Kiongozi huwa ipo hivi.
HAKUNA kitu ambacho kina Nguvu kama Sadaka. japo sadaka yaweza kuwa ya Aina Tofauti kutokana na Dhumuni la Mtoaji.
lakini Moja ya sadaka zenye Nguvu ni hiyo Sadaka Ya kuchinja (Sadaka ya Damu).
lakini unapaswa kutambua,Sadaka huwa zinaweza kwenda sehemu kuu mbili inategemea na mtoa sadaka,Kwa jinsi ya Imani Yake na Misimamo Yake/Nia ya hiyo Sadaka na Manuizi.
1)Kuna sadaka ambayo huwa inatolewa na kwenda kwa Mungu Mkuu.
Hii Ni Aina ya sadaka ambayo,Watu Huitoa na kuipeleka, kwa Mungu Mkuu au wengine huwa wanasema Mungu mwenyezi/Wa Mbinguni.
Kwa kuwa umezungumzia sadaka ya Damu/kuchinja nitaigusia hiyo.
Sadaka ya Damu Ni Aina ya sadaka ambayo hupatikani kwa njia ya kuchinja na kumwaga damu or kukatisha uhai wa kitu chenye uhai na damu.
Ni Moja Ya Sadaka Ambayo huwa INAWEZA kutolewa kwa minajili Kama
-Sadaka Ya Ukumbusho au Alama.
hapa yaweza kuwa Ni ukumbusho wa jambo Kati yako na Mungu .
hapa tunaona jinsi Mungu alivyomuambia mussa wachinje wanyama na damu ya wale wanyama waweke kwenye milango yao Kama alama,pindi atakapotokea malaika wa kifo Basi nyumba zao zisipitiwe na Umauti.
-Sadaka ya Ma Agano/Agano
Hapa tunaona jinsi,Ambavyo Ibrahim baada ya kuweka agano na kuongea na Mungu aliweza kumtolea sadaka za kutekezwa na kuchinjwa Kama ishara ya Agano lake na Mungu.
-Sadaka ya Kujitakasa na Maombi
Hapa tunaangalia jinsi,wakati Taifa la Israel lilipokuwa limekosea au kukosa chakula walikuwa wanatumia Aina Hii kama ishara ya kuomba Toba na Kuomba kitu ambacho walikuwa wanakosa..Hapa tunaona story ya Eliya na wale manabii wa bahari kuhusu Toba na swala la KUOMBEA mvua iliyokata
- LAKINI Pia Ni Moja ya sadaka
Ambayo huwez kutolewa kwa minajili ya manuizo/Manuizi.Au Msaada
Hapa tunaona jinsi Ambavyo Mfalme baada ya kuzidiwa kwenye mapambano alinuizia na kusema kwa Mungu endapo atamshindia Vita,Kitu Cha kwanza kukutana nacho Basi atakitolea sadaka na bahati nzuri Vita Alishinda lakini too badly Mtoto wake alijitokeza wa kwanza so ikamlazimu kumchinja (kumwaga damu Yake).
Nakadhalika.
Lakini nifupishe Habari
Kupitia Gharama na mengineyo. coz hii sadaka ilikuwa ina hatarisha maisha ya watu lakini pia ilikuwa Ina gharimu Sana maisha ya watu.
Ndipo Mungu mwenyezi ikamlazimu amtume Yesu Kristo kwa ajili ya kufanyika kafara na kupitia kafara ya Damu yake pale msalabani Basi kila ambaye ataliita Jina lake atapata nehema na wokovu.kama ilivyo leo hii
Kuna sadaka ambayo hutolewa na kwenda kwa Lucifer na miungu mengine.
Hii inahitaji Umakini na uziada wa kuielewa.
Sent using
Jamii Forums mobile app