Ukweli usemwe: Nandy ni msanii namba moja wa kike ambaye tumebarikiwa kwa sasa

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,210
42,072
Wasalaam wanajamvi.

Kama mnakumbuka ujio wa Nandy alianza baada ya Ruby kukorofishana na Clouds media. Watu wengi nikiwapo mimi walikuwa wana doubt sana kipaji cha Nandy toka awali.. na kama kipindi kile watu walikuwa wakimsikia Nandy basi utawasikia wakisema hamna kitu huyo ameletwa kumfunika Ruby lakini hana kipaji kabisa.

Lakini kwa Msanii Nandy ilikuwa tofauti kwani kila wakati ukipata kusikiliza wimbo wake unagundua kabisa hapa tunaye msanii wakike hodari kabisa.
Msanii Nandy ni bora sana kwenye vitu vingi ukilinganisha na wasanii wenzie wakike kwa sasa.

Ukisikiliza wimbo wa Nandy wa sasa utaona utofauti kabisa na wimbo wa juzi na jana na hiki ndicho kinawashinda wasanii wengi wa kike kwa sasa maana wengi wao karibu nyimbo zote zinafanana kabisa kila kitu.

Pia swala la utulivu kwenye stage linamfanya Nandy awe bora sana kuliko wasanii wenzie wa kike... wasanii wakike wanatatizo la uwezo wa kusikika wakiwa kwenye jukwaaa, wengi wao wanapiga kelele sana tena sana hadi unaweza kujiuliza kama ndio huyu unayemsikia kwenye radio au lah.

Ukimsikiliza Nandy unaona kabisa kipaji kikubwa sana ambacho kinajua kutumiwa vilivyo tofauti kabisa na wasanii wetu wa kike natamani sana kama Rubby angeliamka usingizini akapambana maana ni Rubby pekee ndio ana uwezo mkubwa lakini amelala na aambiliki na ndiye msanii anayefanya Nandy aendelee kutamba kwa Level yake.
 
Kwa mimi ambaye huwa naangalia kazi siangalii mtu / nani naweza kusema Nandy ni Baraka tosha kwa vibao alivyotoa..., kwa kusikiliza kazi zake mimi kama mteja siwezi kulaumu...

Issue kwa kizazi hiki ni utunzi / maneno yaliyomo kwenye nyimbo zao, mengi sio necessary hence kufanya kazi zao zisiweze kusikilizwa na watu wa rika zote..., Mfano Acha Jua Lizame (ingawa alifanya featuring) ni nyimbo nzuri, melody na kila kitu ila maneno sasa yanakwenda kule kule ambao vijana wengi wa Bongo Fleva wanakwenda...., mtu mwenye Busara zako katika jamii lazima uone walakini kusikiliza nyimbo kama hii (sidhani kama babu, baba, mtoto na mjukuu wanaweza wakakaa mezani na kuisikiliza)
 
Upo sawa kabisa..Hata Do me ina melody kali na production kali ila maneno makali kinoma..Bongo Fleva imekuwa ya hovyo sana na kwenye Redio/Tv hawafanyi censorship..

Mfano kwenye hiyo Do me..Billnas anasema "sitotumia kinga hata waseme una virusi"..hii ni lugha ya picha lakini haikuwa necessary kutumika maana ni utopolo tu,jamii inapambana na UKIMWI lakini wewe ni kama unaenda against them.
 
Funguka mkuu, weka na mifano , Ukimsikiliza, ukimsikiliza kipi brother , Nandy ni mbovu kwenye mashairi hlo Tu ndo linamwangusha , syo mwandishi mzur na hapo Zuchu atamkimbiza Sana na pia matusi matusi Sana anaimba ...... Lamba sukari Kwanza mkuu
 
Hivi waimbaji wangapi ni watunzi duniani na watunzi wangapi ni waimbaji ? Hapa huwa watu wanatoa credit zisizostahili kwa baadhi ya watu na kutowapa credit wanaostahili...,

Kwa ufupi kwa sasa mashairi mengi ni mabovu..... sio kwamba hawawezi kutunga mashairi bali wame-concentrate kwenye maneno ya ngono (which is unnessary) na hii ni kwa wengi wao....
 
Back
Top Bottom