Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Mkuu, umepembua vizuri mpaka umenishawishi kuwa inawezehana washauri wa JPJM wana mpotosha halafu yeye anaonekana mkurupukaji.

analysis yako imenifungua macho!
I wish kama hapa JF kungelikuwa na uwezekano wa kujionyesha. Mashine za kutengeneza smartcard zipo nyingi hapa Tanzani ila NIDA ulikuwa ni wizi mtupu
 
Na nasikia walikuwa wakikodi nyumba za watu huko mitaani...mshikaji wangu ananambia yeye kufika kwenye kituo cha kujiandikisha ilibidi akodi boda boda maana address yake haieleweki...most likely nyumba zao...akati NEC walikuwa wanatafuta shule na sehemu accessible
 
good! mtoa maada, umetoa uchanganuzi yakinifu
 
Utafanyia zoezi la kudumu kwenye mashule? Maana NEC ilikuwa mass registration kwa muda mfupi iliwezekana lakini NIDA ni ya kudumu na milele.... kama serikali ingetoa pesa zote in time, haya yote yasingetokea..

Na nasikia walikuwa wakikodi nyumba za watu huko mitaani...mshikaji wangu ananambia yeye kufika kwenye kituo cha kujiandikisha ilibidi akodi boda boda maana address yake haieleweki...most likely nyumba zao...akati NEC walikuwa wanatafuta shule na sehemu accessible[/QUOTE
 
Mimi naona walioshika vipaza sauti vya mikanganyiko ya pasua jipu hawachanganuagi kama wewe. Hiyo ndiyo hulka yao, na watakapochemsha hawaombi msamaha.

Majipu yanayosemekana majipu yanatumbuliwa, mengi ni kusingiziwa hamna kitu.

Mwisho wa yote Mungu ajuae haki atatenda haki. Utaratibu wa kuchanganua kwa Magufuli zero yeye misifa mbele hata kama ni uongo.
 
Huu ni upotoshwaji mkubwa na uongo. Mleta mada Tanzania Njema Yaja, unadai kwamba kitambulisho cha NEC ni cha plastic na kwamba cha NIDA ni smart card.

Nikuulize kwanza je, wewe unacho kitambulisho cha taifa (NIDA)???
Hiki kitambulisho mimi ninacho na ni cha plastic, kama kilivyo cha mpiga kura.

Ukweli ndio huo na hivyo hoja zako hapo juu karibu zote kuanzia #1 - 7 kuwa batili. Gharama za material, sijui printer, technology, smart card reader, fingerprints, blah blah blah ni uongo.

Kama kweli NIDA wangetoa vitambulisho vya ubora huo tungeelewa kidogo. Lakini vitambulisho vyao havina tofauti na vya NEC, hivyo ni sahihi kabisa kwa Rais wetu ama mwananchi yeyote yule mzalendo kuhoji hizi takwimu za NIDA na kutaka uchunguzi kufanyika.
Duuh huu sasa ni mtihani. Ninapata wasiwasi na uwezo wako mkuu utanisamehe lakini. Mimi tangu JK akiri kuwa kuna watu waliwekwa kwa kazi ya kujibu mapigo mitaoni nimeanza kuwa na wasiwasi kuwa hiyo kazi bado inaendelea kwa sasa na lengo lake limebaki kwenye kusafisha regime iliyoko madarakani.
Mkuu Dudubaya naona umeandika kwa hamaki bila hata takwimu. Mimi naamini hata Magufuli mwenyewe kama ataona ufafanuzi huu atakuwa na mawazo na mtizamo tofauti kidogo.

Dudubaya sio kutetea tu mkuu toa na data ili utetezi wako uaminike sio kuposti tu. Au renumeration haiangalii quality ya post inaangalia idadi tu
 
Utafanyia zoezi la kudumu kwenye mashule? Maana NEC ilikuwa mass registration kwa muda mfupi iliwezekana lakini NIDA ni ya kudumu na milele.... kama serikali ingetoa pesa zote in time, haya yote yasingetokea..
Kwani vituo vyote vya NIDA ni permanent? kwa nini wasiwe na ofisi kwenye almashauri kama nchi za wenzetu????
 
Suala hapa ni je, ilikuwa halali kutumia kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha za umma kwa zoezi la vitambulisho vya taifa, ambavyo vinafanana kabisa kiubora na vitambulisho na vya NEC ambavyo gharama yake ni ndogo? Tuwe tu wakweli, kama hatuna fedha za kujenga reli ya kati (ambayo kwangu naona ni muhimu zaidi), tunapata wapi mabilioni yote hayo kwa ajili ya vitabulisho tu vya kawaida? Hata mimi sitaki kuwahukumu sana watu wa NIDA (Maimu na wenzake), tatizo linaweza kuwa linaanzia juu zaidi: yaani kwa viongozi wa juu wanaoamua vipaumbele vya Taifa. Ni nania hasa aliruhusu mradi huu kufanyika kwa gharama kubwa kiasi hicho? Je kweli tuamini kwamba ni Maimu na timu yake ya NIDA?? Rais wangu aingie ndani zaidi.
 
Na ukizingatia wote walikuwa wanalenga watanzania...mmoja alikuwa interested na miaka 18 plus mwingine just mtanzania...sijui kwa nini hawakuwa integrated...huyo aliyefanya maamuzi ya kuwa separate ndio jipu nambari one
 
Dudu baya haujui unachokiongea, mleta mada, tukubali tukatae Pombe anashauriwa vibaya, na kuendelea kum support hata kwa madudu anayoyafanya nikumpotosha na sio kumsaidia. Ukweli nikwamba NIDA na NEC ni mbingu na ardhi, kitambulishwa kuitwa smart card ni ile hali ha kuwa na ile electronic chip na si kinginecho, na hata muheshimiwa rais alivyosema eti vile vitambulisho havina signature sio kweli ni uongo, vile vitambulisho vya NIDA vina signature ambazo ni invisible mpaka zisomwe na card reader, yeye kadanganywa na kukurupuka, mimi nilikuwa namshauri Pombe pale anapoletewa taharaifa awe anawahita wahusika aongee nao asikie na upande wa pili ndio aende kutangaza kwenye public kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.

juzi juzi amewaingilia wenye viwanda na mashamba makubwa na kuwashambulia, kwani vile viwanda walipewa bure na serikali au walivinunua?, na je kama mtu unakiwanda cha kuzalisha Kanga lkn serikali hiyo hiyo inawaacha wafanyabiashara wanaingiza kanga nyingi kiholela na za bei rahisi je wewe utaweza kushindana nao?, au utakachofanya nikufunga tu kiwanda chako na kufanya biashara nyingine zenye faida. Mimi nadhani Pombe kabla yakuwa anaongea na wananchi tena wananchi wa chini kabisa wasiojua nini maana ya uchumi awe anawahita wahusika na kuongea nao ili kuujua ukweli.

KWENYE ILI SUHALA LA NIDA AMECHEMKA, YAANI KWA WATU WANAOIJUA NIDA NA NEC KWAKWELI KWENYE ILI WAMESTUKA KIDIGO JUU YA HABARI ANAZOPELEKEWA MUHESHIMIWA RAIS.
 
under magufuli serikali itapata hasara sana kwa kulipa fidia na malipo mengine kwa wafanyakazi wake.Tatizo Magufuli anathani anaweza kusafisha kila kitu;hio kitu haiwezekani. Yeye aweke mipango mipya na kujenga nchi upya. Ya kale hayanuki,na hapa bado atapiteza kesi nyingi sana.

Unajitahd kurizon, lakn unatumia hoja dhaifu.

Hv wewe ukioa vyombo ulivyo tumia ukiwa bachala utavitupa?

Nacho amini utachambua yapi yatamfaa mwandani wangu na yapi c sahihi.

Magu, anacho fanya ni kurekebsha pabovu
 
Suala hapa ni je, ilikuwa halali kutumia kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha za umma kwa zoezi la vitambulisho vya taifa, ambavyo vinafanana kabisa kiubora na vitambulisho na vya NEC ambavyo gharama yake ni ndogo? Tuwe tu wakweli, kama hatuna fedha za kujenga reli ya kati (ambayo kwangu naona ni muhimu zaidi), tunapata wapi mabilioni yote hayo kwa ajili ya vitabulisho tu vya kawaida? Hata mimi sitaki kuwahukumu sana watu wa NIDA (Maimu na wenzake), tatizo linaweza kuwa linaanzia juu zaidi: yaani kwa viongozi wa juu wanaoamua vipaumbele vya Taifa. Ni nania hasa aliruhusu mradi huu kufanyika kwa gharama kubwa kiasi hicho? Je kweli tuamini kwamba ni Maimu na timu yake ya NIDA?? Rais wangu aingie ndani zaidi.
Kwa wenzetu vitambulisho vya taifa ni kila kitu.... once ukiweza mtambua kila raia wako ni rahisi kukusanya kodi na suala zima la ulinzi na usala wa nchi.... usilinganishe NEC na NIDA mkuu.... kitambualisho kimoja cha NIDA ni Mult application ikiwemo kupiga kura, leseni za udereva, mabank, blood group na hata urithi wako unaweza uweka humo hapo baadae.....
 
Hii mada imeletwa na "systematic purpose" kuja kutetea wizi hapa. Jamaa wamekaa wakaandika kujaribu kujiokoa.
Eti smart card!. Hata Hotel key cards ni smart zaidi ya hizi.
 
Hii mada imeletwa na "systematic purpose" kuja kutetea wizi hapa. Jamaa wamekaa wakaandika kujaribu kujiokoa.
Eti smart card!. Hata Hotel key cards ni smart zaidi ya hizi.
Mkuu fanya utafiti.... card za hotel ni Bar cords..... sijawahi na sintakaa nitetee ufisadi ..... ila sipendi kumezeshwa uwongo wakati mimi ni mtu huru.... njoo na hoja na data tafadhali....
 
Raisi kweli anatujali sisi maskini kwa kweli maana hawa jamaa wametuingiza mkenge kweli.Hawa nao tumeshawalipia fedha leo, hakuna dhamana wala nini, ni kurudisha fedha zetu na kwenda jela.
 
..watanzania ni wapiga dili sana... Huu mchanganuo/ulinganifu wa kadi za NIDA umeonyesha jinsi kadi za NIDA zilivyotakiwa ziwe...kwa maana ya smart card...lakini ukweli ni kwamba kadi zenyewe sio smart na wala hazina micro chip...na ni plastic material...ndio maana watu wanasema mradi wa NIDA ni wa kifisadi....maana kilicho kwenye karatasi sicho kinachoonekana kialisia....
...ufisadi wa NIDA ni mfano wa ufisadi mwingine TZ kama: mabarabara yasiyo na viwango....mabehewa feki.....meli feki...ndege feki....n.k n.k.....
 
Back
Top Bottom