MKUU..! HUO NI UPOTOSHAJI.
Kuhusu speed
Unasema; >
Hekicopter zingekuwa zinatulia angani na kusubiria mji wanaotaka wafike ukufikie. Kwa hyo spidi hapo juu inatakiwa mtu aifeel maana ni spidi kubwa sana.
Hebu fikiria upo kwenye gari lenye mwendo fulani (lets say 80km/hr),na ndani kuna nzi anaranda randa tu humo, tuchukulie huyo nzi yupo mbele kwa dereva na anataka aifike siti ya nyuma, je, kwa huo mtazamo wako unafikiri ataweza kuifikia hiyo siti kwa kuruka na kuganda hewani na kusubiri siti ya nyuma imfikie mahali alipo kisha atue, bila yeye kusafikiri kutoka mbele hadi nyuma kwenye hiyo siti?
Pili, Kuna ndege inaitwa North American X-15, nafikiri ndiyo ndege inayoongoza kwa speed kubwa, inatembea kwa 7,200 km/h.
View attachment 466011
Hiyo sio speed ndogo mkuu, sasa tuchukulie upo humo ndani, unataka kuniambia utaifeel hiyo speed eti kwa sababu tu ni kubwa?
Kuhusu gravity
Unasema;
Wanasayansi wanasema gravity ni kubwa sana inashikilia majengo, maji yaliyopo baharini na kadhalika ila hyo gravity imeshndwa kushikilia vitu vidogo kama wadudu, ndege mnyama na samaki waliopo baharini.
Kwanza, unatakiwa ujue kuwa force ya gravity huathiriwa na medium (fluids), hapa nina maanisha kuwa kitu kikiwa kwenye fluid(hewa au kimiminika) yeyote huwa kuna force inayokinzana na gravity, inaitwa upthrust, kiwango cha upthrust kinategemea nature ya fluid yenyewe(viscosity), pamoja na mass ya kitu chenyewe.
Halafu pia ujue kuwa gravity haijashindwa kushikilia vitu vidogo, hao wadudu na ndege wanaoruka huruka kwa msaada wa hewa (inayo-offer upthrust kwa msaada wa mabawa yao), and trust me, isingekuwa hewa wasingeweza kuruka. Na huwa wanatumia nguvu kubwa kupata momentum ya kuruka juu kukinzana na gravity, hadi watakapopata desired momentum ndio wanarelax. Lakini kwa wadudu wadogo sana garavity huwa inaeffect ndogo sana kwao(kama jinsi ilivyo kwa unyoya mwepesi unaoelea angani),hii ni kwa sababu hewa inakuwa inaoffer upthrust kubwa inakaribiana mno na gravity. Ndio maana wadudu kama mbu,utaona kama hawathiriwi na gravity, ila sio kweli. Effect huwa ipo ila nayo inakuwa cancelled na upthrust ya hewa.