Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

mkuu mi nimefanya utafiti na kuja na data... kama una data tofauti na hizi basi zieleze..... hatutafanikiwa kama tutawakatisha tamaa watendaji wanao pigana kufanikisha jambo eti kwa sababu umesikia 179 bi zilizo tolewa kwa zaidi ya miaka 5... ulizia nchi jirani kenya na Uganda kwenye mchakato wao wameisha tumia sh ngapi....

Mkuu,

Umejitahidi kuchanganua.

Lakini kuna matatizo makubwa mawili.

Kwanza, ni jinsi gani fedha (bilioni 180) zimetumika kutoa vitambulisho milioni 2.5 kati ya watu milioni 6 waloandikishwa, ndani ya miaka mitatu.

Hio ni sambamba na matumizi yasio lazima kwa kupanga katika majengo mbalimbali ilhali NIDA wana ofisi pale Kinondoni.

Isitoshe ni kwanini Joseph Makani aliruhusu kununuliwa Computer Servers zaidi ya 100 ilhali kungeweza kuwepo angalau servers 2, labda back up servers zingine 2 na UPS kama 4 hivi na zikatosha, servers 100 za nini?

Pili, utajiri wa baadhi ya walosimamishwa kazi unatisha mkuu, maana kuna mmoja ana nyumba mtaa mzima. Sasa hata kama ni mkopo wa benki ni kwa mshahara gani unaweza kupewa mkopo wa kununua nyumba zaidi ya tatu tena mtaa mmoja?

Hizi zote ni "facts" na zinatafutiwa mbolea ili ziweze kugeuzwa ushahidi kwenye mashtaka.

Kama kutapatikana maelezo ya kuridhisha kutoka TRA, benki zilizotoa mikopo, maafisa mikopo wa mabenki, na michanganuo yote, basi hakutakuwa na shida.

Hivi unafahamu kwamba kuna maofisa wa mikopo benki wamefanya michezo michafu kwenye kusukuma loan applications kinamna? siendi deep.

Tungoje matokeo ya uchunguzi.
 
Uzuri wa Rais wetu akikurupuka huwa anajirudi fasta na kimya kimya. Hapa tunaongea Dr Feisal Issa alikuwa RAS Mwanza tayari yuko ofisini pale Tamisemi Dodoma anachapa kazi. John Wanga, mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Mwanza aliyesimamishwa kwa mbwembwe naye amerudishwa kinyemela.

Tujiulize, kwa nini hawafanyi uchunguzi wa awali kujiridhisha ndio watimue wao wanatimua tu tena wanaita vyombo vya habari? Kwa nini Takukuru wasikamate na kutupa watu mahakamani moja kwa moja? Siasa mchezo mchafu
yaani mpaka sasa sijaona jambo jipya la jpm,..
zaidi ni kusimamisha kaz watu na kuwarudisha kimyakimya,..
kufanya kaz kwa sifa na kudanganya raIA Ndo kumejaa kichwani na ccm,..wanasimamisha kazi watumishi kwa magazeti na rodio
then mwshowe wanawarudisha kimyakimya,..huu ujinga huuu unajua
kifaa cha muhimbili kimetolewa dodoma kikaja muhimbili then wakajifanya kuwa eti wamenunua kipyaqa
huu ujinga,..
ccm ni walewale hata aje nani chma hakibdliki,..huyu wa nida nae kasimamishwa bila uchunguz wala chochote
huu upuuz2
 
Nimesoma Magazeti mbali mbali na kumsikiliza mhe.Rais, baadhi ya mitandao ya kijamii na utafiti wangu mwenyewe , ki mantiki NEC na NIDA ni mbingu na Ardhi.

Wakati NIDA ni taasisi mpya na zoezi linalofanyika halijawahi kufanyika nchini kwetu kwa maana ya kumtambua mtanzania, mazoezi mengine yalikuwa ni ya usajili tu kama NEC wanavo fanya.

Madhumuni ya NIDA ni kumtambua nani Raia, nani Mgeni mkaazi na nani mkimbizi. Hili zoezi sio rahisi maana nchi yetu inapakana na nchi nyingi na kuwatofautisha watu wake sio rahisi.

Zoezi la NEC ni la kisiasa wakati mfumo wa NIDA una manufaa kiuchumi, kijamii na kiusalama ndo maana kazi yao inafanywa kwa umakini sana kwa kuhusisha vyombo vingine Kama RITA, Uhamiaji, Tamisemi na vyombo vingine vya ulinzi.

NIDA vs NEC.

1. Card ya NEC ni ya plastic na ina expire in 3 yrs kulingana na material iliyo tumika wakati ya NIDA ni smart card na life span yake ni miaka 10. Hivo ununuzi wa card za NIDA utakuwa ni wa juu kuliko wa card za NEC.

2. Kwa kuwa card za NIDA ni smart Card, hata printers zake ni specialized ili kuweza kuingiza data kwenye chip (watu wa IT watanielewa) wakati NEC ni printer za kawaida unazo weza print popote. Hivo ununuzi wa printa za NIDA utakuwa ghali.

3. Teknolojia ya NIDA ni ya kisasa na
ndo inayo tumika kwa sasa ulimwenguni na ni takwa la E. Africa comunity.

4. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo tarehe 08.02.2016, ukurasa wa 4 , mwandishi amegawanya pesa za usajili za NEC (70b) kwa idadi ya vitambulisho (23m) na kupata kila
kimoja ni sh. 3,010 na kwa NIDA kachukua 179.6b kagawa kwa vitambulisho 2m. Kimsingi 70b ya NEC ni ya usajili tu bila kuweka gharama za BVR. Kama sikosei wakati wa zoezi la usajili wa NEC magazeti yaliwahi kureport gharama ya BVR moja kuwa ni kama $ 6,800 na walinunua BVR 8,000 hivo basi NEC walitumia kama $54,400,000 sawa na karibu 120b bila gharama za usafiri (logistics), karatasi nk hivo si kweli NEC walitumia 70b tu. Wakati gharama za NIDA sh179.6b ni pamoja na gharama za kujenga mfumo wa kielectronic, kumlipa mkandarasi, kununua mashine za usajili na consultant aliye andikwa gazeti la Mtanzania la leo, magari, ofisi zao kila wilaya, na jukumu kubwa la utambuzi linalohusisha vyombo mbalimbali ambalo NEC hawalifanyi (nilivo vitaja hapo juu) na kama mnavyojua uanzishwajiwa ofisi ni pamoja na ununuzi wa samani etc.

5. Wakati NEC hizi pesa walipewa ndani ya mwaka mmoja, na kwa sababu ya uchaguzi NEC walikuwa na cut off time, NIDA pesa hizi
wamepewa tangu mradi uanze mwaka 2011.


6. Kama expiration ya card za NEC ni 3 yrs na NIDA ni 10 yrs hivo cost of investment ya NEC ni mara 3 ya NIDA.

7. Kuhusu sahihi (signature) kuto kuwa kwenye kitambulisho ni suala la kiteknolojia na kiusalama zaidi.Vitambulisho vingi vya kisasa na hata vya nchi nyingi tu havina signature on the face ya kitambulisho maana data zimo ndani ya kitambulisho na zinasomeka kielectronic. Vitambulisho vya Nigeria, Malaysia, Philippines etc havina signature . Data za mhusika husomwa na kitu kinaitwa Card reader. Ni kwa sababu za kiusalama tu maana signature inaweza kugushiwa lakini finger prints haziwezi. Nimeona kwenye magazeti mengi NIDA wamepata award (tuzo) mbili za kimataifa kuhusiana na teknolojia yao lakini hapa kwetu hatuvithamini, mi naona kuna shida.

Mpaka sasa hivi, kwa utafiti wangu, toka 2011 NIDA ilipo anza, NIDA imepata 20% ya pesa zilizo idhinishwa na bunge kwa miaka yote hiyo na sababu hii ya ukata ndo maana zoezi linasuasua na hawajaweza malizia usajili na wameshindwa toa elimu kwa Umma sababu ya Ukata.

Sio nia yangu kutetea ufisadi na ndo maana najiita "Tanzania Njema Yaja". Naiona Tanzania ikielekea kwenye nuru lakini hatutafika kilele cha uzuri huo kama ukweli hautaelezwa... ni vema Watanzania wakauelewa ukweli kabla ya kuhukumu. Mh. Raisi alisema, "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" nami naona nimetimiza usemi huo. Na ninaamini baada ya uchunguzi ambao mh. Raisi ameelekeza ufanyike, ukweli utafahamika na haki itatendeka.

Long live Tanzania. Ukweli utatuweka huru.......
uzi mzr umechambua vzr sana mkuu
 
Mkuu sio kweli card zao ni smart card na ni Contactless smart card huwez oba kwa macho
ndo maana haina signature kwenye kitambulisho.... hizo zote utazipata kwenye card reader.... hii nna uhakika 100%.... naipenda nchi, yangu naipenda Tz.....
 
Ukichunguza kwa makini makala nyingi za kwenye magazeti mbali mbali kwa namna moja au nyingine vyanzo vyake ni jf......JF ni kisima cha maarifa....na burudani
Kuna wataalamu wa kila fani humu watakaokufanya ujutie kuikosa JF...
Na ndio maana wengine huwa tunaumia sana pale jukwaa hili linapogeuka kijiwe cha udaku, matusi, kutukanana, kuzushiana, na uongo (wao wakidai eti ni propaganda, kitu ambacho si kweli).

Hebu fikiria ni mangapi yenye manufaa kwa mtu binafsi na kwa taifa kwa ujumla kama kila member akitumia ujuzi na maarifa yake kuwaelimisha wengine?

Tafadhalini wanaJF, tusiruhusu jukwaa hili lipoteze hadhi. Big up Tanzania Njema Yaja, na wengine wote mnaotumia hoja na utafiti kuanzisha au kuchangia threads
 
POSSIBLY MTOA MADA NI MMOJA WA ...../ HILI NI JIPU NA NI LAZIMA LITUMBULIWE! NO WAYOUT / PALE WIZI UNAPOJARIBU KUTETEWA KISOMI
 
Well said Mkuu!!

Hata mimi nilipigwa na butwaa kusikia Rais anadai vitambulisho havina sahihi. The way he put it inakuwa kama ndiyo ilikuwa ni moja ya sababu kuu za kuwafukuza/kuwasimamisha kazi wahusika!!
 
..watanzania ni wapiga dili sana... Huu mchanganuo/ulinganifu wa kadi za NIDA umeonyesha jinsi kadi za NIDA zilivyotakiwa ziwe...kwa maana ya smart card...lakini ukweli ni kwamba kadi zenyewe sio smart na wala hazina micro chip...na ni plastic material...ndio maana watu wanasema mradi wa NIDA ni wa kifisadi....maana kilicho kwenye karatasi sicho kinachoonekana kialisia....
...ufisadi wa NIDA ni mfano wa ufisadi mwingine TZ kama: mabarabara yasiyo na viwango....mabehewa feki.....meli feki...ndege feki....n.k n.k.....

Mkuu nderingosha mleta hoja kadai ni smart Card ila contact-less Card sasa wataalamu wanaweza kutusaidi ukweli wa hilo au mleta hoja akafananua hilo kuwa kweli ID za NIDA ni za kiwango hicho au ndoto.

Images for smart card contactless
 
Huu ni upotoshwaji mkubwa na uongo. Mleta mada Tanzania Njema Yaja, unadai kwamba kitambulisho cha NEC ni cha plastic na kwamba cha NIDA ni smart card.

Nikuulize kwanza je, wewe unacho kitambulisho cha taifa (NIDA)???
Hiki kitambulisho mimi ninacho na ni cha plastic, kama kilivyo cha mpiga kura.

Ukweli ndio huo na hivyo hoja zako hapo juu karibu zote kuanzia #1 - 7 kuwa batili. Gharama za material, sijui printer, technology, smart card reader, fingerprints, blah blah blah ni uongo.

Kama kweli NIDA wangetoa vitambulisho vya ubora huo tungeelewa kidogo. Lakini vitambulisho vyao havina tofauti na vya NEC, hivyo ni sahihi kabisa kwa Rais wetu ama mwananchi yeyote yule mzalendo kuhoji hizi takwimu za NIDA na kutaka uchunguzi kufanyika.
Mdau,KITAMBULISHO CHA NEC ni SMART CARD AU LAH?WW UNAVYO VIWILI HEBU TUFAFANULIE
 
Mkuu wa kaya aliye-question juu ya hiyo kitu naamini ana insight ya what is behind the scene.

Mleta hoja asante umechambua vizuri ila kwa sasa wacha state instruments zilete kile ambacho hatukijui (i hope).

Kwani NIDA hawakuona umuhimu wa kutoa taarifa kabla ya kutuhumiwa?

Utaniambia hawana kitengo cha PR[emoji15]


Well said. All in all the President is not just your average Joe, Lazima ana ushahidi wa kutosha kwa alichokisema.

Wacha watumbuliwe tu, nchi ilishakuwa shamba la bibi hii. Watu wanjinyonyea tu kama maziwa ya mama.
 
Pamoja na uchambuzi wako ila Mheshimiwa Rais mpaka ameongea vile alijuwa kuna nini ndani ya NIDA watulie tu watumbuliwe hilo shipa maana ni zaidi ya jipu
 
Mkuu nderingosha mleta hoja kadai ni smart Card ila contact-less Card sasa wataalamu wanaweza kutusaidi ukweli wa hilo au mleta hoja akafananua hilo kuwa kweli ID za NIDA ni za kiwango hicho au ndoto.

Images for smart card contactless
..hazina hicho kiwango..waje humu wathibitishe...maana naona hii ni strategy ya kujisafisha...take my word...JPM si mzembe kiasi hicho cha kuwapasua live...
 
..hazina hicho kiwango..waje humu wathibitishe...maana naona hii ni strategy ya kujisafisha...take my word...JPM si mzembe kiasi hicho cha kuwapasua live...
Mkuu hata JK aliwahi sema alimfukuza kazi jamaa mmoja maliasili sababu ya fitna za watu na alikuja kujuta baadae baada ya kugundua kuwa yule jamaa ndo alikuwa mpambanaji na mtetea mali za Umma.... tusihukumu kwa fikra tu ndugu zangu...
 
Mkuu nderingosha mleta hoja kadai ni smart Card ila contact-less Card sasa wataalamu wanaweza kutusaidi ukweli wa hilo au mleta hoja akafananua hilo kuwa kweli ID za NIDA ni za kiwango hicho au ndoto.

Images for smart card contactless

Kadi za NIDA hajizafikia uwezo ulokusudiwa na raisi aliepita Jakaya Kikwete wa kutaka kila mtanzania awe na ID smart card.

ID card ya mtanzania inalengwa kuwa smart card ili iweze kuchukua nafasi ya pasi ya kusafiria endapo msafiri hana passport na pia kutambuliwa uraia wake kirahisi popote pale anapokuwa na ID card hio.

Lakini ubora wa ID card ya sasa inayotolewa na NIDA haujafikia kiwango hicho kiasi cha kuweza kuaminiwa hata na nchi zilizo nje ya Africa.

Wakati mwingine inabidi tuamini kabisa pasi na shaka kuwa, adui wa maendeleo ya sisi watanzania ni sisi wenyewe.

Uchumi utawezaje kusogea mbele kama unakwamishwa kw amakusudi na wajinga wachache?

Huu mradi ulikuwa uwe umekamilika kwa asilimia 90 sasa na ndio kwanza haujafikia hata nusu, je hizi ni akili za wapi?
 
Utafiti wa kisayansi zaidi lakini kwa kuwa ccm ni zao la mafisadi harufu ya kifisadi haiwezi kuisha, angalau waliokamatwa watakuwa wamelamba kila mtu 2billion, maana mijumba inayojengwa na iliyojengwa ni ya kutisha, ushahidi ninao naweza kuwawekea picha ikiwezekana.
 
Kadi za NIDA hajizafikia uwezo ulokusudiwa na raisi aliepita Jakaya Kikwete wa kutaka kila mtanzania awe na ID smart card.

ID card ya mtanzania inalengwa kuwa smart card ili iweze kuchukua nafasi ya pasi ya kusafiria endapo msafiri hana passport na pia kutambuliwa uraia wake kirahisi popote pale anapokuwa na ID card hio.

Lakini ubora wa ID card ya sasa inayotolewa na NIDA haujafikia kiwango hicho kiasi cha kuweza kuaminiwa hata na nchi zilizo nje ya Africa.

Wakati mwingine inabidi tuamini kabisa pasi na shaka kuwa, adui wa maendeleo ya sisi watanzania ni sisi wenyewe.

Uchumi utawezaje kusogea mbele kama unakakwamishwa kw amakusudi na wajinga wachache?

Huu mradi ulikuwa uwe umekamilika kwa asilimia 90 sasa na ndio kwanza haujafikia hata nusu, je hizi ni akili za wapi?
Richard una chuki binafsi na NIDA..... inawezekanaje kuachieve 90% wakati umepewa 20% ya bajeti kwa kiaka 5? Ni vizuri uwe na uhakika na unacho kisema..... kama NIDA ingekuwa well financed haya yote yasingekuwepo..... shida hapa ni ukata.... fanya utafiti tafadhali. .... no research no right to speak..... fuatilia historia ya Galileo kuhusu suala la jua na dunia ipi inazunguka mwemzie.... wahafidhina kama wewe wali endup kumfunga mpaka akafia gerezani kwa yeye kusema ukweli..... kamwe NURU ya Tz haitashamili kwa watu kama nyie, msio kuwa na facts lakini mnalazimisha hoja.... huwa nawaita watu wa kutwanga na kupepeta.....
 
nashukuru mkuu... ni vema watanzania tukajenga tabia ya kuwa wakweli, kwetu wenyewe na kwa viongozi wetu.... kama vitambulisho vya NEC haviwezi tumika uchaguzi ujao, vina expire in 3 yrs na vya NIDA vita expire in 10 years, huwez walinganisha wote at per.... hapa ni sawa na kulinganisha chungwa na apple eti kwa sababu yote ni matunda....
Ukiangalia sifa za mtu kuandikishwa kuwa mpiga kura, ndo hizo hizo za mtu kuandikishwa NIDA.

Ndio maana tulihoji toka mwanzo, kwa nini kuwa na vitambulisho vya aina nyingi wakati kimoja kinaweza tengenezwa kuwa multipurpose?

Kuna haja gani ya kutumia pesa nyingi kwa ajili ya vitambulisho hivyo? Kuna mantiki gani kuwa na:-
1. Kitambulisho cha mpiga kura
2. Kitambulisho cha taifa
3. Passport ya kusafiria

Wakati kimoja kilichoboreshwa kinaweza kufanya kazi zote hizo? Ni ufisadi tu na matumizi mabaya ya rasilimali chache tulizonazo
 
Back
Top Bottom