Ukweli kuhusu Dkt. Slaa kuondoka CHADEMA

Ukweli kuhusu Dkt. Slaa kuondoka CHADEMA

Wananchi gani waloipokea habari hii kama sio nyie watu wa mitandao, JF na Chadema?.. Mlisema haya haya mlipounda UKAWA mkapigwa bao la wazi kabisa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM wakapata zaidi ya asilimia 80, bado mkadai namba zenu bora zaidi ya mwaka 2009. Kuna siri ama kitu kilichopokelewa kama UKAWA wakati wa Serikali za Mitaa mbona hamkushinda?
ila hivyo viti vya upinzani vilichukuliwa kutoka ccm. so upinzani walipiga hatua kubwa serikali za mitaa na ccm walipoteza. huo ndio ukweli
 
Lowasa ameondoka CCM sababu kuu ni kukatwa Jina, najiuluza kwanin asingekubali matokeo?

Kwa maana hiyo umemanisha kwamba wale wote 42 ni taka taka wew pekee ndo Msaf na ulifaa kuchukua ile nafasi.

Binafsi naona ni tamaa ya madaraka,

Pia Lowasa unapaswa ujiaweke katika position alikua nayo dr slaa kwa sasa ungejiskiaje au unahisi kwa haiba ulokua nayo wew unge chukua maamuz gan?

So hata Kama slaa atahama chama binafsi sitomlaumu sababu naona amedharirishwa sana kwa hili. Na Kama atauchukua uamuzi huo hapaswi kulaumiwa coz hiyo ni democrasia so tusimsifie tu lowasa kwa mnayoyaita maamuz magum et coz kaja CHADEMA pia tukubaliane na maamuz ye yote ya slaa na tuyaheshimu

Hujaambiwa kwamba lazima alitaka hasikatwe bali alichosema ni kutofutwa kwa taratibu za kawaida kabisa ktk mchakato hazikufuatwa
 
Kukaa kwake kimya kunawapa CCM kutumia vyombo vya habari kuvuruga wananchi. Huu si wakati wa kukaa kimya.
 
Ndio nampongezakwa kujua anao mchango mkubwa wa harakati za ukombozi dhidi ya udhalimu katika Nchi yetu.

Hata hivyo Slaa asitake kupumbaza watu.

Kinacho mtafuna mtima wake ni MATARAJIO makubwa ya Uraisi uliojengwa na kujengeka ndani yake.

Umaarufu mara nyingi huleta KIBURI kibaya sana!

Agenda ya ukombozi kama aliyokuwa
anaipeperusha kila uchao inapaswa kuwa na mbinu mkakati anuai.
Adui yetu mkubwa ni mfumo kandamizi wa Chama Tawala.

Hili lingepaswa kushugulikiwa kwa mbinu zozote, whatever it takes!

Mzee wangu et al wameonesha udhaifu mkubwa katika hili.
Hata kwa utume wake kama Padri,
Mtu asiyejua "kuachia, kusamehe na kusahau" inanipa shaka sana juu ya weledi na uwalei wake

Tunajifunza nini kwa Mandela aliyekuwa tayari kukaa pamoja na maadui zake kwa maslahi mapana ya taifa?!,

Tunajifunza nini kwa Mwl Nyerere aliyekuwa tayari hata kukutaa vyeo ili kwanza ukombozi wa mtanganyika upatikane?!

Tunajifunza nini kwa viongozi kwa fomer east and west germany walivyoona kuwa ipo hoja ya kuzika na ku-amend tofauti zao for national interests!

Kama ushahidi usio na hisia, Lowassa, juzi kaomba mumfikishe mahakamani basi kama upo ushahidi.
Vp Slaa anaweza kulitekeleza hilo kwa maslahi ya Taifa?

Hata YESU aliyekuwa anamtumikia alikuwa tayari kukaa na watoza ushuru ili kuitimiza torati. Nayo ni kumkomboa mwanadamu!

Vinyongo na Kukataa matengenezo na maridhiano ni mpango wa shetani.

TAFAKARI NA CHUKUA HATUA!
 
Kuna kundi limeibuka ghafla wakijifanya kuwa na uchungu sana na CHADEMA kumbe ni wanafiki, moyoni wako CCM. Wakati Magufuli anatangazwa kundi hilo hilo liliibuka na kuwashauri CHADEMA wakomae na ubunge. Ujio wa Lowassa umeonyesha rangi za baadhi ya watu. Sasa ni kama wamechanganyikiwa na kujifanya washauri wa CHADEMA.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyempinga Lowassa na kumuita mwizi wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM ili asipitishwe sababu kubwa niliona upepo wake ulikumba hata wasiokuwemo. Nilijua wakimpitisha tu wapenda mageuzi tumekwisha kwani upepo wake ungepiga hadi kwenye majimbo ya upinzani, na badala ya kuongezeka yangepungua. Kuna wabunge wengi wa CCM walitegemea sana upepo wa Lowassa uwapitie. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanaomba bora wangejitoa CCM mapema kabla kura za maoni CHADEMA hazijafanyika.

Ndugu zangu upepo wa wanasiasa ni mbaya sana kuna wabunge CHADEMA upepo wa Dr.Slaa uliwapitia hadi leo hawaamini kama wapo mjengoni. Lowassa upepo wake ni mbaya sana. Dr.Slaa angemsumbua Dr.Magufuli lakini asingemshinda. Vile vile kwenye UKAWA ujio wa Lowassa umeleta mshikamano zaidi. Ninaamini kuna wana CUF na NCCR wasingeweza kumpigia kura Dr.Slaa zaidi ya wabunge wao. Lakini Lowassa ni kama amekuja kuwaunganisha UKAWA. Zitabebwa kura nyingi sana hapa.

Hawo wasiomtaka Lowassa ni wale waliotaka wapinzani wawe wapinzani milele. Ndio wale utawaskia Urais CCM, Ubunge upinzani. Huo ni unafiki mkubwa. Tunahitaji CCM itoke kabisa. Sasa ujio wa Lowassa ni kama umewachanganya sana wamebaki kujifanya wanakishauri chama kumbe wanafki wakubwa. Lengo kuu la chama ni kushika dola kama kuna upenyo umetokea wa kukupeleka huko utumie ipasavyo. Muda ndio huu ukipita CCM itatawala milele.

Mkuu hayo uliyo yaandika ndio ukweli unaotaka kugeuzwa uongo na hao waumini wa viongozi wa chama tawala kutaka kutudanganya watanzania yubakie kutawaliwa na ccm kama mazuzu tu,huu ndio mwanya wa kuitoa ccm madarakani na hilo halina ubishi hata ccm wenyewe wanalihofia sana,tushikamane kwa sasa kuliko kipindi kingine chochote ili kumtoa ccm
 
Hata kama Slaa hana mpango wa kujitoa CDM, lazima ana mgogoro na viongozi wenzake.

Inakuwaje Katibu mkuu wa chama hajazungumza lolote juu ya ujio wa Lowasa?

Kwanini Naibu katibu wa Zanzibar ndo msemaji mkuu wa sasa kwa mambo mazito ya chama?

Kwanini watu wengine ndio wajibu malalamiko dhidi ya Slaa? Kwanini asijitokeze hadharani kuweka mambo sawa?

Makamanda tuko njia panda, hatuelewi kinachoendelea UKAWA baada ya ujio wa Laigwanani.
 
Unategemea nini kwa nchi iliyojaa waimba taarabu kama Tanzania????

Wameshaguswa kunakowasha, lazima waropoke ropoke kama hivyo wanavyofanya.

The end justifies the means

Kwa yeyote anayeendelea kuitetea ccm kubakia madarakani,huyo atakuwa anatumiwa na ccm au ananufaika na mfumo wa utawala wa ccm haiwezekani leo baada ya miaka 54 ya uhuru mtanzania unatibiwa chini ya kivuli cha mti,watoto wanakaa chini ya mti kusoma ,watoto wana kaalia matofari kusoma wakati misitu yetu inamalizwa na viongozi hawa wa ccm kwa kusafirisha magogo na mbao kwenda nje ya nchi,tuwakatae ccm
 
Kawadanganye walevi wenzio,uchaguzi wa serikali za mitaa ccm mmepigwa bao hadi mkaambulia 63.5%leo unataka kutuongopea eti 80%?

Sasa kama ccm imepata asilmia 63.5 si bao pia au mnafurahia kupitwa kidogo,michadema bwana.
 
atakumbukwa kwa kugomea harakati mwishoni.

Atakumbukwa sio kugomea Bali kusaliti kama kugomea angegoma kule kwenye vikao sio baada ya kukubaliana na vikao halaf anakuja kuonyesha true colour zake
 
Ziko habari za uzushi kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa, zinaandikwa na kuenezwa na Gazeti la Raia Tanzania kwa siku kadhaa mfululizo sasa.

Uongo huo wa Raia Tanzania leo umeendelea kwa kiwango cha juu zaidi kiasi cha gazeti hilo kuandika kuwa eti Katibu Mkuu Dk. Slaa amekabidhi nyaraka za chama kwa dispatch saa 3 usiku juzi.

Wakuu, hakuna uongo uliokubuhu kama huo. Mtakumbuka uongo huo wa kwamba KM Dk. Slaa anarudisha mali za chama zilienezwa usiku wa juzi mitandaoni na mmoja wa waandishi wa habari aitwae Manyerere Jackton.

Kwa bahati nzuri wakati Jackton (mtu ambaye tunaheshimiana kwa sababu ya kikazi na kitaaluma) wakati akijipatia jukumu la kuandika uzushi badala ya habari na kusambaza uongo badala ya taarifa, binafsi nilikuwepo ofisini physically. Nilikanusha kupitia Jamii Forums ambako alidanganya kwa jina lake, huku 'akijiapiza'.

Uongo huo ambao leo umeshadidiwa na Gazeti la Raia Mwema leo, ulisababisha taharuki isiyokuwa ya lazima kwa waandishi wa habari kadhaa ambao walinitafuta (si Raia Tanzania wala Jackton) na nikawaruhusu waje Ofisini wakitaka usiku huo ili waone namna ambavyo wako watu au chombo cha habari kinaweza kujivika kazi ya kusambaza uongo. Kujeruhi na kuua ukweli.

Kazi ya kujeruhi na kuua ukweli hufanywa sana na maadui wakati wa mapambano kama ilivyo sasa katika mchuano wa kisiasa unaoendelea nchini kuelekea Uchaguzi. Maadui wa CHADEMA wako kazini. Lilitarajiwa hilo.

Wakati Raia Tanzania wakikoleza uongo wao kwa kusema eti 'majira ya saa 3.15 hivi' lilifika Gari aina ya Noah maeneo ya ofisini kisha eti watu wawili wakaingia ofisini wakiwa na mkoba mwekundu, muda huo mimi nilikuwa Ofisini. Hakuna kitu cha namna hiyo kilichofanyika. Labda kama Ni Kwenye Ofisi za gazeti hilo.

Naandika haya nikiwa na uchungu. Kwa sababu huwa sijisikii vizuri kabisa kulumbana na wenzangu (senior fellas) kwenye taaluma ya habari. Tena kwenye mambo ya hovyo yanayohusu kuvunja vunja kabisa misingi ya uandishi wa habari i.e accuracy, facts, truth, objectivity etc.

Inapofikia hatua Gazeti kama hilo linashindwa kabisa kusimama kwenye kitu kiitwacho Social Responsible Journalism inatia aibu na kichefuchefu kwa jamii ya watu makini wanaotaka ushindani wa kisiasa unaoendelea nchini ufanyike kwa misingi ya kila mdau kutimiza wajibu wake inavyotakiwa. Uwajibikaji.

Nimalizie kwa kusema yafuatayo; Katibu Mkuu hajajiuzulu. Nafasi yake haiko wazi kama ambavyo gazeti limepotosha.

Agenda ya kuandika uzushi na uongo kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa na CHADEMA wanayotekeleza Gazeti la Raia Tanzania walioko nyuma yake wanajulikana. Ni agenda ya CCM na Mawakala wao. Wasaliti wa mabadiliko ambao hawajaamini kuwa ndege ya mabadiliko hatimaye inaruka wakiwa wametupwa nje kwa sababu ya usaliti wao wa kufanya kazi za CCM wakiwa ndani ya CHADEMA kabla hawajatimuliwa.

Mojawapo ya malengo ni kuwachanganya wanachama, wapenzi, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA katika kipindi hiki muhimu kinachohitaji utulivu wa mwili, akili na roho ili kupanga mikakati ya kumdhibiti adui na kuweka kila kitu sawa kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Inaitwa diversion. Ili badala ya kuendelea kuwa focused kwenye masuala ya msingi eti tuanze kukimbizana na propaganda!

Aidha, baada ya CCM kusambaratikia Dodoma na sasa iko vipande vipande ikiwa ni mwendelezo wa kuanguka kwa 'himaya' hiyo huku Wananchi wakipandisha mori wa mabadiliko kupitia BVR, lengo jingine ni kutaka kuuhadaa umma wa Watanzania kuwa eti CHADEMA nayo imegawanyika. Wanaota.

Mgawanyiko wa chama cha siasa huwa unatokea kwenye vikao pale ambapo maamuzi yanashindwa kufanyika au kufukiwa. Hakujawahi kutokea jambo la namna hiyo ndani ya chama.

Kwa sababu chama kimejenga utamaduni wa kusimamia misingi katika kusimamia na kuendesha masuala yote, kinaendelea kuwa imara kadri tunavyosonga kuelekea Uchaguzi mkuu.

Uimara huu wa CHADEMA kikijiandaa (kwa kushirikiana na vyama wenza katika UKAWA) kwenda kushinda Uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali, ni mpango wa Mungu. Tujiandae kwa propaganda kubwa zaidi ya hizo za Raia Tanzania.


Tutashinda.
Makene

Source: Chadema blog

Chadema Blog: HABARI ZA UZUSHI ZILIZOANDIKWA NA KUENEZWA NA GAZETI LA RAIA TANZANIA KUHUSU KATIBU MKUU WA CHADEMA DR SLAA

Tunashukuru sana kwa taarifa,na hao wanatumiwa kusambaza habari za kijinga namna hiyo hasa hilo gazeti tutaliweka ktk orodha ya vijarida tulivyokwisha kuvisusa na kwa sasa wanavununua wauza vitumbua
 
Siyo vizuri kufanya kejeli kwa kiongozi kama Dr. Slaa aliyejitolea muhanga katika kuimarisha upinzani kwa mbinu na hoja zenye mashiko. Leo hii Chadema/UKAWA imeweza kuwa na nguvu sana na hata kukubalika na wananchi kama mwamvuli wao wa ukombozi kwasababu ya Dr. Slaa. Leo hii vinaonekana viashiria vya UKAWA kuweza kushawishi wananchi na hata kuweza kupata ridhaa kwao ya kuongoza dola, halafu unasema eti Dr. Slaa anatamaa ya kutaka uraisi. Hivi kweli mmesahahu juhudi za huyu kiongozi mara hii? Je Dr. Slaa alikuwa katika mlengo gani na mh. Lowasa? Unajua image ya Dr. Slaa kimataifa na damege aliyonayo mh. Lowasa (nenda katafute taarifa za SFO).

Hivyo siyo vizuri kabisa kumshutumu Dr. Slaa na kumkejeli kwa tuhuma rahisi hivyo. Muacheni mzee wa watu apate faragha na muda mzuri wa kujitafakari na kuona nini anaweza kuendelea kukifanya. Tusimshurutishe kulingana na matakwa yetu, bali hekima kubwa inaweza kutumika katika kushauriana naye.
 
Aondoke! Arudi kanisani! Dr Slaa asingeweza kumshinda Magufuli,tungeleteana habari za ooh tumeibiwa kura ohhh hatumtambui Rais! We fade up! Safari njema Slaa
 
wewe kinachokuuma ni mini kwa masuala yasiyokuhusu
 
Atakumbukwa sio kugomea Bali kusaliti kama kugomea angegoma kule kwenye vikao sio baada ya kukubaliana na vikao halaf anakuja kuonyesha true colour zake
tafakari neno MSALITI
 
Atakumbukwa sio kugomea Bali kusaliti kama kugomea angegoma kule kwenye vikao sio baada ya kukubaliana na vikao halaf anakuja kuonyesha true colour zake

mnaandika wenyewe mna jijibu wenyewe
 
Back
Top Bottom