Mkumbo hata wewe asaiv mawazo yako yapo kifungoni, najua hata sasa una mapenzi na rais magufuli na ana madhaifu makubwa Mara mia afadhali madhaifu ya nyerere uliyosema hapa, lkn sababu ya keki ya taifa unayopata kwa sasa sidhani kama utaona dhaifu hata moja la magufuli, nimefanya hivi ili kukumbusha kuwa koti la kawawa ndo umelivaa wewe muda huu.Katika ku-balance story, msije hangaika kumuuliza Kawawa; huyu hajawahi kuwa na mawazo yake mwenyewe tangu nianze kumsikiliza. Atakachowaeleza ni hayohayo ya Nyerere ambayo tayari mnayajua.
Nimesoma ile article mara kibao, sijaona hata chembe ya chumvi. Alichofanya yule mwandishi ni kusimulia kile ambacho hakijawahi kusimuliwa.
Lazima tukiri kwamba pamoja na mazuri ya mzee wetu Nyerere, ndani ya nguo zake alikuwa ni mtu hatari sana hasa katika kuwafanya wanasiasa wenzake waonekana ovyo mbele ya jamii. communist style. Unakumbuka jinsi Amini alivyochafuliwa: mla watu, alionyeshwa akibeba nyama za watu na huku inzi wakimzonga, lakini wote sasa tunajuwa kwamba pamoja na ubaya wa Amini hakufikia kiwango cha kubeba nyama za watu kwenye mzegazega, huo ulikuwa ni umafia aliofanyiwa.
Pamoja na mapenzi yangu kwa Nyerere, nasikitika kwamba huyu mzee alijaribu kwa mafanikio makubwa kuua kila kipaji cha mtu yeyote mwingine aliyeibuka. As a result, yeye peke yake mpaka leo anaonekana ndiye aliyekuwa hero. Lakini sote tunajua ukweli kwamba isingewezekana yeye tu peke yake alete mazuri. Sasa swali la kujiuliza hao wengine walikuwa akina na nani na kwa nini hatuwajui?