Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Wanawake wachache sana wanaotambua nguvu iliyo kwao.

Na ndio maana familia zao zimesimama imara.

nakuunga mkono. wanawake wengine wana tamaa na husahau kuwa dira kwa familia zao. kwa wale walio kama uzi unavyoeleza waume zao hawana budi kuwaunga mkono na kuwalinda.
 
................................................

Naandika haya through my experience kwa kuona na siyo kihisia, kuna mdau mmoja humu wa kike aliwahi kuandika ndoa ya vijana wa sasa itakayokuwa na amani basi mama wakwe wawe wameshakufa, kitu ambacho kina ukweli mtupu na kamwe hutosikia baba wakwe ndio wenye chokochoko kwenye ndoa za watoto zao.
.....................................

Yaani wee kaka wewe! kama umeandika uliyoyaona through your experience, na mleta uzi nae kaandika aliyoona labda na kuyaishi "through his experience". Sasa kama kuna mtu alisema mama wakwe wanaleta chokochoko kwenye familia na wewe umeshapatwa na tukio kama hilo ila hujawahi kuona wala kusikia baba wakwe wakileta chokochoko kwenye ndoa za watoto wao haimaanishi kuwa hilo jambo halipo au halitatokea, na mtazamo wa mdau ukifanana na experience yako haimaanishi ndo ukweli dunia nzima. Kuwepo mama wakwe wenye kuchokonoa ndoa za watoto wao hakuondoi uwepo wa wanawake wanaojenga ndoa zao. Kwa uzoefu wako maoni yako ni ukweli kwako na yake ni uongo kwako, na yake ni ukweli kwake na yako ni ukweli kwake maana sijaona mahali amebisha kuwa kuna wanawake hawako kama alivyosema.
 
Mwanamke unayemsema kwenye thread yako asiwe anakunywa pombe ndo atakuwa na sifa hizo.
 
Nawasalimia wakuu wangu,
Japo kuwa kuna dhana imejengeka kwenye jamii kuwa mwanaume ndio shababi na mwenye maamuzi ya mwisho katika familia na jamii kwa ujumla,lakini ukweli halisi ulio nyuma ya yote haya,mwanamke ndo mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ..kama tutakavyoona ifuatavyo;

a) Usemi wa kwenye mafanikio yoyote ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake-usemi huu unadhihirisha nguvu ya mwanamke aliyonayo ya kumsaidia mwanaume aweze kufanikisha mambo ambayo yeye kama yeye asingeweza au hata angeweza kukata tamaa au kuvurunda.Hii inawekewa mkazo na desturi za nchi nyingi duniani ambazo hawawezi kumpa madaraka makubwa mwanaume 'bachelor', madaraka kama urais na uwaziri mkuu..Hii ni kwasababu mwanaume kama hajaoa na asie na familia anakuwa haaminiki na anaonekana kama 'muhuni tu' ambae haaminiki katika jamii na ni mtu ambae hana mshauri.Mwanamke huchangia mafanikio ya mwanaume kwa kumpa miongozo na ushauri na hata wakati mwingine kumdhibiti asifanye mambo ya kipuuzi ili kufikia malengo.

b) Maamuzi mengi ya nyumbani hutolewa na mwanamke au huwa yanakuwa shaped na mtazamo wa mama mwenye nyumba- Hii watu wengi wanaweza kujitokeza kuipinga kwa nguvu,lakini ukweli ni kwamba maamuzi mengi ya nyumbani,hata kama yatatolewa na baba,lakini kwa kiasi kikubwa yatazingatia ushauri wa mama au kwa kifupi mama anataka nini,mfano hata kama ni ununuzi wa kitu au kuingia katika ushirikiano wa kibiashara wowote,lazima ushauri wa mama uzingatiwe sana,utasikia mtu akisema 'ngoja nikamshirikishe na wife nitakupa jibu kesho',kama mama asipolikubali hilo wazo ujue ni ngumu sana kwa huo mradi kufanikiwa..na hata kama mwanaume ataamua afosi kibabe kwa hulka ya kiume huku mama akiwa ananung'unika au hataki,ujue kuwa huo mradi hautofika mbali utakufa tu!

c) Kiboko ya mwanaume yoyote alieoa ni mke wake (ikiwamo na mimi)-mtu asikuambie,kiboko ya mwanaume yoyote (mwenye akili timamu) ni mke wake,haijalishi ni rais,mfalme au nani..lakini mbele ya mke wake hakohoi,hii inaweza kusababishwa na mambo mengi,kwanza mke wako ndo anaekujua nje na ndani,mke wako ndo rafiki yako wa ukweli kuliko marafiki zako wote,kipindi cha shida na dhoruba..marafiki zako wote wanaweza kukukimbia na kukuacha na shida zako akabaki mkeo pekee,ambae utakuwa unashinda nae njaa na kulala nae njaa,wale marafiki zako wote mliokuwa mnakesha nao bar unawanunulia bia sita sita watakukimbia na kuanza kukuongelea vibaya, lakini siyo mke wako, pia hata kipindi cha magonjwa,kesi na misukosuko mbalimbali ya kimaisha,ni mkeo pekee ndo atabaki amesimama na wewe..Hii huwa inamfanya mwanaume mwenye akili hata 'akiharibu' mtaani,akitishiwa habari hizo aataenda kuambiwa mkewe huwa ni mdogo,ni bora aharibu kote lakini mkewe asijue.

d) Mwanamke ndo mlinzi wa mwanaume-Kuna mambo mengi ambayo mwanamke anaona mbali kabla ya mwanaume hajayaona,kwa mfano mwanaume unaweza kuwa unaanzisha project fulani..kama mwanamke roho inasita na kukuambia uachane nayo ukifosi huko mbeleni utakuja kulia,au hata unaweza kuwa na urafiki na mtu fulani,lakini mwanamke akawa anasema mimi roho yangu ina wasiwasi na huyu fulani sio mtu mzuri,ukipuuza siku moja utakuja kulia..hata kama ni tabia fulani kila siku mwanamke anakupigia kelele na wewe una mpuuza ipo siku utakuja kulia.Kifupi mwanamke ni mlinzi wa mwanaume na huwa anaona mbali kabla ya sisi wanaume hatujaona.

e) Mwanamke hukomaa kiakili haraka kuliko mwanaume-Inasadikika na ni vyema kuoa mwanamke uliemzidi kiumri maana ndo kiakili mnakuwa sawa kwasababu wanawake wanakomaa kiakili haraka kuliko wanaume.Japo wana madhaifu yao,lakini mwanamke mliezaliwa nae mwaka mmoja anakuwa amekomaa kiakili na kimtazamo wa maisha zaidi kuliko mwanaume. Mwanamume mara nyingi huangalia kufurahisha mwili na marafiki zake muda wote lakini sio mwanamke...Sio ajabu (hata mimi imenitokea mara nyingi),naweza nikawa na marafiki bar nikala laki mbili kwa siku moja..kesho nikaamka nimeshika kichwa huku ninapiga miayo.Lakini mwanamke hata kila siku moja hawezi kufanya huo ujinga wa kula hela hivyo.Ndo mana unaweza kuwa una kipato kikubwa kuliko mwanamke mnaefanya nae kazi ofisi moja lakini yeye akakuzidi maendeleo..ukaishia kusema 'usishindane na mwanamke..wenzetu wanahongwa' lakini kumbe wapo sensitive na maisha.Hata nyumbani unaweza ukawa unamuachia mkeo elfu kumi au zaidi kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku(inategemea na kipato chako) ,atajitahidi kuhudumia familia yako na kusave kwa hichohicho kidogo unachoacha,na usishangae siku moja huna kitu anakupa hela kutoka kwenye kibubu chake alichokuwa anahifadhi wakati kiukweli wewe ndo huwa unashika hela nyingi kuliko yeye...

Wakuu kuna mambo mengi ya kuongelea,lakini ukweli ni kwamba, mwanamke ndo anatawala maisha ya mwanaume na wanaume wengi kuliko aharibu kwa mke wake ajue..bora umpe adhabu yoyote..utasikia 'wife akijua itakuwa noma sana'...au'hii mambo iishie huku huku wife asijue..'nk .Wanaume wengi tunaogopa (tunaheshimu sana) wake zetu na asie mheshimu mke wake huyo ana matatizo.Au wadau mnaonaje?
I love you
 
Labda hujaona, kama umeoa basi unajibaraguza na kujifanya kama mbuni kuficha kichwa kwenye mchanga na kuacha mwili nje

Ukweli utakuweka huru kaka
never trust on someone kwako kufanikiwa, Behind every successfully person there is hard working and God. No a man or woman.
 
Siwezi kupingana na uamuzi na maono yako, nami pia nina maono yangu ambayo yanafanana sana na ya mtoa mada
Bahati nzuri kwenye feedback tunayopata hapa,wengi tuna maoni ya "in every successful man there is a woman behind",hao wanaobeza wanawake ni wachache,tuwapuuze.Mtu anae mdharau mke wake na kumdhalilisha hadharani hana akili...maana anajidhalilisha mwenyewe...
 
Adam angelikuwa kamili asingepewa Eva...labda hukuelewa somo la mchungaji vizuri..
Eeh we nawe!. wasaidizi unawajua vizuri?. Si lazima msaidizi awepo na ndiyo maana wasaidizi wengi huwa hawapati nafasi ya kufanya jambo hadi aelezwe
 
Bahati nzuri kwenye feedback tunayopata hapa,wengi tuna maoni ya "in every successful man there is a woman behind",hao wanaobeza wanawake ni wachache,tuwapuuze.Mtu anae mdharau mke wake na kumdhalilisha hadharani hana akili...maana anajidhalilisha mwenyewe...

Hao ndio wale waliooa
*Bila kupenda/walilazimishiwa wake/kutimiza wajibu
Wana michepuko na ndio wanaofanya wawadharau wake zao cz washalogwa akili ..na hawafaidi wala kuona tamu ya ndoa
Wameoa viruka njia walokutana nao stareheni wasojua wt life z ...
*Au hajaoa kabisaaaa..bachela
*Kalelewa mazingira ya kutoheshimu mchango wala kusikiliza opinions za mwanamke....
 
Eeh we nawe!. wasaidizi unawajua vizuri?. Si lazima msaidizi awepo na ndiyo maana wasaidizi wengi huwa hawapati nafasi ya kufanya jambo hadi aelezwe
Maana ya kupewa msaidizi ni nn sasa kama mhusika anaweza kila kitu peke yake..Msaidizi anapewa mtu anyehitaji msaada..sio mtu anayejitosheleza...elewa hilo kwanza..Mnasaidiana,mnashauriana,mnapendana,etc etc etc..you complement each other...
 
Back
Top Bottom