Ukweli kuhusu tukio la tuhuma za rushwa monduli dhidi ya Masyaga Matinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu tukio la tuhuma za rushwa monduli dhidi ya Masyaga Matinyi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Juma Kilaza, Jun 17, 2012.

 1. J

  Juma Kilaza Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Watanzania wenzangu,

  Nachukua nafasi hii, kwa masikitiko, kutoaTamko fupi kama kaka wa MASYAGA MATINYI - mdogo wangu anayenifuatia kwa baba namama yetu. Aidha, mimi pia ni mtumiaji wa jina la ubini la "MATINYI" na ndiyomaana baadhi yenu mlihisi kwamba ni mimi niliyekamatwa na TAKUKURU. MASYAGA anamwanasheria wake na itakapobidi atatoa Tamko la kisheria lakini ili kuondoaukungu nimeona ni heri nitoe UFAFANUZI wa tukio zima. Zaidi, ni uzalendo wanguna mapenzi yangu kwa haki, na wanaonifahamu wanalijua hili vema.

  Naomba nirudie: KESI NZIMA YA RUSHWA DHIDIYA MASYAGA NA WENZAKE NI UONGO. Huu si utetezi tu bali pia ni UKWELI wakilichotokea. Hakuna kuficha: TAKUKURU ina tatizo.

  Ipo sababu kwa nini imenichukua muda mrefukulisemea jambo hili. Natamka wazi kwamba nina uhakika na hiki nikisemacho;mwenye hadithi tofauti akawasaidie TAKUKURU mahakamani. Kwa kuzingatia kuwakesi haijaanza kusikilizwa, Tamko hili kamwe si kuingilia uhuru wa mahakama(contempt of court) bali ni kuingilia uovu – siyo utendaji - wa TAKUKURU. MASYAGA hakuizungumzia rushwa wala hongo; hakuiomba na wala hakuipokea.
  Kwa wanaofuatilia vizuri habari za Tanzania, MASYAGA ni mmoja wa waandishi wa habari mahiri nchini linapokuja suala lakutetea na kulinda maslahi ya taifa letu na anaijua vema sekta yetu yamaliasili. Sisemi hivi kwa kuwa ni mdogo wangu, bali kwa kuwa maandishi yake yapo kama uthibitisho. Itakumbukwa kwamba wiki moja kabla ya tukio hili alitoahabari nyeti ambayo sitashangaa nikisikia baadaye kwamba ndiyo imemponza.

  MUHTASARI WA AWALI
  Alhamisi Juni 14, 2012, mtandao wa JamiiForum na televisheni ya TBC walisambaza habari duniani na nchini kuhusu tukiola kukamatwa kwa waliowaitwa waandishi wa habari watatu akiwemo MASYAGAMATINYI, Mhariri wa gazeti la Rai. TBC1 walimkariri kamanda wa TAKUKURU wa mkoawa Arusha akidai kwamba akina MASYAGA walimwomba rushwa mtumishi wa Tanescohuko Monduli ya sh. milioni 1.8 na kisha kupokea sh. 200,000 kamakianzio. TBC1 waliinukuu TAKUKURU wakidai eti waandishi hawa walikuwa wakimbanaMtanesko huyo kwa tuhuma kwamba hana sifa za kushika nafasi aliyonayo.

  Ijumaa MASYAGA na wenzake walifikishwamahakamani mjini Arusha na kusomewa mashitaka ya kuomba rushwa ya sh.milioni 1.5 na siyo sh. milioni 1.8 tena na eti walizipokea sh. 200,000.TAKUKURU haikueleza kwa nini kiwango kimebadilika.

  Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambayo nakalayake ninayo kibindoni, mtuhumiwa wa pili amebambikiziwa kosa la pili lakumchukulia MASYAGA huo mzigo wa rushwa. Watuhumiwa wote watatu, wengine wakiwani MWITA CHOMETE na BORA BIDIGA, wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tenaJuni 29, 2012. Tunaishukuru mahakama ya Arusha na mwendesha mashitaka waserikali kwa kuiheshimu haki.

  KILICHOTOKEA
  1...Mtanesko ANDREA MEZAanalalamikiwa na jamii kujihusisha na ufisadi wa magogo ya miti ya stimu nandiyo tatizo lililowapeleka akina MASYAGA kwake pamoja suala la sifa zakezilizompa nafasi ya msimamizi wa mafundi wa TANESCO Monduli.

  2...Mtuhumiwa wa tatu, BORA, simwandishi bali ndiye aliyemwambia MASYAGA kwamba kuna tatizo Tanesco Monduli.Hata kama MASYAGA angetaka hongo, ni wazi kwamba asingeweza kuomba na kupokeambele ya mtu aliyemstua kuhusu suala hili la mistimu. Hii ni common sense tu.

  3...Tatizo lilianzia kwenye kitimutimu cha Mtanesko ANDREA na watu walioko Arusha ambao walikuwa wakimpigiasimu kumtisha kuhusu mambo yake ya mistimu. Hatimaye aliwatumia sh. 400,000zinazodaiwa kuwa ni za TAKUKURU kwa M-PESA na wakazipokea na kukubaliana kujakubeba zingine Alhamisi asubuhi. Wakati akina MASYAGA wanakwenda ofisini kwake Alhamisi asubuhi, ANDREA kwa ujuha wake, alifikiri ni watu wale wa Arusha, hivyo, akawaambia TAKUKURU mchezo umekamilika na wenyewe wakarundikana TanescoMonduli kwa ushari bila kujua wanafanya nini. Kiongozi wa kundi lao alitokaArusha kuja kufanya operesheni ya kikomandoo.

  4...Kwa staili za ushushushu wasinema za James Bond, TAKUKURU walimpa ANDREA kirekodia sauti na kishawakajificha mahali kininja. Ili kuimarisha ushahidi wakamwambia ANDREAamweke Mtanesko mwingine ofisini mwake. Akina MASYAGA walipofika wakaanza mahojiano na ANDREA huku yule kijana (shahidi) akasisitiza kwamba wamalize mambo kishikaji (lengo likiwa kuwadakisha akina MASYAGA hongo na kupata rekodi ya sauti). MASYAGA akasema HAPANA. Kisheria, kumchomokea mtu afanye uhalifu kama walivyofanya Matakukuru hawa ni uhalifu.

  5...ANDREA na huyu kijana wake wakatoka kuzungumza faragha. Waliporejea yule kijana akamwekea sh. 200,000 CHOMETE mfukoni na yeye bila kuchelewa akazitupa nje ya dirisha. Matakukuru zaidi ya sita wakaingia na kutoa kipigo kikali kwa CHOMETE pamoja na matusi yasiyoandikika hapa. Walimpa kipigo kitakatifu na ameishia kutibiwa kwa PF3. Hawakujali kwamba wangeweza kuua. Ni matumaini yetu kwamba atapona vema. Kisheria, kumpiga mtuhumiwa ili umshikishe hongo mkononi ni uhalifu.

  6...Matakukuru wakaenda kwenyegari la akina MASYAGA kupekua kinguvu (bila kibali) ili kupata zile laki nne za M-PESA. Hawakupata kitu. Wakawapeleka Arusha huku wakiamini kuwa MASYAGA ameshapokea laki nne. Kwa akili nyepesi tu hili lilishakuwa suala la mistaken identity lakini Matakukuru wakachagua kuendelea kuwa brutal,unprofessional, unethical, n.k.

  7... Baada tu ya tukio, kamanda wao mkubwa akawaita TBC1 na papo hapo habari zikafika JamiiForum kimazingaombwe na usiku saa 2:00 ikawa ndiyo habari ya kwanza. Hii ni kinyume cha maadili ya kazi za vyombo kama TAKUKURU, Polisi, Uhamiaji, n.k. Ni uhuni. Huwezi kutangaza kitu unachokichunguza na tena ambacho kimeshatoa dalili kwamba kina walakini. Ndiyo maana TBC hawakuelezwa kuhusu zile lakini nne. Kulikuwa na haraka gani wakati "watuhumiwa wao" walishapatikana? Kwa nini waiite TBC1 pekee– televisheni mbovu ya taifa letu?

  8...Katika hali ya ajabu, TBC1 wameishikilia habari hii kuliko wanavyofanya kwenye habari zingine na kuzua maswali kwamba nini hasa lengo lao. TBC1 walilala na kuamka nayo kwa kadri walivyomudu. Aidha, Jamii Forum - wao ni nani katika mfumo wa utoaji habari za TAKUKURU?

  9...TAKUKURU walipofika Arusha wakaisikiliza ile rekodi. Haikuwa na sentensi wala robo ya neno la MASYAGA kuomba rushwa. Kwenye statement wakakwepa kukitaja kile kirekodia sauti lakini MASYAGA akasema hawezi kusaini mpaka waandike ukweli. Kimsingi alikuwa tayari apigwe hadi kufa lakini siyo kusaini uongo. Alitumia ushujaa kuilinda haki yake. Mahojiano yaliisha saa tano usiku na watuhumiwa wakawekwa rumande kusubiri majaliwa ya siku ya pili. Kwa kuheshimu ukweli wa tukio, ni hakika hii ilikuwa unlawful confinement. Huwezi kuwaweka watu ndani baada ya kuwasukumia kosa la uongo, tena kwa kipigo, mateso na matusi. Hiyo ndiyo TAKUKURU yetu.

  10...Ijumaa asubuhi TAKUKURU wakawapeleka mahakamani na suala la sh. laki nne wakaliacha. Kwanini? Aidha, zile sh. milioni 1.8 zikabadilishwa na kuwa sh. milioni 1.5 kwenye hati ya mashitaka. Kwanini? Hata hivyo, gazeti la MAJIRA limechagua kuandika sh.milioni 5; hili ni tatizo jingine kabisa. Si vyombo vingi vya habari vilivyoishadidia habari hii zaidi ya TBC1 kwenye siku ile ya kwanza kutokana na umakini wa wahariri wake.

  11...Kule Jamii Forum kuna wahusika wengi walionunua kesi hii huku wakiwa hawajui chochote cha ndani.Upumbavu wetu wa siku zote Watanzania. Jamii Forum walijifanya kwamba hawaijui TAKUKURU na vioja vyake. Mtanzania mwingine aliyeko Japan naye aliamua kusambaza habari hizi kwa nguvu zake zote kila sehemu aliyoweza; yuko Japan lakini ana kiherehere cha mambo ya Monduli.

  12...Bado kuna maswali kuhusiana na kiu hii ya usambazaji na utangazaji huu wa habari hizi kwa nguvu zote iwapo ina uhusiano na binadamu walioandikwa na MASYAGA hivi karibuni. Kama tujuavyo, mbuga zetu ni shamba la bibi lakini ni upumbavu kuamua kwamba Watanzania wote tukae kimya. TAKUKURU walikuwa na shida gani ya kuwasukumia raia wema mambo haya, tena kwa kipigo, uongo, utesaji, utangazaji wa kihuni, n.k.? Kunasiri gani?

  HITIMISHO
  Hizo laki nne ziko wapi? Kwa nini hazizungumziwi tena? TAKUKURU waeleze tangu lini wakawa na haki ya kumshikisha mtu pesa kwa kipigo. Matakukuru wakitoe kirekodia sauti walichompa Mtanesko waona kamwe wasiseme eti hakuweza kurekodi vema.

  TAKUKURU waoneshe jinsi MASYAGA alivyopokea laki nne huko M-PESA kwani aliwapa simu zake kwa hiyo wasilikwepe hili na ndio jambo walilolidai baada ya kumkamata. TAKUKURU waeleze ni kivipi MASYAGA angeomba rushwa mbele ya mtu aliyekuwa anamlalamikia Mtanesko huyu. TAKUKURU waeleze mikono ya MASYAGA ilikuwa wapi mpaka ikabidi apokelewe hongo na CHOMETE wakati wote walikuwa hapo hapo?

  TAKUKURU waeleze kwa nini walianza na madaiya sh. milioni 1.8 na kesho yake wakapunguza hadi sh. milioni 1.5? TAKUKURU watudokezee tujue uhusiano wao na mwandishi wa TBC1 na mhariri wa TBC1 kwamba hata habari ikiwa na mashaka bado itarushwa tu mfululizo kwa siku kibao - wana ubia gani kwenye hili tu? TAKUKURU waeleze kwamba wana maslahi gani ya kumlinda mtu anayelalamikiwa na wananchi kwamba anafanya uhalifu?

  Mpenda haki yeyote aelewe kinachoendelea na mzushi yeyote aseme lake lakini MAHAKAMA itamaliza mchezo wote.

  Asalam Aleikum!
  MOBHARE MATINYI, WashingtonDC, Juni 17, 2012.
   
 2. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  :couch2:
   
 3. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  tata, taya ng'ola, wewe uko mbali sana, vita umeikimbia, uko USA leo unaongelea habari za TZ, pole sana ndg yangu, unajifanya kama haujui mfumo huu kandamizi, eti unahoji bila hoja, rudi TZ acha hadithi za alinacha.

  Wenzako tuko vitani, tuko kwenye uwanja wa mapambano, pale kwenu Kemange sijui umemuachia nani apakomboe. Mwisho watuhumiwa tunajua wamesingiziwa, tuiache mahakama ifanye kazi yake, unaikumbuka kesi ya JERRY MURO?
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mobhare ulicho kielezea hapa ni ukweli mtu na mimi ndo mmoja wapo na mimi ndiye niliye lazimishwa kupokea hiyo rushwa hakika nilipambana sana ingawa nilipokea kipigo kikali sana mpaka nikafikia hatua ya kusema kwa nini mnaniua kwa kunipiga kwa kitu ambacho mnanibambikizia.

  Na haya nayo yazungumza hata wakileta kile kinasa sauti kitaeleza kila kitu juu ya hawa watu kunipiga na jinsi walivyokuwa wanatoa matusi mazito ambayo ayawezi elezeka hapa au kuandikika hapa jf, na waliniacha kunipiga baada ya wao kuniona nimeanguka chini na kuishiwa nguvu kwa sababu kuna mmoja wao ambaye anaitwa shirima alinipiga teke ambayo ilinifanya kusikia tumbo linawaka moto kwa ndani ndipo nilipokaa chini mwenyewe nakuishiwa nguvu.

  Nilisikia sauti kwa mbali mtu akiagizwa nenda nje ulete zile pesa na ndipo watu walijitokeza wengi sana kutaka kujua kulikoni badaye nilikuwa nasikia mtu akitaja number za pesa lakini aliyekuwa akitaja sikumuona kwa sababu walikuwa nje.

  Baada ya hao kumaliza hilo nikaamliwa nisimame nakuweka saini kwenye ile karatasi waliyokuwa wakiandika zile number ndipo nilipokataa kusaini nikiwaeleza siwezi kusaini kitu ambacho sijui ni nini ndipo bwana mmoja kwa jina aliitwa pale anaitwa shirima akanipiga kofi nikapepesuka na kuanguka chini.

  Basi wakaona juu hili siwez kusaini wakatutoa nje na hayo mengine yakafuata ambayo mobhare ameandika hapo lakini namshukuru Mungu amesimamia hili mpaka sasa hivi niko nje kwa dhamana.

  Najua Mungu atatenda haki.
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Matinyi, JF unaishambulia kwa kosa lipi? Hivi JF ni gazeti? Walio-report event walitakiwa kukaa kimya? Watu walitakiwa kuzuiwa kushiriki mjadala huo? Unadhani JF inaandika?

  chomete, wewe ni member hapa kwa takribani miaka 2, mweleze Mobhare abadilike, JF haiandiki! Maoni ya watu kamwe hauwezi kuwa ndo msimamo wa JF, na hatuwezi kuwaziba midomo watu kisa aliyeguswa ni 'flani'.

  Kwenye hoja:
  Nikupe pole kwanza chomete kwa yaliyokusibu, yawezekana ni mara yako ya kwanza lakini nipende kukufahamisha kuwa 'hali ndivyo ilivyo'. Kuueleza ukweli bayana kunasaidia kuujulisha ulimwengu juu ya unyama unaofanywa na wale tuliowapa dhamana, lakini endapo uliyoeleza ni ya kweli. Inasikitisha sana!

  Ulikuwa na voice recorder?
   
 6. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Haya mapambano dhidi ya udhalimu wa rasilimali zetu yana safari ndefu sana. Hata kama mtu ana mapungufu yake lakini kwa hili Takukuru wamechemka na wametumika na wakatumika vibaya bila kufanya kazi kitaaluma.

  Wakiendelea hivi watapoteza imani kwa umma na kwa kweli wanawaacha wezi na mafisadi wakubwa wanahangaika na kuwalinda wezi na wahujumu uchumi. Ziko wapi kesi za twiga, kesi za meremeta, kagoda, Rada, Richmond, Kiwira, na kadhalika?

  Takukuru wanatia aibu sasa.
   
 7. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  :couch2::couch2::couch2::couch2::couch2::flame:
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe unalalamika kwa kuishambulia JF hujui kama hii ni forum huru, humu wanajadiliwa kina JK, Nyerere, Mkapa, Slaa, Lipumba, Mbowe sembuse wewe hata watu hatukufahamu.
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mobhare ni mtu makini na mwandishi mkongwe, lakini hapa ameteleza. Apime mambo kwa kina na aangalie na kuona kinachotokea. Wachangiaji humu wako huru na wako wenye hoja na wengine hawana hoja. Wako wanaotoa maoni na wako wanaotoa taarifa ya tukio. Bahati mbaya wachangiaji hawana nafasi ya kutafuta upande wa pili kama ilivyo traditional media kama TV, radio na magazeti. Hapa kama alichofanya Juma Kilaza na Chomete ndio upande wa pili unavyotakiwa kufanya si kulaumu. Mwisho naamini Masyaga atapambana kupata haki yake na media itaamsaidia.

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sikuwa na kinasa sauti ila wale maafisa wa takukulu ndiyo walikuwa na kinasa sauti ambacho walimpa bwana meza baada ya ile purukushani kutoa na kumalizika afisa mmoja wapo alimuomba bwana meza kinasa sauti na kusema kazi yangu imekamilika
   
 11. z

  zamlock JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni kweli na swala hapa tusimshambulie mobhare kwa kuteleza kuiandika jf vibaya.

  cha msingi hapa tueleze kwa nn takukulu wanatetea mafisadi wezi wa mali za nchii hii alafu wanakuja kupambana na watu duni kama mimi ambaye sina hata sauti kwenye nchi hii hata sifahamiki. Na pasipo wao kufikili juu hili kuwa ni uzembe na kutokuwa makini ndo wa kwanza kusema wamefanya kazi nzuri sana.

  Nikikumbuka kauli alizokuwa anatoa Shirima ambaye ni afisa TAKUKURU hakika nashanga sana
   
 12. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilidhani JamiiForums inapigwa vita na 'waserikali' pekee kumbe hata 'wamatinyi' ikigusa maslahi yao wanahoji JF ina uhalali gani kumwaga habari zao jamvini.

  Nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa, tumefikia pabaya. Mihimili yote ya dola (hata huu unaojiita muhimili wa nne) imeoza kwa rushwa. Takukuru naona hata aibu kuwazungumza hapa. Mahakama zetu usidhani ni mahakama za marekani, hapa mkuu wa wilaya tu anaweza amuru hukumu isomwe atakavyo yeye achilia mbali viongozi wakuu waandamizi na wafanyabiashara, labda kama 'mmejipanga'!

  Binafsi pamoja na kuwa mwathirika wa rushwa ilokuwa ikifanyika ktk vyombo vya habari, ktk hili kutokana na maelezo yako, 'watakukuru' wamei handle ishu hii kama 'unskilled labours' harakaharaka nawafananisha na mgambo wa jiji la dsm (wasio na sare) wakishambulia huku wakilazimisha kuingiza hela za moto mfukoni mwa mtuhumiwa wakat wale wengine(wa jiji) wanakusachi ili wakuibie.

  Ndipo taifa lilipofikia! TV ya serikali ndo balaa ubabaishaji kila hatua. Tutarealize kwamba hatuna uelekeo soon
   
 13. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Cha kusikitisha ni kwamba hali yetu hapa nchini sasa imekuwa tete. Wale wote wanaokuwa mstari wa mbele kusimamia na kutetea rasilmali zetu ndio wanaokuwa wa kwanza kupata suluba (vipigo, mateso hata kuuwawa) na vyombo vya dola, vilivyopata dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria kutoka kwa WANANCHI.

  TAKUKURU nayo iko mstari wa mbele kukandamiza nguvu ya umma dhidi ya ufisadi wa rasilmali na nchi yetu. Hii ndiyo kazi ya TAKUKURU? Ndio. Kwa mujibu wa mafisadi.

  Lakini tusikate tamaa. chomete usife nguvu. Tuko nyuma yako. Tutafunga na kukuombea. Yaliyomkuta Jerry Muro sasa yamewakuta ninyi. Mtapona. Mungu yu nanyi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu chomete na Matinyi poleni sana.

  Nakumbuka Matinyi amewahi na amekuwa akiandika habari nyingi sana kuhusu uovu unaofanywa kwenye mbuga zetu likiwemo suala la vitalu. Pia nakumbuka makala yake moja kumhusu mtu mmoja ambaye nasikia ilikuwa ateuliwe kuwa waziri wa maliasili na utalii mwaka 2010 lakini kutokana na makala ile iliyohusu mambo ya vitaku na maliasili basi mamalaka ya uteuzi ilisita. Hiyo vita ni kubwa hata Maige amekiri hivyo isije ikawa ndio kisa cha MAtinyi kupata misukosuko.

  Namuamini Matinyi kama mwandishi mahiri asiyetafuna maneno kwenye makala zake. Hizi habari za wanyamapori hasa Loliondo nakumbuka ziliwahi kuandikwa na Katabalo (RIP) kwenye gazeti la Mfanyakazi miaka hiyo lakini mwisho wa Katabalo ulikuwa wa ajabu ajabu.

  Matinyi pambana na isirudi nyuma kama hutapata taji duniani utavikwa taji mbinguni.
   
 15. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  pole sana chomete, ukombozi una ghalama, tetea, pigana na mfumo huu, hakika iko siku tutashinda, kwa kipindi hiki uwe na moyo wa subira, tunajua umedhalilishwa sana machoni mwa watanzania ila mungu yuko pamoja nanyi, nuru ya matumaini imetimu, hakika tuko pamoja, mwisho jaribu kunitumia namba yako. siku njema ndg yetu na pole sana
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hivi takukuru wana haki ya kumpiga mtu? nilifikiri kazi yao ni kuchunguza na kuwakamata watuhumiwa wa rushwa lakini sio kwa kutoa kipigo
   
 17. z

  zamlock JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sawa ndugu yangu nashukuru number yangu ndiyo hii 0765714359
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  chomete

  Nimeisoma story yote na naomba kutoa yaliyo moyoni mwangu (sio lazima yawe sahihi). Hili suala ni kama ile kesi ya Muro.

  Kama lilivyokuwa suala la Muro, inaonekana ni kweli kulikuwepo na uombaji wa rushwa kutoka upande wa media lakini kukurupuka kwa TAKUKURU kukaharibu kila kitu. Kama ilivyokuwa kwa Muro, kuna vitu vingi sana kwenye maelezo aliyotoa Matinyi mkubwa ambavyo havijakaa sawasawa kuni-convince kuwa TAKUKURU walimbambikia jamaa. Inaonekana rushwa iliombwa lakini mtego ukategwa vibaya.

  Huu ni mtizamo wangu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mlolongo wa hii issue ni kwamba huyu Meza alishawai kuwapa watu wasiojulikana pesa kwa njia ya m pesa na baada ya matinyi kupewa taarifa ikambidi afuatilie na ndipo alipo mpigia simu bwana Meza akimuomba waonane ofisini kwake Monduli.

  Sasa kilichofuata hapa huyu bwana Meza akawataarifu watu wa PCCB na wakampa pesa za moto awatumie, bwana Meza akafanya hivyo. Kwa hyo tulivyofika pale jamaa wakajua watu wetu wamekuja nani lazima tuwashike kabla ya hapo walikuwa na ushahidi wa number ya simu ambayo walitueleza kuwa walitutumia hizo pesa na ndipo wakawa na simu zetu kama mtego na walipokuwa wanatuhoji walikuwa wanatuliza hiyo number ni ya nani kati yetu!

  Walipokuja kutambua wamechemka walianza kusemezana kuwa tumechemka uenda hawa watu siyo tuliokuwa tunawatafuta na swala la pesa hii laki mbili. Baada ya kuona hatujawaomba rushwa ndipo wakatumia nguvu kubambikie pesa za moto kwa sababu walijua tayari hata wakitukagua watakuta ile number waliyoitumia pesa tutakuwa nayo
   
 20. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Vipi Edo, hana mkono humo?
   
Loading...