Ukweli kuhusu Shahada zetu za Chuo Kikuu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Wengi tumesoma na tunajiendeleza kielimu ili ku secure nafasi zetu za ajira maofisini.
Elimu zetu zimekuwa ni matumbo joto kwa mabosi tuliowapita kisomo.
Elimu zetu zimetujengea maadui wengi ambao usoni tuwaonapo tunawaona wamejaa tabasamu kumbe mioyoni mwao wamesha tuweka kwenye jeneza.
Elimu hii alituletea Mr. Mkoloni ili tupate kazi za kizungu, kama ukarani na ualimu.
Tangu zama hizo hadi leo wengi tunakuwa tunasoma ili tuajiriwe.
Wasomi wa leo ni waoga sana, wanaogopa kujiajiri, wanaogopa ku take risk.
Kuna haja sasa vyuo vyetu na sisi wenyewe tubadilishe namna yetu ya kufikiri.
Tuifanye elimu yetu ituopatie uwanja mpana wa ajira. Sio tushupalie tu ajira rasmi, ila tuvuke pia mipaka twende kwenye ajira isiyo rasmi.
Tukawekeze na kukuza vipato vyetu binafsi na uchumi wa taifa letu kwa ujumla.
 
Bujibuji siku hizi umekua,unaongea poiti tu,safi. I couldn't have said it any better! Ila yote hii kwa maono yangu yanaanza na uongozi mbovu unaoendesha nchi!
 
Mi mwenyewe kinachonikwaza ni hofu, naogopa kuingia kwenye sekta isiyo rasmi, si unajua tena ukizoe kukinga mwisho wa mwezi pia na hutu tu allowance tunatutia wazimu.
 
Siyo kweli kwamba wahitimu wanaogopa kujiajiri,tatizo ni nini kinafundishwa ili baadae wahitimu waweze kujiajiri wao wenyewe...hii ni techinical problem
 
Buji, thank you for the useful thread.
Leo umeamkia kwa mwanamke gani? Maana umetoa shule ya maana kweli, usimuache huyo (just a joke)
 
Bujibuji the great, asante sana kwa changamoto, binafsi wacha nijichunguze nafsi yangu ni kipi kipaumbele changu, kujiajiri au kuajiriwa.
 
Mkuu umenena na ndio maana wengi wetu mara tu baada ya kustaafu hali huwa mbaya sana. Mungu akuzidishie fikra pevu.
 
Tatizo wasomi wengi wa Tanzania wanasoma kwa kukariri ili waje wajibu mitihani lakini ukweli wanatoka University bado vichwa maji matupu, naomba nieleweke nimesema baadhi.
Ujerumani kuanzia Darasa la 4 wanafunzi wanaanza kusomea kazi mpaka level atakayoishia. ndio maana wazungu wajanja wakija hapa kuwekeza hawataki habari ya vyeti, wanajuwa IQ ndio cha msingi, na hata wao wenyewe wengi wao hawana hata Diploma lakini upstairs ni zaidi ya PHD. huu ndio ukweli wenyewe.
 
Mkuu umenena na ndio maana wengi wetu mara tu baada ya kustaafu hali huwa mbaya sana. Mungu akuzidishie fikra pevu.

ndio maana wastaafu wengi huifa siku chache baada ya kustaafu
 
Tatizo wasomi wengi wa Tanzania wanasoma kwa kukariri ili waje wajibu mitihani lakini ukweli wanatoka University bado vichwa maji matupu, naomba nieleweke nimesema baadhi.Ujerumani kuanzia Darasa la 4 wanafunzi wanaanza kusomea kazi mpaka level atakayoishia. ndio maana wazungu wajanja wakija hapa kuwekeza hawataki habari ya vyeti, wanajuwa IQ ndio cha msingi, na hata wao wenyewe wengi wao hawana hata Diploma lakini upstairs ni zaidi ya PHD. huu ndio ukweli wenyewe.
Nakubaliana na wewe kabisa, mi pia nimelishuhudia hilo ulilosema kuhusu IQ!
 
safi sana bjbj,wasomi inabidi wabadilike,na kuanzia july kuna wimbi kubwa wataingia mtaani kutoka vyuoni hapo sijui itakuaje.
 
Huwa nachukia sana watanzania tunapopenda kujidanganya, Kwa Elimu gani utakayoitoa hapa nchini itakayoogopwa na mabosi wako labda kama unafanyakazi kiwanda cha urafiki wakati bado vikiwa chini ya serikali. Hatuna cha kuogopwa hatuna tunachokisoma na hayo makaratasi tunayoyakimbilia mwisho wake tutaishia kama ilikoishia fedha yetu tunayodai inalinda uchumu unaokua. Tutapata Phd na kurudi huku kwetu tuwaajiri kama wafagiaji na wasafisha vyoo. Hayo mnayodai wenzetu mmeshuhudia huko mliko yanamwisho. Great thinkers gani badala ya kuchambua hali kwa upana wanatuletea usharobaro hapa mimi ningetegemea kwa pamoja tuwapigie kelele hawa walioshika dau tunajidanganya. Na hata hizo international na academy zetu zilizojaa wakenya hazitusaidii kitu. mtoto huyo huyo ukimlinganisha na wa shule ya kata utashangaa, wa kata ana content hana lugha wala haendi na wakati, lakini huyo wa international school ni lugha tu lakini content hakuna. wauza bar wa kenya na school drop outs wakatufundishie watoto wetu, ratiba za shule zimejaa masaa ya PE na swimming na sisi tunaona sawa tu, sasa naamini huyo aliyetuloga kafa. Shule pekee zenye uwezo wakutuzalishia hazishikiki kwa fees , hivi chuo gani kwa leo hapa Tanzania zaidi ya vile vya uganga unaweza kusema kinatoa products za maana, haya nenda huko primary bila ya ISM, IST, Hopac, Agakhan, Academic umeliwa, ESACS sijui wamekuaje hata majengo yao bado yamebaki kama ma godown wakati mwenye shule ni msomi aliyebobea. Nilitaka kusahau na Tumusiime. Hapa sijazizungumzia zile za dini kama marian boys for obvious reasons. Sasa wewe jiangalia hizo tunaziweza? licha ya fee hata access. utashangaa watanzania wasomi wamepeleka watoto wao kwa wafanyabiashara vilaza wa academic ndio wawaelimishie watoto wao. Utashangaa ardhi wanayo, pesa wanazo tatizo lao hawana uwezo wa kufikiri, wavivu, wamezoea kufanyiwa na hawathamin wala kuelewa elimu ni nini maana wao pia wamesoma lakini hawajaelimika. Watanzania AMKENI AMKENI AMKENI la sivyo mtawageuza watoto wenu mananmba katika nchi yao wenyewe, dhambi kubwa
 
Back
Top Bottom