Kutoka Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya UVCCM taifa
Majibu kwa Madai ya John Mnyika,Katibu Mkuu wa Chadema.Ukweli Dhidi ya Upotoshaji
1. Ukweli kuhusu Mamlaka ya TAMISEMI
Madai ya John Mnyika kwamba TAMISEMI imepokea majukumu kinyume na sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ni upotoshaji wa wazi na unaonyesha ukosefu wa uzalendo na Weledi kwa masuala ya kitaifa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 10(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya mwaka 2024, ni kweli kwamba Tume Huru ya Uchaguzi inatakiwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa. Hata hivyo, utekelezaji wa jukumu hili utaanza mara tu baada ya Bunge kutunga sheria mpya itakayoiwezesha Tume hiyo kushika majukumu hayo kikamilifu. Kwa sasa, TAMISEMI inaendelea kusimamia uchaguzi huu kwa mujibu wa sheria zilizopo, ambazo hazijarekebishwa.
Kutofahamu hili au kupotosha makusudi ni dalili ya upungufu wa weledi kwa upande wa Chadema na uongozi wake. Wanashindwa kufahamu mchakato wa kisheria ambao upo wazi. Kushambulia taasisi muhimu kama TAMISEMI kwa masuala ya msingi kama uchaguzi ni kuonesha ukosefu wa uzalendo kwa maslahi ya kitaifa.
2. Uhamasishaji wa CCM kuhusu Uandikishaji
Madai kwamba CCM na TAMISEMI hawahamasishi wananchi kujiandikisha kwa uchaguzi ni upotoshaji. Kila mtu anajua kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,Mwenyekiti wa CCM na DKt Emanuel nchimbi Katibu wa CCM taifa na Dkt Hussein Mwinyi Makama mwenyekiti wa CCM zanzibar na pia Rais wa Zanzibar kupitia ziara zao nyingi, wamekuwa wakihimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi. Hili ni jukumu ambalo CCM limekuwa likilitekeleza kwa dhati, kwa kuhimiza vijana na makundi mengine ya kijamii kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa mfano, UVCCM ilizindua kampeni ya 'Kijana na Kijani' tarehe 6 Julai 2024, Uwanja wa benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam yenye lengo la kuhamasisha vijana kushiriki siasa na uchaguzi.
Hii inaonesha jinsi vijana wa CCM walivyoandaliwa vizuri na chama. Wamepata mafunzo bora ambayo yamewafanya kuwa viongozi wa kizalendo wanaohakikisha masuala ya uchaguzi na ushiriki wa wananchi yanapewa kipaumbele.
Upotoshaji wa Mnyika unadhihirisha kukosa maono ya kitaifa na kujikita zaidi kwenye propaganda zisizo na msingi.
3. TAMISEMI na Vyombo vya Habari
Kinyume na madai ya Mnyika, TAMISEMI imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu uchaguzi ujao. Kwa kushirikiana na vyombo vya habari, mabango, na mitandao ya kijamii, ratiba ya uchaguzi tayari imetangazwa rasmi. Uchaguzi utafanyika tarehe 27 Novemba 2024, na zoezi la uandikishaji litafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024. Vibao vya kuhamasisha vimewekwa maeneo mengi nchini, kama barabara ya Kibondo kuelekea Kagera (Nyakanazi), ambavyo vinaonesha wazi uhamasishaji unaofanywa na serikali na TAMISEMI.
4. Propaganda za Mabalozi wa Nyumba Kumi
Madai ya John Mnyika kwamba mabalozi wa nyumba kumi wanatumika kuandaa orodha ya wapiga kura ni upotoshaji wa wazi na wa kusikitisha. Mabalozi wa nyumba kumi ni sehemu ya mfumo wa uongozi wa kijamii uliojengwa kwa muda mrefu na katiba ya CCM. Majukumu yao ni kuthibitisha na kuhakiki orodha ya wanachama wa CCM, si kuandaa orodha ya wapiga kura kwa lengo la kudhibiti mchakato wa uchaguzi, kama Mnyika anavyodai. Kutokuelewa au kupotosha ukweli wa majukumu ya mabalozi ni dalili ya kukosa weledi kwa Chadema, na ni kielelezo cha jinsi chama hicho kimeshindwa kutafsiri vizuri mifumo ya ndani ya vyama na majukumu yake.
Kwa jumla, CCM ni chama makini, ambacho kimeandaa viongozi wake, hasa vijana, kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu. Madai ya Mnyika ni propaganda za kutaka kupotosha ukweli na kujaribu kuonyesha udhaifu ambao haupo. Ukweli ni kwamba CCM imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata haki yao ya kushiriki uchaguzi, huku vijana wa UVCCM wakiwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanaelimishwa na kuhamasishwa.
Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya UVCCM-taifa.
#kijanaNaKijani
#TunazimaZoteTunawashaKijani