Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Hujajibu swali nililokuuliza na swali ulilojibu sijakuuliza.

Unaelewa maana ya methali ya Kiswahili inayosema "Usiige tembo kunya, utapasuka msamba"?

Facebook walioanzisha waliparamia biashara wasiyoiweza?

Unafananisha Shirika la Ndege Tanzania na Facebook?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Hiyo ya facebook ni mifano tu, katika kujenga hoja huwezi kukwepa mifano.

Hakuna anayeiga kunya kwa tembo, waliopewa majukumu ya kufufua shirika la ndege wanajua wanalolifanya, ila sisi humu JF ni kama tunataka kuwapotezea malengo waliyonayo kiutendaji.

Sisi humu JF ni kama tunawawangia katika kitu wanachokifanya, kuyumba kwa biashara ya ndege kwa sababu ya corona sio kumuiga tembo kunya. Njia wanazotumia Ethiopia kuendesha shirika lao sizo zinazotumiwa na Kenya, sizo zinazotumiwa na Tanzania, hivyo tuepuke kuishi kwa kukariri zile stori tunazozisoma magazetini na katika maongezi ya jioni wakati tukiwa bar.

Hakuna aliyeparamia biashara asiyoiweza, tatizo mtu mmoja anakuwa hamjui yule aliyepewa dhamana ya biashara, hili suala la corona ni upepo tu na utatulia na maisha yataendelea kama kawaida.
 
Kwa hiyo unafananisha vitu visivyofanana ilimradi ufananishe tu?

Serikali imeingilia biashara isiyoiweza, ndiyo maana hata inakataa ukaguzi wa kihasibu kwenye shirika la ndege hata kabla ya Corona virus.

Unataka kulazimisha tuige tembo kunya, tutapasuka msamba.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Kwa hiyo unafananisha vitu visivyofanana ilimradi ufananishe tu?

Serikali imeingilia biashara isiyoiweza, ndiyo maana hata inakataa ukaguzi wa kihasibu kwenye shirika la ndege hata kabla ya Corona virus.

Unataka kulazimisha tuige tembo kunya, tutapasuka msamba.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Kuhusu serikali kuingilia biashara isiyoiweza, naweza kuthubutu kukwambia kwamba hujui unaloliongea, waache wanaoelewa wanafanya nini wafanye wanachokielewa.

Kila mtu akisikilizwa maoni yake basi hakutakuwa na haja ya kuwa na wachache wenye kupewa majukumu makubwa kwa niaba ya taifa.

Tupasuke msamba mara ngapi?, unajua tangu tupate uhuru tumeshafanya blunders ngapi?. Mbona bado kama taifa tunaendelea kuwepo?. Uoga ule ule unaoufanya umaskini uendelee kuwepo miongoni mwetu.
 
Umekubali shirika la ndege litapata hasara, halafu unalazimisha serikali inaweza hii biashara?

Kwa kuwa huko nyuma tumefanya blunders, basi tuendelee kufanya blunders?

Kwa kuwa Rwanda huko nyuma wakifanya mauaji ya kimbari, waendelee kufanya mauaji ya kimbari?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Umekubali shirika la ndege litapata hasara, halafu unalazimisha serikali inaweza hii biashara?

Kwa kuwa huko nyuma tumefanya blunders, basi tuendelee kufanya blunders?

Kwa kuwa Rwanda huko nyuma wakifanya mauaji ya kimbari, waendelee kufanya mauaji ya kimbari?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Kupata hasara sasa hivi sio kigezo cha serikali kushindwa kufanya biashara ingawa siamini kwamba serikali moja kwa moja inafanya biashara hii, serikali ni mdhamini wa ATCL, kwa maana kwamba hawa wakishindwa wanaweza kupewa hata Precision Air waendeshe, TCAA inamtambua hazina kama mdhamini.

Tatizo letu ni kupenda kutoa hukumu za mapema, mwenendo wa kudorora leo hii sio kigezo kwamba mwakani kutakuwa na mdororo, wenye kuendesha mashirika makubwa ya ndege wangekuwa ni waoga mashirika yao yasingekuja kuwa makubwa na maarufu.

Corona ni tatizo la muda tu, joto likiwa kali katika ya mwaka huu hiki kirusi kitakufa na kupotea mazima, mizunguko ya watu kutoka nchi moja kwenda kwingine itaanza upya.
 
Ujinga wako ni kunilaumu mimi kutoa hukumu ya mapema.

Halafu na wewe unaenda kutoa hukumu ya mapema kusema Corona ni tatizo la muda tu joto likizidi litakwisha.

Do you even know what you are advising me to not do is the same thing you are doing?

You are contradicting yourself.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Wewe lazima ni mmoja katika genge linalohujumu uchumi wa nchi!! Hizo ndege mpya zikija zitatia hasara shirika kwani hakuna
Wateja wa kuzipanda!! Ndege hazitakiwi kukaa ardhini zinatakiwa kuwa angani!!
Nenda Airport kajithibitishie ndio uje hapa. Hizi issue huwezi kuandika ukiwa umejibanza Kyela huko.
 
Ujinga wako ni kunilaumu mimi kutoa hukumu ya mapema.

Halafu na wewe unaenda kutoa hukumu ya mapema kusema Corona ni tatizo la muda tu joto likizidi litakwisha.

Do you even know what you are advising me to not do is the same thing you are doing?

You are contradicting yourself.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Mkuu yanayotokea yanapita tu. Hali ikitulia mashirika yote ya ndege yataanza kufanya biashara kama zamani tu.

Hawa hawa ATCL watasimama tena kama watakavyosimama wengine.

Siwezi kuliombea dua mbaya shirika letu la ndege eti kisa kipindi ni kigumu kibiashara sababu ya magonjwa ya muda mfupi.
 
Dhana nzima ya serikali kujishirikisha kwenye biashara ya ndege imepitwa na wakati.

Ndiyo maana walioanzisha usafiri wa ndege na waliotupita kwenye biashara Wamarekani husikii serikali ikawa na shirika la ndege.

Sisi hatujui tunaenda au tunarudi, mara tutaifishe mashirika, mara tubinafishe, mara tutaifishe, mara tubinafsishe.

Kwa mark time hii hatuwezi kuendelea.
 
Serikali imejiweka kama mdhamini tu katika suala zima la uendeshaji wa ATCL, ndio maana rais alisema ikiwa na wao watashindwa basi ndege watakabidhiwa wengine waziendeshe.

Serikali inaitumia hazina kama guarantee ya lolote litakalotokea, waendeshaji ni wengine. Kuwa na subira mkuu wa Oysterbay ya zamani.
 
Pole sana mkuu, jifunze kupokea na kuyakubali maoni yasiyofanana na ya kwako.

Huo ndio ukomavu wa kifikra, vinginevyo huna tofauti na kina Maria Sarungi, wanakosoa kila siku lakini wakikosolewa wana-block watu.
Basi Maria Sarungi ndiyo kati ya tunu za Taifa. Kama huwezi ku appreciate Tanzania kuwa na wadada shupavu na wenye akili kama Maria, Fatma Karume, Halima Mdee, Dr Vicencia Shule, Rebecca Gyumi, Mwanaamis Singano etc basi wewe siyo mtu makini.
 
Serikali imejiweka kama mdhamini tu katika suala zima la uendeshaji wa ATCL, ndio maana rais alisema ikiwa na wao watashindwa basi ndege watakabidhiwa wengine waziendeshe.

Serikali inaitumia hazina kama guarantee ya lolote litakalotokea, waendeshaji ni wengine. Kuwa na subira mkuu wa Oysterbay ya zamani.
Mdhamini tu maana yake nini?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Mdhamini tu maana yake nini?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Huwezi kulisajili shirika la ndege kama mamlaka ya anga TCAA hawawezi kuhakikishiwa uwezo wako kifedha kwa maana ya akaunti za pesa zenye kuonyesha uwezo wako kujiendesha. Kwa upande wa ATCL hazina ndio mdhamini wake ndio maana zinaponunuliwa serikali inazikabidhi wakiwepo mashuhuda kutoka hazina.

Fastjet walipoambiwa wajipange ili waweze kupewa upya leseni mojawapo ya matatizo yalikuwa ni masuala haya ya nani ni mdhamini wa kampuni kifedha ili leseni iweze kutolewa.

Mkuu Kiranga wenye kufanya hizi shughuli kwa sasa wanao utaalam wa haya masuala sio watu wanaopelekeshwa na wanasiasa kama ilivyozoeleka enzi za miaka ya nyuma.
 
Basi Maria Sarungi ndiyo kati ya tunu za Taifa. Kama huwezi ku appreciate Tanzania kuwa na wadada shupavu na wenye akili kama Maria, Fatma Karume, Halima Mdee, Dr Vicencia Shule, Rebecca Gyumi, Mwanaamis Singano etc basi wewe siyo mtu makini.
Anayekuwa makini kwangu kwako anaweza akawa pimbi tu. Anayeweza kuwa makini kwako kwangu anaweza kuwa pimbi mwingine tu.
 
Back
Top Bottom