Ukweli kuhusu Mishahara Serikalini

MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
777
911
Asalaam Wana-JF,

Nikiwa kama Mtumishi Serikalini na ambaye ninahusika na masuala ya Mishahara ya Watumishi, nimesikitishwa na namna ambavyo baadhi ya wadau wanavyojaribu kupotosha umma kuhusu mlinganyo wa mishahara ki-sekta!

Hivyo nachukua fursa hii kuleta ukweli kuhusu tofauti ya viwango hivyo ki-sekta/ki-kada. Angalieni kiambatanisho mtaona summary niliyoiandaa ambayo inatoa picha halisi kuhusu viwango hivyo! Viwango hivi ni kwa watumishi wanaoanza kazi (vyeo vya kuanzia).

NB:
Summary hii ni kwa mujibu wa waraka wa mishahara serikalini wa mwaka 2011/2012, sikuweza ku-attach waraka huo kwani una muhuri wa "Confidential".

Thanks!
 
Attachments

  • Salary Scales Summary.pdf
    5.7 KB · Views: 3,670
Tanzania Government Salary Scales for Teachers, Health
Sector and Other sectors as of 2011/2012

TGHS B1 - 472,000/=
TGHS C1 - 682,000/= Health Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGHS D1 - 792,200/=

TGTS B1 - 244,400/=
TGTS C1 - 325,700/= Education Sector (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
TGTS D1 - 469,200/=

TGS B1 - 221,600/=
TGS C1 - 309,800/= Other sectors, incl. Agriculture & Livestock
TGS D1 - 446,100/= (Certificate, Diploma & Degree consecutively)
 
Tunashukuru kwa kuleta ukweli huu maana yule aliyeleta zile taarifa za mwanzo alidanganya kupita kiasi
 
sio vizuri kuonyesha mshahara wa baba yangu any way mbona hela zenyewe ndogo kuliko tunavyotumia
 
Hapa ndio umechefua kabisa mkuu ona: mtu mwenye certificate ya health (ambaye ni Form 4 tu) anapata mshahara mkubwa(i.e 472,000/=) kuliko mtu mwenye degree ya kilimo/livestock au mwalimu, (ambaye anaweza kuwa ni Form six/Diploma holder plus 3 or 4 years of Bsc/BA) anayepata 446,100/ and 469,200/=, respectively. Tatizo langu au letu? ni kwamba kwa nini watu wawili waliograduate mwaka mmoja na Qualifications sawa , say MA Finance, Mmoja akaajiriwa TRA na Mwingine TANESCO wanalipwa mishahara tofauti?
 
ukweli ni kwamba mishahara serikalini imepitwa na wakati. Laki tatu unaishije hapa mjini???
 
Hapa ndio umechefua kabisa mkuu ona: mtu mwenye certificate ya health (ambaye ni Form 4 tu) anapata mshahara mkubwa(i.e 472,000/=) kuliko mtu mwenye degree ya kilimo/livestock au mwalimu, (ambaye anaweza kuwa ni Form six/Diploma holder plus 3 or 4 years of Bsc/BA) anayepata 446,100/ and 469,200/=, respectively. Tatizo langu au letu? ni kwamba kwa nini watu wawili waliograduate mwaka mmoja na Qualifications sawa , say MA Finance, Mmoja akaajiriwa TRA na Mwingine TANESCO wanalipwa mishahara tofauti?

Mkuu hapo umeongea jambo la msingi. Kwa nini mishahara ya serikali hata kwa kada moja haifanani?
 
elimu na kilimo ndo mishahara midogo zaidi

Sasa linganisha na unyeti wa kazi, nani atakayekua daktari either wa binadamu au mifugo ikiwa hajafunzwa vizuri na mwalimu? wote wanategemeana, serikali inataka kutugawa jambo ambalo litaleta tabu baadae. haki itendeke...
 
Vp mishahara ya sector zingine kama engineering and technology, law, humanities e.t.c
 
Ndio maana WALIMU wanadharauriwa sana kuonekana wao ndo maskini na kazi mbaya/mbovu kwa sababu ya Mshahara mdogo.Inakuwaje wote msome degree ,miaka 3 taaluma tofauti baada ya mwaka wewe MWALIMU ni maskini wenzako wanaendesha magari?MWALIMU anaweza kujenga nyumba miaka 15 ,wakati Mwenye Accounts TRA anajenga nyumba kwa mwaka 1? HUU NI UJINGA WALIMU AMKENI USINGIZINI.
 
Kinachonishangaza mimi ni kuwa mwl amemfundisha mpk rais lkn anadharulika. Tanzania bwana yote yanawezekana.
 
Asalaam Wana-JF,

Nikiwa kama Mtumishi Serikalini na ambaye ninahusika na masuala ya Mishahara ya Watumishi, nimesikitishwa na namna ambavyo baadhi ya wadau wanavyojaribu kupotosha umma kuhusu mlinganyo wa mishahara ki-sekta!

Hivyo nachukua fursa hii kuleta ukweli kuhusu tofauti ya viwango hivyo ki-sekta/ki-kada. Angalieni kiambatanisho mtaona summary niliyoiandaa ambayo inatoa picha halisi kuhusu viwango hivyo! Viwango hivi ni kwa watumishi wanaoanza kazi (vyeo vya kuanzia).

NB:
Summary hii ni kwa mujibu wa waraka wa mishahara serikalini wa mwaka 2011/2012, sikuweza ku-attach waraka huo kwani una muhuri wa "Confidential".

Thanks!
Mimi sikubaliani na wewe kabisaa. umesahau kuwa uwe kwenye shirika la umma, taasisi yoyote ya serikali, serikali za mitaa au serikali kuu na kada nyingine yoyote ya serikali, wote mnalipwa kwa kutumia fedha za umma ambazo asilimia kubwa hutokana na kodi za wananchi. TOFAUTI ZA MISHAHARA KWA KAZI ILEILE, KIWANGO KILEKILE CHA ELIMU NA UZOEFU ULEULE NI KIKUBWA MNO HASA UKILINGANISHA NA MISHAHARA YA MASHIRIKA YA UMMA. tofauti zapaswa kuwepo lakini sio kwa kiwango kikubwa namna hiyo tena kuwe na vigezo maalumu vinavyotumika kufikia tofauti hizo. hay sasa mwangalie Dactari wa degree akiajiriwa na TBS uone mshahara atakao anza nao. kweli sungura ni mdogo ila hatugawani sawa
 
Ni kweli kabisa na huo ndio udhaifu wa serikali yetu maana hakuna mantiki kabisa ya mishahara ya watumishi wenye sifa zinazofanana kupata mishahara tofauti ati kwa sababu huyu yupo sekta ya umma na huyu yupo taasisi, lakini wote pesa zinatoka hazina.
Kama serikali ingekubali kufuta posho zote na kuwekwa kweye mishahara kama baadhi ya mashirika yanavyofanya, uwajibikaji ungeongezeka, tofauti na sasa maana moja ya tatu ya pesa nyingi zinakwenda kwenye posho, wna wanazozipata hizo posho ni wenye madaraka makubwa.
 
Kwa upande wa sector ya afya, salary scale hizi hasa kwa degree ni kwa nursing, pharmacy, haematology na shahada nyingine za miaka minne. Kwa dakatari anayeanza kazi scale yake ni TGHS E1 ambayo ni laki tisa ushee kama sijakosea, hivyo mtoa mada scale ya daktari hapo haipo,

Back
Top Bottom