Nandy tafuta hela uanzishe media station

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,342
4,801
Nikimuangalia Nandy namuona kama mwanangu kwa umri wake. Ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana na pia ndiye msanii pekee wa kike nchini mwenye Personality nzuri sana.

Ninatamani kuona siku moja akijikomboa kwa kuanzisha media station yake NA HAKIKA INGEBAMBA SANA kuliko Wasafi media.

Nimeshauri hivyo baada ya kuona jinsi Mond alivyofanikiwa hasa baada ya kuanzisha media stn yake. Mond kabla ya kuwa na media yake ilionekana kuminywa na kubaniwa sana na media kongwe hasa Cloud media enzi za Ruge.

Kwasasahivi Mond ana nguvu kubwa sana na ushawishi hata kwa media station zingine kwasababu wanaogopa kumbania wakijua anaweza kuwaajiri kwenye media zao. Wanahabari hawataki yawakute ya Mpoki ambaye alikuwa anamponda Mondi na kumkuza Harmonize.

Japo kwasasa naye Mond ameshageuka na kuwafanyia zengwe wasanii wenzake ili kubaniwa wasichanue kabisa, anatumia nguvu za chombo chake na hata alishalalamikiwa kuwahonga presenters wa media station zingine.

Ukombozi pekee ni kuanzisha media station na hapo ndipo itakuwa mwisho wa zengwe.

Ali Kiba na Harmonize ni wasanii wakubwa sana lakini ndio hivyo sio rahisi kupambana na Mond mwenye kituo cha radio na luninga na hii imemsaidia kumuongezea status Serikalini na kuchukuliwa kama mdau mkubwa wa vyombo vya habari.

Nandy wake up please
 
Mnadhan kuanzisha media ni kama kwenye kunya chooni? Wenye pesa na ushawishi mkubwa hizo media zao tu zimewahenyesha na bado wana hisa chache katika umiliki wa hizo media.

Tabia ya kichawi na kishirikina mliyojifunza huko Clouds mnataka kuwaambukiza na wasanii wengine ili mlete uhasama na chuki za kijinga.

Wasanii wenu hao mnaoona wamekua ni bora muwashauri watafute management bora ili wazidi kusonga mbele na sio kuanzisha medias au lebo za muziki ambazo nazo wanashindwa kuziendesha zinaishia kujifia, wapi King music label? Wapi konde music kabel? Wapi Next level music label? Takataka zote zishajifia,

Tatizo la wasanii wa Bongo sio media wala makundi ya muziki, bali Usimamizi mzuri na wenye Sheria kali zinazowafanya wasanii wawe na adabu ktk tasnia ya muziki, nje na hapo hakuna la maana.
 
Sio Kila msanii na presenter akipata pesa kidogo afungue media,Kuna uwekezaji zaidi ya media msikalili Wala kulalishwa,Mandy atakuwa kawekeza kwengine
 
Mnadhan kuanzisha media ni kama kwenye kunya chooni? Wenye pesa na ushawishi mkubwa hizo media zao tu zimewahenyesha na bado wana hisa chache katika umiliki wa hizo media.

Tabia ya kichawi na kishirikina mliyojifunza huko Clouds mnataka kuwaambukiza na wasanii wengine ili mlete uhasama na chuki za kijinga.

Wasanii wenu hao mnaoona wamekua ni bora muwashauri watafute management bora ili wazidi kusonga mbele na sio kuanzisha medias au lebo za muziki ambazo nazo wanashindwa kuziendesha zinaishia kujifia, wapi King music label? Wapi konde music kabel? Wapi Next level music label? Takataka zote zishajifia,

Tatizo la wasanii wa Bongo sio media wala makundi ya muziki, bali Usimamizi mzuri na wenye Sheria kali zinazowafanya wasanii wawe na adabu ktk tasnia ya muziki, nje na hapo hakuna la maana.
We unafuatilia kweli muziki ? Au shabiki WA diamond tu
 
Nikimuangalia Nandy namuona kama mwanangu kwa umri wake. Ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana na pia ndiye msanii pekee wa kike nchini mwenye Personality nzuri sana.

Ninatamani kuona siku moja akijikomboa kwa kuanzisha media station yake NA HAKIKA INGEBAMBA SANA kuliko Wasafi media.

Nimeshauri hivyo baada ya kuona jinsi Mond alivyofanikiwa hasa baada ya kuanzisha media stn yake. Mond kabla ya kuwa na media yake ilionekana kuminywa na kubaniwa sana na media kongwe hasa Cloud media enzi za Ruge.

Kwasasahivi Mond ana nguvu kubwa sana na ushawishi hata kwa media station zingine kwasababu wanaogopa kumbania wakijua anaweza kuwaajiri kwenye media zao. Wanahabari hawataki yawakute ya Mpoki ambaye alikuwa anamponda Mondi na kumkuza Harmonize.

Japo kwasasa naye Mond ameshageuka na kuwafanyia zengwe wasanii wenzake ili kubaniwa wasichanue kabisa, anatumia nguvu za chombo chake na hata alishalalamikiwa kuwahonga presenters wa media station zingine.

Ukombozi pekee ni kuanzisha media station na hapo ndipo itakuwa mwisho wa zengwe.

Ali Kiba na Harmonize ni wasanii wakubwa sana lakini ndio hivyo sio rahisi kupambana na Mond mwenye kituo cha radio na luninga na hii imemsaidia kumuongezea status Serikalini na kuchukuliwa kama mdau mkubwa wa vyombo vya habari.

Nandy wake up please
Acha kumdanganya mtoto wa watu akaishia kula hasara. Mondi aliwekeza kwenye social media ndo katobolea huko so hata hizo media hakuna zilichomsaidia zaidi ya kutaka kumpoteza, na hata sasa hazitegemei kwa lolote zaidi ya wao tu kuanza kujipendekeza baada ya kumshindwa. Nandy dada jichanganye uone
 
Nandy na Beyonce nani mwanamuziki mkubwa?

😅😅

Okey huyo ni wa kitambo.

Nandy na Ice Spice nani ana mafanikio kimuziki mpaka sasa hivi?

Ukiniuliza mimi nitasema kwamba dawa siyo media station yake dawa ni jinsi gani anacheza na social media na platforms zilizopo.

Ngoja nikupe mfano;

Una wimbo wa Nandy wa Dah, wimbo wa Nyashinski wa Perfect Design na una wimbo wa Loliwe wa Zahra.

Unaambiwa chagua mmoja ukawakilishe Africa kwenye tuzo mfano za Grammy.

Utachagua upi? Na hiyo haiishii kwa Nandy pekee ni karibia kwa wanamuziki wengi wa Bongo. Nyimbo zao hazina taste ambayo international audience wataelewa, wala lyrics zetu hazionyeshi kipaji cha utunzi.

So bongo msanii anakua relevant siyo kwa muziki wake bali kwa matukio.
 
Kuna idea moja ya maana sana Nandy akipata mshauri mzuri anapata hela kuliko kuwekeza kwenye redio wakachambane. Tena anapata hela kwa branding na kusaidia marketing huku kazi zikiwa za wataalamu. Nikizipata hela namtafuta 🫡
 
Mbonaa km unamwonea mond Kwa kumsingizia anaonga media zisipige nyimbo za wasanij wenziee ingalii media zake zote zinashinda zikipiga hzo nyimbo za hao wasanii unaosema wanabaniwaa ...

Ili utafiti wake umefanya wapi mkuu??
 
Mkuu kuanzisha media kama radio/tv hadi ije kuanza kulipa sio mchezo mchezo aisee

Unaweza kukuta Wasafi na uwekezaji uliowekwa bado hawajaanza kuvuna faida

Kuna njia nyingi za kufanya kupata hela nje ya muziki sio lazima atembee kama Mondi
 
"Usiige kunya kwa tembo utapasuka msamba"

Baada ya Diamond kufanikiwa katika lebo yake ya Wasafi, kila msanii akaanzisha lebo pia na kusajili wasanii chini yake, ila hadi leo hakuna lebo nyingine nje ya Wasafi iliyofanikiwa.

Kuanzisha chombo cha habari iwe gazeti au radio sio kazi ya kuiga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom