, zinazazushwa na watu wenye wivu na kumuonea kijicho dhidi ya mafanikio yake lima Isha na jinsi alivyoshinda vita hii ya madawa ya kulevya kwa muda mfupi.

Wito wangu kwa Makonda ni kuendelea kutulia hivyo hivyo, kwa kunyamaza, usijibu kitu, just keep calm, endelea kuchapa kazi kwa sababu hawa watu watakusema mchana na usiku watalala, kesho yake wateandelea kusema, watasema wee, watasema wee mwisho watachoka.

Kanuni ya tuhuma zozote kwa kawaida ni "he who alleges must prove" waache waendelee kujifurahisha kwa kujaza severs za JF.

Yote yanayosemwa kuhusu Makonda Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Tuwapuuze! .

Na huu ni wito wangu kwa wazushi hawa, msiendelee kutujazia severs zetu. Kama tuhuma zenu zinaukweli wowote, kwanini mpaka leo mmeshindwa kuzithibitisha?!.

Ningeamua kufanya investigative piece ya hii story lakini...
1. Hakuna hata mtu mmoja aliyekwenda kijiji cha Kolomije kuuliza majina ya wazazi wa Paul Cristian Makonda kama hayo yao na kuuliza jina la mtoto wao wa pekee kama kweli ni Paul Christian Makonda?. Pia watawauliza wazazi wao Paul alizaliwa lini alipewa majina gani, alikulia wapi, alibatizwa wapi, alibatizwa wapi kws majina gani, aliandikishwa darasa la lini, shule gani kwa majina gani, katika simulizi hiyo ya wazazi wake, kusipoibuka majina ya Daudi Albert Bashite, wanaweza kuwauliza wazazi wake kama wanajua lolote kuhusiana na majina ya Daudi Albert Bashite.
Baada ya kupata taarifa hizo, hizo zinakuwa ni primary sources, ukitoka hapo unazitafutia collaborative sources za majirani hapo kijijini ku verfy taarifa za wazazi wake.
2. Hatua ya pili ni kuripoti shule ya Kolomije si bado ipo, wameshindwa nini kwenda kuwauliza jina la huyo mwanafunzi Paul Chirtian Makonda waliotajiwa na wazazi wake kisha wamuulizie na Daudi Albert Bashite aliandikishwa lini alimaliza lini na kwa majina gani na kama alifaulu au alifeli.
3. Baada ya hapo ni kwenda Shule ya Sekondari ya Pamba na kuulizia mwafunzi aliyefeli shule ya msingi, amewezaje kuingia Sekondari ya serekali. Kisha waulizie kuhusu mwafunzi Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite walijiunga lini kwa majina yapi, wakamaliza lini na matokeo yao ni yapi.
4. Unakwenda chuo cha uvuvi Nyegezi unapata details na documentary evidence ya jina la Paul Christian Makonda alilojisajili na vyeti alivyo wasilisha wakati alijiunga na vyeti alivyo hitimu. Hapo Nyegezi ukikuta majina tofauti ya shule na vyeti, unafanya back to back ya shule ulizokuta na kuzipitia ku verfy Paul Christian Makonda alisoma hapo.
5. Unaripoti Mbegani unapata details za Paul Christian Makonda na documentary evidence ya majina aliyotumia kujiunga na vyeti aliyotumia na vyeti vya kuhitimu.
6. Unaripoti chuo cha Ushirika you do the same.
Mkumbuke hizo info zote ni public info ambazo ziko freely accessible. Kama Kuna any discrepancies zozote za majina kwenye hivyo vyeti kati ya Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite then una launch secondary investigation kwa kuandika barua kutumia kipengele cha sheria ya "the right to information act ku access protected info kutaka
7.Vizazi na vifo alipozaliwa aliandikishwaje? .
8. Idara ya Uhamiaji ina file la DN Number alipoomba passport aliwasilisha nyaraka gani na za wazazi wake zikiwemo affidavits zao.
9. Unakwenda mamlaka yake ya ajira kuangalia aliwasilisha vyeti gani
10. Unamkabili Paul Makonda mwenyewe na vielelezo vyote kuthibitisha yeye ni Daudi Albert Bashite bila kusema kuwa ni mwizi wa jina wala amefanya forger or fraud. Kazi ya mwandishi ni kuwalisha facts only hivyo unaibuka na big headline "Uthibitisho Paul Chritian Makonda ndiye Daudi Albert Bashite " huku umetutundikia hizo evidence.

Kinyume cha hapo sisi akina Tomaso wote tunaendelea kuamini kuwa kumbe tuhuma zote hizi dhidi ya Makonda ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!.

Watanzania tuponguze kushadadia uzushi, Paul Makonda endelea kupiga kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa.

Paskali
Jumatano Njema.
Utumwa wa fikra huo.....

Wapo waliokwenda kwa wazazi wao na kuwahoji ... majibu yapo.

Kijijini kwao sio mbali, tulioko jijini Mwanza tumeishapewa ukweli wa kila kitu ...

Muulize kama hawafahamu akina Poneja ... wanamfahamu vizuri sana hata yeye anajua hilo.

Kama unataka akujali kwenye maslahi yako binafsi useme ila hatutaki uongo hapa JF.
 
Back
Top Bottom