Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,569
- 34,700
Ningependa wachangiaji wajadili hili kwa undani. Ni hoja mujarabu inayoweza kutusaidia"JokaKuu, post: 19146579, member: 221"]..
..ukiuliza wachangiaji humu ndani serikali imepeleka mradi gani wa maendeleo Kilimanjaro tangu tupate uhuru wachache wataweza kuitaja.
Na hili pia..lakini zaidi ukiuliza ni mradi gani umepelekwa Kilimanjaro na haukustahili kupelekwa huko hakuna mradi hata mmoja.
Jingine hili hapa,ahsante mkuu..Sasa ndiyo hapo ninapotofautiana na hicho unachoita " ujasiri " wa watendaji toka Kilimanjaro waliopewa dhamana ktk serikali zetu tangu tupate uhuru.
..Kama ni " ujasiri" hebu nionyeshe mwenyeji wa Kilimanjaro aliyeuza nyumba za serikali nchi nzima. I mean the whole country, mtu anachukua uamuzi wa kuuza nyumba za serikali tena kwa bei ya hasara.
Naweza kusema, ndiyo kuna +ve effect..Kuhusu kutaja watu wa Kilimanjaro ambao wamekuwa +ve influence mahali pengine Tz sidhani kama ni sahihi.
Ukuaji wa mkoa wa Arusha unachangiwa sana na uhamiaji wa wananchi wa Kilimanjaro
Kwasasa Tanga kunabadilika kutokana na uhamiaji.
Nenda Muheza, Handeni uone namna watu walivyoweza kubadilika kutoka ''superstitious mind'' na kuwa entrepreneurs kutokana na kujifunza kutoka kwa wageni
Lakini pia lazima watu waangalie mbali.
Mtu anapotoka K'njaro na kubadilisha mtazamo wa wananchi wa Mkuranga ni jema.
Leo watu wa Mkuranga wanatambua mananasi ni utajiri, mihogo ni utajiri
Hwakutambua hilo miaka 40 iliyopita hadi walippojikuta wanauza ardhi kwa wageni ambao siku chache tu wanageuka kuwa bora kuliko wao. Ni ukweli tuuseme tu
Effect kubwa ni hii ambayo watu wanawajadili na kuanzisha curiosity kwanini wamefanikiwa ukilinganisha na maeneo mengine
Mchango mkubwa tu ambao wachache wanaweza kuuona...Lakini kama unapenda kujisomea matukio makubwa ya nchi hii kama harakati za uhuru, vita vya kagera, etc etc huwezi kukosa michango ya wananchi wa Kilimanjaro au kanda ya kaskazini.
Na hili ni kosa kubwa wanalofanya watu...Umetumia neno "ujasiri" ktk mada yako. Sasa kuna "ujasiri" ulioenea hapa nchini wa kushambulia integrity ya wananchi wa Kilimanjaro.
Badala ya ku learn na kuhamisha 'values' wanashambulia kwa kuchagizwa tu na hisia.
Ni hisia mbaya sana zilizojengwa na CCM katika kupambana na upinzani...imekuwa ni kitu cha kawaida kulaumu, kutuhumu, na kuzusha, dhidi ya wananchi wa Kilimanjaro na sasa kanda ya kaskazini.
Madhara ya jambo hili yataonekana muda mrefu ujao na hakutakuwa na namna ya kuzuia matatizo yanayotokana
Mbinu hii ya kuwagawa wananchi ni ya kisiasa zaidi. Haijengi bali kubomoa..Tumefika mahali people are not held to the same standards. Kwa mfano, mwanasiasa mwenyeji wa Kilimanjaro au kaskazini anatakiwa achunge kauli na matendo yake, huku wale wa maeneo mengine wakiachwa wadhalilishe na kubeza wananchi.
Tuhuma zinazotolewa hazina mashiko ni hisia tu.
Ndiyo maana nimeomba wachangiaji warudi katika maswali yako ya awali kuhusu upendeleo, waonyeshe na si ku hisi
Imetolewa jana hakuna anayeona ni tatizo...Hebu rejea kauli ya "kila mtu abebe msalaba wake." Sasa linganisha ilivyopokelewa ilipotolewa na mwanasiasa toka Kilimanjaro vs ilipotolewa na mwanasiasa toka Geita.
Watu watambue kuwa mafanikio ya K'Njaro hayakuremka kama mvua.
Yalikuwa na sacrifice na jitihada nyingi.
Niliona watu wakiwa masikini sana kwasababu ya kuwekeza katika elimu.
Leo wanakula matunda ya uwekezaji wao inakuwa tabu
Ninaweza kueleza jinsi K'njaro ilivyo sacrifice katika elimu kwa ajili ya Taifa hili
Wao hawakuvunjika moyo wala kulalamika, walitafuta njia mbadala