Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Kibongo bongo ni hela nyingi sana.. Ila kwa Marekani gharama za maisha ziko tofauti sana sana na bongo…
Nchi Kama marekani kiwango Cha chini kulipwa kwa saa ni dola 10. Ndio kiwango kilichopitishwa na serikali yaani hizo ndio zile kazi mbaya mbaya Kama kufagia barababara au kurudisha vile vitorori vya supermarket ndani ..Sasa ukipiga masaa 14..manake unadola 140.ni sawa na 300000tsh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemaliza mkuu kila kitu opened....
Tatizo wengi tunasikia stor tu na kujilipua , unatumia gharama kubwa alafu ukifika kule jau tu bora kukomaaa tu hapa bongo nina uzoefu na nchi za magharibi kutoboa siyo kazi ndogo na kule ndo hamna uhuru kabisaaa kutengwa sana kama mfungwa tu kwa wazungu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umeenda mbele kutafuta maisha/hela au umeenda kutaka kua huru kama wazungu?

Ukitaka kua huru bora ubaki tu huku Igunga boss.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za humu wa wadau wa JF,

Nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa neema na baraka nyingi ambazo ametupa na kikubwa zaidi ni afya njema na maarifa mazuri aliyoturuzuku. Lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Great thinkers wote wa JF ambao walitoa mawazo yao juu ya Mpango wangu wa kuzamia Nchini Marekani mara baada ya kupata Visa ya nchi hiyo.

Nafahamu wapo watu ambao walitamani sana kujua nini kilichojiri baada ya mimi kufika USA na kilichoendelea baada ya kuzamia huku Ughaibuni. Niwakumbushe tu kidogo kuwa nilisafiri tarehe 15 August mwaka huu 2019 kwaajili ya kuhudhuria mkutano ambao ulifanyika na nilihudhuria Nchini Marekani katika mji wa Washington DC ambapo ilinichukua siku 3 kukamilisha kile nilichotumwa na ofisi yangu kukikamilisha.

Nakumbuka watu wengi wa JF walinipa ushauri baada ya kumaliza mkutano nirudi Bongo kwa sababu sina pa kuanzia Marekani ila kwangu mimi hiyo haikuwa sababu ya kunizuia nisizamie Marekani.Kiukweli Marekani ni kuzuri mno japokuwa sijawahi kwenda nchi yeyote hiyo ndio Mara yangu ya kwanza tangu nizaliwe ila sidhani kama kuna nchi nzuri kuliko Marekani hapa duniani,Ni kuzuri nashindwa hata kuelezea kwa kweli.

Mara baada ya kutuma ile Post hapa jukwaani kuna jamaa alinitafuta Private kabla ya kuruka akanipa mchongo akaniambia hapo Marekani hapafai akasema atanipa njia niende Canada ila nikifika nijiripue kama mkimbizi wa Kisomali ndivyo Wazanzibari wengi hufanya hivyo na alinitumia Makaratasi ya Somalia niyasome ili niijue vizuri Somalia kuna maeneo Somalia wanaongea kiswahili.

Nilipomtumia picha yangu akasema nafanana sana na Msomali hivyo nikifika Marekani nimtafute ataniunganisha na mtu nitakayemlipa anivushe upande wa pili yaani Nchini CANADA. Kwa kweli nilikuwa naogopa sana na niliogopa isije ikawa anataka kunipoteza ila nilikuwa na moyo wa ujasiri na nilishachunguza kuwa watu wengi wanatoka Marekani na kuingia Canada kupitia Illegal borders.hivyo nilijipa moyo na kusema ntaweza.

Hivyo nilipomaliza mkutano nikawasiliana na jamaa mvushaji akasema niende New York atakuja kunipokea Airport,kwasababu nilikuwa na Pocket money ya kutosha nilijiamini sana.Baada ya kufika akanipeleka hoteli fulani akasema atakuja kesho asubuhi, Ilipofika majira ya saa 4 asubuhi akafika akiwa yeye na mwenzake ambae alikuwa ni Mmexico na huyo alienipokea alikuwa ni Mzanzibari.

Kwa hiyo tukapanda bus mpaka sehemu ambapo tulishuka na tukachukua Taxi tukawa tunaenda nikaona msitu tu nilipouliza akaniambia kuwa huku sasa ndio tunaelekea CANADA nikashangaa sana tuliposimama sehemu tukashuka na kukutana na watu watano na wale wawili wakawa saba wakaniambia niwape hela tuliyokubaliana yaani Dollar 3000 ikabidi niwape then tukaendelea na safari nikiwa nahofia kuwa nisije nikawa naenda kuchinjwa na kutolewa viungo vya mwili wangu maana hakuna ninaemjua pale na hata huyo Connector wangu nilikuwa simjui ila ilikuwa balaa la hofu limetanda naona sifiki.

Hatimaye nilifika sehemu nikaoneshwa bendera ya Canada na kuambiwa nenda pale na waeleze kuwa wewe ni mkimbizi kutoka Somalia utasaidiwa.Nikaenda na nikavuka mpaka nilipofika nikapigwa pingu palepale kwa kosa la kuvuka kinyume na utaratibu.

Itaendelea...

Nitawaeleza siku nyingine baada ya Pale ila kwasasa nipo Canada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuendelee kuwatia moyo wazamiaji ila kiukweli kama huna elimu ya kueleweka Canada utaenda kusota.
ataishia kifanya kazi za warehouse ambazi nyingi zinalipa $16 kwa saa ambapo kwa wiki kisheria utafanya masaa 20 tu. na hapa ndipo linapokuja suala la kuwa na multiple Jobs.
Mkuu US Na sehemu nyingi kwa wiki minimum ni 40Hrs ukiweka overtime wastan hata 50Hrs Kwa wiki
 
Sikupigwa ila sitaki kuwaaminisha watu njia hii niliyotumia mimi maana mimi nilikuwa na msimamo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Iko hivi,unapoingia marekani ukuwa kwenye system za nchi ya marekani.unapokuwa unasafiri popote marekani wanajua kuwa hyu mtu iko wapi na watakutafutia watu.mfano umeenda marekani kwasababu ya shule,ukikarbia kumalzia shule wanaanza kukutumia barua za visa yako kwisha muda wake.na wanajua watakupata wapi maana marekani umeingia una wenyeji wako.kama umepewa siku tatu na ziwe siku tatu unapozidisha wanaanza kufatia kwa wenyej wako na wenyej wako wasipojua ulipo iyo ni kesi kwao.

Ndo umefanikiwa kuingia nchini marekani kwenda canada huwezi kuvuka border ya marekani kuingia canada bila vitambulisho vinavyokutambulisha wewe ni nani na unaenda canada kufanya nini.wanapokuingiza kwenye system zao wanajua kabisa wazi kuwa wewe ni mgeni ulikuja kwa visa ya kutembea hiyo ni kesi nyngine na huwez kuruhusiwa kuingia canada kamwe.

Acha kudanganya watu mkuu,marekani kwenda state nyingine tu lazima uwe na vitambulisha sembuse kuvuka border ya nchi kuingia lazma wawe na taarifa zao na kutoka lazima wapata taarifa zako

Kwaiyo marekani haiwezi kukuruhusu kuvuka border kuingia canada kama wewe uko umekuka marekani kwa njia na vikao mkuu.

Mimi niko marekani,nimeenda canada mara nyingi na nimetembea marekani sehemu nyingi na utaratbu huu wa kusafr naufahamu vizuri sana.

NB:hakuna mkimbizi nchini canada kutokea mpaka wa marekani na sheria ya canada na marekani hairuhusu ukimbiz wa mipakani.

Na kama utakataa nitakuzibishia kwa vitendo.

Na wanaoruhusiwa kuvuka mpaka wa marekani bila ukaguzi ni raia wa marekani ambao wana pasport na ukitoka kuingia canada wanajua kuwa kuna raia wetu ipo kama na hata gari uliotumia utatambulika.hata namba za gari tu wanatambua kuwa gari hii imeshaingia nchi canada au kifika kwenye mipaka ya nchi fulani

Na kama na hili unabisha nitadhibitiha hapa

Marekani kila ktu kipo kwenye system unapofinga tu tayar unashikwa.
 
Ulisoma maelezo yake vizuri asee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa mnafikiri Canada maisha ni Ubwete,siku ukifika ndio utajua Canada ikoje pia watu waliotangulia huwa hawasemi ukweli kwa wenzao wanaotamani kwenda huko,maisha ni expensive labda unaishi miji midogo,
Wewe umewahi kufika hata Nairobi tu??? Yaani unafananisha maisha ya Toronto na kwenu Shinyanga? Una akili kweli wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemaliza mkuu kila kitu opened....
Tatizo wengi tunasikia stor tu na kujilipua , unatumia gharama kubwa alafu ukifika kule jau tu bora kukomaaa tu hapa bongo nina uzoefu na nchi za magharibi kutoboa siyo kazi ndogo na kule ndo hamna uhuru kabisaaa kutengwa sana kama mfungwa tu kwa wazungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watabisha
 
Canada nayo sio mbaya au nchi za scandinavia,na akifanikiwa kujichanganya uraiani. Atafute kazi za kwenye ma-shoprite,za kurudishia bidhaa kwenye shelvu,au kupanga mabox. Hizo kazi ni rahisi tu kuzipata,ksbb ni wenyeji wanaziona za ki-rocko. Mshahara wake mzuri tu,na kazi zenyewe rahisi tu,unalipwa kwa masaa unayofanya kazi. Kwa hiyo ni wewe tu,kama umeenda kutafuta maisha unaweza kuandikisha masaa hata 14 kwa siku,unaacha tu masaa ya mapumziko na kulala. Kwa nini usirudi na hela. Hata huyu atarudi na hela,kama ataamua kurudi

Sent using Jamii Forums mobile app
Point

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom