Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Tarehe 30 agosti 2017 Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo na msemaji Mkuu wa serikali alivitisha vyombo vya habari juu ya kuripoti zoezi la bomoa bomoa Kimara hadi kiruvia kwa sababu zoezi hilo linafanyika kisheria.

Ukweli ni kuwa bomoa bomoa hii ni kinyume cha Katiba ya nchi, Sheria ya barabara Namba 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009, inakiuka pia hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi iliyotolewa na Jaji S.B.Bongole tarehe 31 Mei 1013 katika shauri namba 80 la 2005. Na pia inakiuka hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyotolewa na Jaji S.A.N Wambura tarehe 13 Juni 2016 katika shauri namba 151 la 2015. (Naambatanisha Hukumu za mahakama husika)

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitamka kuwa Kanuni ya Sheria “The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”. Na ikaendelea kuwa ardhi inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara ya Morogoro, iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa opereshani vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999, ardhi hiyo ni mali halali ya wananchi waliofungua malalamiko.

Aidha katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ilitambua kuwa kuwa eneo husika (Jiji la Dar es Salaam) hivi sasa linatawaliwa na Sheria ya Mipango Miji ambayo inataka hifadhi ya barabara kuu kuwa ni mita 60 tu, yaani mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

Baada ya kushindwa Wizara ya ujenzi (Serikali) ikiiongozwa na Rais wa sasa Mhe John Pombe Magufuli ilikata rufaa Mahakam ya Rufaa katika shauri na 151 la 2015, ambalo lilitupiliwa mbali kwa kukosa hoja za msingi.

Tunasema kuwa Mhe Rais anavunja katiba aliyoapa kuilinda katika bomoa bomoa hii kwa kuwa Kifungu 107 (A) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kinatamka “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki”.

Hivyo basi kwa kuwa wananchi walishapatiwa haki ya ardhi yao na mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa bomoa bomoa inayoendelea inakiuka katiba ya nchi ambayo Mhe John Pombe Magufuli aliapa kuilinda.

Hivyo kitendo cha kuwapora wananchi ardhi yao waliyoipata kihalali na kwa mujibu wa sheria za nchi ni na umiliki huo kuthibitishwa na mahakama ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi, Mhe Rais aliyoapa kuilinda, tena baada ya kuwaharibia mali zao ikiwemo nyumba n.k. Kifungu 24 (1) cha Katiba ya Tanzania kinachotamka Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. (2) “Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili”.

Dhima ya Jeshi la Polisi ni “Kulinda usalama wa raia na mali zao, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kudhibiti uhalifu, kuwakamata watuhumiwa na kudumisha amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Lakini cha kushangaza ni jeshi hili hili ambalo linalotakiwa kulinda mali za watanzania kwa mujibu wa katiba, sheria za nchi na dhima yake ndilo ilnalotoa ulinzi kwa Tanroads kuharibu nyumba na mali za watanzania kwa kukiuka hukumu za Mahakama kuu na mahakama ya Rufaa. Kwa hili tumtaje IGP Mpya kujitafakari upya Na kuishauri mamlaka take ya uteuzi kuhusu ukiujwaji huu mkubwa wa Katuba ya nchi.

Kifungu 29 b cha Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, GN No 21 ya tar 23 Januari 2009 kinatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa eneo la kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mita 60 tu toka katikati ya barabara kila upande kama inavyoelekezwa barua ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani ya tarehe tarehe 21 Oktoba 2010 yenye Kumb Na TRD/CR/R.10/13/Vol.III/34 kwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha. Tokea kupitishwa kwake 2007, Tanroads walikuwa wakiheshimu sheria hii lakini tokea Mhe John Pombe Magufuli aliporejeshwa kuwa Waziri wa Ujenzi tarehe 24 Novemba 2010, akatoa maagizo kwa Tanroads kuwa wavunje sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake za 2009. Na alipochaguliwa Rais anatumia wadhifa wake kukiuka Katiba, Sheria Na haki za binadamu.

Bomoa bomoa hii pia inakiuka mikataba mbali mbali ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia kama ifuatavyo:-

  • Ibara ya 25 ya Tamko la Haki za Binadamu (Universal Decralation of Human Rights) inatambua haki za makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu.

  • Ibara ya 11 (1) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni wa 1966, ulioridhiwa na Serikali ya Tanzania tarehe 11 Juni 1976, (ambao Kamati ya Prof Osolo aliutumia kujenga hoja ya nchi kuwa haki zaidi juu ya raslimali zake) unazitaka Serikali zilizouridhia kutambua kuwa kila raia na familia yake wana haki ya kupata kiwango stahiki cha hali ya kimaisha ikiwemo chakula, mavazi, makazi na kuendelea kuboreshwa kwa hali zao za kimaisha.

  • Tamko namba 77 la 1993 la Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadumi linatamka kuwa “uhamishwaji kimabavu” (Forced eviction) ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaopelekea uvunjifu wa haki zingine za kibandamu kama vile kuwakosesha raia makazi, chakula, maji safi, afya, elimu, ajira, kipato, usalama, na kinga dhidi ya vitendo vya kinyama na udhalilishwaji n.k

  • Tamko namba 7 la 1997 la Kamati hiyo kupinga “Uhamishwaji Kimabavu” linasisitiza kuwa haki ya makazi ni pamoja na binadamu kuishi mahali kwa usalama, amani na heshima; na kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane na uhuru wa raia kulindwa dhidi ya uhamishwaji kimabavu na uharibifu wa makazi yake; kuwa na faragha katika makazi yake na kulindwa dhidi ya kuingiliwa isivyo halali. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi hivyo ni haki yetu sisi kama raia kupatiwa ulinzi dhidi ya vitendo vya Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi yetu vinavyolenga kutuhamisha kimabavu kwa kutuzuia kuendeleza mali zetu halali, kuharibu kwa makusudi majengo yatu na vitisho vya aina mbali mbali.
Tamko hilo lilifafanua zaidi kuwa haki ya makazi ni lazima iambatane ulinzi wa umiliki wa ardhi na makazi; fidia ya makazi, ardhi na maendelezo mengine; usawa katika kupata haki za makazi; na kushirikishwa katika maamuzi mbali mbali yanayohusu masuala ya makazi katika ngazi ya jamii na kitaifa. Kwa kuwa Mahakama kuu imeshatamka kuwa ardhi ambayo Wizara ya Ujenzi na Tanroads walikuwa wakidai ni hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha ni mali halali ya wananchi. Sisi raia tunaomiliki kihalali ardhi na makazi katika eneo husika tunayo haki kamili ya kushirikishwa katika maamuzi yote yanayohusu ardhi na makazi yetu.


Katika shauri lililokuwa mbele ya Mahakama ya Haki za binadamu ya Umoja wa Afrika (African Court on Human and Peoples’ Rights-Applications No 009&011of ka hiy2011), Serikali ya Tanzania ilinukuliwa kuthibitisha mbaele ya mahakama hiyo kuwa “it fully adheres to principles of the rule of law, separation of powers and independence of the judiciary as provided for under the Constitution of the United Republic of Tanzania”[1]. Hivyo vitendo vya Rais John Magufuli aliyekula kiapo kuilinda Katiba ya nchi kupuuza na kudharau hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa havikubalika hata kidogo katika nchi inayoongozwa kwa utawal wa sheria. Ni wakati sasa Mwalimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu kinchoheshimika cha Dar es salaam Prof Kabudi akamshauri Mhe Rais umuhimu wa kuheshimu hukumu za mahakama Na kujiepusha uvunjwaji wa Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.

Ibara ya 27 ya mkataba wa kimataifa wa Vienna (Vienna Convention on the Law of Treaties)provides that: “A party may not invoke the provisions of its internal law as justification for its failure to perform a treaty. Additionally, Article 32 of the International Law Commission Articles on State Responsibility 2001 provides that “the Responsible State may not rely on the provisions of its internal law as justification for failure to comply with its obligations”. Furthermore in the matter before the African Court on Human and Peoples’ Rights[1], in its judgement the court determined that “Having ratified the Charter, the Respondent (Tanzania Governmnet) has an obligation to make laws in line with the intents and purposes of the Charter.

Vile vile wajibu wa Serikali chini ya mikatba ya kimataifa imewahi kutolewa maamuzi na mahakama ya rufaa ya Tanzania katika shauri the Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia , ambapo mahakama ya rufaa ilitumia vifungu vya mkataba uitwao International Covenant on Civil and Political Rights kutafisiri haki za raia chini ya kifungu 15 kinachotoa haki za uhuru binafsi wa raia kwa kuamua “The fact that an International Convention to which Tanzania is a party is not incorporated into Tanzanian law does not absolve the government of its duty to adhere to its undertakings in the agreement.”[2]

K
wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikatba ya kimataifa kama ilivyotajwa hapo juu kifungu 29 B cha Kanuni za Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 zilizopitishwa katika gazeti la serikali kwa Tangazo namna 21 la 23 Jan 2009 hakiwezi kuwapokonya haki za kibanadamu za kumiliki ardhi na makazi yetu (viliyoko nje ya mita 30 toka katikati ya barabara ya Morogoro) kwa mujibu wa wajibu Serikali ya Tanzania ilionao chini ya mikataba ya kimataifa iliyotajwa hapo juu, hivyo ni wajibu wa Waziri wa sheria Prof Kabudi kumshauri Rais kuhusu wajibu nchi ilionao chini ya mikataba husika kulinda haki za binadamu hapa nchini.

Kifungu 27 cha kanuni hizo kinatamka upana wa njia za barabara za lami katika barabara kuu hapa nchini na hautakiwi kupungua mita 3.25 meters. Hivyo basi hifadhi ya barabara ya upana wa mita 60 meters, yaani mita 30 toka katikati ya barabara kila upande inaweza kujengwa njia za barabara (lanes) 18 (Meters 60/meter 3.25=18) 18 au pungufu yake na kuacha ardhi ya kutosha kwa shughuli zingine zinazohusiana na barabara kama vile njia za watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki maegesho ya magari na hata usafiri wa treni bila ya Serikali kudharau hukumu za Mahakam kuu na kuwavunjia wananchi haki zao za kibinadamu. Hivyo upanuzi wa barabara ya morogoro kuwa ya nji 6 za lami unahitaji mita 19.5 tu (3.25X6=19.5); hivyo bomoa bomoa hii sio kwa ajili ya upanuzi wa barabara bali kiongozi Fulani kutimiza kiu yake ya kutesa wananchi anaowatuhumu kuchagua vyama vya upinzani. (Naambatanisha kanuni za sheria ya barabara)
[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania

[2] Civil Application No. 19 of 1993 CAT Dsm, Transport Equipment and A versus D.P Valambhia.


[1] Judgement to Applications no. 009/2011 and no. 011/2011 before the African Court on Human and Peoples’ Rights at Arusha Tanzania
Taratibu za e-communications ni pamoja na brevit. sasa ndugu unaandika maelezo kama hukumu ya mahakama!!
Naomba nikuulize kwa maelezo hayo uliyoandika
The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”.
Kwa nini isiwe kinyume kwamba Sheria ya vijiji ni batili maana iliandikwa wakati Ordinance Cap ikiwa hai na ikaendelea kuwa hai?
 
Tatizo la nchi hii ni CCM na wabunge wake.

Hatima ya nchi hii mpaka sasa iko mikononi mwa CCM na wabunge wake.
Kama kuna anayeipoteza nchi hii tangu awali ni CCM na wabunge wake.

Hakuna linalofanyika ambalo halikua sera ya chama cha mapinduzi.
Mh.Rais anatekeleza kile kulichowekwa mezani na CCM ndio maana hakuna kada mpaka leo anayetoa hata maoni mbadala mana uwezo wao ndio uliopanga hayo.

CCM wanajua wanachofanya kuwa wamekipanga. Barabara ya juu na chini mpaka Chalinze sio tamko la leo la Rais bali lilitajwa tangu wakati wa awamu ya nne.
Reli ya standard gage sio haikuasisiwa na awu ya tano. Ilishapangwa tangu awamu ya nne. Awamu ya tano kazi yake ni kutekeleza ilani ya CCM iliyopangwa muda mrefu.

CCM ndio walipaswa waweke mipango yao na kuishauri serikali walioipa madaraka namna bora ya kuwapa wananchi haki yao bila kujali itikadi zao wala maiabila yao alimradi ni watanzania. CCM ndio walipaswa waielekeze serikali yao namna bora ya kutekeleza ilani yao ya uchaguzi bila kuhararisha maisha na uhai wa watanzania. CCM ndiyo ilipaswa isimamie kanuni yake inayosema " binadamu wote ni sawa", "Nitasema kweli daima."
CCM ndiyo ilipaswa iielekeze serikali yake kuwa JKT iliasisiwa kwa madhumuni ya kujenga Taifa na kutumika wakati wa majanga.

Bunge ni la CCM kwa maana kwamba wapinzani hawana uwezo wowote wa kuzuia jambo lolote lisipite wala achilia mbali kutoa ushauri wa jambo lolote na ukakubalika na kuwa ni hoja ya maana tangu alipoondoka marehemu Samweli Sita.
Bunge lilipaswa liweke sheria ya kulinda utu wa mtanzania kwa namna yoyote ile na iwe ni kosa la kiutendaji kwa mtu yeyote kuudhalilisha utu wa mtanzania kwa sababu yoyote ile alimradi isiwe ni sababu ya kutenda jinai.
Mtanzania maskini amejenga kajumba kake kwenye ENEO AMBALO HALIKUPIMWA HATA KWA WALE WALIOMZUNGUKA anavunjiwa nyumba yake ALIYOIJENGA SIO KWA LENGO LA KUFANYA UHALIFU BALI KUISHI NA KUJISETIRI MAISHA YAKE NA UTU WAKE KAMA BINADAMU ambaye kama CCM na Wabunge wake na Serikali yake wangekua makini angepimiwa eneo lake au angejengewa nyumba ya kuishi mana ndiye anayewapa hayo madaraka na kuifanya nchi iitwe Taifa ( Mana bila watu hakuna taifa ) . Bunge la CCM na CCM kama chama Tawala kilipaswa kuwajenge watanzania wote maskini nyumba za kuishi kwa malipo kidogo kwenye maeneo yote ya mijini. Huu ujenzi holela ni matokeo ya serikali ya CCM kutojali watu na maisha yao. Ujenzi usiofaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama maji,umeme,shule, maeneo ya michezo, usafiri, zima moto n.k. Haya yanathibitisha kuwa CCM sio chama kilichopaswa kuunda serikali ya kijamaa na hakifahamu maana ya ujamaa. Kimebaki na neno kujitegemea na kuua neno ujamaa kama kilivyoua Azimio la Arusha.

Haiwezekana bunge lenye nguvu kubwa ya CCM ikwepe lawama hii ya watu kuukoswshwa haki zao za msingi kama binadamu. Mahakama imejitahidi lakini bunge la CCM linawaacha wananchi waliolituma na kuamua kushikana na serikali kuwaumiza wananchi.
Siamini kuwa bunge lilishindwa kuweka kanuni au sheria na kuielekeza serikali itenge fedha kidogo tu kwa ajili ya makazi ya watanzania kabla ya kuwavunjia nyumba.


Siamini kabisa kuwa CCM na serikali yake na bunge lake inayotumia mabilioni ya fedha wakati wa uchaguzi kununua magari ya washawasha,kulipa vinwamgongo vya wabunge kwa miaka mitano, kununua magari ya kifahari ya serikali, kunua ndege, kununua madiwani na kuitisha uchaguzi wa mamilioni ( kwa mujibu wa Mbowe) n.k. inashindwa kuwatumia magereza , wafungwa na JKT kujenga nyumba za kutosha kabisa maeneo ya Mabwe pande na meneo mengine mengi yenye eneo la kutosha kwa ajili ya kuwahamishia wale wote walioko maeneo yanayohitajika kwa ajili ya miradi ya serikali ya maendeleo ya watanzania wote.

Wengine wanakuja na hoja nyepesi kuwa eti kuna watu wanajichomeka huko ili nao wapate fidia.Hayo ni matokeo ya mipango mibovu na malengo ya ubinafsi ya baadhi ya watawala. Kwa nini kila mtu alipwe fedha wakati amejenga kwenye eneo la mji bila kupimwa? Yani apewe fedha mkononi ili aende tena kujenga kiholela?

Kuwalipa watu 1000 kulinagana na aina ya nyumba za kuishi walizovunjiwa ni gharama mara kumi ya kuwajengea nyumba za kuishi kwa kutumia mfano magereza na wafungwa pamoja na JKT. Hawa wanatumia mishahara ya serikali tayari wanatakiwa wanunuliwe vifaa tu vya ujenzi ambavyo vinaweza kununuliwa kutoka kiwandani bila hata kodi na kujenga nyumba haraka kijeshi.
TUNASHINDWA NINI HAPO MPAKA WANADAMU NA WATANZANIA WENZETU WALALE NJE KWA SABABU YA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO?

Sio wamiliki tu wa nyumba bali hata wapangaji wao kuna uwezokano wa kuwajengea nyumba na wakalipia pango la nyumba kwa bei ndogo.

Haya mambo ya kuacha watu wanajenga majumba ya kupangishia wananchi wenzao kwa bei kubwa bila udhibiti na ubora wa mazingira na miundo mbinu ndiyo yanayosababisha watu wanakuwa wezi na wapiga dili kwa sababu wanatafuta pesa za kujenga ili wapangishe na mara nyingine wanajenga holela bila kuzingatia mipango miji. Kama serikali ingedhibiti ujenzi holele na kuhakikikisha kuwa inawapa wananchi wake nyumba za bei nafuu za kupanga hata wizi na ufisadi ungepungua. Watu wangekuwa wazalendo wa kweli sio wa kuigiza .

BILA CCM NA BUNGE LAKE KUJALI WATANZANIA NA HAKI ZAO NA UTU WAO NA UHAI WAO tutaendelea kuilaumu serikali tu bure wakati ndivyo ilivyoangizwa kwenye ilani yao.

Makamba alisema " Huyu aliyepo anawabatiza kwa maji bali ajaye atawabatiza kwa moto."
CCM ikisema kwamba sasa wabatizeni kwa maji, basi watabatizwa kwa maji ,na ikisema wabatizwe kwa moto watabatizwa kwa moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unahamisha goli 1000 digits
Issue sio CCM, hapa tunawazungumzia watawala wa awamu ya 5. Katika awamu 2 zilizopita ujenzi wa barabara na madaraja, viwanja vya ndege etc ulifanyika kwa kiwango kikubwa sana. WaPo watu walioumizwa lkn Wengi either walifidiwa na hata wale ambao hawakua na haki bado walisadiwa.. kumbuka kesi ya watu wa Jangwani waliopelekwa mabwepande.. etc.
Hili la sasa Nadhani si la chama ni watu wachache. Huwezi kusema kupuuza mahakama ni sehemu ya ilani ya ccm, au kuteka watu ni sehemu ya ilani ya ccm.
My intention here sio kuitetea ccm bali tuujadili huu uongozi kwa ku pinpoint sehemu yenye shida rather than kuwa vague na kupoteza focus. Our biggest problem ni watawala wa leo, ofkoz ccm ndio sponsor wao.
 
Kwa kweli mkuu wetu anafanya mambo ya aibu sana kwa mtu mwenye akili timamu!! Hii ni wazi kabisa analipiza kisasi cha kushindwa mahakamani na hao wananchi kipindi alipokuwa waziri wa ujenzi. Sasa kwa vile ameshika muhimili ambao mzizi wake umejichimbia chini zaidi ameamua kuwakomoa!! Rais wa awamu ya 6 ajiandae kulipa fidia kwa haya mambo ya aibu yanayofanywa na awamu hii ya 5!! Lawama hizi zimfikie Kikwete, ndiye aliyetufikisha hapa tulipo sasa hivi!!
Mahakama zetu nazo angalieni zinavyofanyakazi. Ndo hao majaji wanapangiwa hata bei za kuachia makosa ya mauaji. Ndo hao wamekuwa wakiwalinda wanaovamia viwanja vya wenzao eti aliyepoteza kiwanja apatiwe kingine, nk.

Usijisikie vibaya serikali ikiamua kuachana na maamuzi yao bora tu iwe ni kwa lengo la manufaa kitaifa. Tukianza kuendeshwa kwa amri za mahakama, nchi haiendi. Tuna majaji wadhaifu sana kuliko unavyoamini. Duniani kote hakuna aliyeendelea kwa mtindo huo au eti demokrasia. Hakuna nchi iliyoendelea kwa sababu ya demokrasia. demokrasia huja baada ya maendeleo.
 
Kimara wamekomolewa kwa sababu
1.Wengi ni kutoka kaskazini
2.Walichagua upinzani
Ndio maana hata mkuu wa mkoa hajahanqaika kuwatembelea wala kuzuia unlike tuangoma ambako mbunge ni wa ccm.Huu ubaguzi wa wazi .
Tuangoma Na mabondeni ilikuwa bomoa bomoa feki ili kuuchanganya umma baada ya serikalu kulazimika kuitii zuo la mahakama Kinara
 
Tatizo letu wengi hatutaki kusoma. Kwa faida yako njia 6 za lami zinahitaji mita 19.5 tu. Soma mada upate ufahamu
Tatizo lako ni kwamba post uliyoweka ipo biased.

Mnahangaika mitandaoni kupambana na serikali. Kinachotakiwa ni kurudi kwenye mstari. Sheria ya Barabara kuu ya mita 121 kila upande izingatiwe.

Watu wanajua wanatakiwa kubomoa kisha wanawauzia wengine baada ya fidia halafu badala ya kuangalia mzizi wa tatizo mnakimbilia kuilaumu serikali....

Nimesoma narration yako kule juu nilichoambulia ni HATE approach and not reconciliation seeking
 
Mahakama zetu nazo angalieni zinavyofanyakazi. Ndo hao majaji wanapangiwa hata bei za kuachia makosa ya mauaji. Ndo hao wamekuwa wakiwalinda wanaovamia viwanja vya wenzao eti aliyepoteza kiwanja apatiwe kingine, nk.

Usijisikie vibaya serikali ikiamua kuachana na maamuzi yao bora tu iwe ni kwa lengo la manufaa kitaifa. Tukianza kuendeshwa kwa amri za mahakama, nchi haiendi. Tuna majaji wadhaifu sana kuliko unavyoamini. Duniani kote hakuna aliyeendelea kwa mtindo huo au eti demokrasia. Hakuna nchi iliyoendelea kwa sababu ya demokrasia. demokrasia huja baada ya maendeleo.
Unasemaje kuhusu utekelezaji wa sheria moja kibaguzi kulingana Na wananchi walipiga kura kivipi?
Ungekuwa umesoma mada yangu ndio ungeweza kuniambia hayo maendeleo unayoyasema ni yapi!
 
Mkuu Jatropha umefanya assumption kuwa sheria Bado zinafuatwa na kuheshimiwa Tz , what if that assumption is not adhered
 
Tatizo lako ni kwamba post uliyoweka ipo biased.

Mnahangaika mitandaoni kupambana na serikali. Kinachotakiwa ni kurudi kwenye mstari. Sheria ya Barabara kuu ya mita 121 kila upande izingatiwe.

Watu wanajua wanatakiwa kubomoa kisha wanawauzia wengine baada ya fidia halafu badala ya kuangalia mzizi wa tatizo mnakimbilia kuilaumu serikali....

Nimesoma narration yako kule juu nilichoambulia ni HATE approach and not reconciliation seeking
Unajitahidi sana kuitetea serikali lakini ukweli utabaki pale pale. Ndio mahakama zote zikawapa wananchi haki
 
Hivi hakuna namna tunaweza kufungua kesi ya kikatiba dhidi ya Rais apokiuka katiba aliyoapa kuilinda? Tumpeleke mahakamani huyu. Najua Wanasheria mmo humu JF toeni ushauri ili kusaidia watanzania wenzetu wanaonyanyasika na hii bomoa bomoa.
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mauziano yote huratibiwa na serikali kwa namna moja au nyingine, (kuanzia serikali ya mtaa hadi TRA)
There's no excuse!
Serikali katili kupindukia.
 
Taratibu za e-communications ni pamoja na brevit. sasa ndugu unaandika maelezo kama hukumu ya mahakama!!
Naomba nikuulize kwa maelezo hayo uliyoandika
The Highway Ordinance Cap 167” Tangazo la Serikali la 161 la tarehe 5 Mei 1967 “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”.
Kwa nini isiwe kinyume kwamba Sheria ya vijiji ni batili maana iliandikwa wakati Ordinance Cap ikiwa hai na ikaendelea kuwa hai?
Mkuu hayo sio maneno yangu, nimenukuu hukumu ya mahakama kuu. Kwa kutokukubakiana Na hukumu husika ndio serikaki ilikata rufaa mahakama ya rufaa, Na rufaa hiyo kutupiliwa mbali kwa kukosa hoja za msingi
 
Kwa nyakati hizi msitegemee haki ukiamsha kicha wanaku-sanane kama si kuku-roma, ubishi ukiendelea wataku-IMMMA.
 
Na huenda ile zuga ya konda kwenda tuangoma ili kufake hii bomoabomoa na ku-seek sympathy na baadae kidogo mkulu akatangaza kusimamisha ubomoaji ni sanaa tu. Huenda wajuvi wa sheria waliongea naye juzi na kamtuma mwanaye kipenzi kwenda ili kupooza hali ya hewa. Yaani kuua uue wewe na kwenye msiba uende na kujifanya una huzuni kuliko wafiwa! Ni kwa tz tu hii kitu inafanya kazi! Tulieni ofisini mkitafuta rejea za mambo unayotaka kuyafanya kwani haiwezekani wewe ukawa wa kwanza kufanya jambi hilo na huenda lilishawahi kufanyika na kuishia mahali fulani. Kitendo cha kuwabomolea watu ni kinyume na mipango ya Mungu!
 
Unahamisha goli 1000 digits
Issue sio CCM, hapa tunawazungumzia watawala wa awamu ya 5. Katika awamu 2 zilizopita ujenzi wa barabara na madaraja, viwanja vya ndege etc ulifanyika kwa kiwango kikubwa sana. WaPo watu walioumizwa lkn Wengi either walifidiwa na hata wale ambao hawakua na haki bado walisadiwa.. kumbuka kesi ya watu wa Jangwani waliopelekwa mabwepande.. etc.
Hili la sasa Nadhani si la chama ni watu wachache. Huwezi kusema kupuuza mahakama ni sehemu ya ilani ya ccm, au kuteka watu ni sehemu ya ilani ya ccm.
My intention here sio kuitetea ccm bali tuujadili huu uongozi kwa ku pinpoint sehemu yenye shida rather than kuwa vague na kupoteza focus. Our biggest problem ni watawala wa leo, ofkoz ccm ndio sponsor wao.


[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hapo kwenye kuhamisha goli umenipata sana.

Hata ivyo nikukumbushe tu kuwa CCM ni chama cha mapinduzi kweli kweli sio utani.

CCM ninaifananisha na jamaa mmoja alikuaga mbabe ,mkabaji na mwizi.
Alikua anamkaba mtu mchana kweupe akiwa amefunika uso. Baada ya tukio hilo anakua wa Kwanza kufika kutoa pole na kumfariji mhanga tena anamsindikiza polisi ili akatoe taarifa. Anamsindikiza polisi sio kwa lengo jema bali kumdhibiti mlalamikaji ili akiulizwa kuwa anamuhisi nani aliyemuibia iwe vigumu kumtaja japo kwa hakika kabisa ilikua inajikana kuwa ndiye aliyetenda kosa hilo. Ilikua ni vigumu kwa watu kumtaja kutokana na kuhofia ubabe wake wakati pia ushahidi ulikosekana.

Nikirejea kwenye msingi wa kuwa CCM ndiye mhusika mkuu wa matatizo yanayojitokeza na sio serikali pekee, ni kutokana na muundo wa katiba ambayo inapata viongozi kupitia vyama vya siasa. Na utekelezaji maendeleo hufanywa kutokana na ilani za chama kinachoshinda uchaguzi au maelekezo ya vikao vyake. Nakumbuka wakati wa awamu ya nne Katibu mkuu ali.wambia rais kuwa kuna mawaziri mizigo na hata kuwataja kwa wizara zao.
Kama serikali ingekua imekosea bila kuelekezwa na CCM naamini kuwa wangeikosoa. Lakini ni mara nyingi tumewasikia wakiisifu na kuinga mkono serikali kwa kusimamia vyema ilani yake ya uchaguzi. Kwa nini mazuri tuyaite ya CCM na mabaya tuyaite ya serikali?
Mazuri ni ya CCM na mabaya pia pale inapokaa kimya na bunge lake.


Ukirejea kauli za viongozi na wa CCM utafahamu kuwa haya yanayotokea ni makubaliano na utekelezaji wa ilani ya CCM. Rejea kauli ya Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake wakati wa kampeni " Mulisema kuwa mie ni mpole mpole sasa nawaletea hiki chuma hapa ,na ameanza kutema cheche" wanachama wa CCM wakatia shangwe na vigelegele[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji33] [emoji33] [emoji33] [emoji33] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
Makamba kwenye mkutano mkuu wa CCM akawaambia "Huyu aliyepo anawabatiza kwa maji lakini huyu ajaye atawabatiza kwa moto"
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] Wajumbe wa mkutano mkuu wakalipuka kwa shangwe vigelegele na nderemo wakiongozwa na wimbo wa wataisoma namba CCM ,mbele kwa mbele[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji33] [emoji33] [emoji33] [emoji23] [emoji23] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji108] [emoji108] [emoji108] [emoji108] [emoji108] [emoji108] [emoji108] [emoji108] .

Haya mambo yalipangwa kuwa ni lazima yaende kama walivyopanga iwe mchana au usiku ,mvua inyeshe au jua liwake. Ndio maana hata wabunge wa CCM hawaoni tena hadhi ya mbunge na bunge kuwa sehemu ya kutema checha matokeo yake bunge linatemewa cheche na vikao vya chama mana wote ni wajumbe. Wanatekeleza ilani ya chama chao.
Wabunge mwanzoni walikua ni wamoja wanapotoka bungeni na walikua wanatetea hadhi ya bunge na ndioa maana kuna wakati walikua wanatembeleana hata gerezani kuonyesha kuwa bunge ni mhimili mmoja na una heshima yake na kinga yake. Leo wabunge wanaposimama na kuwanyanyasa wabunge wenzao ndani na nje ya bunge kwa sababu ya kuubeba muhimili mwingine hili sio jambo la kawaida ni jambo la kichama mana wanaowajibishwa vikali ni wa vyama vingine. Ingekua wote wanawajibishwa bila kujali chama tungeona ni sawa.

Mimi binafsi naamini kuwa serikali ya awamu ya tano kama zilivyokuwa zilizotangulia zinaelekezwa na bunge(Wengi ni CCM) na pia Chama tawala( CCM).Na serikali imekua ikipokea ushauri na pongezi toka kwa wabunge na wanachama wa CCM kwa kutekeleza vema ilani ya yake.
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama walishalipwa iwaje mahakama itoe zuio? Na tulisoma makaratasi ya zuio yaliyobandikwa lkn bado nyumba zilibomolewa tu....!!! Ifike sehemu km watanzania tunaofundishwa upendo na dini zetu tuwe na utu badala ya kushabikia siasa zinazo waingiza binadamu kwenye umasikini mkubwa wa kukosa sehemu za kuishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu hii amri za mahakama hazifatwi!

Ova
 
Tatizo umekurupuka kuchangia haukusoma mada yangu. Nimesema sheria ya barabara Na 13 ya 2007 Na Kanuni zake za 2009 kwa kipande hiki kutika Ubungi hadi Tamco Kibaha inatamka hifadhi ya barabara ni mita 60 kila upande, kwa maana ya mita 120 kama bomoa bomoa ilivyofanyika Maili Moja Kibaha kwa sababu vingozi wa kuchagu
liwa kule ni kutoka CCM. hivyo kwa barabara ya unazozisema za njia 24 za lami zingehitaji mita 78 tu ( 3.25x24=78) kwa mujibu wa sheria niliyoitaja ktk mada yangu hapi juu; Na eneo hifadhi ya Barbara LA mita 48 kusalia.

Sasa kama sio hila za kisiasa kwanini eneo la Kimara hadi Kiruvia serikali inabomoa mita 240, yaani mita 120 kila upande toka katikati ya bsrabara? Yaani sheria moja inabagua sehemu ambapo Mbunge Na madiwani ni kutoka CCM Na upinzani?

Ndiyo maana nikasema compensation ni lazima kabla ya bomoabomoa!
 
Back
Top Bottom