Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Kwanza kabisa The Road ACT ya 2007 pia na Road Management Regulations za 2009 kifungu cha 29(1) na (2) zinasema upana ni mita 60 kwa barabara ya morogoro yani hio mita 125 haipo hata kwenye sheria sijui imetoka wapi huyu jamaa anakwenda kulipa fidia tena maradufu kwa kutozingatia sheria huyu jamaa ni adui namba moja wa Tanzania kwa kutia hasara nchi...
 
Wananchi wakafungue kesi Canada na Marekani wazuie Dream-liner na Bombadia Kama Serikali inavunja Sheria dawa yake ndio hiyo Dawa ya Jeuri ni kusudi.. Siamini ukatiri kama huu unafanyika yaani idara zote zinavunja Katiba wazi wazi wakumbuke waliapa kwa Mungu wao...! Nawataka wawalipe fidia na wawajengee upesi nyumba kwenye maeneo yao sema this time kuwe na mpangilio bomba
Hakuna sababu ya kutumia fedha za malipa kodi kulipa. Eneo LA hifadhi halali ya barabara LA mita 60, 30 kila upande linaweza kujengwa njia za lami 18. Hats marekani, Japan n.k hakuna barabara kama hiyo. Manispaa ya ubungo wanakomolewa kwa kuchagua mbunge na madiwani wa chadema
 
OMG.. Mungu akusaidie, i repeat again where did you copy & paste all these?

6 lanes unahitaji 19 meters? Uko duniani na una macho na ubongo? Uuuuhh.. Ur gone, ur lifeless, nyie ndio wasomi? Hii copying & pasting ni hatari sana..

I won't help you, the world will help you..!!
Mkuu hizo nondo nilizoweka ni research ambsyo natakiwa kupewa award. So don't speculate without references. Kiingereza chenyewe huna. Weka references kama zangu hapo juu. Soma mada hapo juu ndio uwe Na uwezo wa kuchangia
 
Si kila mtu anafaa kuwa kiongozi!!.

Tujiandae tena kulipa watu fidia.

Kama Kawaida tunaingia tena kwenye fidia, na tukichelewa kulipa itakuwa mambo yale ya Bomberdier, so sasa kuna kazi ya kuikomboa Bomberdier, Kuna samaki, na hili nalo linaingia
 
Je, waliokumbwa na haya matukio ya kutisha ya kuvunjiwa nyumba zao watalipwa fidia wanazostahili!?

Je, waliohusika na huu uvunjaji wa sheria za nchi watachukuliws hatua stahiki ikiwemo kufukuzwa kazi na kupandishwa kizimbani!?

Wote waliotoa matinga tinga ya uvunjaji walioamrisha polisi na ffu kusimamia hilo tukio haramu.

Inakuwaje Mkuu wa Mkoa, Waziri wa ardhi, wa mambo ya ndani na huyo wa Ikulu wasijue uvunjwaji wa sheria za nchi ambao kila siku ulikuwa unaandikwa katika magazeti na kutangazwa na TV na Radio katika taarifa za habari zao!?

Tarehe 30 agosti 2017 Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo na msemaji Mkuu wa serikali alivitisha vyombo vya habari juu ya kuripoti zoezi la bomoa bomoa Kimara hadi kiruvia kwa sababu zoezi hilo linafanyika kisheria.
Ukweli ni kuwa bomoa bomoa hii ni kinyume cha Katiba ya nchi, Sheria ya barabara Namba 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009, inakiuka pia hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi iliyotolewa na jaji S.B.Bongole tarehe 31 Mei 1013 katika shauri namba 80 la 2005. Na pia inakiuka hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyotolewa na jaji S.A.N Wambura tarehe 13 Juni 2016 katika shauri namba 151 la 2015. )Naambatanisha Hukumu za mahakama husika)

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitamka kuwa Kanuni ya Sheria “The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”. Na ikaendelea kuwa ardhi inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara ya Morogoro, iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa opereshani vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999, ardhi hiyo ni mali halali ya wananchi waliofungua malalamiko.

Aidha katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitambua kuwa kuwa eneo husika (Jiji la Dar es Salaam) hivi sasa linatawaliwa na Sheria ya Mipango Miji ambayo inataka hifadhi ya barabara kuu kuwa ni mita 60 tu, yaani mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

Baada ya kushindwa Wizara ya ujenzi )Serikali0 ikiiongozwa na Rais wa sasa Mhe John Pombe Magufuli ilikata rufaa Mahakam ya Rufaa katika shauri na 151 la 2015, ambalo lilitupiliwa mbali kwa kukosa hoja za msingi.

Tunasema kuwa Mhe Rais anavunja katiba aliyoapa kuilinda katika bomoa bomoa hii kwa kuwa Kifungu 107 (A) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kinatamka “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki”.
Hivyo basi kwa kuwa wananchi wal,ishapatiwa haki ya ardhi yao na mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa bomoa bomoa inayoendelea inakiuka katiba ya nchi ambayo Mhe John Pombe Magufuli aliapa kuilinda.

Hivyo kitendo cha kuwapora wananchi ardhi yao waliyoipata kihalali na kwa mujibu wa sheria za nchi ni ukiukwaji tena baada ya kuwaharibia mali zao ikiwemo nyumba n.k ni ukiukwaji wa Kifungu 24 (1) cha Katiba ya Tanzania kinachotamka Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. (2) “Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili”.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni “Kulinda usalama wa raia na mali zao, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kudhibiti uhalifu, kuwakamata watuhumiwa na kudumisha amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Lakini cha kushangaza ni jeshi hili hili ambalo linatakiwa kulinda mali za watanzania kwa mujibu wa katiba, sheria za nchi na dhima yake ndilo ilnalotoa ulinzi kwa Tanroads kuharibu nyumba na mali za watanzania kwa kukiuka hukumu za Mahakama kuu na mahakama ya Rufaa.

Kifungu 29 b cha Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, GN No 21 ya tar 23 Januari 2009 kinatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa eneo la kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni hadi mita 60 tu toka katikati ya barabara kila upande kama inavyoelekezwa barua ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani ya tarehe tarehe 21 Oktoba 2010 yenye Kumb Na TRD/CR/R.10/13/Vol.III/34 kwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha. Tokea kupitishwa kwake 2007, Tanroads walikuwa wakiheshimu sheria hii/ lakini tokea Mhe John Pombe Magufuli aliporejeshwa kuwa Waziri wa Ujenzi tarehe 24 Novemba 2010, akatoa maagizo kwa Tanroads kuwa wavunje sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake za 2009; na ndio msingi wa bomoa bomoa hii ya sasa.

Bomoa bomoa hii pia inakiuka mikataba mbali mbali ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia kama ifuatavyo:-

  • Ibara ya 25 ya Tamko la Haki za Binadamu (Universal Decralation of Human Rights) inatambua haki za makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu.

  • Ibara ya 11 (1) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni wa 1966, ulioridhiwa na Serikali ya Tanzania tarehe 11 Juni 1976, (ambao Kamati ya Prof Osolo aliutumia kujenga hoja ya nchi kuwa haki zaidi juu ya raslimali zake) unazitaka Serikali zilizouridhia kutambua kuwa kila raia na familia yake wana haki ya kupata kiwango stahiki cha hali ya kimaisha ikiwemo chakula, mavazi, makazi na kuendelea kuboreshwa kwa hali zao za kimaisha.

  • Tamko namba 77 la 1993 la Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadumi linatamka kuwa “uhamishwaji kimabavu” (Forced eviction) ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaopelekea uvunjifu wa haki zingine za kibandamu kama vile kuwakosesha raia makazi, chakula, maji safi, afya, elimu, ajira, kipato, usalama, na kinga dhidi ya vitendo vya kinyama na udhalilishwaji n.k

  • Tamko namba 7 la 1997 la Kamati hiyo kupinga “Uhamishwaji Kimabavu” linasisitiza kuwa haki ya makazi ni pamoja na binadamu kuishi mahali kwa usalama, amani na heshima; na kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane na uhuru wa raia kulindwa dhidi ya uhamishwaji kimabavu na uharibifu wa makazi yake; kuwa na faragha katika makazi yake na kulindwa dhidi ya kuingiliwa isivyo halali. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi hivyo ni haki yetu sisi kama raia kupatiwa ulinzi dhidi ya vitendo vya Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi yetu vinavyolenga kutuhamisha kimabavu kwa kutuzuia kuendeleza mali zetu halali, kuharibu kwa makusudi majengo yatu na vitisho vya aina mbali mbali.
Tamko hilo lilifafanua zaidi kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane ulinzi wa umiliki wa ardhi na makazi; fidia ya makazi, ardhi na maendelezo mengine; usawa katika kupata haki za makazi; na kushirikishwa katika maamuzi mbali mbali yanayohusu masuala ya makazi katika ngazi ya jamii na kitaifa. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi. Sisi raia tunaomiliki kihalali ardhi na makazi katika eneo husika tunayo haki kamili ya kushirikishwa katika maamuzi yote yanayohusu ardhi na makazi yetu.


Katika shauri lililokuwa mbele ya Mahakama ya Haki za binadamu ya Umoja wa Afrika (African Court on Human and Peoples’ Rights-Applications No 009&011of ka hiy2011), Serikali ya Tanzania ilinukuliwa kuthibitisha mbaele ya mahakama hiyo kuwa “it fully adheres to principles of the rule of law, separation of powers and independence of the judiciary as provided for under the Constitution of the United Republic of Tanzania”[1]. Hivyo vitendo vya Rais John Magufuli aliyekula kiapo kuilinda Katiba ya nchi kupuuza na kudharau hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa havikubalika hata kidogo katika nchi inayoongozwa kwa utawal wa sheria. Ni wakati sasa Mwalimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu kinchoheshimika cha dar es salaam Prof Kabudi akamshauri Mhe raisd umuhimu wa kuheshimu hukumu za mahakama.

Ibara ya 27 ya mkataba wa kimataifa wa Vienna (Vienna Convention on the Law of Treaties)provides that: “A party may not invoke the provisions of its internal law as justification for its failure to perform a treaty. Additionally, Article 32 of the International Law Commission Articles on State Responsibility 2001 provides that “the Responsible State may not rely on the provisions of its internal law as justification for failure to comply with its obligations”. Furthermore in the matter before the African Court on Human and Peoples’ Rights[1], in its judgement the court determined that “Having ratified the Charter, the Respondent (Tanzania Governmnet) has an obligation to make laws in line with the intents and purposes of the Charter.

Vile vile wajibu wa Serikali chini ya mikatba ya kimataifa imewahi kutolewa maamuzi na mahakama ya rufaa ya Tanzania katika shauri the Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia , ambapo mahakama ya rufaa ilitumia vifungu vya mkataba uitwao International Covenant on Civil and Political Rights kutafisiri haki za raia chini ya kifungu 15 kinachotoa haki za uhuru binafsi wa raia kwa kuamua “The fact that an International Convention to which Tanzania is a party is not incorporated into Tanzanian law does not absolve the government of its duty to adhere to its undertakings in the agreement.”[2]

K
wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikatba ya kimataifa kama ilivyotajwa hapo juu kifungu 29 B cha Kanuni za Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 zilizopitishwa katika gazeti la serikali kwa Tangazo namna 21 la 23 Jan 2009 hakiwezi kutupokonya haki zetu za kibanadamu za kumiliki ardhi na makazi yetu (viliyoko nje ya mita 30 toka katikati ya barabara ya Morogoro) kwa mujibu wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikataba ya kimataifa iliyotajwa hapo juu, hivyo ni wajibu wa Waziri wa sharia kumshauri Rais kuhusu wajibu nchi ilionao chini ya mikataba husika kulinda haki za binadamu hap nchini.

Kifungu 27 cha kanuni hizo kinatamka upana wa njia za barabara za lami katika barabara kuu hapa nchini na hautakiwi kupungua mita 3.25 meters. Hivyo basi hifadhi ya barabara ya upana wa mita 60 meters, yaani mita 30 toka katikati ya barabara kila upande inaweza kujengwa njia za barabara (lanes) 18 (Meters 60/meter 3.25=18) 18 au pungufu yake na kuacha ardhi ya kutosha kwa shughuli zingine zinzohusiana na barabara kama vile njia za watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki maegesho ya magari na hata usafiri wa treni bila ya Serikali kudharau hukumu za Mahakam kuu na kutuvunjia haki zetu za kibinadamu. Hivyo upanuzi wa barabara ya morogoro kuwa ya nji 6 za lami unahitaji mita 19.5 tu (3.25X6=19.5); hivyo bomoa bomoa hii sio kwa ajili ya upanuzi wa barabara bali kiongozi Fulani kutimiza kiu yake ya kutesa wananchi anaowatuhumu kuchagua vyama vya upinzani. (Naambatanisha kanuni za sheria ya barabara)
[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania

[2] Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia.


[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania
 
Ngoja nitasoma tena maana vifungu ni vingi. Yapo mazingatio katika andiko hili.
 
Je, waliokumbwa na haya matukio ya kutisha ya kuvunjiwa nyumba zao watalipwa fidia wanazostahili!?

Je, waliohusika na huu uvunjaji wa sheria za nchi watachukuliws hatua stahiki ikiwemo kufukuzwa kazi na kupandishwa kizimbani!?

Wote waliotoa matinga tinga ya uvunjaji walioamrisha polisi na ffu kusimamia hilo tukio haramu.

Inakuwaje Mkuu wa Mkoa, Waziri wa ardhi, wa mambo ya ndani na huyo wa Ikulu wasijue uvunjwaji wa sheria za nchi ambao kila siku ulikuwa unaandikwa katika magazeti na kutangazwa na TV na Radio katika taarifa za habari zao!?

Bomoa bomoa hii ndio brain child ya mkulu. Kila MTU anaogopa kumwambia ukweli ili asifukuzwe Kazi. Sijui kama Prof Kabudi ataweza kumwambia ukweli kuwa "you're going against the constitution" au atalinda kitumbua chake. Tunajua kuwa hapa JF wapo wanafunzi wengi ea Prof Kabudi. Tunaomba mumfikishie ujumbe huu kuwa "we have to live by what we said and taught". Jamii nzima itamshangaa Prof Kabudi ataendelea kulinda dharau hii kwa mihimili ya dola..

uKuhusu upande wa mahakama niwatoe wasiwadi wote wenye nawazo kuna "Mhimili Chimbifu" jana tar 30:Agosti 2017 ndio ilikuwa siku ya kesi ya wanaobomolewa. Mahakama ilikuwa firm ndio siku 3 kabla ya tarehe ya kesii ilizushwa bomoa bomoa feki mabondebi na Tuangoma na kusitishwa kesho yake. Nia ilikuwa juuchanganya umma usibaini kuwa serikali (executive) imelazimika kuitii Stop Order ya mahakama.

Kwa kuwa mkoa wa pwani eneo la maili moja wabunge na madiwani ni kutoka CCM ubomoaji ulifanyika mita 60 kati ya daraja la Kiluvya hadi Tamco Kibaha. Yaani sheria moja ya barabara namba 13 ys 2007 na kanuni zake za 2009 tekelezaji tofauti kulingana Na wabunge Na madiwani wanatoka chama tawala au upinzani.
 
Mkuu kama hii habari ilikuwepo tangu January mwaka huu Magufuli, Mkuu wa Mkoa, Waziri wa ardhi na wa mambo ya ndani walifanya yepi ili kuhakikisha uvunjwaji holela unasimamishwa!?

Tangu January 2016 hadi August 2017 uvunjwaji unaendelea halafu tunatazugwa eti Magufuli alikuwa hajui chochote!!!!!

Meneja wa Magufuli apinga bomoabomoa

Bomoa bomoa hii ndio brain child ya mkulu. Kila MTU anaogopa kumwambia ukweli.
Waziri Mbarawa alitumia msdaraka yakr kama Waziri wa Ujenzi kutekeleza sheria ya barabara Na 13 ya 2007 kwa mkoa pwani, ubomoaji kule ulifanyika mita 60 kila upande badala ya mita 120 toka daraja la Kiluvya hadi Tamco Kibaha kwa kuwa kule wabunge na madiwani ni kutoka CCM
 

OMG.. Mungu akusaidie, i repeat again where did you copy & paste all these?

6 lanes unahitaji 19 meters? Uko duniani na una macho na ubongo? Uuuuhh.. Ur gone, ur lifeless, nyie ndio wasomi? Hii copying & pasting ni hatari sana..

I won't help you, the world will help you..!!
Aisee wewe umelewa nyagi nini !!?? Au unachuki binafsi na mleta mada ? Au ujui tofauti ya mt 3.5 na ft 3.5 wewe vipi !!???
 
Kama Kawaida tunaingia tena kwenye fidia, na tukichelewa kulipa itakuwa mambo yale ya Bomberdier, so sasa kuna kazi ya kuikomboa Bomberdier, Kuna samaki, na hili nalo linaingia
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji106]
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu kama hii habari ilikuwepo tangu January mwaka huu Magufuli, Mkuu wa Mkoa, Waziri wa ardhi na wa mambo ya ndani walifanya yepi ili kuhakikisha uvunjwaji holela unasimamishwa!?

Tangu January 2016 hadi August 2017 uvunjwaji unaendelea halafu tunatazugwa eti Magufuli alikuwa hajui chochote!!!!!

Meneja wa Magufuli apinga bomoabomoa
BAK naomba chukua muda soma mada. Kuna watu wanatoa JF huwa wanatoa maneno ya kuudhaririisha mhimili wa mahakama.

Tar 30 jana ndio ilikuwa kesi kwa Pilato. Executive siku 3 kabla ikazusha bomoa bomoa feki mabondeni Na Tuangoma Na kusitishwa kesho yake kwa amri ya Mkuu wa Mkoa.

Sarakasi zote hizo ilikuwa ni mhimili wa Serikali kuuchanganya umma kwa sababu Mahakama ina uwezo wa kuwashughulikia wote walioidharau. For the purpose of respecting judicial process sitaweza kuweka hadharani kilichoongelewa ktk shauri hili na kupelekes mhimili wa serikali kuitii mahakana. Kwa hiyo Natangaxa wazi kuwa mahakama zetu bado ziko nguvu na ziko huru, wewe peleka kesi yako ndio tofauti ya Ubabe ba utawala ws sheria.Katika shauri hili mhimili wa serikali umelazimika kuutii Mhimili wa mahakama.

Ndio maana hatavupuuzi wa Lissu tuiliupinga.
 
Mhimili wa Serikali umelazimika kutii mhimili wa mahakama kwa usanii and for some it is too late with nowhere to go. They're officially homeless people due to dictatorship policies.

BAK naomba chukua muda soma mada. Kuna watu wanatoa maneno ya kuudhririsha mhimili wa mahakama. Tar 30 jana ndio ilikuwa kesi kwa Pilato. Executive siku 3 kabla ikazusha bomoa bomoa feki mabondeni Na Tuangoma Na kusitishwa kesho take kwa amri ya Mkuu wa Mkoa. Sarakasi zote hizo ilikuwa ni mhimili wa Serikali kuuchanganya umma. Ukweli ni kuwa mhimili wa serikali umelazimika kutii Mhimili wa mahakama.
Ndio maana hats upuuzi wa Lissu niliupinga.
 
Kwanza kabisa The Road ACT ya 2007 pia na Road Management Regulations za 2009 kifungu cha 29(1) na (2) zinasema upana ni mita 60 kwa barabara ya morogoro yani hio mita 125 haipo hata kwenye sheria sijui imetoka wapi huyu jamaa anakwenda kulipa fidia tena maradufu kwa kutozingatia sheria huyu jamaa ni adui namba moja wa Tanzania kwa kutia hasara nchi...
naona samaki hao wanakuja!!
 
Mhimili wa Serikali umelazimika kutii mhimili wa mahakama kwa usanii and for some it is too late with nowhere to go. They're officially homeless people due to dictatorship policies.
BAK as a mere citizen, I think iva done my part. It is up Prof Kabudi to live to his teachings. I will appreciate if any one his students could bring this topic to his attention and notify us accordingly that he is informed of such unbecoming between the 3 branches of the rule of law.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo la nchi hii ni CCM na wabunge wake.

Hatima ya nchi hii mpaka sasa iko mikononi mwa CCM na wabunge wake.
Kama kuna anayeipoteza nchi hii tangu awali ni CCM na wabunge wake.

Hakuna linalofanyika ambalo halikua sera ya chama cha mapinduzi.
Mh.Rais anatekeleza kile kulichowekwa mezani na CCM ndio maana hakuna kada mpaka leo anayetoa hata maoni mbadala mana uwezo wao ndio uliopanga hayo.

CCM wanajua wanachofanya kuwa wamekipanga. Barabara ya juu na chini mpaka Chalinze sio tamko la leo la Rais bali lilitajwa tangu wakati wa awamu ya nne.
Reli ya standard gage sio haikuasisiwa na awu ya tano. Ilishapangwa tangu awamu ya nne. Awamu ya tano kazi yake ni kutekeleza ilani ya CCM iliyopangwa muda mrefu.

CCM ndio walipaswa waweke mipango yao na kuishauri serikali walioipa madaraka namna bora ya kuwapa wananchi haki yao bila kujali itikadi zao wala maiabila yao alimradi ni watanzania. CCM ndio walipaswa waielekeze serikali yao namna bora ya kutekeleza ilani yao ya uchaguzi bila kuhararisha maisha na uhai wa watanzania. CCM ndiyo ilipaswa isimamie kanuni yake inayosema " binadamu wote ni sawa", "Nitasema kweli daima."
CCM ndiyo ilipaswa iielekeze serikali yake kuwa JKT iliasisiwa kwa madhumuni ya kujenga Taifa na kutumika wakati wa majanga.

Bunge ni la CCM kwa maana kwamba wapinzani hawana uwezo wowote wa kuzuia jambo lolote lisipite wala achilia mbali kutoa ushauri wa jambo lolote na ukakubalika na kuwa ni hoja ya maana tangu alipoondoka marehemu Samweli Sita.
Bunge lilipaswa liweke sheria ya kulinda utu wa mtanzania kwa namna yoyote ile na iwe ni kosa la kiutendaji kwa mtu yeyote kuudhalilisha utu wa mtanzania kwa sababu yoyote ile alimradi isiwe ni sababu ya kutenda jinai.
Mtanzania maskini amejenga kajumba kake kwenye ENEO AMBALO HALIKUPIMWA HATA KWA WALE WALIOMZUNGUKA anavunjiwa nyumba yake ALIYOIJENGA SIO KWA LENGO LA KUFANYA UHALIFU BALI KUISHI NA KUJISETIRI MAISHA YAKE NA UTU WAKE KAMA BINADAMU ambaye kama CCM na Wabunge wake na Serikali yake wangekua makini angepimiwa eneo lake au angejengewa nyumba ya kuishi mana ndiye anayewapa hayo madaraka na kuifanya nchi iitwe Taifa ( Mana bila watu hakuna taifa ) . Bunge la CCM na CCM kama chama Tawala kilipaswa kuwajenge watanzania wote maskini nyumba za kuishi kwa malipo kidogo kwenye maeneo yote ya mijini. Huu ujenzi holela ni matokeo ya serikali ya CCM kutojali watu na maisha yao. Ujenzi usiofaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama maji,umeme,shule, maeneo ya michezo, usafiri, zima moto n.k. Haya yanathibitisha kuwa CCM sio chama kilichopaswa kuunda serikali ya kijamaa na hakifahamu maana ya ujamaa. Kimebaki na neno kujitegemea na kuua neno ujamaa kama kilivyoua Azimio la Arusha.

Haiwezekana bunge lenye nguvu kubwa ya CCM ikwepe lawama hii ya watu kuukoswshwa haki zao za msingi kama binadamu. Mahakama imejitahidi lakini bunge la CCM linawaacha wananchi waliolituma na kuamua kushikana na serikali kuwaumiza wananchi.
Siamini kuwa bunge lilishindwa kuweka kanuni au sheria na kuielekeza serikali itenge fedha kidogo tu kwa ajili ya makazi ya watanzania kabla ya kuwavunjia nyumba.


Siamini kabisa kuwa CCM na serikali yake na bunge lake inayotumia mabilioni ya fedha wakati wa uchaguzi kununua magari ya washawasha,kulipa vinwamgongo vya wabunge kwa miaka mitano, kununua magari ya kifahari ya serikali, kunua ndege, kununua madiwani na kuitisha uchaguzi wa mamilioni ( kwa mujibu wa Mbowe) n.k. inashindwa kuwatumia magereza , wafungwa na JKT kujenga nyumba za kutosha kabisa maeneo ya Mabwe pande na meneo mengine mengi yenye eneo la kutosha kwa ajili ya kuwahamishia wale wote walioko maeneo yanayohitajika kwa ajili ya miradi ya serikali ya maendeleo ya watanzania wote.

Wengine wanakuja na hoja nyepesi kuwa eti kuna watu wanajichomeka huko ili nao wapate fidia.Hayo ni matokeo ya mipango mibovu na malengo ya ubinafsi ya baadhi ya watawala. Kwa nini kila mtu alipwe fedha wakati amejenga kwenye eneo la mji bila kupimwa? Yani apewe fedha mkononi ili aende tena kujenga kiholela?

Kuwalipa watu 1000 kulinagana na aina ya nyumba za kuishi walizovunjiwa ni gharama mara kumi ya kuwajengea nyumba za kuishi kwa kutumia mfano magereza na wafungwa pamoja na JKT. Hawa wanatumia mishahara ya serikali tayari wanatakiwa wanunuliwe vifaa tu vya ujenzi ambavyo vinaweza kununuliwa kutoka kiwandani bila hata kodi na kujenga nyumba haraka kijeshi.
TUNASHINDWA NINI HAPO MPAKA WANADAMU NA WATANZANIA WENZETU WALALE NJE KWA SABABU YA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO?

Sio wamiliki tu wa nyumba bali hata wapangaji wao kuna uwezokano wa kuwajengea nyumba na wakalipia pango la nyumba kwa bei ndogo.

Haya mambo ya kuacha watu wanajenga majumba ya kupangishia wananchi wenzao kwa bei kubwa bila udhibiti na ubora wa mazingira na miundo mbinu ndiyo yanayosababisha watu wanakuwa wezi na wapiga dili kwa sababu wanatafuta pesa za kujenga ili wapangishe na mara nyingine wanajenga holela bila kuzingatia mipango miji. Kama serikali ingedhibiti ujenzi holele na kuhakikikisha kuwa inawapa wananchi wake nyumba za bei nafuu za kupanga hata wizi na ufisadi ungepungua. Watu wangekuwa wazalendo wa kweli sio wa kuigiza .

BILA CCM NA BUNGE LAKE KUJALI WATANZANIA NA HAKI ZAO NA UTU WAO NA UHAI WAO tutaendelea kuilaumu serikali tu bure wakati ndivyo ilivyoangizwa kwenye ilani yao.

Makamba alisema " Huyu aliyepo anawabatiza kwa maji bali ajaye atawabatiza kwa moto."
CCM ikisema kwamba sasa wabatizeni kwa maji, basi watabatizwa kwa maji ,na ikisema wabatizwe kwa moto watabatizwa kwa moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom