Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Tarehe 30 agosti 2017 Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo na msemaji Mkuu wa serikali alivitisha vyombo vya habari juu ya kuripoti zoezi la bomoa bomoa Kimara hadi kiruvia kwa sababu zoezi hilo linafanyika kisheria.

Ukweli ni kuwa bomoa bomoa hii ni kinyume cha Katiba ya nchi, Sheria ya barabara Namba 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009, inakiuka pia hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi iliyotolewa na Jaji S.B.Bongole tarehe 31 Mei 1013 katika shauri namba 80 la 2005. Na pia inakiuka hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyotolewa na Jaji S.A.N Wambura tarehe 13 Juni 2016 katika shauri namba 151 la 2015. (Naambatanisha Hukumu za mahakama husika)

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitamka kuwa Kanuni ya Sheria “The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”. Na ikaendelea kuwa ardhi inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara ya Morogoro, iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa opereshani vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999, ardhi hiyo ni mali halali ya wananchi waliofungua malalamiko.

Aidha katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitambua kuwa kuwa eneo husika (Jiji la Dar es Salaam) hivi sasa linatawaliwa na Sheria ya Mipango Miji ambayo inataka hifadhi ya barabara kuu kuwa ni mita 60 tu, yaani mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

Baada ya kushindwa Wizara ya ujenzi (Serikali) ikiiongozwa na Rais wa sasa Mhe John Pombe Magufuli ilikata rufaa Mahakam ya Rufaa katika shauri na 151 la 2015, ambalo lilitupiliwa mbali kwa kukosa hoja za msingi.

Tunasema kuwa Mhe Rais anavunja katiba aliyoapa kuilinda katika bomoa bomoa hii kwa kuwa Kifungu 107 (A) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kinatamka “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki”.

Hivyo basi kwa kuwa wananchi walishapatiwa haki ya ardhi yao na mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa bomoa bomoa inayoendelea inakiuka katiba ya nchi ambayo Mhe John Pombe Magufuli aliapa kuilinda.

Hivyo kitendo cha kuwapora wananchi ardhi yao waliyoipata kihalali na kwa mujibu wa sheria za nchi ni na umiliki huo kuthibitishwa na mahakama ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi, Mhe Rais aliyoapa kuilinda, tena baada ya kuwaharibia mali zao ikiwemo nyumba n.k. Kifungu 24 (1) cha Katiba ya Tanzania kinachotamka Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. (2) “Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili”.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni “Kulinda usalama wa raia na mali zao, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kudhibiti uhalifu, kuwakamata watuhumiwa na kudumisha amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Lakini cha kushangaza ni jeshi hili hili ambalo linalotakiwa kulinda mali za watanzania kwa mujibu wa katiba, sheria za nchi na dhima yake ndilo ilnalotoa ulinzi kwa Tanroads kuharibu nyumba na mali za watanzania kwa kukiuka hukumu za Mahakama kuu na mahakama ya Rufaa. Kwa hili tumtaje IGP Mpya kujitafakari upya Na kuishauri mamlaka take ya uteuzi kuhusu ukiujwaji huu mkubwa wa Katuba ya nchi.

Kifungu 29 b cha Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, GN No 21 ya tar 23 Januari 2009 kinatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa eneo la kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mita 60 tu toka katikati ya barabara kila upande kama inavyoelekezwa barua ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani ya tarehe tarehe 21 Oktoba 2010 yenye Kumb Na TRD/CR/R.10/13/Vol.III/34 kwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha. Tokea kupitishwa kwake 2007, Tanroads walikuwa wakiheshimu sheria hii lakini tokea Mhe John Pombe Magufuli aliporejeshwa kuwa Waziri wa Ujenzi tarehe 24 Novemba 2010, akatoa maagizo kwa Tanroads kuwa wavunje sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake za 2009. Na alipochaguliwa Rais anatumia wadhifa wake kukiuka Katiba, Sheria Na haki za binadamu.

Bomoa bomoa hii pia inakiuka mikataba mbali mbali ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia kama ifuatavyo:-

  • Ibara ya 25 ya Tamko la Haki za Binadamu (Universal Decralation of Human Rights) inatambua haki za makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu.

  • Ibara ya 11 (1) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni wa 1966, ulioridhiwa na Serikali ya Tanzania tarehe 11 Juni 1976, (ambao Kamati ya Prof Osolo aliutumia kujenga hoja ya nchi kuwa haki zaidi juu ya raslimali zake) unazitaka Serikali zilizouridhia kutambua kuwa kila raia na familia yake wana haki ya kupata kiwango stahiki cha hali ya kimaisha ikiwemo chakula, mavazi, makazi na kuendelea kuboreshwa kwa hali zao za kimaisha.

  • Tamko namba 77 la 1993 la Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadumi linatamka kuwa “uhamishwaji kimabavu” (Forced eviction) ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaopelekea uvunjifu wa haki zingine za kibandamu kama vile kuwakosesha raia makazi, chakula, maji safi, afya, elimu, ajira, kipato, usalama, na kinga dhidi ya vitendo vya kinyama na udhalilishwaji n.k

  • Tamko namba 7 la 1997 la Kamati hiyo kupinga “Uhamishwaji Kimabavu” linasisitiza kuwa haki ya makazi ni pamoja na binadamu kuishi mahali kwa usalama, amani na heshima; na kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane na uhuru wa raia kulindwa dhidi ya uhamishwaji kimabavu na uharibifu wa makazi yake; kuwa na faragha katika makazi yake na kulindwa dhidi ya kuingiliwa isivyo halali. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi hivyo ni haki yetu sisi kama raia kupatiwa ulinzi dhidi ya vitendo vya Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi yetu vinavyolenga kutuhamisha kimabavu kwa kutuzuia kuendeleza mali zetu halali, kuharibu kwa makusudi majengo yatu na vitisho vya aina mbali mbali.
Tamko hilo lilifafanua zaidi kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane ulinzi wa umiliki wa ardhi na makazi; fidia ya makazi, ardhi na maendelezo mengine; usawa katika kupata haki za makazi; na kushirikishwa katika maamuzi mbali mbali yanayohusu masuala ya makazi katika ngazi ya jamii na kitaifa. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi. Sisi raia tunaomiliki kihalali ardhi na makazi katika eneo husika tunayo haki kamili ya kushirikishwa katika maamuzi yote yanayohusu ardhi na makazi yetu.


Katika shauri lililokuwa mbele ya Mahakama ya Haki za binadamu ya Umoja wa Afrika (African Court on Human and Peoples’ Rights-Applications No 009&011of ka hiy2011), Serikali ya Tanzania ilinukuliwa kuthibitisha mbaele ya mahakama hiyo kuwa “it fully adheres to principles of the rule of law, separation of powers and independence of the judiciary as provided for under the Constitution of the United Republic of Tanzania”[1]. Hivyo vitendo vya Rais John Magufuli aliyekula kiapo kuilinda Katiba ya nchi kupuuza na kudharau hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa havikubalika hata kidogo katika nchi inayoongozwa kwa utawal wa sheria. Ni wakati sasa Mwalimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu kinchoheshimika cha Dar es salaam Prof Kabudi akamshauri Mhe Rais umuhimu wa kuheshimu hukumu za mahakama Na kujiepusha uvunjwaji wa Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.

Ibara ya 27 ya mkataba wa kimataifa wa Vienna (Vienna Convention on the Law of Treaties)provides that: “A party may not invoke the provisions of its internal law as justification for its failure to perform a treaty. Additionally, Article 32 of the International Law Commission Articles on State Responsibility 2001 provides that “the Responsible State may not rely on the provisions of its internal law as justification for failure to comply with its obligations”. Furthermore in the matter before the African Court on Human and Peoples’ Rights[1], in its judgement the court determined that “Having ratified the Charter, the Respondent (Tanzania Governmnet) has an obligation to make laws in line with the intents and purposes of the Charter.

Vile vile wajibu wa Serikali chini ya mikatba ya kimataifa imewahi kutolewa maamuzi na mahakama ya rufaa ya Tanzania katika shauri the Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia , ambapo mahakama ya rufaa ilitumia vifungu vya mkataba uitwao International Covenant on Civil and Political Rights kutafisiri haki za raia chini ya kifungu 15 kinachotoa haki za uhuru binafsi wa raia kwa kuamua “The fact that an International Convention to which Tanzania is a party is not incorporated into Tanzanian law does not absolve the government of its duty to adhere to its undertakings in the agreement.”[2]

K
wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikatba ya kimataifa kama ilivyotajwa hapo juu kifungu 29 B cha Kanuni za Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 zilizopitishwa katika gazeti la serikali kwa Tangazo namna 21 la 23 Jan 2009 hakiwezi kuwapokonya haki za kibanadamu za kumiliki ardhi na makazi yetu (viliyoko nje ya mita 30 toka katikati ya barabara ya Morogoro) kwa mujibu wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikataba ya kimataifa iliyotajwa hapo juu, hivyo ni wajibu wa Waziri wa sheria Prof Kabudi kumshauri Rais kuhusu wajibu nchi ilionao chini ya mikataba husika kulinda haki za binadamu hapa nchini.

Kifungu 27 cha kanuni hizo kinatamka upana wa njia za barabara za lami katika barabara kuu hapa nchini na hautakiwi kupungua mita 3.25 meters. Hivyo basi hifadhi ya barabara ya upana wa mita 60 meters, yaani mita 30 toka katikati ya barabara kila upande inaweza kujengwa njia za barabara (lanes) 18 (Meters 60/meter 3.25=18) 18 au pungufu yake na kuacha ardhi ya kutosha kwa shughuli zingine zinazohusiana na barabara kama vile njia za watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki maegesho ya magari na hata usafiri wa treni bila ya Serikali kudharau hukumu za Mahakam kuu na kuwavunjia wananchi haki zao za kibinadamu. Hivyo upanuzi wa barabara ya morogoro kuwa ya nji 6 za lami unahitaji mita 19.5 tu (3.25X6=19.5); hivyo bomoa bomoa hii sio kwa ajili ya upanuzi wa barabara bali kiongozi Fulani kutimiza kiu yake ya kutesa wananchi anaowatuhumu kuchagua vyama vya upinzani. (Naambatanisha kanuni za sheria ya barabara)
[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania

[2] Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia.


[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania
 

Attachments

  • Road Reserve Land Case Judgement.pdf
    2.1 MB · Views: 88
  • Ruling Appeal 151 0f 2015.docx
    1.2 MB · Views: 84
  • Tanroad Letter stipulating the Road Reserve for 16 to 37 Kms.pdf
    733.6 KB · Views: 140
Sasa bomoa si tayari, zoezi liendelee tu...maana kuzuia tena haina maana, watu washabomolewa tayari na wengine walibomoa wenyewe kutii amri...wengine pia salishafidiwa...wengine bado

Sent using Jamii Forums mobile app
Tusiingize masihara kwenye maisha ya watu unaweza kutupatia ushahidi ya waliolipwa fidia kama ambavyo nimeweka Mimi hapo juu?
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ingekuwa hivyo huo ushahidi wa kulipa fidia serikali ingeutoa mahakamani isingeshindwa mahakamani
 
Hii Copy & Paste umetoa wapi? Mnajua C & P tu.. Maendeleo yana gharama zake, na tunahitaji hiyo barabara ya 6 lanes haraka sana to Chalinze.. Watu watahama tu, na maeneo watapata tu, serikali yetu inachapa kazi acheni kuturudisha nyuma kama Tundu Lissu
Tatizo letu wengi hatutaki kusoma. Kwa faida yako njia 6 za lami zinahitaji mita 19.5 tu. Soma mada upate ufahamu
 
Aliposema mtaishi kama Mazombie na Mashetani wengi walijua anamaanisha watu kama Manji. Hawa wajane waliotupwa nyuma miaka 25 kimaendeleo kwa kubomolewa nyumba zao kibabe sasa wataishi kama mashetani 1000 times than yale mafisafi yaliyokuwa/yapo TRA, Bandarini etc
 
Wananchi wakafungue kesi Canada na Marekani wazuie Dream-liner na Bombadia Kama Serikali inavunja Sheria dawa yake ndio hiyo Dawa ya Jeuri ni kusudi.. Siamini ukatiri kama huu unafanyika yaani idara zote zinavunja Katiba wazi wazi wakumbuke waliapa kwa Mungu wao...! Nawataka wawalipe fidia na wawajengee upesi nyumba kwenye maeneo yao sema this time kuwe na mpangilio bomba
 
Tatizo letu wengi hatutaki kusoma. Kwa faida yako njia 6 za lami zinahitaji mita 19.5 tu. Soma mada upate ufahamu


OMG.. Mungu akusaidie, i repeat again where did you copy & paste all these?

6 lanes unahitaji 19 meters? Uko duniani na una macho na ubongo? Uuuuhh.. Ur gone, ur lifeless, nyie ndio wasomi? Hii copying & pasting ni hatari sana..

I won't help you, the world will help you..!!
 
Kuna viongozi wa Tanzania watafungwa jela baada ya miaka michache sana , akiwemo huyu Dr Abass na wenzake , hawa hawana kinga hata chembe .
 
Back
Top Bottom