Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Ukweli ni kwamba wanaume wengi wanaogopa wake zao

Dah....wanawake hawahawa ambao imeandikwa tuishi nao kwa akili....na kule wakaitwa viumbe dhaifu....na huku tukaambiwa mwalimu wao ni kipofu?
Mleta uzi ni nani hasa hadi apingane na maandiko? Au ndiyo kalazimishwa aulete uzi na mkewe?
Pumzikeni kwa amani
Mshua Adam.... Bro Samson... Herode...nk
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama huu ni ukweli basi dunia inaelekea shimoni.......

Mwanaume haupaswi kumuogopa mkeo ni udhaifu mkubwa sana na mkeo akilitambua hilo kwa maana umepoteza sehemu ya uanaume wako na huwezi kubaki salama......
 
Nawasalimia wakuu wangu,
Japo kuwa kuna dhana imejengeka kwenye jamii kuwa mwanaume ndio shababi na mwenye maamuzi ya mwisho katika familia na jamii kwa ujumla,lakini ukweli halisi ulio nyuma ya yote haya,mwanamke ndo mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ..kama tutakavyoona ifuatavyo;

a) Usemi wa kwenye mafanikio yoyote ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake-usemi huu unadhihirisha nguvu ya mwanamke aliyonayo ya kumsaidia mwanaume aweze kufanikisha mambo ambayo yeye kama yeye asingeweza au hata angeweza kukata tamaa au kuvurunda.Hii inawekewa mkazo na desturi za nchi nyingi duniani ambazo hawawezi kumpa madaraka makubwa mwanaume 'bachelor', madaraka kama urais na uwaziri mkuu..Hii ni kwasababu mwanaume kama hajaoa na asie na familia anakuwa haaminiki na anaonekana kama 'muhuni tu' ambae haaminiki katika jamii na ni mtu ambae hana mshauri.Mwanamke huchangia mafanikio ya mwanaume kwa kumpa miongozo na ushauri na hata wakati mwingine kumdhibiti asifanye mambo ya kipuuzi ili kufikia malengo.

b) Maamuzi mengi ya nyumbani hutolewa na mwanamke au huwa yanakuwa shaped na mtazamo wa mama mwenye nyumba- Hii watu wengi wanaweza kujitokeza kuipinga kwa nguvu,lakini ukweli ni kwamba maamuzi mengi ya nyumbani,hata kama yatatolewa na baba,lakini kwa kiasi kikubwa yatazingatia ushauri wa mama au kwa kifupi mama anataka nini,mfano hata kama ni ununuzi wa kitu au kuingia katika ushirikiano wa kibiashara wowote,lazima ushauri wa mama uzingatiwe sana,utasikia mtu akisema 'ngoja nikamshirikishe na wife nitakupa jibu kesho',kama mama asipolikubali hilo wazo ujue ni ngumu sana kwa huo mradi kufanikiwa..na hata kama mwanaume ataamua afosi kibabe kwa hulka ya kiume huku mama akiwa ananung'unika au hataki,ujue kuwa huo mradi hautofika mbali utakufa tu!

c) Kiboko ya mwanaume yoyote alieoa ni mke wake (ikiwamo na mimi)-mtu asikuambie,kiboko ya mwanaume yoyote (mwenye akili timamu) ni mke wake,haijalishi ni rais,mfalme au nani..lakini mbele ya mke wake hakohoi,hii inaweza kusababishwa na mambo mengi,kwanza mke wako ndo anaekujua nje na ndani,mke wako ndo rafiki yako wa ukweli kuliko marafiki zako wote,kipindi cha shida na dhoruba..marafiki zako wote wanaweza kukukimbia na kukuacha na shida zako akabaki mkeo pekee,ambae utakuwa unashinda nae njaa na kulala nae njaa,wale marafiki zako wote mliokuwa mnakesha nao bar unawanunulia bia sita sita watakukimbia na kuanza kukuongelea vibaya, lakini siyo mke wako, pia hata kipindi cha magonjwa,kesi na misukosuko mbalimbali ya kimaisha,ni mkeo pekee ndo atabaki amesimama na wewe..Hii huwa inamfanya mwanaume mwenye akili hata 'akiharibu' mtaani,akitishiwa habari hizo aataenda kuambiwa mkewe huwa ni mdogo,ni bora aharibu kote lakini mkewe asijue.

d) Mwanamke ndo mlinzi wa mwanaume-Kuna mambo mengi ambayo mwanamke anaona mbali kabla ya mwanaume hajayaona,kwa mfano mwanaume unaweza kuwa unaanzisha project fulani..kama mwanamke roho inasita na kukuambia uachane nayo ukifosi huko mbeleni utakuja kulia,au hata unaweza kuwa na urafiki na mtu fulani,lakini mwanamke akawa anasema mimi roho yangu ina wasiwasi na huyu fulani sio mtu mzuri,ukipuuza siku moja utakuja kulia..hata kama ni tabia fulani kila siku mwanamke anakupigia kelele na wewe una mpuuza ipo siku utakuja kulia.Kifupi mwanamke ni mlinzi wa mwanaume na huwa anaona mbali kabla ya sisi wanaume hatujaona.

e) Mwanamke hukomaa kiakili haraka kuliko mwanaume-Inasadikika na ni vyema kuoa mwanamke uliemzidi kiumri maana ndo kiakili mnakuwa sawa kwasababu wanawake wanakomaa kiakili haraka kuliko wanaume.Japo wana madhaifu yao,lakini mwanamke mliezaliwa nae mwaka mmoja anakuwa amekomaa kiakili na kimtazamo wa maisha zaidi kuliko mwanaume. Mwanamume mara nyingi huangalia kufurahisha mwili na marafiki zake muda wote lakini sio mwanamke...Sio ajabu (hata mimi imenitokea mara nyingi),naweza nikawa na marafiki bar nikala laki mbili kwa siku moja..kesho nikaamka nimeshika kichwa huku ninapiga miayo.Lakini mwanamke hata kila siku moja hawezi kufanya huo ujinga wa kula hela hivyo.Ndo mana unaweza kuwa una kipato kikubwa kuliko mwanamke mnaefanya nae kazi ofisi moja lakini yeye akakuzidi maendeleo..ukaishia kusema 'usishindane na mwanamke..wenzetu wanahongwa' lakini kumbe wapo sensitive na maisha.Hata nyumbani unaweza ukawa unamuachia mkeo elfu kumi au zaidi kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku(inategemea na kipato chako) ,atajitahidi kuhudumia familia yako na kusave kwa hichohicho kidogo unachoacha,na usishangae siku moja huna kitu anakupa hela kutoka kwenye kibubu chake alichokuwa anahifadhi wakati kiukweli wewe ndo huwa unashika hela nyingi kuliko yeye...

Wakuu kuna mambo mengi ya kuongelea,lakini ukweli ni kwamba, mwanamke ndo anatawala maisha ya mwanaume na wanaume wengi kuliko aharibu kwa mke wake ajue..bora umpe adhabu yoyote..utasikia 'wife akijua itakuwa noma sana'...au'hii mambo iishie huku huku wife asijue..'nk .Wanaume wengi tunaogopa (tunaheshimu sana) wake zetu na asie mheshimu mke wake huyo ana matatizo.Au wadau mnaonaje?
NO HAPANA Hayo ni mapungufu makubwa, na nahisi wale wote wanao support hii dhana watakuwa wamelelewa na family zenye mapungufu ya upande wa baba,

Aidha mama ndie alikuwa na Bargaing Power kuliko Baba, kama vile Single mother n.k

Inasikitisha sana kuonyesha dhahiri jamii yetu kubwa inaelekea huko, Wa BABA wenye sifa stahiki za kulea family ni wachache sana sana na wanaendelea kupungua kila siku, matokeo yake ndio haya.

Fikilia zipo family zenye wake zaidi ya mmoja, Mzee ana wake 3, na wote wanaishi eneo moja au boma moja na wamama ki umri wanakaribiana na watoto pia, kwa UJINGA wako huu huwezi kuilea hio family kamwe. wote mnao support hii style naweza sema ni watoto wa mama..

Mambo yote mnajadiliana kushauriana bado UAMUZI NI WA BABA hata kama utakuwa tofauti kwa wote, cha msingi yeye ni kuwaelimisha sababu za yeye kuamua vinginevyo.
 
Kama huu ni ukweli basi dunia inaelekea shimoni.......

Mwanaume haupaswi kumuogopa mkeo ni udhaifu mkubwa sana na mkeo akilitambua hilo kwa maana umepoteza sehemu ya uanaume wako na huwezi kubaki salama......
Kweli kabisa mkuu, DUNIA SASA IKO HATARINI inaendeshwa na wanawake, Mzee zima kichwa cha family unadiliki kusema haya ? ? sidhani kama ulilelewa na baba wewe,

Haya ndio matokeo ya single mama,

HAO WOTE WANAOKUWEKEA LIKE NI WANAWAKE NA BADO WANAKUONA BOYA LAO
 
Hakika wewe ni mke mwema kabisa, yani mwanamke na akili zake akipendwa ndio linakuwa kosa anataka apande kichwani kabisa anye hapohapo, mwanamke wa hivyo ni zuzu peke yake ndio atakayevumilia upuuzi huu.

Mleta mada somehow naye ni walewale ameshakamatwa na akakamatika anadhani uzoba ni uniform kwa kila mwanaume.

Mwanaume kamili kabla ya kuinvest project yoyote tunafanya research ya kutosha then ndio tunajitosa, sasa mke akikataa hiyo ni shauri yake cha msingi si pesa ya mke ninayoinvest, na dunia ya leo successful people ni wale tu risk takers.

Nachukia sana viwanaume kama hawa kila mnaloongea wanaume anapeleka kwa mkewe kwa ajili ya maamuzi wakati wanawake wengi kwenye mambo yao huamuwa wenyewe na ukupa taarifa baadaye akipenda.

Huu uzungu uzungu unaondoa hata maana ya mwanaume na kumfanya Mungu kama mjinga wakati anafanya uumbaji.
Ni moja ya wanaume wachache wanaotumia vyema akili zao dhidi ya wanawake.....hongera kwa kusimama vyema kwenye uanaume wako.....
 
NO HAPANA Hayo ni mapungufu makubwa, na nahisi wale wote wanao support hii dhana watakuwa wamelelewa na family zenye mapungufu ya upande wa baba,

Aidha mama ndie alikuwa na Bargaing Power kuliko Baba, kama vile Single mother n.k

Inasikitisha sana kuonyesha dhahiri jamii yetu kubwa inaelekea huko, Wa BABA wenye sifa stahiki za kulea family ni wachache sana sana na wanaendelea kupungua kila siku, matokeo yake ndio haya.

Fikilia zipo family zenye wake zaidi ya mmoja, Mzee ana wake 3, na wote wanaishi eneo moja au boma moja na wamama ki umri wanakaribiana na watoto pia, kwa UJINGA wako huu huwezi kuilea hio family kamwe. wote mnao support hii style naweza sema ni watoto wa mama..

Mambo yote mnajadiliana kushauriana bado UAMUZI NI WA BABA hata kama utakuwa tofauti kwa wote, cha msingi yeye ni kuwaelimisha sababu za yeye kuamua vinginevyo.
Mkuu ukiona mada inashabikiwa sana na wanawake basi jua kuwa imebeba madhaifu makubwa ya wanaume........Alichokiandika mtoa mada ndio hali halisi ya wanaume wengi walivyokuwa makondoo kwenye familia zao......ni jambo la kusikitisha sana.......
 
Kweli kabisa mkuu, DUNIA SASA IKO HATARINI inaendeshwa na wanawake, Mzee zima kichwa cha family unadiliki kusema haya ? ? sidhani kama ulilelewa na baba wewe,

Haya ndio matokeo ya single mama,

HAO WOTE WANAOKUWEKEA LIKE NI WANAWAKE NA BADO WANAKUONA BOYA LAO
Mkuu nadhani ulikusudia kumquote mtoa mada.....
 
Hii mada imenishangaza na kunipa uoga wa namna dunia inapoelekea......kumbe ndio dunia inaenda mrama.....kwa sababu wanawake ndio wameshika usukani......
Sababu zinaweza kuwa nyingi ikiwemo
1.Style ya maisha tunayoiga kupishana na uwezo wetu kiuchumi ngazi ya family,
2. Hakuna Ndoa sikuhizi lengo pesa tu
3. Nahisi kwa watoto 100 wanazaliwa 40% ni nje ya ndoa yaan HARAMU, 50% malezi upande mmoja
4. Mapungufu au ukosefu wa maadili, mira na desturi ikiwemo IMANI
5. Uchumi kwa ujumla wake

nakuendelea.......
 
Yote yanawezekana mkuu.....lakini hali inatisha mkuu.....
 
NO HAPANA Hayo ni mapungufu makubwa, na nahisi wale wote wanao support hii dhana watakuwa wamelelewa na family zenye mapungufu ya upande wa baba,

Aidha mama ndie alikuwa na Bargaing Power kuliko Baba, kama vile Single mother n.k

Inasikitisha sana kuonyesha dhahiri jamii yetu kubwa inaelekea huko, Wa BABA wenye sifa stahiki za kulea family ni wachache sana sana na wanaendelea kupungua kila siku, matokeo yake ndio haya.

Fikilia zipo family zenye wake zaidi ya mmoja, Mzee ana wake 3, na wote wanaishi eneo moja au boma moja na wamama ki umri wanakaribiana na watoto pia, kwa UJINGA wako huu huwezi kuilea hio family kamwe. wote mnao support hii style naweza sema ni watoto wa mama..

Mambo yote mnajadiliana kushauriana bado UAMUZI NI WA BABA hata kama utakuwa tofauti kwa wote, cha msingi yeye ni kuwaelimisha sababu za yeye kuamua vinginevyo.
Bahati mbaya hujaelewa hata concept ya hii thread. Hizo no FACTS..niwe nazipenda au huzipendi...haijalishi. It's the way of the world..Bahati mbaya sijalelewa na mama wala dada.. hivyo observation zako kwangu haziaapply kwangu
 
Sasa mtu wewe umelala hujitambui yeye yupo macho anakuangalia, kwanini usimuogope??
 
Back
Top Bottom