engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Kinachonishangaza mimi ktk hili swala ni pale nilitumiwa sms ktk mail yangu kuwa nami nimeshiriki kusambaza habari ya waandishi waliokamtwa na rushwa huko arusha na sasa wamediriki hata kutoa habari ktk wanabidii na mabadiliko kuwa nipo kizimbani kwa swala la uchochezi na uongo nimeshangaa sana, kwanini wahusika wasiwaweke kizimbani TBC1 waliotangaza habari hiyo mara 2 na sisi kama wananchi kuzileta habari hizo JF na mitandao mingine kwani tunaelewa kuwa TBC1 ni chombo cha umma na habari zake huwa ni za uhakika na ukweli kwa hiyo mwana mtandao ana haki ya kuchukua habari toka TBC1 na kuwahabarisha wengine.
Mimi natumia jina halisi niletapo habari huwa naweka chanzo, muda na siku, ili kama kuna mtu anadhani habari ni ya uongo ama ni ya uchochezi basi anaweza fuata chanzo ili kujiridhisha, lakini kilichotokea ni kwamba muhusika hakutaka kufuata hilo na kuweka habari kuwa Eng Ibrahim Mtolera kizimbani kwa habari za uongo na uchochezi. Inasikitisha sana kiukweli.
Nimejiandaa na najipanga sasa ili niweze kuona wanasheria wanasema vipi juu ya hili
Kwa upande wangu nawapa pole wahusika lakini tuache tabia ya kutishana na kuombeana mabaya