UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel

Wazazi msiwape watoto wenu mzigo wa kununua upendo wenu kwa kuhangaika ili kuwapa pesa na mali. Upendo haununuliwi. Tabia ya kudai malipo kisa mliwasomesha au kuwazaa na kuwatunza huo ni uhuni. Kuwapenda watoto wenye vipato au wanaowapa vijizawadi ni dalili moja wapo inayoharibu ile dhana kuwa wazazi mnaupendo wa kweli kwa watoto wenu. Itaonekana kama propaganda tuu lakini uhalisia ni kinyume.

Kuna wale wenzangu na miye wanaokwambia hakuna upendo wa kweli kama upendo wa mama. Hakuna kitu kama hicho. Wanaosema hivyo ni wale wanaoongozwa na mihemko.
Taikon kama nitaulizwa katika huu ulimwengu nani mwenye upendo wa kweli basi karata yangu itadondokea kwa wanaume waliooa.

Yaani mume akimpenda mke. Huo ndiyo upendo wa kweli. Hizo nyingine ni drama. Kumpenda mtu ambaye hauna uhusiano naye, undugu naye na pengine humfahamu kabisa, huo ndiyo upendo halisi. Yaani upendo unaokuja naturally siyo upendo wa wajibu. Najua kuna watu watabisha hapa. Lakini huo ndiyo ukweli.

Upendo wa wazazi waliyowengi ni upendo wa faida. Wengi tumezaa watoto ili baadaye waje watusaidie. Hatuzai kwa sababu tunawapenda watoto bali tunazaa kwa sababu ya manufaa yetu ya baadaye. Mzazi anakusomesha siyo kwa sababu anakupenda, siyo kwa sababu ati uwe na maisha mazuri, wengi wanasomesha ili baadaye uwasaidie. Yaani kwa kifupi unaitwa uwekezaji au biashara.

Yaani mzazi wako alivyokuwa anakusomesha ni kama mfanyabiashara anayefanya biashara ya kupanda miti ya mbao. Anategemea siku moja atapata return ya uwekezaji wake. Huo hauitwi upendo, hiyo inaitwa biashara!

Kadiri unavyokua mkubwa ndivyo utakavyoona kuwa hata wazazi wenyewe hawana upendo wa kweli. Uhakika uliyokuwepo ni kuwa upendo wa kweli upo baina ya mume na mke/yaani baba na mama. Ila upendo wa wazazi na watoto au watoto na wazazi huo hauitwi upendo bali wajibu😊😊.

Mume kumpenda mke siyo wajibu wala siyo jukumu lake bali hiyo inatokana na silika/hulka ambayo huja automatically/naturally. Na huo ndiyo upendo wa kweli.

Ni kama vile mtu kuwa na njaa. Huo siyo wajibu bali ni silika/hulka ya mwanadamu. Huwezi sema unaowajibu wa kusikia njaa. Hiyo haipo. Ndivyo ilivyo kwenye upendo. Upendo wenye wajibu siyo wa asili. Upendo wa kweli ni ule wa mke na mume. Yaani huo unakuja automatically/naturally.

Unaweza kujitahidi kuuzuia lakini ndani yako unaumia, ni kama kuizuia njaa, lazima uumie. Huwezi fundishwa kumpenda mke au mume hiyo haipo kwa sababu inakuja naturally. Lakini watu hufundishwa kupenda watoto wao, au kupenda wazazi wao huko makanisani na misikitini. Na jambo lolote la kufundishwa huwezi liita la asili.

Upendo ni maamuzi ya uchaguzi yanayokuja automatically/naturally kutoka moyoni na kujikuta unampenda na kuvutiwa na mwanamke au mwanaume fulani. Lakini yote hayo hufanyika kutokana na utashi na vile mtu apendavyo mtu atakayempenda aweje.

Mzazi hakujua atakuzaa wewe. Pengine alitamani kuzaa mtoto wa aina fulani mwenye maumbile fulani, au mwenye akili fulani, lakini hiyo huwa siri ya mzazi mwenyewe. Hata hivyo zile sifa mbaya ulizonazo mara nyingi mzazi mmoja hupenda kuzihusisha na upande wa mzazi mwingine.

Halikadhalika, mtoto hukutegemea kama ungezaliwa na baba au mama uliyenaye. Watoto huweza kuwa walitamani kuwa wangekuwa na wazazi wa namna fulani, wenye maumbile au hali fulani ya maisha. Hizo ni siri za watoto.

Ndiyo maana kuna kanuni na sheria isemayo, "Waheshimu wazazi wako." Sheria haijasema wapendeni wazazi wenu. Kwani inajua kuwa upendo unahusu uchaguzi na siyo amri/siyo lazima. Kwani haukuamua wala kuchagua huyu awe baba au mama yako, wala yeye hakuchagua, ila imetokea tuu.

Hii ni tofauti na upendo wa mume na mke. Hawa wao walichaguana, waliamua wakiwa na akili timamu. Hivyo kwao kupendana kwao ni amri/lazima. Yaani nature itawalazimisha kufanya hivyo automatically.

Sisi wanaume ndiyo wenye upendo wa kweli hasa kwa wake zetu. Kwani ndiyo tunauwezo wa kuonyesha mapenzi yetu kwao pasipokutegemea malipo hasa ya vitu/pesa au mali. Sisi tunachohitaji ni heshima na utiifu.

Sisi wanaume tunaweza kutunza mke na watoto kwa furaha kubwa miaka nenda rudi pasipo kudai malipo ya fedha au mali. Hiyo ni mpaka tunakufa. Tunachohitaji ni heshima na utiifu tuu ambapo hayo hayapo kwenye mambo ya biashara.

Lakini ni wazazi wachache sana ambao wanaupendo wa namna hiyo. Narudia wazazi wachache Sana. Yaani kwenye wazazi 100 basi mzazi mmoja ndiye mwenye upendo wa kweli. Hao 99 waliobaki ni wafanyabiashara wanaotaka malipo ya fedha au mali au kitu chochote kinachoshikika (materials).

Siyo ajabu ukipata tuu kazi, badala ya kufurahia kazi yako unaweza kujikuta kwenye mtihani mzito sana. Kwani baadhi ya wazazi huweza kukuletea shida mpaka ukajuta. Ni kama walikukopesha sasa unatakiwa kurudisha marejesho.

Shida inakuwa kubwa zaidi kijana wao wa kiume mwenye kazi akipata mke, hapo ndiyo mambo huweza kuwa mabaya zaidi. Wengine hufikia hatua ya kuwaloga watoto wao. Wengine kuwavurugia nyumba za vijana wao.

Nina uhakika mzazi wako akiambiwa achague mtu mmoja ambaye anampenda katika maisha yake yote hawezi kukuchagua wewe. Tena mkiwa watoto wengi ndiyo Kabisa.

Wazazi wa siku hizi wengi ukiona anakupenda ujue ni kwasababu kuna kitu unampatia, na kitu hicho ni materials aidha iwe pesa au zawadi ndogondogo, na huo hauitwi upendo bali ni biashara.

Hata hivyo wazazi wetu wengi wapo hivyo au tupo hivyo kwa sababu ya umasikini. Ingawaje wapo wazazi matajiri lakini bado wanatabia ya kutokupenda watoto wao.

Upendo wa wazazi mara nyingi unafanana na upendo wa mke Kwa mume wake. Yaani kama hutoi materials basi uwezekano wa kupendwa unakuwa ni mdogo sana. Lakini kamwe hautofikia upendo wa mume kwa mkewe.

Sisi kama wazazi tunaowajibu wa kuwapenda watoto wetu pasipo kutarajia malipo ya fedha na mali. Wao kutuheshimu na kututii kama wazazi wao inatosha.

Tuwekeze kwenye miradi, tuweke akiba ili uzee ukitukuta utukute tukiwa tumejiandaa vyema. Watoto wetu watupe vitu kwa mioyo yao kadiri wanavyowiwa na sisi tusiwe na kinyongo kuwa mbona hawatupi vingi kama sisi tulivyotoa kwao. Huo hauitwi upendo bali ni biashara.

Tuwapende watoto wote bila kujali hadhi na hali zao. Wote ni watoto wetu. Hii itamfanya nao wapendane. Kwani ninyi mtaonyesha mnaupendo wa dhati bila kujali hali zao za vipato. Mbona sisi wanaume tunawapenda wake zetu kwa mioyo yetu yote bila kujali hali zao za vipato?

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Subiri uzae ndiyo uje na hili andiko, kwa sasa liko obsolete.

Yani oa, kisha mpate mtoto, umshuhudie since akiwa tumboni anavyomvuruga mama yake, siku anazaliwa, akiwa na wiki, mwezi, mwaka, miaka nk. Hii kitu inajenga upendo wa ajabu mnoo kati ya mzazi na mtoto.

Hata kama wewe wazazi wako walikuneglect ila wanao hautaweza kufanya ivo unless itokee a very strong bond breaker...
 
Subiri uzae ndiyo uje na hili andiko, kwa sasa liko obsolete.

Yani oa, kisha mpate mtoto, umshuhudie since akiwa tumboni anavyomvuruga mama yake, siku anazaliwa, akiwa na wiki, mwezi, mwaka, miaka nk. Hii kitu inajenga upendo wa ajabu mnoo kati ya mzazi na mtoto.

Hata kama wewe wazazi wako walikuneglect ila wanao hautaweza kufanya ivo unless itokee a very strong bond breaker...

Nilichoandika ni kile kilichopo kwenye jamii.

Unampenda Kwa sababu ni mwanao. Huo sio Upendo. Huo ni wajibu😂😂
 
Umesema kweli kabisa wazazi wa kibongo wanazaa ili wasaidiwe na usipowasaidia wanakulaan
Na kweli kina mama wanapenda waume zao kuliko watoto wao

Mtoto ukifanikiwa kila mzazi anataka atambulike Kwa jina lako.
Mfano Baba Ommy Dimpo, ilhali anawatoto wengine zaidi ya kumi ambao ni apeche Akili.
Au Mama Kanumba, ilhali wapo watoto wengine.

Hata mtoto mwenye kipato akifariki mama au Baba husikia uchungu zaidi kuliko akifa apeche Alolo.
Rejea Mama Kanumba, kafiwa na watoto wawili lakini haachi kumtaja Kanumba kuwa huyo mtoto ndiye kamuuma zaidi.

Lakini Kwa upande wa Mume na Mke hiyo ni tofauti Kabisa. Hata kama Mkeo ni Masikini, kifo cha mke achana nacho
 
Naomba kujua tofauti kati ya wazazi na baba
Umemtaja mwanaume kama mtu mwenye upendo wa kweli anayehudumia mkewe, watoto na pia kuwasomesha na kila kitu kwa upendo tu
Lakini umewashutumu wazazi kufanya hivyo kwa ku expect matokeo
Swali: huyu mwanaume anasimama kama nani sasa
 
Kaka umenijibu maswali yangu mengi sana natamani huu ujumbe umfikie baba yangu aliyenitenga nikiwa sina kitu na kuwajali watoto wengine waliokuwa wakimtumia fedha na zawadi mimi kapuku hata kuulizwa uhali gani ilikuwa mtihani ila Mungu mkubwa amenifanikisha nipo nchi ya ahadi alivyopata taarifa naishi nje ndio akaanza kunitafuta kwa juhudi kutaka yaishe ila najua kabisa upendo hana na mimi ila amenitafuta kwasababu anataka pesa zangu hili andiko lako limenigusa na kunibariki sana .. kiuhalisia wazazi wengi wa wenye roho za kimaskini wapo hivyo na wamefanikiwa kuvuruga watoto wao sana.. nilichojifunza kwenye maisha haya ni kwamba upendo ni utu sio vitu. Mungu akutunze kamanda karibu sana canada.
 
Back
Top Bottom