Kwa hisani ya Malisa GJ
Kwa wasioelewa yanayoendelea kuhusu Masele. Ni kwamba Masele ni Makamu wa kwanza Rais wa bunge la Afrika (PAP). Hivi karibuni ameingia kwenye mgogoro na Rais wa bunge hilo Bw.Roger Nkodo Dang raia wa Cameroon. Masele anamtuhumu Dang kwa ubadhirifu wa pesa za bunge hilo, hivyo ameunda kamati ya kumchunguza.
Dang amekasirishwa na uamuzi huo na anaona Masele anafanya mbinu za kumuondoa ili yeye akalie kiti cha Urais wa bunge hilo. Kwahiyo Dang ameamua kumng'oa Masele kwenye nafasi yake ili yeye aweze kuwa 'safe'.
_
Dang amempigia Spika Ndugai kumuomba amuite Masele nchini ili yeye aweze kusurvive. Na Spika Ndugai leo kwa jazba amemsimamisha Masele ubunge wake na kuagiza arudi nchini haraka kwa kile alichokiita mambo ya hovyo. Lengo la Spika ni kumuokoa Rais 'fisadi' wa bunge la Afrika, Roger Dang. Yani Ndugai anatumika kwenye mgogoro usiomhusu.
Leo Masele ameliambia bunge la Afrika kwamba hatarudi nchini kwa agizo la Spika kama alivyoamriwa. Amesema Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemruhusu aendelee na shughuli zake za bunge la Afrika (PAP).
_
Amesema Rais wa bunge hilo Roger Nkodo Dang hataweza kumng'oa kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Rais kwa sababu hakuteuliwa, bali alichaguliwa na wabunge wa bunge hilo. Amesema na kushangiliwa na wabunge hao.
Nafikiri mmeelewa sasa. Maana wengine mlishaanza kumuwazia jiwe.!
View attachment 1100051