Ukweli kuhusu kujamba

Spaghetti

Member
Jan 27, 2016
78
7,577
1661860183943.png

1. Unazalisha takriban mililita 500 hadi 1,500 za gesi kwa siku, na kuitoa kwa mara 10 hadi 20.

2. Unaweza kuiwasha gesi ya kijambo kwa moto. Ina gesi aina ya methane na hydrogen ambazo zinawaka kirahisi.

3. Kulingana na ripoti ya NBC News, kijambo kinaweza kusafiri kwa spidi ya takriban maili 6.8 kwa saa au 11km/saa.

4. Wanawake wanaweza kujamba mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

5. Sulfuri ndiyo inayofanya kijambo kunuka.
 
Ni jambo la kiafya zaidi na ni kawaida ijapokuwa baadhi ya watu wanalionea haya jambo hili.

Hapo No. 5 ni Hydrogen sulphide.

Gesi tumboni isipoondolewa/ondoka ni Tatizo na mtu atajisikia vibaya na pia mchakato wa uyeyushaji wa chakula tumboni utavurugika. Mtu Utajisikia kana kwamba "Umejaa" - tumefaction.

Kwa kifupi: Jisikie vizuri na uwe huru kujamba. Kwa heshima na adabu nzuri Jitenge pembeni kidogo au nenda faragha na achia gesi hiyo itoke kwa kimya au kwa sauti usijali wewe achia tu itoke.

Kumbuka hakuna binadamu yeyote(Hata wanyama) asiyejamba. Hii ni Asili ( call of Nature) usipingane na kitu cha kiasili - utaumia.
 
Back
Top Bottom