pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,565
Bro fanya utafiti kwanza, unasema asilete habari za kwenye vitabu wakati hata wewe hayo mambo umeyasoma sehemu fulani....
Ukiwa kwenye gari ambalo lipo kwenye mwendo na wewe pia unakuwa kwenye mwendo sawa sawa na lile gari.... ndio maana gari likifungwa breki ghafla utajikuta kama unavutwa kwenda mbele ni kwa kuwa wewe bado unakuwa upo kwenye mwendo wakati gari linakuwa limesimama. Pia hiyo ndio sababu ikitokea gari limegonga kitu mfano ukuta watu waliopo ndani ya gari kurushwa kupitia kioo cha mbele, hiyo ni kwa kuwa gari linakuwa limesimama ghafla huku likiwaacha wao wakiwa kwenye mwendo.
mfano wako huo uliotoa ni kwamba ukisimama juu ya hilo gari ambalo lipo kwenye mwendo halafu ukaruka juu basi utatua pale pale kwa kuwa na wewe pia unakuwa kwenye mwendo sawa sawa na hilo gari.
mkuu msome Newton na umuelewe
Hapo nilipobold hapana mkuu...ni kwamba kama gari ilikuwa inasafiri kwa 80km/h na wewe ukaruka...basi kwa muda fulani utaendelea kusafiri kwa hyo hyo speed ya 80km/h then speed itapungua na wewe utaanguka chini PWAAAAA...hapo air resistance inachukua nafasi ndo maana utapunguza speed na kujibwaga chini...ila isingekuwepo air resistance basi ungendelea kusafiri kwa speed hyo hyo mpaka wapi sijiui..