Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Nawasalimia wakuu wangu,
Japo kuwa kuna dhana imejengeka kwenye jamii kuwa mwanaume ndio shababi na mwenye maamuzi ya mwisho katika familia na jamii kwa ujumla,lakini ukweli halisi ulio nyuma ya yote haya,mwanamke ndo mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ..kama tutakavyoona ifuatavyo;

a) Usemi wa kwenye mafanikio yoyote ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake-usemi huu unadhihirisha nguvu ya mwanamke aliyonayo ya kumsaidia mwanaume aweze kufanikisha mambo ambayo yeye kama yeye asingeweza au hata angeweza kukata tamaa au kuvurunda.Hii inawekewa mkazo na desturi za nchi nyingi duniani ambazo hawawezi kumpa madaraka makubwa mwanaume 'bachelor', madaraka kama urais na uwaziri mkuu..Hii ni kwasababu mwanaume kama hajaoa na asie na familia anakuwa haaminiki na anaonekana kama 'muhuni tu' ambae haaminiki katika jamii na ni mtu ambae hana mshauri.Mwanamke huchangia mafanikio ya mwanaume kwa kumpa miongozo na ushauri na hata wakati mwingine kumdhibiti asifanye mambo ya kipuuzi ili kufikia malengo.

b) Maamuzi mengi ya nyumbani hutolewa na mwanamke au huwa yanakuwa shaped na mtazamo wa mama mwenye nyumba- Hii watu wengi wanaweza kujitokeza kuipinga kwa nguvu,lakini ukweli ni kwamba maamuzi mengi ya nyumbani,hata kama yatatolewa na baba,lakini kwa kiasi kikubwa yatazingatia ushauri wa mama au kwa kifupi mama anataka nini,mfano hata kama ni ununuzi wa kitu au kuingia katika ushirikiano wa kibiashara wowote,lazima ushauri wa mama uzingatiwe sana,utasikia mtu akisema 'ngoja nikamshirikishe na wife nitakupa jibu kesho',kama mama asipolikubali hilo wazo ujue ni ngumu sana kwa huo mradi kufanikiwa..na hata kama mwanaume ataamua afosi kibabe kwa hulka ya kiume huku mama akiwa ananung'unika au hataki,ujue kuwa huo mradi hautofika mbali utakufa tu!

c) Kiboko ya mwanaume yoyote alieoa ni mke wake (ikiwamo na mimi)-mtu asikuambie,kiboko ya mwanaume yoyote (mwenye akili timamu) ni mke wake,haijalishi ni rais,mfalme au nani..lakini mbele ya mke wake hakohoi,hii inaweza kusababishwa na mambo mengi,kwanza mke wako ndo anaekujua nje na ndani,mke wako ndo rafiki yako wa ukweli kuliko marafiki zako wote,kipindi cha shida na dhoruba..marafiki zako wote wanaweza kukukimbia na kukuacha na shida zako akabaki mkeo pekee,ambae utakuwa unashinda nae njaa na kulala nae njaa,wale marafiki zako wote mliokuwa mnakesha nao bar unawanunulia bia sita sita watakukimbia na kuanza kukuongelea vibaya, lakini siyo mke wako, pia hata kipindi cha magonjwa,kesi na misukosuko mbalimbali ya kimaisha,ni mkeo pekee ndo atabaki amesimama na wewe..Hii huwa inamfanya mwanaume mwenye akili hata 'akiharibu' mtaani,akitishiwa habari hizo aataenda kuambiwa mkewe huwa ni mdogo,ni bora aharibu kote lakini mkewe asijue.

d) Mwanamke ndo mlinzi wa mwanaume-Kuna mambo mengi ambayo mwanamke anaona mbali kabla ya mwanaume hajayaona,kwa mfano mwanaume unaweza kuwa unaanzisha project fulani..kama mwanamke roho inasita na kukuambia uachane nayo ukifosi huko mbeleni utakuja kulia,au hata unaweza kuwa na urafiki na mtu fulani,lakini mwanamke akawa anasema mimi roho yangu ina wasiwasi na huyu fulani sio mtu mzuri,ukipuuza siku moja utakuja kulia..hata kama ni tabia fulani kila siku mwanamke anakupigia kelele na wewe una mpuuza ipo siku utakuja kulia.Kifupi mwanamke ni mlinzi wa mwanaume na huwa anaona mbali kabla ya sisi wanaume hatujaona.

e) Mwanamke hukomaa kiakili haraka kuliko mwanaume-Inasadikika na ni vyema kuoa mwanamke uliemzidi kiumri maana ndo kiakili mnakuwa sawa kwasababu wanawake wanakomaa kiakili haraka kuliko wanaume.Japo wana madhaifu yao,lakini mwanamke mliezaliwa nae mwaka mmoja anakuwa amekomaa kiakili na kimtazamo wa maisha zaidi kuliko mwanaume. Mwanamume mara nyingi huangalia kufurahisha mwili na marafiki zake muda wote lakini sio mwanamke...Sio ajabu (hata mimi imenitokea mara nyingi),naweza nikawa na marafiki bar nikala laki mbili kwa siku moja..kesho nikaamka nimeshika kichwa huku ninapiga miayo.Lakini mwanamke hata kila siku moja hawezi kufanya huo ujinga wa kula hela hivyo.Ndo mana unaweza kuwa una kipato kikubwa kuliko mwanamke mnaefanya nae kazi ofisi moja lakini yeye akakuzidi maendeleo..ukaishia kusema 'usishindane na mwanamke..wenzetu wanahongwa' lakini kumbe wapo sensitive na maisha.Hata nyumbani unaweza ukawa unamuachia mkeo elfu kumi au zaidi kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku(inategemea na kipato chako) ,atajitahidi kuhudumia familia yako na kusave kwa hichohicho kidogo unachoacha,na usishangae siku moja huna kitu anakupa hela kutoka kwenye kibubu chake alichokuwa anahifadhi wakati kiukweli wewe ndo huwa unashika hela nyingi kuliko yeye...

Wakuu kuna mambo mengi ya kuongelea,lakini ukweli ni kwamba, mwanamke ndo anatawala maisha ya mwanaume na wanaume wengi kuliko aharibu kwa mke wake ajue..bora umpe adhabu yoyote..utasikia 'wife akijua itakuwa noma sana'...au'hii mambo iishie huku huku wife asijue..'nk .Wanaume wengi tunaogopa (tunaheshimu sana) wake zetu na asie mheshimu mke wake huyo ana matatizo.Au wadau mnaonaje?
Umesema ukweli mtupu hakuna la kuongeza leah2 na Mkebora
 
Mahubiri ya Mch Dr. Gwajima yanasema mwanaume ni kiumbe kamili na hakihitaji hata kuoa. Mafanikio yapo kama kawaida, nimenukuu baadhi ya mahubiri ya huyo bwana ambayo yanapatikana ktk mafundisho yake ya "Siri ya Kusubiri kabla ya ndoa, Uoe au Uolewe na nani?"
 
Hiyo ni kweli...
Hubby ana tabia ya kuwajibu watu...'subiri kwanza ni discuss na wife'...
Huwa namwambia asipende kusema hivyo kwani akija kata watasema wife kakataa...
Asemege tu 'ntakupa jibu baadae...'
Maana waswahili wakijua wife ndie in charge utaambiwa limbwata...

 
nimegundua mtoa mada anaishi maisha ya kukariri, hakuna mwenye hatma ya maisha yako tofauti na ww mwenyewe.Lewa, punguza kujiamini, kuwa dependant Kwa mkeo, Fanya maamuzi ya hovyo afu uje hapa kutudanganya na Feminism idea zako hapa. Maisha ni ww utakavyojipanga, kufanya, kuamua na Mungu wako acha kudanganya umma
 
Strength for a woman.
Yes mke ana nguvu sana sbb ana uwezo wa kujenga au kubomoa nyumba yake km vitabu vya dini vinavyosema.
Wana power yao kubwa sn km sumaku hasa akizira na kununa hapo ndani ht km we rais unakuwa mdogo km pipi.
strength for a woman ya shaggy anasema woman is a god
 
ukiwa umelenga sawia.....kitu cha kwanza mnatakiwa kuwa marafiki....mengine umbea tuuu.......ila wengi ni vimeo,,,,ukimuheshimu anataka ukupandie juuuu......tupa kuleeeeeee
 
Mahubiri ya Mch Dr. Gwajima yanasema mwanaume ni kiumbe kamili na hakihitaji hata kuoa. Mafanikio yapo kama kawaida, nimenukuu baadhi ya mahubiri ya huyo bwana ambayo yanapatikana ktk mafundisho yake ya "Siri ya Kusubiri kabla ya ndoa, Uoe au Uolewe na nani?"
Biblia inasema Mungu aliona si vyema mtu huyu,Adam,akae mwenyewe akamfanyia msaidizi wa kufanana naye,ndoa ni mpango wa Mungu
 
Mzee Mwi..I nchi ilikuwa inaongozwa na mama Si..i chezea mwanamke wewe
 
Biblia inasema Mungu aliona si vyema mtu huyu,Adam,akae mwenyewe akamfanyia msaidizi wa kufanana naye,ndoa ni mpango wa Mungu
Sawa, lakini si aliumba Mwanaume kwanza, wazo la kumpatia Eva lilikuja baada. Kuoa si lazima, mafanikio yapo kama Mungu alivyokuandalia na wala hachelewi wala hawahi bali anatenda kwa wakati. Ukitegemea ukioa ndpo utafanikiwa utakuwa unajidanganya, hilo ni kusudi la Mungu litakuwa liliandaliwa. Hata Yesu mwenyewe hakuoa na alifanya mambo makubwa ambayo hadi sasa tunajivunia kupitia yeye, Najaribu ku_Quote baadhi ya maneno hapa
 
Wanawake wachache sana wanaotambua nguvu iliyo kwao.

Na ndio maana familia zao zimesimama imara.
Haswaa upo sahihi,utakuta mfano mwanaume wa pwani kaoa mwanamke wa bara ambaye ni mchapakazi,kama tujijuavyoavyo watu wa pwani kwa uvivu,hapa mara mama anakua na nguvu ya ubunifu wa kiutaftaji kuliko baba hasa wale wasiokua na ajira maalum,na ukikuta mama kautambua mchango wake basi akaa familia itaenda vizuri.
 
Pengine nifupishe tu kwa maelezo yako mfuma uzi.
Mwanamke ni;
Mlinzi wa familia
Mtunza hazina wa familia
Ndiye anaefanya familia inakuwa thabiti kimaadili na kimafanikio
Ndiye utambulisho wa familia yake!
 
Back
Top Bottom