Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,409
Tunasubiri kujifunza mkuu
Nimemuelewa vizuri sana, ni kwamba sija maanisha nilicho comment.Nahisi Utakua Hujamuelewa Mtoa Mada
Haha hapana mkuu...nenda kahaso...bidii yako tu ndo itakayokuokoa...MAmbo si mepesi kivip mkuu?! Mbona unataka kutukatisha tamaa?
Okay! Sawa broHaha hapana mkuu...nenda kahaso...bidii yako tu ndo itakayokuokoa...
Kumbe kazi zako zile zinakupatia wazungu wa kutosha..HongeraUSA (Boston), UK (London & Birmingham).
In the bucket List for the coming year.- France & Belgium Huku natakiwa nikawakilishe taifa kwenye uwanja wa 6X6 😁 😁
NB: Siendi kuzamia huko anytime nikitaka kwenda napeleka tu kitabu nagongewa tu mhuri.
Hizo nimekutajia nilizokaa mwezi na kundelea.
Zile ambazo nimekaa not more than a week kwa safari za kikazi ziko kibao.
Naomba usiwe tomaso tafadhali
Duh!!!😂😂😂Sasa ulivyojisingizia kuwa ni shoga si itakuwa uliletewa mtu ili apprive na tangu hapo ukawa kweli au?
We unadhani wote ni waoga kama wewe,sie tunaishi popote kwani huko newyork wanaishi maraika hawaishi watu jombaaa,mbona unakuwa muoga dogoExactly my point kiongozi....sasa msikie huyu jamaa Papi Chulo anavyojidanganya... Kule kama ni mzamiaji na huna mwelekeo mzuri utaelewa maisha ni nini....kuna watu wanazurula daily kule newyork hopeless... Kodi tu room standard $2,600...bado chakula,usafir cjui starehe na ugumu wa kupata kazi huo....kule ukienda jipange...
At least Canada mchomoko upo...
hadi wewe nimecheka unavyofuatilia kwa makiniInaendelea lini tena jamani
Sawa wacha niwe dogo lako... Na wala hakuna aliyesema huwezi ishi new York... Mm sio muoga sababu sijawahi ingia marekani kwa mbinu za kuzamia....Ungekuwa na akili ungeuliza watu waliyokwisha kukutangulia ili upate dira fulani ya maisha ya huko.... Unfortunately akili hiyo huna... Unaanza kuita watu wadogo zako....We unadhani wote ni waoga kama wewe,sie tunaishi popote kwani huko newyork wanaishi maraika hawaishi watu jombaaa,mbona unakuwa muoga dogo
Kumbe njaa zenu ndizo zinaichafua nchi yetu,kisa tu mupate kibali cha kuishi Kanada.Habari za leo Wana JF,Natumai mko poa sana na wale ambao hawako vizuri kwa namna moja au nyingine namuomba mwenyezimungu awaondoe katika hali hiyo na awapeleke katika hali nzuri zaidi ili waweze kuendelea na mapambano ya maisha ya kila siku.Nichukue nafasi hii kipekee kabisa kuweza kumshukuru mwenyezimungu,Mwenyezimungu ambae anatupenda sana sisi Wanaadamu na ametuumba umbile zuri kuliko kiumbe mwingine yeyote yule na ametufanya kuwa na akili ya kufikiria na kuamua na kuchagua kile ambacho tunakitaka hivyo hatuna budi kumshukuru.Ntakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawashukuru wana JF ambao wamesoma na kucoment hadithi yangu ya ukweli na sio ya kutunga hivyo nawashukuru sana.
Inaendelea...........
Baada ya kuvuka ile border ya USA na Canada nilikutana na polisi na bila ya kunihoji walinipiga Pingu jambo ambalo lilinishitua sana na moyo wangu ukaanza kwenda mbio nikaona sasa nimejiingiza kwenye matatizo maana sikuambiwa kuwa ntapigwa Pingu niliambiwa ntasaidiwa tu.Nikasachiwa mwili mzima then nikapelekwa kwenye kituo cha polisi,Nilipofika mule ndani nikafunguliwa pingu kisha kikafunguliwa chumba kidogo sana ambacho kilikuwa na Choo chake nikaingizwa ndani kisha nikaambiwa na Polisi wawili wa CANADA nivue nguo zangu zote hivyo kubaki uchi kama nilivyozaliwa kisha wakanifungia mlango wakaondoka.Walipoondoka nikaanza kukiangalia kile chumba huku nikiwa na wasiwasi mkubwa na mawazo nikaona heater na Camera nne nikawasha heater maana kulikuwa na baridi kiukweli nilikuwa katika wakati mgumu sana nilikumbuka nyumbani hasa mama yangu,Watoto wangu,mke wangu na ndugu zangu nikaanza kutokwa na machozi nikikumbuka nilivyosoma kwa shida na kupata kazi na nikawa namudu maisha yangu na kusaidia ndugu zangu nikajiona katika watu wapumbavu mimi ni mpumbavu kwelikweli.Chumba hakikuwa hata na kigodoro hivyo sikuweza kulala Usiku mzima.
Ilipofika asubuhi majira ya saa tatu mlango ukafunguliwa na Polisi wawili wakafungua mlango kisha wakaingia ndani ya chumba changu wakanipa nguo zangu na kisha wakaniambia niwafuate.Tukaingia chumba kingine mulemule ndani nikakutana na Afisa mwengine wa Polisi akaniuliza kwa ukali "Why did you cross the border Illegally?" Nikamwambia kuwa mimi ni mkimbizi kutoka Somalia nimeletwa na Agent Marekani na amenipokea mtu ambae amenileta mpaka hapa akaniambia nivuke ntasaidiwa hivyo wakaniuliza tangu naianza hii Safari nimetokea wapi na nimepita wapi mpaka nimefika hapa,Waliniuliza maswali mengi sana ambayo sitaweza kuyaandika yote humu Pia waliniuliza kwanini nisiombe Asylum USA nikawaambia kuwa nimeambiwa USA hawapokei wakimbizi na uzuri nilishapangwa cha kusema hivyo nilikuwa naigiza vilevile nilivyofundishwa kujibu na wakati wananiuliza walikuwa wanaandika kwenye computer walipomaliza tu wakatoa Karatasi ambayo ilikuwa inaonesha maswali niliyoulizwa na nilichojibu kisha nikaambiwa nitie Signature yangu.
Baada ya hapo nikaambiwa niwafuate Polisi wale wawili walionitoa mule chumbani kisha tukatoka nje nikaambiwa nipande gari hivyo nikaingia kwenye gari ikiwa na Polisi wengine wapya watatu .Gari ikaanza mwendo ambapo nakumbuka ilituchukua masaa matatu mpaka Kufika mji mkubwa kidogo nakumbuka unaitwa Québec ambapo mji huo wanazungumza Sana Lugha ya Kifaransa.Nilipofika Quebec nikapelekwa sehemu kwenye mjengo mkubwa Sana ulivyo kama Hotel nikakabidhiwa kwa Ofisa mmoja mwanamke na akapewa karatasi zangu huku akiaambiwa kwa Kifaransa kisha wakaniaga wale walionileta wakaniambia wananitakia kila la kheri
Mwanamke huyo akaniuliza Je nkilichoandikwa kwenye zile karatasi ni kweli au uongo nikajibu ni kweli,Akatoka akaniletea kitambulisho kinachoonesha kuwa mimi Mkimbizi kutoka Somalia kisha ikapigwa simu kwa Security wakanipeleka sehemu humohumo ndani nikapewa Lotions,Sabuni za kuogea,Shuka na Blanket kisha nikapelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa na watu wawili tu ila kilikuwa ni chumba kidogo ambacho kilikuwa na vitanda vya Double decker viwili yaani kitanda kimoja mmoja analala juu na mwingine chini kwahiyo chumba kimoja hulala watu wanne japo nilikuta watu wawili tu ila ikiwa mtu na mkewe wanapewa chumba kimoja peke yao na kitanda kikubwa.Nilikaa pale mwezi mmoja huku nikapata breakfast na lunch na dinner kwenye Kantini kubwa iliyokuwa na watu wengi Sana ikiwa wengi wao ni Waarabu wa Syria,Yemen na Afghanistan pia kulikuwa na Wasomali wengi na Watanzania ambao wengi walikuwa Wazanzibari na Kutoka Dar ilikuwa nipo peke yangu ila hawakunibagua.
Niliiishi pale kwa miezi miwili huku nikiutembea mji maana tulipewa ticket za bure kwa mwezi mzima na ikiisha muda unapewa nyingine na tulikuwa tunalipwa kwa mwezi pesa kidogo bila ya kufanya kazi.Kwa kweli nilipata marafiki wengi wa Kizanzibar pale kambini na kupeana hope kuwa tutashinda kesi na kupata Papers za kuishi na kukubalika kisheria.Na tulipeana Technic nyingi za kushinda case maana kuna Wazanzibari walijiripua kuwa ni Wasomali na walipoulizwa kwenye Interview ya kesi zao walisema kuwa Walitoa rushwa ili wapate Passport za Tanzania na wengine walisema wao ni mashoga kwahiyo jamii zao zimewatenga na wanataka kuuliwa maana jambo hilo halikubaliki kisheria kwetu na wengine walisema wao ni Wanasiasa hivyo Serikali inawaua na kuwapoteza na wengine walisema kuwa ni Waandishi wa habari na vyeti feki wametengeneza vya Uandishi wa habari kwa kweli Wazanzibari uzamiaji upo kwenye Damu.
Baada ya mwezi mmoja niliitwa kwenye Interview yangu ya kwanza ya kuhojiwa kilichonikimbiza Somalia na nikienda nikahojiwa kwa muda wa masaa 6 na maswali niliyoulizwa ni mengi sana..........
ITAENDELEA................
Ntataja maswali yote niliyoulizwa kwasababu dhamira yangu sio kuwafundisha watu kuzamia ila wayajue maisha halisi ya kuzamia ili mtu akiamua kuja ajue nini kitakachotokea hivyo Kujiandaa kisaikolojia mapema
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mnajifunza ujinga wa kusema uongo na kuipaka matope nchi yenu kisa muishi KanadaLeo nilikuwa nafatilia hii issue tu unatililika vizuri hapa tutajifunza mengi sana Mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
ila dada zao kwenye sekta ya kuuza nyama wapo nyuma sana.Wazanzibar kweli ni mabingwa wa kujilipua, wao ikitokea janga kwao ni fulsa, waandishi wanakamatwa na kuuliwa wao wanaunda vyeti feki na kusepa, kina Lisu wanapigwa lisasi wao ni fulsa Asylum.