Ukweli kuhusu Mishahara Serikalini

Ukweli kuhusu Mishahara Serikalini

Ujanjaujanja unahusika kwa karibu. Formulae ni simple 'they pretend to pay you, you pretend to work'

Madaktari oyeeeh!
ukweli ni kwamba mishahara serikalini imepitwa na wakati. Laki tatu unaishije hapa mjini???
 
Tanzania Government Salary Scales for Teachers, Health
Sector and Other sectors as of 2011/2012

TGHS B1 - 472,000/=
TGHS C1 - 682,000/= Health Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGHS D1 - 792,200/=

TGTS B1 - 244,400/=
TGTS C1 - 325,700/= Education Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGTS D1 - 469,200/=

TGS B1 - 221,600/=
TGS C1 - 309,800/= Other sectors, incl. Agriculture & Livestock
TGS D1 - 446,100/= (Certificate, Diploma & Degree consecutively)

Kila siku hi hawa hawa tuuu, vipi kuhusu sectors nyingine kama Engineering?
 
ukweli ni kwamba mishahara serikalini imepitwa na wakati. Laki tatu unaishije hapa mjini???

na hiyo ndio sababu itafanya rushwa iendelee...mshahara kiduchu na wakati huo huo gharama za maisha zinapanda
 
hapa utaona wahasibu, maafisa maendeleo/ustawi, watu wa ardhi, engeners, HRO n.k hawajatajwa cjajua nao hal ikoje.
 
Asalaam Wana-JF,

Nikiwa kama Mtumishi Serikalini na ambaye ninahusika na masuala ya Mishahara ya Watumishi, nimesikitishwa na namna ambavyo baadhi ya wadau wanavyojaribu kupotosha umma kuhusu mlinganyo wa mishahara ki-sekta!

Hivyo nachukua fursa hii kuleta ukweli kuhusu tofauti ya viwango hivyo ki-sekta/ki-kada. Angalieni kiambatanisho mtaona summary niliyoiandaa ambayo inatoa picha halisi kuhusu viwango hivyo! Viwango hivi ni kwa watumishi wanaoanza kazi (vyeo vya kuanzia).

NB:
Summary hii ni kwa mujibu wa waraka wa mishahara serikalini wa mwaka 2011/2012, sikuweza ku-attach waraka huo kwani una muhuri wa "Confidential".

Thanks!



Umenifanya nitabasamu....Mhuri ndio confidential au content?? weka doc yote ndio naweza kuiamini then tuingie kwenye mjadala.
 
Kweli jamaa yangu unanifurahisha sana. Katika awamu hii ya ****** bado kuna confidential? Katika kipindi ambacho siri nyingi zimvuja ni cha ****** sasa una shaka gani? Vasco Da Gama yeye hana siri kabisa. Kama ishu ni mhuri you can hide it and scan the document. Nina mashaka na na huhyu jamaa ni mamluki amekuja kupotosha ukweli. Ili tuamini upload hizo document ukiwa umefuta mihuri. La sivyo huaminiki.
 
Kuna kazi inaitwa law? au education? hapa tunaongelea kazi zinazoangukia katika mikondo hiyo mkuu.
 
NB:
Sikuweza ku-attach waraka huo kwani una muhuri wa "Confidential".

Thanks!

Mkuu MpiganiaUhuru,
Hata Documents za EPA na nyaraka alizokuwa anatumia Dk Slaa Bungeni zilikuwa na Mihuri ya Confidential tena ya mihuri ya moto na wino mzito lakini ililetwa hapa JF. Kwa hiyo usiogope kitu. Siku hizi hakuna Confidential Documents!

 
Mnapo ongea kuhusu hiri kumbukeni kuna kodi hapo hivyo take home itakuwa pungufu' ukitoka kukatwa kodi kwenye mshahara unakuta tena kodi kwenye vifaa vya madukani na vyakula'hapo hujalipia kodi ya pango la kuishi kumbukeni na mfumuko huu wa bei,sisi wafanyakazi hata kumiliki gari ni ndoto labda uwe mwizi' tunatembea na viraka hadi matakoni nani atakaye tusaidia?.
 
udogo wa mishahara ya kada nyingine usitumike kupuuza madai ya msingi ya watu wa AFYA.kilio chao sio udogo wa mishahara ya kada nyingine, wameongelea yao. Katika madai yao hawajasema mishahara ya walimu au maafisa ugani ni mikubwa. Wanachodai hela wanayolipwa haiwatoshi/hailingani na kazi pamoja na hatari wanazokutana nazo.hizo taaluma nyingine nao kama wanaona wanalipwa kiduchu watoe madai yao.ila sio sawa kabisa kusema degree ualimu wanalipwa hivi na diploma afya wanalipwa vile, kwa hiyo sio haki kwao kudai nyongeza.kuna ukweli mmoja ambao najua wengi hawatopenda kuubali.WATU WENGI KAMA SIO WOTE WANAOSOMA AU WALIOSOMEA KADA ZA AFYA WALIPENDA/NI NDOTO ZAO KUSOMA TAAALUMA HIZO TANGU WAKIWA WATOTO,SIO LAST OPTION,HAWAENDI HUKO KWA KUKOSA MBADALA,KITU AMBACHO NI TOFAUTI KABISA NA UALIMU NYAKATI HIZI,WATU WANASOMA KWA SABABU HAWANA JINSI,NDIO YENYE QUALIFICATION CRITERIA ZA CHINI,hawana mpango na taalum hiyo,kwa hiyo hata mapambano ya kuboreshewa hali zao wanayafanya kwa usanii,ili madocto wanafanya kweli.
 
Tanzania Government Salary Scales for Teachers, Health
Sector and Other sectors as of 2011/2012

TGHS B1 - 472,000/=
TGHS C1 - 682,000/= Health Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGHS D1 - 792,200/=

TGTS B1 - 244,400/=
TGTS C1 - 325,700/= Education Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGTS D1 - 469,200/=

TGS B1 - 221,600/=
TGS C1 - 309,800/= Other sectors, incl. Agriculture & Livestock
TGS D1 - 446,100/= (Certificate, Diploma & Degree consecutively)

Duh .. sijukua. hawa wa Tshs 221,600 gawa kwa siku 30 gawa kwa dola rate (Tsh 1600) = $ 4.6 per day (just over global poverty line)!
 
Nchi ya ujanjaunja viongozi nao wajanjawajanja,unadhani kuna maendeleo. Ni km wimbo wa DEFAO Birika ya chai ya maziwa ya moto najenga mwili,kikwembe moja kushona kushone nerea......Takula nini.....
 
Kwa upande wa sector ya afya, salary scale hizi hasa kwa degree ni kwa nursing, pharmacy, haematology na shahada nyingine za miaka minne. Kwa dakatari anayeanza kazi scale yake ni TGHS E1 ambayo ni laki tisa ushee kama sijakosea, hivyo mtoa mada scale ya daktari hapo haipo,

You are right!
 
Therefore ?

Naomba ieleweke kuwa madhumuni yangu kuweka hii taarifa hadharani ni mawili:
  1. Kuondoa upotoshaji juu ya tofauti za mishahara ki-sekta (kwamba Kilimo/Mifugo wanaongoza kwa mishahara mikubwa, wakati ndio wanashika mkia)
  2. Kuonyesha hali halisi ya mishara ya watumishi wa Umma ili mjue ni kwa nini watumishi hao hawana Mori ya kufanya kazi. Muda mwingi wanautumia kutafuta namna ya kuishi! Otherwise, they can't survive! Si mnaona jinsi mishahara ilivyo midogo?
 
NB:
Summary hii ni kwa mujibu wa waraka wa mishahara serikalini wa mwaka 2011/2012, sikuweza ku-attach waraka huo kwani una muhuri wa "Confidential".Thanks!
Mtu safi hafichi wala hajifichi. Watanzania tumechoshwa na Confidentialities. Watumishi wa serikali kuanzia raisi hadi msafishaji choo, wote wanalipwa kwa pesa za walipa kodi na vyanzo vyengine kutoka rasilimali zetu, iweje leo mlipa kodi afichwe kujua/kuona mishahara anayowalipa? Nikiingia kwenye website yoyote ya nchi makini, masuala ya mishahara na marupurupu yamewekwa hadharani kiasi kwamba hata mimi nisiyekuwa raia wa nchi hiyo ninayaona, Tanzania kulikoni na SIRI hizi zisizokwishwa?
 
Back
Top Bottom