Ukweli ni upi kuhusu THE PHILADELPHIA EXPERIMENT??

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,239
Reaction score
39,813
images (19).jpg
WanaJF intelligence habari za asbuhi.... Bila kupoteza muda ningependa kwenda mojamoja kwenye mada ...... Je upi ni ukweli kuhusu philadelphia experiment?

17zpws4686yknjpg.jpg
Inasemekana mnamo october 28, 1943 meli vita ya marekani USS Eldridge huko philadelphia jimbo la Pennsylvania marekani ilitumika kufanya majaribio ya formula za Albert Einstein kuhusu TELEPORTATION yaani kuhamisha kitu kutoka point A kwenda point B kwa kukitowesha kutoka point A alafu ikajiumba upya point B mfano ikulu ya magogoni uamue kuihamisha dodoma kwa sekunde chache tu yaani kwa spidi ya mwanga wa radi hivyo unaitowesha hapo Dar alafu inatokea huko dodoma!!

Sasa hiyo USS eldridge kutokana na vita kuchachamaa kipindi hicho wamarekani wakawa wanatafuta silaha za kila aina kummaliza adui sasa wanadai kabla mbinu hii haijatumika vitani ilibidi ifanyiwe majaribio ndani kwa ndani ndio yakafanyika majaribio haya mawili

La kwanza lilikuwa july 1943 ambapo meli hiyo hiyo USS Eldridge iliweza kufanywa majaribio ya kisayansi na isionekane kwa macho... kwa ufupi ikayayushwa!! (Wavuvi waliona meli ikitoweka ikabaki moshi wa kijani tu )

Sasa walipoona wamefanikiwa kufanya meli iyayuke/isionekane ili adui asiione kwenye uwanja wa vita wakajaribu kufanya majaribio ya kuiteleport kwa kuihamisha kutoka eneo A kwenda eneo B kwa kutumia hizo sheria za kisayansi za QUANTUM TELEPORTATION (unified field theories) zilizoimarishwa na Albert Einstein

Kuendana na maelezo ya morris jessup mtu aliyeiibua SIRI hii na kuuawa miaka michache baadae meli hiyo ilitoweka kweli kutoka philadelphia na baada ya sekunde chache ikatokea upande wa New york yaani meli iyayuke pale bandari Dar alafu ionekane mpendae huko pemba sekunde chache baadae!!!!

Mwandishi anasema licha ya jaribio hili kufanikiwa ila wanajeshi waliokuwepo kwenye meli wengi walipata madhara mfano kuna watu walikutwa wamebanwa katikati ya vyuma.... Wengine wamekufa, wengine meli ilipoyeyuka hawakurudi, wengine waliopona walirukwa na akili na baadae wengi wao kufa vifo vya kiutatanishi (inasemekana walifuatiliwa na kuuawa ili wasitoe siri)
Noi-marturii-înspăimântătoare-despre-Experimentul-PHILADELPHIA.jpg

Story hii ilivuja kupitia mmoja wa wanajeshi aliyeitwa miguel ailende aliepona kwenye tukio hilo ambaye kabla naye hajasakwa alitoa siri zote alizoziona kwenye meli kwa mwandishi huyu morris Jessup ambaye naye kwa kuandika makala hii na kutoa kitabu aliishia kufa kifo cha kutatanisha!!!

Sasa nimeleta kisa hiki kwa wana JF ili wajuvi wa mambo mtusaidie je upi ni ukweli kuhusu the philadelphia experiment??

Je tukio hili ni la kweli au limeongezwa chumvi na wamarekani ili waoagopeke??

Je kweli waliweza kuiteleport meli??

Je huenda bado wanayo hyo teknolojia au waliachana nayo baada ya kufeli vibaya??

Je kama teknolojia hiyo ikiwepo sahvi itabadilishaje mambo kwenye uwanja wa kivita??

NB: Teleportation sio jambo la kufikirika linawezekana sema kwa vitu vidogo na iko proven na wanasayansi kuwa unaweza ukakihamisha kitu dar ukakifikisha morogoro bila kusafirisha physically.... Na wanasayansi wa japan wameweza kuteleport element chache kutoka ardhini zikatokea upya huko kwenye satellite yao angani!!

Naomba kuwasilisha

CC Malcom Lumumba Elungata Kiranga hearly Mshana Jr Habibu B. Anga Palantir Da'Vinci Kudo900 Kipanga boy izzo Eiyer Ziroseventytwo na wanajukwaa wote
 
Hivi mods mnamoderate nini kwa masaa zaidi ya 12??? Kma mnaona haufai si muufute tu sasa Y all this tym mnauweka pending wakati kule MMU wati wanapost thread za kujadili makalio ya wema alafu huwa hamna time nazo

Mnakera sana kwa kweli..... Jaribuni kuwa professional sababu nkiamua kuipaste mada hii kule jukwaa la hoja mchanganyiko itakuwa publicly displayed sasa kinachochelewesha huku ni nni???
 
Mkuu mods nahisi watakua wamekuelewa vilivyo, but wabadilike kwa kweli raha ya thread unapoiandaa na kuipost unatamani kuona inaachiliwa haraka kwa jukwaa na kuanza kujadiliwa

Lakini pia hii inakatisha tamaa na moyo wa kuandaa thread nyingine kwani ukishaanza kufikilia kusubirishwa shauku inapotea kabisa ya kuandika thread nyingine.
 
Kwangu hii nimesha wahi kuisikia mara kadhaa Kuhusu teknolojia hii ya ajabu kabisa lakini sikuwa na uhakika sana pia nilijua ni mwendelezo tu wa drama za marekani, hivyo sikulitilia maanani Sana

Lakini hapa naweza pata elimu zaidi na kuongeza maarifa ngoja tusubiri wakuu waje kutujuza zaidi.
 
Angalia na wewe usije potea kwa kutatanisha[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna movie moja inaitwa "Anti matter " kuna michezo kama hiyo ya kuhamisha hamisha vitu.
 
Sayansi is all about witch craft hamna science wala nn et!! Limeli lipote dar es salaam then lifike japan kwa seconds wapi na wapi
Ndo waafrika tulichobarikiwa na mungu "Haiwezekani" chochote kile kwetu huwa haiwezekani....Tanzania ya viwanda Haiwezekani mpaka wenzetu wataanza kwenda kuishi Mars cc kwetu huku Africa Haiwezekani....[emoji28] [emoji28]
 
Wachangiaji wameadimika namna hii!!!!! tumebaki na wanasiasa tu
 
Mkuu mods nahisi watakua wamekuelewa vilivyo, but wabadilike kwa kweli raha ya thread unapoiandaa na kuipost unatamani kuona inaachiliwa haraka kwa jukwaa na kuanza kujadiliwa

Lakini pia hii inakatisha tamaa na moyo wa kuandaa thread nyingine kwani ukishaanza kufikilia kusubirishwa shauku inapotea kabisa ya kuandika thread nyingine.
Kweli kabisa juzi juzi nlipost Uzi kuhusu uwepo wa aliens kwenye dunia yetu ime kaa pending wee hadi ika potelea hewani skuiona tena ina katisha tamaa kwa kweli
 
. Wote walio andika walikufa, wewe huogopi?
View attachment 754936 WanaJF intelligence habari za asbuhi.... Bila kupoteza muda ningependa kwenda mojamoja kwenye mada ...... Je upi ni ukweli kuhusu philadelphia experiment?
View attachment 754937 Inasemekana mnamo october 28, 1943 meli vita ya marekani USS Eldridge huko philadelphia jimbo la Pennsylvania marekani ilitumika kufanya majaribio ya formula za Albert Einstein kuhusu TELEPORTATION yaani kuhamisha kitu kutoka point A kwenda point B kwa kukitowesha kutoka point A alafu ikajiumba upya point B mfano ikulu ya magogoni uamue kuihamisha dodoma kwa sekunde chache tu yaani kwa spidi ya mwanga wa radi hivyo unaitowesha hapo Dar alafu inatokea huko dodoma!!
Sasa hiyo USS eldridge kutokana na vita kuchachamaa kipindi hicho wamarekani wakawa wanatafuta silaha za kila aina kummaliza adui sasa wanadai kabla mbinu hii haijatumika vitani ilibidi ifanyiwe majaribio ndani kwa ndani ndio yakafanyika majaribio haya mawili
La kwanza lilikuwa july 1943 ambapo meli hiyo hiyo USS Eldridge iliweza kufanywa majaribio ya kisayansi na isionekane kwa macho... kwa ufupi ikayayushwa!! (Wavuvi waliona meli ikitoweka ikabaki moshi wa kijani tu )
Sasa walipoona wamefanikiwa kufanya meli iyayuke/isionekane ili adui asiione kwenye uwanja wa vita wakajaribu kufanya majaribio ya kuiteleport kwa kuihamisha kutoka eneo A kwenda eneo B kwa kutumia hizo sheria za kisayansi za QUANTUM TELEPORTATION (unified field theories) zilizoimarishwa na Albert Einstein
Kuendana na maelezo ya morris jessup mtu aliyeiibua SIRI hii na kuuawa miaka michache baadae meli hiyo ilitoweka kweli kutoka philadelphia na baada ya sekunde chache ikatokea upande wa New york yaani meli iyayuke pale bandari Dar alafu ionekane mpendae huko pemba sekunde chache baadae!!!!
Mwandishi anasema licha ya jaribio hili kufanikiwa ila wanajeshi waliokuwepo kwenye meli wengi walipata madhara mfano kuna watu walikutwa wamebanwa katikati ya vyuma.... Wengine wamekufa, wengine meli ilipoyeyuka hawakurudi, wengine waliopona walirukwa na akili na baadae wengi wao kufa vifo vya kiutatanishi (inasemekana walifuatiliwa na kuuawa ili wasitoe siri)
View attachment 754945
Story hii ilivuja kupitia mmoja wa wanajeshi aliyeitwa miguel ailende aliepona kwenye tukio hilo ambaye kabla naye hajasakwa alitoa siri zote alizoziona kwenye meli kwa mwandishi huyu morris Jessup ambaye naye kwa kuandika makala hii na kutoa kitabu aliishia kufa kifo cha kutatanisha!!!
Sasa nimeleta kisa hiki kwa wana JF ili wajuvi wa mambo mtusaidie je upi ni ukweli kuhusu the philadelphia experiment??
Je tukio hili ni la kweli au limeongezwa chumvi na wamarekani ili waoagopeke??
Je kweli waliweza kuiteleport meli??
Je huenda bado wanayo hyo teknolojia au waliachana nayo baada ya kufeli vibaya??
Je kama teknolojia hiyo ikiwepo sahvi itabadilishaje mambo kwenye uwanja wa kivita??
NB: Teleportation sio jambo la kufikirika linawezekana sema kwa vitu vidogo na iko proven na wanasayansi kuwa unaweza ukakihamisha kitu dar ukakifikisha morogoro bila kusafirisha physically.... Na wanasayansi wa japan wameweza kuteleport element chache kutoka ardhini zikatokea upya huko kwenye satellite yao angani!!
Naomba kuwasilisha

CC Malcom Lumumba Elungata Kiranga hearly Mshana Jr Habibu B. Anga Palantir Da'Vinci Kudo900 Kipanga boy izzo Eiyer Ziroseventytwo na wanajukwaa wote
 
extra terrestrial technology.
hizo ndio zile teknolojia ambazo inadaiwa taasisi za ulinzi za marekani wanazipata kupitia kwa viumbe wanaotoka sayari za mbali(aliens) baada ya kufanya makubaliano fulani ya win win situation kati ya binadamu na viumbe hao wa ajabu.
 
Back
Top Bottom