Ukweli kuhusu bomoa bomoa ya Kimara hadi Kiluvya

Without law and order we are nothing but a group of savages. Kuna vitu jpm anavurunda sana mpaka inashangaza kama ana hekima ya kutosha kushika ile ofisi.

Ninaamini kwamba huyu ni kichaa.
 
OMG.. Mungu akusaidie, i repeat again where did you copy & paste all these?

6 lanes unahitaji 19 meters? Uko duniani na una macho na ubongo? Uuuuhh.. Ur gone, ur lifeless, nyie ndio wasomi? Hii copying SABABU YA YEYE KUANDIKA HIVO& pasting ni hatari sana..

I won't help you, the world will help you..!!
WEWE UNAMDHARAU MENZAKO YEYE ANA AKILI ZAKE. HIVI KAMA KILA NJIA MOJA UPNA NI MITA 3 SASA BARABARA YA NJIA 6 INAHITAJI UPANA GANI? AU UMESHAWAHI ONA GARI PANA ZAIDI YA MITA 3? KAMA UNA LORI PIMA UPANA WAKE UTAELEWA
 
Tusiingize masihara kwenye maisha ya watu unaweza kutupatia ushahidi ya waliolipwa fidia kama ambavyo nimeweka Mimi hapo juu?
Bro, ukianza kudadavua haki usiegemee upande.
Suala la bomoabomoa linachukiza sana, hasa unapoangalia utekelezaji wake.
Ulivyoichambua sheria yawezekana kabisa serikal ina makosa yake katika zoezi hili.
Je sisi raia ni weupe kabisa, nikimaanisha kuwa hakuna mwananchi hata mmoja wa kunyooshewa kidole?
Nijuavyo mimi kuna viongozi wa mitaa waliohusika sana kupotosha sheria za umiliki wa ardhi kwa kugawa maeneo ovyo na baadaye, "aridhi" kuja kuhalalisha makazi kwa kutoa hati miliki.
Pili, kuna watu baada ya kugundua wanaishi kijinai eneo husika, harakaharaka waliyauza maeneo ama makazi yao "kihalali"na kuondoka wakiacha eneo linafukuta kwa mgogoro.
Tatu, kuna wamiliki wa mwanzo walitangaziwa kuwa makazi yao yapo ndani ya hifadhi ya barabara na wakalipwa wakitakiwa kuhama. Lakini kwa udhaifu wa utekelezaji wa sheria, wananchi waliofidiwa waliachwa wakiendelea kuishi maeneo hayo hadi wengine wakayauza ki rushwa kwa wamiliki wengine.
Hayo machache niliyoyaeleza yamo kwenye "mduara" wa kadhia hii.
Kama nilivyokwisha eleza, maelezo yako yameegemea upande mmoja tu wa maslahi yako binafsi, yaani ulipoguswa wewe.
Hiyo ni dosari.
Halafu kwa nini ninyi wajuvi wa sheria, huwa mna-comment pale tu maslahi yenu binafsi yanapokuwa yameguswa na si maslahi ya umma mpana?
Kwa mfano, hivi suala la fukuzafukuza ya bila malipo kwa watumishi wa vyeti bandia, ulisimama ukatoa ushauri wowote wa kisheria unaopaswa kufuatwa na wale wote waliodhulumiwa haki zao katika muktadha wa vyeti?
Watu wanafukuzwa bila malipo na hawajui waanzie wapi huku wanasheria mpo tu kimya!
Dhuluma ngapi serikali imefanya, lakini wanasheria kimya! Kwamba haiwahusu.
Sasa tingatinga limekuja kuporomosha majumba yenu ndiyo mnaanza kukumbuka mlipoweka kalamu zenu?
Tumieni taaluma yenu kwa manufaa ya raia wote ili kuokoa taifa lisitumbukie kwenye mgogoro wa kisheria
 
Mkuu wewe ni mtaalamu wa civil engineering?
Sihitaji kuwa Na utaalamu huo. Nimekuwekea kifungu cha sheria kuhusu upana wa lane moja ya barabara ya lami inavyotakiwa kua. Kama tunajenga 6 lanes it is simple multiplication. Mbona mnahangaika?
 
Bro, ukianza kudadavua haki usiegemee upande.
Suala la bomoabomoa linachukiza sana, hasa unapoangalia utekelezaji wake.
Ulivyoichambua sheria yawezekana kabisa serikal ina makosa yake katika zoezi hili.
Je sisi raia ni weupe kabisa, nikimaanisha kuwa hakuna mwananchi hata mmoja wa kunyooshewa kidole?
Nijuavyo mimi kuna viongozi wa mitaa waliohusika sana kupotosha sheria za umiliki wa ardhi kwa kugawa maeneo ovyo na baadaye, "aridhi" kuja kuhalalisha makazi kwa kutoa hati miliki.
Pili, kuna watu baada ya kugundua wanaishi kijinai eneo husika, harakaharaka waliyauza maeneo ama makazi yao "kihalali"na kuondoka wakiacha eneo linafukuta kwa mgogoro.
Tatu, kuna wamiliki wa mwanzo walitangaziwa kuwa makazi yao yapo ndani ya hifadhi ya barabara na wakalipwa wakitakiwa kuhama. Lakini kwa udhaifu wa utekelezaji wa sheria, wananchi waliofidiwa waliachwa wakiendelea kuishi maeneo hayo hadi wengine wakayauza ki rushwa kwa wamiliki wengine.
Hayo machache niliyoyaeleza yamo kwenye "mduara" wa kadhia hii.
Kama nilivyokwisha eleza, maelezo yako yameegemea upande mmoja tu wa maslahi yako binafsi, yaani ulipoguswa wewe.
Hiyo ni dosari.
Halafu kwa nini ninyi wajuvi wa sheria, huwa mna-comment pale tu maslahi yenu binafsi yanapokuwa yameguswa na si maslahi ya umma mpana?
Kwa mfano, hivi suala la fukuzafukuza ya bila malipo kwa watumishi wa vyeti bandia, ulisimama ukatoa ushauri wowote wa kisheria unaopaswa kufuatwa na wale wote waliodhulumiwa haki zao katika muktadha wa vyeti?
Watu wanafukuzwa bila malipo na hawajui waanzie wapi huku wanasheria mpo tu kimya!
Dhuluma ngapi serikali imefanya, lakini wanasheria kimya! Kwamba haiwahusu.
Sasa tingatinga limekuja kuporomosha majumba yenu ndiyo mnaanza kukumbuka mlipoweka kalamu zenu?
Tumieni taaluma yenu kwa manufaa ya raia wote ili kuokoa taifa lisitumbukie kwenye mgogoro wa kisheria
Hongera kwa kujitahidi kuitetea serikali kwa hoja za jumla. Ili tuelimishane mada hii ilihitaji documentary evidence. Laiti ungedownload hukumu nilizo attach Na kuzisoma usingeandika hayo uliyoandika.
Nikuulize swali Dogo. Je Kamishna wa Ardhi anaweza kutoa hati miliki kwenye Road Reserve?.
Mbona baadhi ya wanaobomolewa wa hati miliki Na zilizolipiwa uptodate?
 
Without law and order we are nothing but a group of savages. Kuna vitu jpm anavurunda sana mpaka inashangaza kama ana hekima ya kutosha kushika ile ofisi.
Na utashangaa bado kuna wananchi wanaotetea huu uhalifu
 
Km ulilipwa alafu ukaendelea kuishi kwa ubishi lawama kwa nani wasio lipwa ndio waendelee kutafuta akiyao kwakuwa awakupata jasho lao wengine wanalipwa kwa makusudi wanauza alafu yuleanaekuja ndio yanamkuta majanga muda mwingine tusiweke lawama kwaserekali pekee wakati kunawatu wanashirikiana na serikali za mitaa kurubuni watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili yako inashida.
 
Hakuna sababu ya kutumia fedha za malipa kodi kulipa. Eneo LA hifadhi halali ya barabara LA mita 60, 30 kila upande linaweza kujengwa njia za lami 18. Hats marekani, Japan n.k hakuna barabara kama hiyo. Manispaa ya ubungo wanakomolewa kwa kuchagua mbunge na madiwani wa chadema

Acha kusema uongo, kuna barabara za lane 12 yaani sita za kwenda na sita kurudi zinaitwa interstate highways! Nimeziona ila nilishangaa mpaka ikabidi nipate ufafanuzu kwa wenyeji, tembea uone! Hapo ilikuwa wapate compensation(fidia) kabla ya ubomoaji. Barabara za Dar - Mwanza, Dar Arusha/Namanga/Taveta na Dar - Tunduma ni vema zingekuwa 12 lanes roads ili miaka 100 ijao iwe imekuwa ni vision ya taifa.
 
Acha kusema uongo, kuna barabara za lane 12 yaani sita za kwenda na sita kurudi zinaitwa interstate highways! Nimeziona ila nilishangaa mpaka ikabidi nipate ufafanuzu kwa wenyeji, tembea uone! Hapo ilikuwa wapate compensation(fidia) kabla ya ubomoaji.
Tatizo umekurupuka kuchangia haukusoma mada yangu. Nimesema sheria ya barabara Na 13 ya 2007 Na Kanuni zake za 2009 kwa kipande hiki kutika Ubungi hadi Tamco Kibaha inatamka hifadhi ya barabara ni mita 60 kila upande, kwa maana ya mita 120 kama bomoa bomoa ilivyofanyika Maili Moja Kibaha kwa sababu vingozi wa kuchagu
liwa kule ni kutoka CCM. hivyo kwa barabara ya unazozisema za njia 24 za lami zingehitaji mita 78 tu ( 3.25x24=78) kwa mujibu wa sheria niliyoitaja ktk mada yangu hapi juu; Na eneo hifadhi ya Barbara LA mita 48 kusalia.

Sasa kama sio hila za kisiasa kwanini eneo la Kimara hadi Kiruvia serikali inabomoa mita 240, yaani mita 120 kila upande toka katikati ya bsrabara? Yaani sheria moja inabagua sehemu ambapo Mbunge Na madiwani ni kutoka CCM Na upinzani?
 
Bro, ukianza kudadavua haki usiegemee upande.
Suala la bomoabomoa linachukiza sana, hasa unapoangalia utekelezaji wake.
Ulivyoichambua sheria yawezekana kabisa serikal ina makosa yake katika zoezi hili.
Je sisi raia ni weupe kabisa, nikimaanisha kuwa hakuna mwananchi hata mmoja wa kunyooshewa kidole?
Nijuavyo mimi kuna viongozi wa mitaa waliohusika sana kupotosha sheria za umiliki wa ardhi kwa kugawa maeneo ovyo na baadaye, "aridhi" kuja kuhalalisha makazi kwa kutoa hati miliki.
Pili, kuna watu baada ya kugundua wanaishi kijinai eneo husika, harakaharaka waliyauza maeneo ama makazi yao "kihalali"na kuondoka wakiacha eneo linafukuta kwa mgogoro.
Tatu, kuna wamiliki wa mwanzo walitangaziwa kuwa makazi yao yapo ndani ya hifadhi ya barabara na wakalipwa wakitakiwa kuhama. Lakini kwa udhaifu wa utekelezaji wa sheria, wananchi waliofidiwa waliachwa wakiendelea kuishi maeneo hayo hadi wengine wakayauza ki rushwa kwa wamiliki wengine.
Hayo machache niliyoyaeleza yamo kwenye "mduara" wa kadhia hii.
Kama nilivyokwisha eleza, maelezo yako yameegemea upande mmoja tu wa maslahi yako binafsi, yaani ulipoguswa wewe.
Hiyo ni dosari.
Halafu kwa nini ninyi wajuvi wa sheria, huwa mna-comment pale tu maslahi yenu binafsi yanapokuwa yameguswa na si maslahi ya umma mpana?
Kwa mfano, hivi suala la fukuzafukuza ya bila malipo kwa watumishi wa vyeti bandia, ulisimama ukatoa ushauri wowote wa kisheria unaopaswa kufuatwa na wale wote waliodhulumiwa haki zao katika muktadha wa vyeti?
Watu wanafukuzwa bila malipo na hawajui waanzie wapi huku wanasheria mpo tu kimya!
Dhuluma ngapi serikali imefanya, lakini wanasheria kimya! Kwamba haiwahusu.
Sasa tingatinga limekuja kuporomosha majumba yenu ndiyo mnaanza kukumbuka mlipoweka kalamu zenu?
Tumieni taaluma yenu kwa manufaa ya raia wote ili kuokoa taifa lisitumbukie kwenye mgogoro wa kisheria
Lete ushahidi wa fidia mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, waliokumbwa na haya matukio ya kutisha ya kuvunjiwa nyumba zao watalipwa fidia wanazostahili!?

Je, waliohusika na huu uvunjaji wa sheria za nchi watachukuliws hatua stahiki ikiwemo kufukuzwa kazi na kupandishwa kizimbani!?

Wote waliotoa matinga tinga ya uvunjaji walioamrisha polisi na ffu kusimamia hilo tukio haramu.

Inakuwaje Mkuu wa Mkoa, Waziri wa ardhi, wa mambo ya ndani na huyo wa Ikulu wasijue uvunjwaji wa sheria za nchi ambao kila siku ulikuwa unaandikwa katika magazeti na kutangazwa na TV na Radio katika taarifa za habari zao!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli ni kati ya watawapa wa Afrika mashetani haiwezekani mtu ana furaha maumivu ya wananchi wake mbaya zaidi kudharau mahakama halafu tu nasema tuna utawala wa sheria cha aibu
 
Kimara wamekomolewa kwa sababu
1.Wengi ni kutoka kaskazini
2.Walichagua upinzani
Ndio maana hata mkuu wa mkoa hajahanqaika kuwatembelea wala kuzuia unlike tuangoma ambako mbunge ni wa ccm.Huu ubaguzi wa wazi .
 
Si kila mtu anafaa kuwa kiongozi!!.

Tujiandae tena kulipa watu fidia.
Kwa kweli mkuu wetu anafanya mambo ya aibu sana kwa mtu mwenye akili timamu!! Hii ni wazi kabisa analipiza kisasi cha kushindwa mahakamani na hao wananchi kipindi alipokuwa waziri wa ujenzi. Sasa kwa vile ameshika muhimili ambao mzizi wake umejichimbia chini zaidi ameamua kuwakomoa!! Rais wa awamu ya 6 ajiandae kulipa fidia kwa haya mambo ya aibu yanayofanywa na awamu hii ya 5!! Lawama hizi zimfikie Kikwete, ndiye aliyetufikisha hapa tulipo sasa hivi!!
 
Mkuu umenikumbusha ule weledi wa jamii forums ya enzi hizo. Asante kwa uchambuzi uliotoa. Kama kuna mwenye mawazo tofauti adadavue zaidi ya hapa ili tupate ilim zaidi
 
Back
Top Bottom