Ukweli usemwe: Msanii Harmonize bado anashikilia rekodi ya Album bora lakini Darasa atatu-suprise mwaka huu kupitia album yake(Slave becomes King)

Unazungumzia album bora ya mwaka au album bora ya wakati wote? Ya mwaka naweza kukubalia kwavile miaka hii hakuna album nyingi za kuzishindanisha, ila ukizungumzia album bora za wakati wote hiyo ya Mmakonde ni takataka mbele ya Album kama Machozi Jasho na Damu, Ulimwengu ndio mama, Aka Mimi, Cinderella, Machozi ya Jide, Mama ya Banana, n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app

Aka Mimi, kwa Bongo hii ndiyo album yangu bora ya muda wote.
 
Unazungumzia album bora ya mwaka au album bora ya wakati wote? Ya mwaka naweza kukubalia kwavile miaka hii hakuna album nyingi za kuzishindanisha, ila ukizungumzia album bora za wakati wote hiyo ya Mmakonde ni takataka mbele ya Album kama Machozi Jasho na Damu, Ulimwengu ndio mama, Aka Mimi, Cinderella, Machozi ya Jide, Mama ya Banana, n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu hapa nazungumzia 2020/2021 huna haja ya kutukana mtu weka hoja hayo ni maoni yangu mkuu..punguza jaziba...
 
Darrasa ametoa wakati sahihi ila tatizo album haukupewa promo,ila album yake kali.

Si unajua siku hizi radio promo wanawapa Ali Kiba na Konde wakiamini wanawakomoa WCB,hili bonge moja la mistake na inawaumiza sana wasanii wasiokuwa kwenye makundi.

We si unaona promo aliyopewa Konde alivyo zindua album,imerushwa live na media mbili Clouds na EFm,imepewa promo zaidi ya mwezi.Kiba wakati anatoa Mvumo wa radi alipewa promo siku nzima kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tano usiku hii haijawahi kutokea kwa msanii yoyote zaidi ya Kiba.

Beef la Clouds,Efm,EATV,Harmonize na Kiba against Diamond na Wasafi lina waumiza sana wasanii wasio husika huku Harmonize,Kiba na label zao wakipata promo na airtime ya kutosha kuliko wasanii wengine.

Wewe Barnaba mtoto wa CMG katoa album juzi lkn hajapewa promo ya kutosha,Young D naye hivyo hivyo,hata Jux nae,Navy Kenzo nk hawa wote hawakupewa airtime ya kutosha kabisa.

Hili beef lina faida kwa Diamond,Harmonize na Kiba na si kwamba labda ni wasanii wakali kuliko wenzao bali ni watu waliokuwa pamoja baadae wakafarakana.
Katika hili nakubaliana na wewe kabisa kuna madhaifu makubwa kwenye promotion kwa Darasa... ni either ana mkono wa birika au ana chukulia poa kuamini kuwa anapendwa atatoboa tuu... ukweli ni kwamba album yake ikipata promotion na akiwekeza kwa promotion lazima hii album itakwenda mbali sana tena sana.
 
Unavyosema album Ni Bora Ni vizuri ukatoa vigezo ulivyotumia au ukatoa matunda ya album Ni yapi? kwa kuonesha data wabongo mnakwama wapi? au hamjifunzi kupitia nchi Kama marekani
Kwani matunda ya album nilizo zieleza yamejificha si yako wazi kabisa?
 
DARASA KATOA ALBUM WAKATI MBAYA SANA.HUU NI WAKATI AMBAO AINA YA NYIMBO ZINAZOTAMBA NI ZA AINA KAMA YA AKINA MABANTU.HEBU USIKILIZE WIMBO WA WHOZU AU HUU WA SASA WA KINA LAVALAVA UNAITWA BADO SANA.
HII NI AINA YA MUZIKI AMBAO UNASHIKA CHAT SASA
Sio lazima aimbe kama wakina mabantu ndio asikilizwe... ukweli ni kwamba Darasa anatakiwa kufanyia promotion album yake ..... kuna shida kwenye promotion
 
Darasa flow zake ni zile zile zinazoeleka kwasababu habadiliki ,labda album itambeba kwa ajili ya colabo na wasanii tofauti
hili nalo ni tatizo kwenye album yake
 
Unavyosema album Ni Bora Ni vizuri ukatoa vigezo ulivyotumia au ukatoa matunda ya album Ni yapi? kwa kuonesha data wabongo mnakwama wapi? au hamjifunzi kupitia nchi Kama marekani
Hapa Tanzania sio marekani Dada
Basi bado sana ya lavalava ndo Kali au vipi?
 
Yan harmonize itabaki kuwa bora coz Ya utofauti wa uimbaji,darasa flow ni ile ile icho ndo kimeboa watu wengi,wabongo siku hizi wengi wanaelewa mziki wanataka vitu tofauti..hata aslay nae kuna kipindi ngoma zake zote zilikuwa zinafanana uimbaj mpaka beat,watu wakaanza kumtema taratibu taratibu
 
Unajua Darasa asili yake ni Hiphop, hivyo usimtarajie sana kwenye kubadili melody maana ni kama anarap (haimbi)

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hapa Tanzania sio marekani Dada
Basi bado sana ya lavalava ndo Kali au vipi?
Sasa mzee baba lavalava kaingiaje hapa? Anyway Leo hii tunazungumzia album Bora Kama za professor jay, Cinderella ya king kiba,Machozi na damu ya Jide n.k nikutokana na mauzo yao pamoja ngoma hizo kufikiwa na Watanzania wengi kwa hizo ngoma kufanya vizuri na kuacha alama kwenye bongo fleva industry so unavyoleta hoja ya kwamba album ya darassa na Harmonize Ni Bora ndio nimeuliza hivyo vigezo gani amevitumia? Labda aseme kwa mapenzi yake binafsi tutamuelewa
 
Unazungumzia album bora ya mwaka au album bora ya wakati wote? Ya mwaka naweza kukubalia kwavile miaka hii hakuna album nyingi za kuzishindanisha, ila ukizungumzia album bora za wakati wote hiyo ya Mmakonde ni takataka mbele ya Album kama Machozi Jasho na Damu, Ulimwengu ndio mama, Aka Mimi, Cinderella, Machozi ya Jide, Mama ya Banana, n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Promise ya Hussein machozi
 
hii album ni ya kawaida sana na hakuna hit hata moja ngoma zote za kawaida na itapita kimya kimya haitaacha impact yoyote.
 
Sasa mzee baba lavalava kaingiaje hapa? Anyway Leo hii tunazungumzia album Bora Kama za professor jay, Cinderella ya king kiba,Machozi na damu ya Jide n.k nikutokana na mauzo yao pamoja ngoma hizo kufikiwa na Watanzania wengi kwa hizo ngoma kufanya vizuri na kuacha alama kwenye bongo fleva industry so unavyoleta hoja ya kwamba album ya darassa na Harmonize Ni Bora ndio nimeuliza hivyo vigezo gani amevitumia? Labda aseme kwa mapenzi yake binafsi tutamuelewa
Umeambiwa ni kwa mwaka huu
Sasa kina prof jay wameingiaje?

Uwe muelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom