"Single Again" ya Harmonize yaingia tano bora ya Spotify Best Afrobeats Songs of 2023

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,314
Hongera sana #Kondeboy kwa kuingiza wimbo 1 kwenye top 5 ya nyimbo bora za Afrobeats kwa mwaka 2023 huko Spotify..

Siku zote kazi bora huwa inaonekana, kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Ukitoa wimbo mkali utabaki kuwa mkali tuu hata usipofanya promo. Tujifunze kwa wanaijeria, hawana shobo na promo ila kazi ndizo zinaongea. Hata hii Single again hakuna nchi Harmonize ameenda kuifanya promo lakini imevuma bara zima na mabara mengine.

Kuna kasumba imeibuka kwa wasanii wa bongo, kwamba kila ngoma anayoitoa basi ni lazima aitengee bajeti ya promotion. Nani aliwadanganya huu ujinga? Mtu anatoa ka wimbo kamoja tena kabaya baya ila promo lake utadhani boonge la wimbo.

Wasanii jifunzeni kwa wenzenu wa Nigeria na SA, hawana muda wa kupoteza kufanya unnecessary promotions. Wao wanachofanya ni kuachia mawe makali makali kisha yenyewe yanajiuza bila nguvu kubwa.

Kwa sasa hizi radio na tv stations hazina nguvu tena ya kuufikisha wimbo wako duniani. Mziki wa sasa upo kidijitali zaidi. Digital platforms ndizo zinazodetermine uhai wa wimbo au album yako. Kama wimbo ni mzuri, lazima utaenda viral tuu, hata usipofanya media tour yoyote.
HarmonizeSpotify.jpg
 
Back
Top Bottom