Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,352
9,809
Nawasalimia wakuu wangu,
Japo kuwa kuna dhana imejengeka kwenye jamii kuwa mwanaume ndio shababi na mwenye maamuzi ya mwisho katika familia na jamii kwa ujumla,lakini ukweli halisi ulio nyuma ya yote haya,mwanamke ndo mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ..kama tutakavyoona ifuatavyo;

a) Usemi wa kwenye mafanikio yoyote ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake-usemi huu unadhihirisha nguvu ya mwanamke aliyonayo ya kumsaidia mwanaume aweze kufanikisha mambo ambayo yeye kama yeye asingeweza au hata angeweza kukata tamaa au kuvurunda.Hii inawekewa mkazo na desturi za nchi nyingi duniani ambazo hawawezi kumpa madaraka makubwa mwanaume 'bachelor', madaraka kama urais na uwaziri mkuu..Hii ni kwasababu mwanaume kama hajaoa na asie na familia anakuwa haaminiki na anaonekana kama 'muhuni tu' ambae haaminiki katika jamii na ni mtu ambae hana mshauri.Mwanamke huchangia mafanikio ya mwanaume kwa kumpa miongozo na ushauri na hata wakati mwingine kumdhibiti asifanye mambo ya kipuuzi ili kufikia malengo. Mfano mwanaume kama hajaoa anaweza kuwa analala popote, anaweza kuwa hata anatembea na nguo na viatu kwenye gari. Lakini kama Ana mke lazima arudi nyumbani na tena kwa wakati,Sasa hiyo wakati mwingine inamsaidia kuepukana na majanga

b) Maamuzi mengi ya nyumbani hutolewa na mwanamke au huwa yanakuwa shaped na mtazamo wa mama mwenye nyumba- Hii watu wengi wanaweza kujitokeza kuipinga kwa nguvu,lakini ukweli ni kwamba maamuzi mengi ya nyumbani,hata kama yatatolewa na baba,lakini kwa kiasi kikubwa yatazingatia ushauri wa mama au kwa kifupi mama anataka nini,mfano hata kama ni ununuzi wa kitu au kuingia katika ushirikiano wa kibiashara wowote,lazima ushauri wa mama uzingatiwe sana,utasikia mtu akisema 'ngoja nikamshirikishe na wife nitakupa jibu kesho',kama mama asipolikubali hilo wazo ujue ni ngumu sana kwa huo mradi kufanikiwa..na hata kama mwanaume ataamua afosi kibabe kwa hulka ya kiume huku mama akiwa ananung'unika au hataki,ujue kuwa huo mradi hautofika mbali utakufa tu!

c) Kiboko ya mwanaume yoyote alieoa ni mke wake (ikiwamo na mimi)-mtu asikuambie,kiboko ya mwanaume yoyote (mwenye akili timamu) ni mke wake,haijalishi ni rais,mfalme au nani..lakini mbele ya mke wake hakohoi,hii inaweza kusababishwa na mambo mengi,kwanza mke wako ndo anaekujua nje na ndani,mke wako ndo rafiki yako wa ukweli kuliko marafiki zako wote,kipindi cha shida na dhoruba..marafiki zako wote wanaweza kukukimbia na kukuacha na shida zako akabaki mkeo pekee,ambae utakuwa unashinda nae njaa na kulala nae njaa,wale marafiki zako wote mliokuwa mnakesha nao bar unawanunulia bia sita sita watakukimbia na kuanza kukuongelea vibaya, lakini siyo mke wako, pia hata kipindi cha magonjwa,kesi na misukosuko mbalimbali ya kimaisha,ni mkeo pekee ndo atabaki amesimama na wewe..Hii huwa inamfanya mwanaume mwenye akili hata 'akiharibu' mtaani,akitishiwa habari hizo aataenda kuambiwa mkewe huwa ni mdogo,ni bora aharibu kote lakini mkewe asijue.

d) Mwanamke ndo mlinzi wa mwanaume-Kuna mambo mengi ambayo mwanamke anaona mbali kabla ya mwanaume hajayaona,kwa mfano mwanaume unaweza kuwa unaanzisha project fulani..kama mwanamke roho inasita na kukuambia uachane nayo ukifosi huko mbeleni utakuja kulia,au hata unaweza kuwa na urafiki na mtu fulani,lakini mwanamke akawa anasema mimi roho yangu ina wasiwasi na huyu fulani sio mtu mzuri,ukipuuza siku moja utakuja kulia..hata kama ni tabia fulani kila siku mwanamke anakupigia kelele na wewe una mpuuza ipo siku utakuja kulia.Kifupi mwanamke ni mlinzi wa mwanaume na huwa anaona mbali kabla ya sisi wanaume hatujaona. Kuna mfano mmoja siku moja tupo kwenye gari mzee mmoja wa kanisa alikuwa anahadithia kuwa kuna jamaa mmoja huko kanisani kwao alikuwa mchungaji aliunga urafiki nae, lakin toka siku ya kwanza tu huyo mchungaji kufika nyumbani kwake mke wake alipomuona tu akamwambia huyo sio mtu mzuri aachane nae. Lakin mzee akakomaa akaendeleza urafiki motomoto na yule jamaa
Kilichotokea mwishoni mzee alipigwa million 4 na yule mchungaji feki..Mwisho wa siku akawa anasema anajuta kwanini hakumsikiliza mke wake mapema. Wanawake Wana maono ya mbele.

e) Mwanamke hukomaa kiakili haraka kuliko mwanaume-Inasadikika na ni vyema kuoa mwanamke uliemzidi kiumri maana ndo kiakili mnakuwa sawa kwasababu wanawake wanakomaa kiakili haraka kuliko wanaume.Japo wana madhaifu yao,lakini mwanamke mliezaliwa nae mwaka mmoja anakuwa amekomaa kiakili na kimtazamo wa maisha zaidi kuliko mwanaume. Mwanamume mara nyingi huangalia kufurahisha mwili na marafiki zake muda wote lakini sio mwanamke...Sio ajabu (hata mimi imenitokea mara nyingi),naweza nikawa na marafiki bar nikala laki mbili kwa siku moja..kesho nikaamka nimeshika kichwa huku ninapiga miayo.Lakini mwanamke hata kila siku moja hawezi kufanya huo ujinga wa kula hela hivyo.Ndo mana unaweza kuwa una kipato kikubwa kuliko mwanamke mnaefanya nae kazi ofisi moja lakini yeye akakuzidi maendeleo..ukaishia kusema 'usishindane na mwanamke..wenzetu wanahongwa' lakini kumbe wapo sensitive na maisha.Hata nyumbani unaweza ukawa unamuachia mkeo elfu kumi au zaidi kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku(inategemea na kipato chako) ,atajitahidi kuhudumia familia yako na kusave kwa hichohicho kidogo unachoacha,na usishangae siku moja huna kitu anakupa hela kutoka kwenye kibubu chake alichokuwa anahifadhi wakati kiukweli wewe ndo huwa unashika hela nyingi kuliko yeye...

Wakuu kuna mambo mengi ya kuongelea,lakini ukweli ni kwamba, mwanamke ndo anatawala maisha ya mwanaume na wanaume wengi kuliko aharibu kwa mke wake ajue..bora umpe adhabu yoyote..utasikia 'wife akijua itakuwa noma sana'...au'hii mambo iishie huku huku wife asijue..'nk .Wanaume wengi tunaogopa (tunaheshimu sana) wake zetu na asie mheshimu mke wake huyo ana matatizo.Au wadau mnaonaje?
 
c) Kiboko ya mwanaume yoyote alieoa ni mke wake (ikiwamo na mimi)-mtu asikuambie,kiboko ya mwanaume yoyote (mwenye akili timamu) ni mke wake,haijalishi ni rais,mfalme au nani..lakini mbele ya mke wake hakohoi,hii inaweza kusababishwa na mambo mengi,kwanza mke wako ndo anaekujua nje na ndani,mke wako ndo rafiki yako wa ukweli kuliko marafiki zako wote,kipindi cha shida na dhoruba..marafiki zako wote wanaweza kukukimbia na kukuacha na shida zako akabaki mkeo pekee,ambae utakuwa unashinda nae njaa na kulala nae njaa,wale marafiki zako wote mliokuwa mnakesha nao bar unawanunulia bia sita sita watakukimbia na kuanza kukuongelea vibaya, lakini siyo mke wako, pia hata kipindi cha magonjwa,kesi na misukosuko mbalimbali ya kimaisha,ni mkeo pekee ndo atabaki amesimama na wewe..Hii huwa inamfanya mwanaume mwenye akili hata 'akiharibu' mtaani,akitishiwa habari hizo aataenda kuambiwa mkewe huwa ni mdogo,ni bora aharibu kote lakini mkewe asijue.
Mliooa mna bahati sana.
 
No Hero to a Woman.

-Adam & Eve
-Samson & Delilah
-Herode & His wife.

Hata Viongozi wa nchi nyingi wanatawala baada ya kushauriana na wake zao usiku na wengi wanaharibu.
Wengi au wachache?Mwangalie Clinton na mke wake..au Obama na mke wake,inapendeza sana kumpenda na kumheshimu mke wako
 
Back
Top Bottom