KWA HESABU za haraka haraka tuseme kila mchezo wa bahati nasibu iwe Jivulie au Mkopo au Mwanakuliwa au Mjingahajui na kadhalika inayoendesha na makampuni ya simu za mkononi kwenye televisheni inapata washiriki 300,000 tu ambayo ni idadi ya chini mno, kisha kwa kila mmoja wao anacheza mara 10 tu kitu ambacho sio rahisi lazima acheze zaidi kutokana na uroho wa kutaka kuukata; halafu kila mmoja anakatwa shilingi 1,000 tu kwa ujumbe mfupu. Piga hesabu : jumla hii ya chini inatupa hesabu ya shilingi bilioni tatu- safi kabisa na sijui hata kama zinalipiwa kodi wala ushuru wowote. Na hata wakikata theluthi ya hapo wakatoa bilioni moja hivi bado wana faida pale wasipopanda lakini wanavuna kama vile vichaa. Mtu akinunua magari ya mtumba 100 kwa bei ya shilingi milioni 10 kila gari anakuwa ametumia shilingi bilioni moja tu. Wapi na wapi ? Nani kaliwa kama sio mtumiaji simu za mkononi mlalahoi. Kwa hiyo kaa ukitambua kwamba michezo hiyo ya kamari na hasa kwa wewe unayestahili kuiogopa dini yako na yule aliyekuumba inazidi kukufanya wewe uwe masikini zaidi na zaidi na haikupi nafuu yoyote.
Kuna wasiwasi kuwa michezo hii yote ya bahati nasibu kupitia simu za mkononi ina nia ya kufadhili vyama fulani vya siasa, yaani, mapato yatakuwa yakigawiwa kati ya kampuni ya simu mkononi na chama shirika cha kisiasa. Je, ni kweli ?
Kuna wasiwasi kuwa michezo hii yote ya bahati nasibu kupitia simu za mkononi ina nia ya kufadhili vyama fulani vya siasa, yaani, mapato yatakuwa yakigawiwa kati ya kampuni ya simu mkononi na chama shirika cha kisiasa. Je, ni kweli ?