Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

NIDA wahukumiwe kwa slow roll out of the registration proram. It is in mature at this moment in time to judge them on per capita cost
All in all NIDA wanaboa sana. Mie niliandikishwa mnamo Septemba 2013, mpaka naandika ujumbe huu sijapatiwa kitambulisho, pamoja na kufuatilia mara kadhaa ofisini tulikoelekezwa kuchukua. Mpaka sasa sina hamu nacho, wabaki nacho tu, nitatumia kitambulisho cha kura ama passport ama leseni ya kuendeshea baby walker pale itakapobidi.
 
nashukuru mkuu... ni vema watanzania tukajenga tabia ya kuwa wakweli, kwetu wenyewe na kwa viongozi wetu.... kama vitambulisho vya NEC haviwezi tumika uchaguzi ujao, vina expire in 3 yrs na vya NIDA vita expire in 10 years, huwez walinganisha wote at per.... hapa ni sawa na kulinganisha chungwa na apple eti kwa sababu yote ni matunda....
Magufuli mwanasayansi ameshindwaje kujua tofauti hii!? au kama kawaida vilaza ndio washauri? Au kama kawaida ya puppets wanaojipendekeza wanajifanya nao watumbua majipu? Kwa Rais asiye na subira kama huyu anahitaji washauri makini na wenye akili ya kujitegemea!! Bado hatujaona mengi!!
 
ee
Nimesoma Magazeti mbali mbali na kumsikiliza mhe.Rais, baadhi ya mitandao ya kijamii na utafiti wangu mwenyewe , ki mantiki NEC na NIDA ni mbingu na Ardhi.

Wakati NIDA ni taasisi mpya na zoezi linalofanyika halijawahi kufanyika nchini kwetu kwa maana ya kumtambua mtanzania, mazoezi mengine yalikuwa ni ya usajili tu kama NEC wanavo fanya.

Madhumuni ya NIDA ni kumtambua nani Raia, nani Mgeni mkaazi na nani mkimbizi. Hili zoezi sio rahisi maana nchi yetu inapakana na nchi nyingi na kuwatofautisha watu wake sio rahisi.

Zoezi la NEC ni la kisiasa wakati mfumo wa NIDA una manufaa kiuchumi, kijamii na kiusalama ndo maana kazi yao inafanywa kwa umakini sana kwa kuhusisha vyombo vingine Kama RITA, Uhamiaji, Tamisemi na vyombo vingine vya ulinzi.

NIDA vs NEC.

1. Card ya NEC ni ya plastic na ina expire in 3 yrs kulingana na material iliyo tumika wakati ya NIDA ni smart card na life span yake ni miaka 10. Hivo ununuzi wa card za NIDA utakuwa ni wa juu kuliko wa card za NEC.

2. Kwa kuwa card za NIDA ni smart Card, hata printers zake ni specialized ili kuweza kuingiza data kwenye chip (watu wa IT watanielewa) wakati NEC ni printer za kawaida unazo weza print popote. Hivo ununuzi wa printa za NIDA utakuwa ghali.

3. Teknolojia ya NIDA ni ya kisasa na
ndo inayo tumika kwa sasa ulimwenguni na ni takwa la E. Africa comunity.

4. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo tarehe 08.02.2016, ukurasa wa 4 , mwandishi amegawanya pesa za usajili za NEC (70b) kwa idadi ya vitambulisho (23m) na kupata kila
kimoja ni sh. 3,010 na kwa NIDA kachukua 179.6b kagawa kwa vitambulisho 2m. Kimsingi 70b ya NEC ni ya usajili tu bila kuweka gharama za BVR. Kama sikosei wakati wa zoezi la usajili wa NEC magazeti yaliwahi kureport gharama ya BVR moja kuwa ni kama $ 6,800 na walinunua BVR 8,000 hivo basi NEC walitumia kama $54,400,000 sawa na karibu 120b bila gharama za usafiri (logistics), karatasi nk hivo si kweli NEC walitumia 70b tu. Wakati gharama za NIDA sh179.6b ni pamoja na gharama za kujenga mfumo wa kielectronic, kumlipa mkandarasi, kununua mashine za usajili na consultant aliye andikwa gazeti la Mtanzania la leo, magari, ofisi zao kila wilaya, na jukumu kubwa la utambuzi linalohusisha vyombo mbalimbali ambalo NEC hawalifanyi (nilivo vitaja hapo juu) na kama mnavyojua uanzishwajiwa ofisi ni pamoja na ununuzi wa samani etc.

5. Wakati NEC hizi pesa walipewa ndani ya mwaka mmoja, na kwa sababu ya uchaguzi NEC walikuwa na cut off time, NIDA pesa hizi
wamepewa tangu mradi uanze mwaka 2011.

6. Kama expiration ya card za NEC ni 3 yrs na NIDA ni 10 yrs hivo cost of investment ya NEC ni mara 3 ya NIDA.

7. Kuhusu sahihi (signature) kuto kuwa kwenye kitambulisho ni suala la kiteknolojia na kiusalama zaidi.Vitambulisho vingi vya kisasa na hata vya nchi nyingi tu havina signature on the face ya kitambulisho maana data zimo ndani ya kitambulisho na zinasomeka kielectronic. Vitambulisho vya Nigeria, Malaysia, Philippines etc havina signature . Data za mhusika husomwa na kitu kinaitwa Card reader. Ni kwa sababu za kiusalama tu maana signature inaweza kugushiwa lakini finger prints haziwezi. Nimeona kwenye magazeti mengi NIDA wamepata award (tuzo) mbili za kimataifa kuhusiana na teknolojia yao lakini hapa kwetu hatuvithamini, mi naona kuna shida.

Mpaka sasa hivi, kwa utafiti wangu, toka 2011 NIDA ilipo anza, NIDA imepata 20% ya pesa zilizo idhinishwa na bunge kwa miaka yote hiyo na sababu hii ya ukata ndo maana zoezi linasuasua na hawajaweza malizia usajili na wameshindwa toa elimu kwa Umma sababu ya Ukata.

Sio nia yangu kutetea ufisadi na ndo maana najiita "Tanzania Njema Yaja". Naiona Tanzania ikielekea kwenye nuru lakini hatutafika kilele cha uzuri huo kama ukweli hautaelezwa... ni vema Watanzania wakauelewa ukweli kabla ya kuhukumu. Mh. Raisi alisema, "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" nami naona nimetimiza usemi huo. Na ninaamini baada ya uchunguzi ambao mh. Raisi ameelekeza ufanyike, ukweli utafahamika na haki itatendeka.

Long live Tanzania. Ukweli utatuweka huru.......
eeh bana eeh hayo yatakua kwenye utetezi. sidhani kama kuna justification ya matumizi makubwa nida wangetiwa katika shutuma. kinachoonekana sasa ni juhudi za wapambe
 
nashukuru mkuu... ni vema watanzania tukajenga tabia ya kuwa wakweli, kwetu wenyewe na kwa viongozi wetu.... kama vitambulisho vya NEC haviwezi tumika uchaguzi ujao, vina expire in 3 yrs na vya NIDA vita expire in 10 years, huwez walinganisha wote at per.... hapa ni sawa na kulinganisha chungwa na apple eti kwa sababu yote ni matunda....
Kwa hiyo kiongozi unamaanisha wanaotoka hadharani kuituhumu NIDA ni mazombie? Nashangaa sana sijui kwa nini wa-Tz huwa hutupendi kushughulisha vichwa vyetu! Watu hata hawapewi nafasi ya kujieleza unastukia mtu kafutwa kazi tu! Ukiyasikiliza matutusa eti yanashangilia Magu hataki mchezo! Kazi tunayo!
 
Nashukuru kwa ushauri kuwa nifanye tafiti. Barcode, magnetic slip or embedded microprocessors sio issue kabisa hapa. Suala hapa ni mazingira yanayoashiria wizi makubwa na mada nene yenye muelekeo wa kutetea. Kwa mnaodhani Magu anakurupuka nadhani mko wrong sana. Tulieni ili ripoti itoke mje kupinga na hizi hoja zenu.
 
Mleta mada umetuwekea mahesabu yako kwamba kitambulisho cha NEC kimegharimu kama Tanzania shilingi 3010, Lakini hujatuwekea gharama ya kitambulisho cha NIDA.
 
Mkuu nakushukuru sana kwakweli umetoa darasa kama nikweli basi NIDA wamepga kazi
 
Halafu mkuu mleta mada umelinganisha vitambulisho visivyo na saini/sahihi Nigeria na singapore. Umeviona vya nchi yeyote ya Ulaya vikoje? Binafsi nafahamu vya Ujerumani vina saini ya mmiliki.
Kwa huu utetezi wenu subirini jamaa wanaendelea na uchunguzi.
 
Hapa kinacho kosekana ni Elimu ya card hizi na mfumo wake mkubwa ulivo.... nimeeleza hapo mwanzo, 179b za nida huwez gawa kwa idadi ya vitambulisho kama nilivo sema, kuna one time investment kama machines za kuregister, magari, ofisi, wafanyakazi, etc na kadri watakavo endele gharama ya kitambulisho itashuka....
Kuna mdau mmoja yupo nida, niliwasiliana naye kutaka kupata opinion yake baada ya rais kumtumbua boss wake.

Nilimwuliza, ni kweli pesa zimeliwa? Alijibu kwa kifupi, hivi tz ya JK kuna taasisi haijapiga hela kweli?[emoji3]
 
Mkuu nakushukuru sana kwakweli umetoa darasa kama nikweli basi NIDA wamepga kazi
Mkuu na hizi sheria za cyber siwez andika uwongo hapa hasa ukzingatia na mheshimia Raisi kaligusia..... inauma saa nyingine career za watu zinaumizwa tu kwa sab zisizo za msingi... kama ni mafisadi waadhibiwe lakini kama sio basi hata wasifikiliwe kuwa ni mafisadi maana hii inakatisha tamaa sana....
 
Kitambulisho cha Utaifa hakipaswi ku expire (kuisha muda wake). Ila inapaswa taarifa ziwe zinaboreshwa (updated), kotokana na kufa na kuzaliwa, hasa Wilayani.

Kitambulisho cha NIDA, ninacho mm HAKINA UBORA WOWOTE (Kuanzia rangi, material, design, nk) hata hiyo Magnetic ya Kielectronic unayo isema ni Magumashi tu haipo!! Angalia ATM Card zote zina kama kichuma, ila hiki kitambulisho cha Utaifa hakina!!

Taarifa zilizopo katika ID hii ni chache sana! Kuna Majina matatu tu (3) na Kimeandikwa 19460714-33001-000002-28. Ina maana umezaliwa mwaka 1946, mwezi wa 7 na tarehe 14, basiii. Hakina kata/mtaa/kijiji wala Tarafa wala Wilaya wala MKOA!!! Hivyo taarifa hazijafichwa kokote zipo nje nje tu tofauti na unavyo dai ww hapo!!

- Zoezi la utambuzi wa Raia au si raia halikufanyika na halijawahi kufanyika. Wakongo wengi na Wakenya wengi walijiandikisha. Mf, vyuoni utaratibu ni wa ajabu hamna anae mfahamu mwenzie. Na hii nchi ilipo fikia mtu ukitoa taarifa za ukweli unatolewa roho ww na POLISI wanamuachia mharifu huru, cha msingi awe na mawe tu basiii.

Hiki kitambulisho kingekuwa bora sn Kingejumuisha vituatavyo:
- Umezaliwa wapi-Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Nchi. Hizi taarifa walizichukua ila zipo ktk data base yao ila c ktk hii ID (Si cha kielectronic).
- Primary school, SEC schools (O-Level & A-level), University attended (Ingesaidia kuwakamata Polisi/Wanajeshi mamluki wa Rwanda/Kenya, nk kumbuka yule wa IT alie sepa hadi leo). Hata suala la ajira kwa wazawa kwanza. Pia hapa HESLB (Mikopo ya Elimu ya Juu) wasingetafuta kampuni za kukusanya madeni yao (ungetambulika kwa urahisi mnooo!!)
- Employed/Unemployed/Businessman or woman/Farmer/Fisherman, nk (Employment status). Tupo 45 million walipa kodi ni 6 million tu.
-Marital status-Married/single,divorced/widow, nk. Status ingekuwa inakuwa updated na hapa National Statistics Board wangekuwa wanaripoti ukweli ila sasa ni magumashi tu. Na hii ingefanyika kila siku miaka yote, Wilayni- make ndio kazi yao kuwa ofisini (Kufa na kuzaliwa ni kila siku). Hata hawajui wafanyakazi ni wangapi? Wa Tz walio olewa au kuoa au maseja ni wangapi? Kuna upungufu wa wanaume kiasi gani? Hii ingerahihishia wachungaji kupiga dua hasa Vijana waweke sketi ndani!!

HIZI TAARIFA ZOTE ZINGEHIFADHIWA KIELECTRONIC KTK ID HUSIKA.
In summary, maelezo yako hayaja justify hiyo gharama ya 179 billion!! Ni bora wangefanya utambuzi wa Raia tu kwanza bila kutoa ID.
 
Muumbue tu, si amependa mwenyewe?
 
Mwandishi kaelezea uhalisia wa kilichofanyika na sina Tatizo na Hilo. mfano electronic signature na conventional signature ambapo dunia inaelekea kwenye electronic signature (ziko aina nyingi tu toka biometric features na authentication zingine) kutokana na kuongezeka kwa matukio ya uharifu yakihusisha forgery ya authentication ya nyaraka. Na ni kweli nchi za EAC zilikubaliana standards za pamoja za vitambulisho vya kitaifa. Hii kwangu sio issue na sidhani kama inatakiwa iwe issue eti tu kwa ajiri rais aliitaja au kushauriwa vibaya. Issue ni pesa zetu zilitumika kama tunavyoambiwa na hao waliozitumia au kulikuwa na ubadhirifu na kujinufaisha kwa aina yoyote hata kama ubora uliotakiwa umepatikana?

Ninahakika mkuu wa nchi hawezi kukulupuka kutoa tuhuma nzito kama hizi pamoja na kwamba sio vigezo vyote vya kuonyesha mashaka ya matumizi ya NIDA vikawa vinaushawishi kama ambavyo mwandishi amejitahidi kuonyesha. Kama mlitumia 1,000 na kuonyesha kuwa pesa yote 10,000 mliyoomba imetumika na kuweka mifukoni mwenu 9,000 badala ya kuturudishia, ni lazima muirudishe hiyo change. Siyo haki yenu! Hivyo utetezi wa mwandishi uko sawa kama tutadhihirishiwa hilo kwamba pesa mliyopewa imetumika vizuri kama ilivyotakiwa na si vinginevyo! Corruption in maana kuna manufaa binafsi umeyapata mbali na haki yako ya utumishi regardless of what you delivered! Prove it and your innocent but not a parallel comparison of expenditures!

QUOTE="Tanzania Njema Yaja, post: 15277865, member: 305345"]Nimesoma Magazeti mbali mbali na kumsikiliza mhe.Rais, baadhi ya mitandao ya kijamii na utafiti wangu mwenyewe , ki mantiki NEC na NIDA ni mbingu na Ardhi.

Wakati NIDA ni taasisi mpya na zoezi linalofanyika halijawahi kufanyika nchini kwetu kwa maana ya kumtambua mtanzania, mazoezi mengine yalikuwa ni ya usajili tu kama NEC wanavo fanya.

Madhumuni ya NIDA ni kumtambua nani Raia, nani Mgeni mkaazi na nani mkimbizi. Hili zoezi sio rahisi maana nchi yetu inapakana na nchi nyingi na kuwatofautisha watu wake sio rahisi.

Zoezi la NEC ni la kisiasa wakati mfumo wa NIDA una manufaa kiuchumi, kijamii na kiusalama ndo maana kazi yao inafanywa kwa umakini sana kwa kuhusisha vyombo vingine Kama RITA, Uhamiaji, Tamisemi na vyombo vingine vya ulinzi.

NIDA vs NEC.

1. Card ya NEC ni ya plastic na ina expire in 3 yrs kulingana na material iliyo tumika wakati ya NIDA ni smart card na life span yake ni miaka 10. Hivo ununuzi wa card za NIDA utakuwa ni wa juu kuliko wa card za NEC.

2. Kwa kuwa card za NIDA ni smart Card, hata printers zake ni specialized ili kuweza kuingiza data kwenye chip (watu wa IT watanielewa) wakati NEC ni printer za kawaida unazo weza print popote. Hivo ununuzi wa printa za NIDA utakuwa ghali.

3. Teknolojia ya NIDA ni ya kisasa na
ndo inayo tumika kwa sasa ulimwenguni na ni takwa la E. Africa comunity.

4. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo tarehe 08.02.2016, ukurasa wa 4 , mwandishi amegawanya pesa za usajili za NEC (70b) kwa idadi ya vitambulisho (23m) na kupata kila
kimoja ni sh. 3,010 na kwa NIDA kachukua 179.6b kagawa kwa vitambulisho 2m. Kimsingi 70b ya NEC ni ya usajili tu bila kuweka gharama za BVR. Kama sikosei wakati wa zoezi la usajili wa NEC magazeti yaliwahi kureport gharama ya BVR moja kuwa ni kama $ 6,800 na walinunua BVR 8,000 hivo basi NEC walitumia kama $54,400,000 sawa na karibu 120b bila gharama za usafiri (logistics), karatasi nk hivo si kweli NEC walitumia 70b tu. Wakati gharama za NIDA sh179.6b ni pamoja na gharama za kujenga mfumo wa kielectronic, kumlipa mkandarasi, kununua mashine za usajili na consultant aliye andikwa gazeti la Mtanzania la leo, magari, ofisi zao kila wilaya, na jukumu kubwa la utambuzi linalohusisha vyombo mbalimbali ambalo NEC hawalifanyi (nilivo vitaja hapo juu) na kama mnavyojua uanzishwajiwa ofisi ni pamoja na ununuzi wa samani etc.

5. Wakati NEC hizi pesa walipewa ndani ya mwaka mmoja, na kwa sababu ya uchaguzi NEC walikuwa na cut off time, NIDA pesa hizi
wamepewa tangu mradi uanze mwaka 2011.

6. Kama expiration ya card za NEC ni 3 yrs na NIDA ni 10 yrs hivo cost of investment ya NEC ni mara 3 ya NIDA.

7. Kuhusu sahihi (signature) kuto kuwa kwenye kitambulisho ni suala la kiteknolojia na kiusalama zaidi.Vitambulisho vingi vya kisasa na hata vya nchi nyingi tu havina signature on the face ya kitambulisho maana data zimo ndani ya kitambulisho na zinasomeka kielectronic. Vitambulisho vya Nigeria, Malaysia, Philippines etc havina signature . Data za mhusika husomwa na kitu kinaitwa Card reader. Ni kwa sababu za kiusalama tu maana signature inaweza kugushiwa lakini finger prints haziwezi. Nimeona kwenye magazeti mengi NIDA wamepata award (tuzo) mbili za kimataifa kuhusiana na teknolojia yao lakini hapa kwetu hatuvithamini, mi naona kuna shida.

Mpaka sasa hivi, kwa utafiti wangu, toka 2011 NIDA ilipo anza, NIDA imepata 20% ya pesa zilizo idhinishwa na bunge kwa miaka yote hiyo na sababu hii ya ukata ndo maana zoezi linasuasua na hawajaweza malizia usajili na wameshindwa toa elimu kwa Umma sababu ya Ukata.

Sio nia yangu kutetea ufisadi na ndo maana najiita "Tanzania Njema Yaja". Naiona Tanzania ikielekea kwenye nuru lakini hatutafika kilele cha uzuri huo kama ukweli hautaelezwa... ni vema Watanzania wakauelewa ukweli kabla ya kuhukumu. Mh. Raisi alisema, "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" nami naona nimetimiza usemi huo. Na ninaamini baada ya uchunguzi ambao mh. Raisi ameelekeza ufanyike, ukweli utafahamika na haki itatendeka.

Long live Tanzania. Ukweli utatuweka huru.......[/QUOTE]
 
Acha umbulula kwan humu jukwaani hakuna waandishi wa habari?? Je , kama huo uzi uliwekwa na mwandishi huyohuyo wa gazeti la mwananchi???
Tatizo ni nini?
Nimesema kuhusu JF, sio waandishi. Haijalishi huyo huyo ndo muandishi, nilichomaanisha ni kwamba hiyo habari ilianzia JF.
 
Yaan Billion 179 kwa vitambulisho Million 2 tu?... Je wakiwapa watz wote c watatumia matrillion? Ndg yangu ukitaka unusurike huo utetez wako upeleke kwa magufuli cyo humu Jf
 
Ha haaa.... Fikra pevu pekee ndo wanaweza changia uzi huu.... inaonyesha hata hujausoma uzi mzima....
 
Back
Top Bottom