Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Tusiingize masihara kwenye maisha ya watu unaweza kutupatia ushahidi ya waliolipwa fidia kama ambavyo nimeweka Mimi hapo juu?
Mtahangaika sana lakini hamtashinda! Wenye maeneo walilipwa siku nyingi nyinyi mlikuja kuvamia tu au mlipigwa changa la macho poleni sana... sisi tunataka maendeleo siyo blabla!
 
OMG.. Mungu akusaidie, i repeat again where did you copy & paste all these?

6 lanes unahitaji 19 meters? Uko duniani na una macho na ubongo? Uuuuhh.. Ur gone, ur lifeless, nyie ndio wasomi? Hii copying & pasting ni hatari sana..

I won't help you, the world will help you..!!
Mkuu huyo ni zero hajui kitu ni kweli amekopi na kupasti hapa JF eti m 19 inatoka 6 lanes!!
 
Mahakama zetu nazo angalieni zinavyofanyakazi. Ndo hao majaji wanapangiwa hata bei za kuachia makosa ya mauaji. Ndo hao wamekuwa wakiwalinda wanaovamia viwanja vya wenzao eti aliyepoteza kiwanja apatiwe kingine, nk.

Usijisikie vibaya serikali ikiamua kuachana na maamuzi yao bora tu iwe ni kwa lengo la manufaa kitaifa. Tukianza kuendeshwa kwa amri za mahakama, nchi haiendi. Tuna majaji wadhaifu sana kuliko unavyoamini. Duniani kote hakuna aliyeendelea kwa mtindo huo au eti demokrasia. Hakuna nchi iliyoendelea kwa sababu ya demokrasia. demokrasia huja baada ya maendeleo.

Demakrasia ya KWELI ndio msingi wa maendeleo endelevu.

Kama CCM itaendelea kuwa na makada wenye mawazo kama yako juu ya demokrasia taifa hili litachelewa sana.

Na nchi hii itakua haina maendeleo zaidi ya ujinga utakaoshamiri kwa kile watakachowajaza watu kwa hofu. Na ili uwatawale watu milioni 45 wa makabila 125 na dini tofauti kwa mfumo wa kibabe ni lazima wawe wajinga.Lazima wanaosoma vyuo wawe wachache sana kwa lengo la kuwapatia vyeo. Tena wasomeshwe kwa sifa ya kuwa makada wa chama.

Ulaya kuna vinchi vingi sana vidogovidogo vyenye maendeleo makubwa kuliko bara zima la Afrika kwa kanch kamoja tofauti na Afrika nzima kutokana na ukweli kuwa wenzetu walipinga kwa karne nyingi kutawaliwa kibabe. Kila ufalme na Lugha ziliamua kujitawala na kuheshimu utu wao na watu wake na kupinga ubabe wa watu wengune na kuamua kujitenga. Ingekua wazungu wanaendekeza ubabe basi wote wangemuunga mkono Adolf Hittler ili aitawale ulaya kidikteta. Wazungu walijua kuwa pamoja na maendeleo lakini heshma ya mzungu ilitakiwa ipiganiwe isije ikapotea na kupoteza rasilimali watu (Wayahudi) ambao walikua ni nguzo kuu ya teknolojia kwa nchi za ulaya.

Unaweza ukawa mbabe kwa nchi jirani ili wasiingie kienyeji au kufanya uvamizi lakini huwezi kuwa mbababe kwa wananchi wako.
Serikali ni lazima isimamie uhuru,usalama na umoja wa watu wake na haki zao kikamilifu. Watu wenye usalama wa kutosha ndio wanaoweza kujenga taifa lao na kuwekeza bila hofu.

Ukijenga taifa la kibabe kwa muda mrefu sikua ukilazimika kuleta demokrasia basi ujue utaidumbukiza nchi kwenye ghasia. Itakua sawa na kuwafungulia wafungwa wote magerezani na kuwaacha waranderande mitaani mana walikua wamebanwa na kunyanyasika gerezani.

Nilitegemea makada wa CCM waishauri serikali itumie ubabe kukamata vijana wazururaji wasio na makazi na kuwapeleka porini na kuwapimia mashamba kulima na viwanja kwa lazima .Wajiajiri kwenye kilimo na ufugaji. Pia Kuwalazimisha wapige matofali na kuyachoma . Kutoa amri ya Kupeleka mafundi wa magereza na JKT kusimamia ujenzi wa makazi ya wananchi kwa faida yao wenyewe.
Serikali ingetumia ubabe kuwalazimisha wenye viwanda kutoa mabati ,nondo, misumari,sementi, marumaru n.k. na kuwaikabidhi serikali kwa bei ya ndogo sana ikiwezekana kurudisha gaharama za uzalishaji tu ili kila mwaka ijenge nyumba 100000 za wananchi wake maskini na wale wanaovunjiwa nyumba.Kwa miaka 10 ni nyumba 1000000.
Wananchi wangehamasika sana naaendeleo ya haraka yangeonekana.
Baada ya hapo unawalazimisha wanchi kuchimba barabara na kuchimba mitaro na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme na kuzisimamisha kwa faida yao wenyewe. Pia Kuchimba mitaro na kuweka mabomba ya maji.Kupiga matofali na Kujenga mashule kwa ajili ya watoto wao. Kujenga mahosipitali kwa ajili ya afya zao na kwa faida yao. Lakini pia ni lazima waambiwe ni kwa ajili ya faida yao wenyewe.
Huu ndio ubabe wa kimaendeleo. Ndio ubabe utakaojenga uchumi kwa kasi. Ndio ubabe utakaoinua maisha ya wanyonge.
Ndio ubabe utakaoleta ajira ya uhakika kwa vijana wa taifa hili. Hapa ndipo tunapoweza kusema demokrasia isiingilie maendeleo

Lakini ubabe wa nchi nyingi za kiafrika kwa wananchi wao ni kwa ajili ya kuwalinda watawala na vyama vyao wasije wakatolewa madarakani.
Mtu anaweza akaangamiza na kutisha kundi moja kwa lengo la kufurahisha kundi linalomuunga mkono. Hii sio mbinu sahihi ya kuleta maendeleo kwa kuharibu maendeleo ya watu waliokuwa wanajitafutia riziki zao kwa kubangaiza. Ni kuongeza umaskini kwa wanyonge.
 
tatizo ni kwamba maadamu wameona mamba majini wanamiminia dawa kumbe kwenye maji hayo kuna viumbe vingine.uongozi sio hivyo
 
Unasemaje kuhusu utekelezaji wa sheria moja kibaguzi kulingana Na wananchi walipiga kura kivipi?
Ungekuwa umesoma mada yangu ndio ungeweza kuniambia hayo maendeleo unayoyasema ni yapi!
Hiyo unayoiita mada, nimekuuliza ukaruka kwamba umenukuu hukumu ya mahakama kuu. sasa kwa hili tena unasema ni makara yako.'

Tuachane na maisha ya ushabiki. Siamini kwamba rais ni dikteta, au hajui anachokifanya. Utawala uliopita ningeweza kusema maana mifano ya kutosha ipo. Au nawe unaamini hivyo kama huyo anayejiita mwanasheria wakati anaelewa vitendo vya dikteta huwa vikoje?
 
Tuache theory. Niambie nchi gani iliyoendelea ambayo imefika hapo kwa sababu ya demokrasia. Moja tuu unayoijua.
 
Wananchi wakafungue kesi Canada na Marekani wazuie Dream-liner na Bombadia Kama Serikali inavunja Sheria dawa yake ndio hiyo Dawa ya Jeuri ni kusudi.. Siamini ukatiri kama huu unafanyika yaani idara zote zinavunja Katiba wazi wazi wakumbuke waliapa kwa Mungu wao...! Nawataka wawalipe fidia na wawajengee upesi nyumba kwenye maeneo yao sema this time kuwe na mpangilio bomba

Mahakama haisikilizwi wala kuheshimiwa, ila Daud A.B ndiye anayesikilizwa na kutiiwa.
 
Habari na maelezo cku hizi ndio wasemaji wa ccm ....mara paap binti kawawa kajibu mara paaap oooooh tunadaiwa ila sio vizuri kuongelea.idara ya maelezo hawana kazi lazma waishi kwa kutumia nguvu nyingi waonekane wanafanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu anajaza kurasa kumbe anawatetea wengine walishalipwa wakala na sahivi wanajifanya kudai eti wanaonewa. Wanasheria uchwara wanahangaika kuwatafuta wajinga ili wawalie pesa zao, wajinga ndio waliwao
 
Nasikia kuna hukumu ya mahakama ya juu kabisa kutengua hukumu za chini. Kwa mantiki hiyo bado zoezi kisheria ni sahihi na hakuna zuio la mahakama za chini lenye nguvu.
Tarehe 30 agosti 2017 Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo na msemaji Mkuu wa serikali alivitisha vyombo vya habari juu ya kuripoti zoezi la bomoa bomoa Kimara hadi kiruvia kwa sababu zoezi hilo linafanyika kisheria.

Ukweli ni kuwa bomoa bomoa hii ni kinyume cha Katiba ya nchi, Sheria ya barabara Namba 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009, inakiuka pia hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi iliyotolewa na Jaji S.B.Bongole tarehe 31 Mei 1013 katika shauri namba 80 la 2005. Na pia inakiuka hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyotolewa na Jaji S.A.N Wambura tarehe 13 Juni 2016 katika shauri namba 151 la 2015. (Naambatanisha Hukumu za mahakama husika)

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitamka kuwa Kanuni ya Sheria “The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”. Na ikaendelea kuwa ardhi inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara ya Morogoro, iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa opereshani vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999, ardhi hiyo ni mali halali ya wananchi waliofungua malalamiko.

Aidha katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitambua kuwa kuwa eneo husika (Jiji la Dar es Salaam) hivi sasa linatawaliwa na Sheria ya Mipango Miji ambayo inataka hifadhi ya barabara kuu kuwa ni mita 60 tu, yaani mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

Baada ya kushindwa Wizara ya ujenzi (Serikali) ikiiongozwa na Rais wa sasa Mhe John Pombe Magufuli ilikata rufaa Mahakam ya Rufaa katika shauri na 151 la 2015, ambalo lilitupiliwa mbali kwa kukosa hoja za msingi.

Tunasema kuwa Mhe Rais anavunja katiba aliyoapa kuilinda katika bomoa bomoa hii kwa kuwa Kifungu 107 (A) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kinatamka “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki”.

Hivyo basi kwa kuwa wananchi walishapatiwa haki ya ardhi yao na mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa bomoa bomoa inayoendelea inakiuka katiba ya nchi ambayo Mhe John Pombe Magufuli aliapa kuilinda.

Hivyo kitendo cha kuwapora wananchi ardhi yao waliyoipata kihalali na kwa mujibu wa sheria za nchi ni na umiliki huo kuthibitishwa na mahakama ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi, Mhe Rais aliyoapa kuilinda, tena baada ya kuwaharibia mali zao ikiwemo nyumba n.k. Kifungu 24 (1) cha Katiba ya Tanzania kinachotamka Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. (2) “Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili”.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni “Kulinda usalama wa raia na mali zao, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kudhibiti uhalifu, kuwakamata watuhumiwa na kudumisha amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Lakini cha kushangaza ni jeshi hili hili ambalo linalotakiwa kulinda mali za watanzania kwa mujibu wa katiba, sheria za nchi na dhima yake ndilo ilnalotoa ulinzi kwa Tanroads kuharibu nyumba na mali za watanzania kwa kukiuka hukumu za Mahakama kuu na mahakama ya Rufaa. Kwa hili tumtaje IGP Mpya kujitafakari upya Na kuishauri mamlaka take ya uteuzi kuhusu ukiujwaji huu mkubwa wa Katuba ya nchi.

Kifungu 29 b cha Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, GN No 21 ya tar 23 Januari 2009 kinatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa eneo la kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mita 60 tu toka katikati ya barabara kila upande kama inavyoelekezwa barua ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani ya tarehe tarehe 21 Oktoba 2010 yenye Kumb Na TRD/CR/R.10/13/Vol.III/34 kwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha. Tokea kupitishwa kwake 2007, Tanroads walikuwa wakiheshimu sheria hii lakini tokea Mhe John Pombe Magufuli aliporejeshwa kuwa Waziri wa Ujenzi tarehe 24 Novemba 2010, akatoa maagizo kwa Tanroads kuwa wavunje sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake za 2009. Na alipochaguliwa Rais anatumia wadhifa wake kukiuka Katiba, Sheria Na haki za binadamu.

Bomoa bomoa hii pia inakiuka mikataba mbali mbali ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia kama ifuatavyo:-

  • Ibara ya 25 ya Tamko la Haki za Binadamu (Universal Decralation of Human Rights) inatambua haki za makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu.

  • Ibara ya 11 (1) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni wa 1966, ulioridhiwa na Serikali ya Tanzania tarehe 11 Juni 1976, (ambao Kamati ya Prof Osolo aliutumia kujenga hoja ya nchi kuwa haki zaidi juu ya raslimali zake) unazitaka Serikali zilizouridhia kutambua kuwa kila raia na familia yake wana haki ya kupata kiwango stahiki cha hali ya kimaisha ikiwemo chakula, mavazi, makazi na kuendelea kuboreshwa kwa hali zao za kimaisha.

  • Tamko namba 77 la 1993 la Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadumi linatamka kuwa “uhamishwaji kimabavu” (Forced eviction) ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaopelekea uvunjifu wa haki zingine za kibandamu kama vile kuwakosesha raia makazi, chakula, maji safi, afya, elimu, ajira, kipato, usalama, na kinga dhidi ya vitendo vya kinyama na udhalilishwaji n.k

  • Tamko namba 7 la 1997 la Kamati hiyo kupinga “Uhamishwaji Kimabavu” linasisitiza kuwa haki ya makazi ni pamoja na binadamu kuishi mahali kwa usalama, amani na heshima; na kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane na uhuru wa raia kulindwa dhidi ya uhamishwaji kimabavu na uharibifu wa makazi yake; kuwa na faragha katika makazi yake na kulindwa dhidi ya kuingiliwa isivyo halali. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi hivyo ni haki yetu sisi kama raia kupatiwa ulinzi dhidi ya vitendo vya Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi yetu vinavyolenga kutuhamisha kimabavu kwa kutuzuia kuendeleza mali zetu halali, kuharibu kwa makusudi majengo yatu na vitisho vya aina mbali mbali.
Tamko hilo lilifafanua zaidi kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane ulinzi wa umiliki wa ardhi na makazi; fidia ya makazi, ardhi na maendelezo mengine; usawa katika kupata haki za makazi; na kushirikishwa katika maamuzi mbali mbali yanayohusu masuala ya makazi katika ngazi ya jamii na kitaifa. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi. Sisi raia tunaomiliki kihalali ardhi na makazi katika eneo husika tunayo haki kamili ya kushirikishwa katika maamuzi yote yanayohusu ardhi na makazi yetu.

Katika shauri lililokuwa mbele ya Mahakama ya Haki za binadamu ya Umoja wa Afrika (African Court on Human and Peoples’ Rights-Applications No 009&011of ka hiy2011), Serikali ya Tanzania ilinukuliwa kuthibitisha mbaele ya mahakama hiyo kuwa “it fully adheres to principles of the rule of law, separation of powers and independence of the judiciary as provided for under the Constitution of the United Republic of Tanzania”[1]. Hivyo vitendo vya Rais John Magufuli aliyekula kiapo kuilinda Katiba ya nchi kupuuza na kudharau hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa havikubalika hata kidogo katika nchi inayoongozwa kwa utawal wa sheria. Ni wakati sasa Mwalimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu kinchoheshimika cha Dar es salaam Prof Kabudi akamshauri Mhe Rais umuhimu wa kuheshimu hukumu za mahakama Na kujiepusha uvunjwaji wa Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.

Ibara ya 27 ya mkataba wa kimataifa wa Vienna (Vienna Convention on the Law of Treaties)provides that: “A party may not invoke the provisions of its internal law as justification for its failure to perform a treaty. Additionally, Article 32 of the International Law Commission Articles on State Responsibility 2001 provides that “the Responsible State may not rely on the provisions of its internal law as justification for failure to comply with its obligations”. Furthermore in the matter before the African Court on Human and Peoples’ Rights[1], in its judgement the court determined that “Having ratified the Charter, the Respondent (Tanzania Governmnet) has an obligation to make laws in line with the intents and purposes of the Charter.

Vile vile wajibu wa Serikali chini ya mikatba ya kimataifa imewahi kutolewa maamuzi na mahakama ya rufaa ya Tanzania katika shauri the Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia , ambapo mahakama ya rufaa ilitumia vifungu vya mkataba uitwao International Covenant on Civil and Political Rights kutafisiri haki za raia chini ya kifungu 15 kinachotoa haki za uhuru binafsi wa raia kwa kuamua “The fact that an International Convention to which Tanzania is a party is not incorporated into Tanzanian law does not absolve the government of its duty to adhere to its undertakings in the agreement.”[2]

K
wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikatba ya kimataifa kama ilivyotajwa hapo juu kifungu 29 B cha Kanuni za Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 zilizopitishwa katika gazeti la serikali kwa Tangazo namna 21 la 23 Jan 2009 hakiwezi kuwapokonya haki za kibanadamu za kumiliki ardhi na makazi yetu (viliyoko nje ya mita 30 toka katikati ya barabara ya Morogoro) kwa mujibu wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikataba ya kimataifa iliyotajwa hapo juu, hivyo ni wajibu wa Waziri wa sheria Prof Kabudi kumshauri Rais kuhusu wajibu nchi ilionao chini ya mikataba husika kulinda haki za binadamu hapa nchini.

Kifungu 27 cha kanuni hizo kinatamka upana wa njia za barabara za lami katika barabara kuu hapa nchini na hautakiwi kupungua mita 3.25 meters. Hivyo basi hifadhi ya barabara ya upana wa mita 60 meters, yaani mita 30 toka katikati ya barabara kila upande inaweza kujengwa njia za barabara (lanes) 18 (Meters 60/meter 3.25=18) 18 au pungufu yake na kuacha ardhi ya kutosha kwa shughuli zingine zinazohusiana na barabara kama vile njia za watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki maegesho ya magari na hata usafiri wa treni bila ya Serikali kudharau hukumu za Mahakam kuu na kuwavunjia wananchi haki zao za kibinadamu. Hivyo upanuzi wa barabara ya morogoro kuwa ya nji 6 za lami unahitaji mita 19.5 tu (3.25X6=19.5); hivyo bomoa bomoa hii sio kwa ajili ya upanuzi wa barabara bali kiongozi Fulani kutimiza kiu yake ya kutesa wananchi anaowatuhumu kuchagua vyama vya upinzani. (Naambatanisha kanuni za sheria ya barabara)
[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania

[2] Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia.

[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania
 
Tuache theory. Niambie nchi gani iliyoendelea ambayo imefika hapo kwa sababu ya demokrasia. Moja tuu unayoijua.

Siwezi kukutajia nchi moja kutokana na ukweli kuwa kula nchi inatafsiri demokrasia kwa mapana zaidi kulingana na mifumo na mazingira yake. Mbali na ile tafsiri ya msingi lakini neno utawala wa watu kwa ajili ya watu ni lazima ibaki kama msingi.
Inategemea wewe unaitafsiri vipi demokrasia katika utekelezaji wake wenye kuzingatia haki na uhuru wa watu.

Nchi nyingi za Afrika zinatizama Demokrasia kama mfumo pekee ulioletwa na wazungu bila kujua hata mifumo mingine wanayotumia kwenye serikali zao pia zililetwa na wazungu.

Demokrasia wanaposema ni utawala wa watu kwa ajili ya watu. Hii ni tafsiri nzuri kwa watu wenye akili waliopita na kuvuka kwa ugumu na vita nyingi kwenye mifumo ya kishenzi na kibabe na kuona kuwa haileti maendeleo ya haraka zaidi ya kujenga himaya za kundi fulani kutawala kwa miaka mingi bila maendeleo makubwa zaidi ya kumwaga damu za watu kwa uhasama wa kisiasa.

Dunia nzima inaeendelea kutokana na kuingia kwa mfumo wa kidemokrasi ( kutawala kwa ajili ya watu) baada ya kuondoka kwa mfumo kandamizi na wakikoloni.
Maana ya kupigania uhuru ilikua ni ili watu wajitawale wenyewe kwa manufaa ya watu wa jamii ile na sio vinginevyo. Leo wameibuka watu ndani pia ya nchi yetu wanataka warudishe ukoloni kwa kuondoa demokrasia.Kundi moja litawale bunge ,litawale dola na kila sekta kwa manufaa ya wachache wanaotaka kukaa madarakani milele.
Ni kundi lenye uroho wa madaraka kwa kisingizio cha nia ya kuleta maendeleo kwa kugandamiza demokrasia.

Watu wenye akili na nia njema wanaamini kuwa dwmokarasia ni dhana njema sana ndani ya jamii.

Mfano panapotokea waty wawili kwenye eneo moja wenye sifa,ushawishi na uwezo uanaokariabia kwenye uongozi; wenzetu wenye akili sawasawa walitafiti na kugundua kuwa ni muhimu na busara kuwashindanisha kwa kura ili kumpata kiongozi mmoja bila upendeleo au kutumia mabavu.

Demokrasia( utawala kwa ajili ya watu) inapigwa vita na watawala wa nchi za kiafrika kwa sababu ya woga wa kutoka madarakani sio kwa sababu ya kuzuia maendeleo.
Afrika ina maendeleo makubwa sana ya watawala na himaya zao tofauti na ulaya ambayo Watawala hawanaaendeleo yanayotokana na utawala .
Hii ndio maana ya demokrasia.
Hapa ndipo wanapokwepa viongozi wetu na wapiga debe wao.Kutawala kwa ajili ya watu( demokrasia) hakutakiwi Afrika .
Wanatawala kwa manufaa ya watawala na jamaa zao. Ndio maana viongozi wa kiafrika ni matajiri ili hali wananchi wao na nchi zao ni maskini. Hawataki demokrasia( kutawala kwa ajili ya watu).
Wenzetu wanademokrasia (Wanatawala kwa ajili ya watu) ndio maana waliendelea.

Afrika walipokubali mfumo wa vyama vingi wakaupa jina la Demokrasia kwa maana ya vyama vya upinzani. Unapotaja jina Demokrasia Afrika watawala wanaweweseka kwa kudhani kuwa ni vyama vingi tu.

Hata hapa kwetu Tanzania tumekua na tatizo la tafsiri ya demokrasia kwa kuiona kama ni mfumo adui wa vyama vya upinzanu vinavyogombania kuwatoa kwenye watawala madarakani.

Tulipaswa kukaa na kupanga kwa umakini namna ya kutafsiri kivitendo maana ya Demokrasia kulingana na watu wetu bila kutoka kwenye maana ya utawala wa watu kwa ajili ya watu. Huu ndio msingi halisi wa demokrasia. Kabla ya kuanza kutekeleza mfumo wa utawala watu kwa ajili ya watu tulipaswa tuweke vigezo vya kuzingatia badala yake watawala wakawa ni wa kwanza kuupinga utawala wenye nia ya kuwanufaisha watu. Woga na hofu yao ikawa ni kuondolewa madarakani. Wakawa hawawazi tena namna ya kuweka utawala kwa ajili ya watu bali ikawa ni vita ya kugombania kushikilia madaraka kwa muda mrefu.

Watawala wakaamua kuhamisha maana na nia nja ya dokrasia.

Demokrasia ni pamoja na kuwapa watu nafasi ya kupinga udhalimu wa serikali na hata kuwatoa madhalimu serikalini ili wangine wajifunze kuwa waadilifu na wanaotawala kwa ajili ya watu.
 
Mahakama haisikilizwi wala kuheshimiwa, ila Daud A.B ndiye anayesikilizwa na kutiiwa.

Acha ujinga.. Omba radhi haraka, fanya hivyo, CCM sasa iko makini hatutaki ujinga ujinga, Mh. RC Makonda anapiga kazi sana kwa vitendo, ww unaleta upuuzi.. Omba radhi upesi
 
Ushahidi. Uliopo ni kuwa eneo lililopiwa fidia ni mita 22.85 toka katikati ya barabara pande zote
 
Nasikia kuna hukumu ya mahakama ya juu kabisa kutengua hukumu za chini. Kwa mantiki hiyo bado zoezi kisheria ni sahihi na hakuna zuio la mahakama za chini lenye nguvu.
Si utuwekee hapa hiyo hukumu ya mahakama ya juu unayodai ipo. Mimi nimeweke hukumu hadi ya mahakama ya rufaa zinxowapa wananchi ushindi. Ingekuwa hukumu kama hiyo ipo mawakili wa serikali wangeitumia kuitetea serikali wakati maombi zuio yalipowasilishwa mahakamani. Kabla ya zuio kutolewa pande zote husikilizwa
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wew kwanz kusoma hujui ata kuandika,,,,umeona vifungu vya sheria vinavyosema???au unakurupuka tu,,ni wapi palipoandikwa kuwa mtu anatakiwa kulipwa baada ya haki yake kukandamizwa,,,, acha ulimbukeni mkuu tafakar na uchukue hatuaa shenzii

Ni miMi CHalIIiiii Ya "R"
 
Nauliza tu, eti kweli nyumba zote kando kando ya Morogoro road kuanzia Ubungo kwenda Mail moja hazina building permits na viwanja havina hati?
 
Hiyo unayoiita mada, nimekuuliza ukaruka kwamba umenukuu hukumu ya mahakama kuu. sasa kwa hili tena unasema ni makara yako.'

Tuachane na maisha ya ushabiki. Siamini kwamba rais ni dikteta, au hajui anachokifanya. Utawala uliopita ningeweza kusema maana mifano ya kutosha ipo. Au nawe unaamini hivyo kama huyo anayejiita mwanasheria wakati anaelewa vitendo vya dikteta huwa vikoje?
Kwani kuna ajabu gani MTU kunukuu andiko Fulani ktk mada yake? Ushabiki ni pale tunapishabikia utekelezaji wa sheria kibaguzi kama ilivyofanyika sheria moja ya barabara sehemu zenye wabunge Na madiwani wa CCM wamebomos Mira 60 tu, sehemu zenye wabunge wa madiwani wa upinzani wanabomoa Mira 120
 
Nauliza tu, eti kweli nyumba zote kando kando ya Morogoro road kuanzia Ubungo kwenda Mail moja hazina building permits na viwanja havina hati?
Historia ya mgogoro huu haya maeneo yalikuwa vijiji vya ujamaa vya Kumara, Mbezi, Kibamba Na Kiruvya, hivyo wanavijiji wengi walijenga vijijini hawakuhitaji kuwa Na vibali vya ujenzi. Kuhusu hati miliki wengi tu wanazo
 
Back
Top Bottom